BBC News, Swahili - Habari
Habari Kuu
Trump aahidi 'pigo kali sana' dhidi ya Iran iwapo itathibitika kuhusika na tukio la flydubai
Rais wa Marekani Donald Trump ameapa kuipiga Iran "pigo kali sana" ikiwa itathibitishwa kuwa ilihusika katika shambulio dhidi ya rubani wa shirika la ndege la flydubai.
'Utekelezaji wa hukumu ya kifo ya Christa Pike uliotibuka: Nini nilitokea na nini kinafuata?"
Muuaji huyo aliyepatikana na hatia amelazwa hospitalini Tennessee baada ya kunusurika sindano mbili za sumu, katika kesi iliyoibua maswali mengi.
Jinsi kampuni kubwa ya viatu vya michezo duniani ilivyopoteza mvuto wake
Nike imekabiliwa na miaka migumu kutokana na makosa ya kimkakati, kupungua kwa ubunifu wa bidhaa na ushindani kutoka kwa chapa mpya kama On na Hoka. Kupungua kwa mauzo na kupoteza baadhi ya wanamichezo wakubwa kumeongeza changamoto katika juhudi za kampuni hiyo kurejesha nguvu yake.
Vyakula 6 vinavyoweza kukusaidia kupunguza kasi ya kuzeeka
Utafiti mpya unaonyesha uhusiano kati ya kile unachokula na jinsi unavyozeeka—na vyakula ambavyo vinaweza kusaidia kupunguza kasi ya mchakato wa kuzeeka.
Paka mweusi wa ajabu anayepatikana Afrika pekee
Paka wa porini 'Serval' wamekuwa wakionekana katika maeneo ya mwinuko mkubwa, kama vile Nyanda za Juu za Aberdare nchini Kenya, ambako hali ya hewa ya baridi na yenye ukungu inaonekana kuendana zaidi na manyoya yao meusi.
'Nilivuta usukani': Abiria asimulia Jinsi alivyoinusuru ndege rubani alipochomwa kisu
Shirika la ndege la Flydubai limetangaza kusitisha safari zake kuelekea Tel Aviv hadi uchunguzi wa tukio hilo utakapokamilika.
Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa: Real Madrid yavutiwa na Quansah
Quansah alikuwa akiwaniwa na Arsenal, ambayo iliwasilisha ofa ya kumsajili majira ya joto yaliyopita, huku Chelsea nayo ikiulizia upatikanaji wake.
Sir Wicknell alipataje utajiri wake?
Chivayo ameacha kampuni, mali na mahusiano na watu wenye ushawishi, lakini pia ameacha maswali ambayo huenda baadhi ya majibu yake ameondoka nayo.
Teknolojia 5 zinazombadilisha binadamu kuwa nusu mashine
Kuruka angani kwa muda mrefu kumekuwa ndoto ya binadamu, kuanzia simulizi ya Kigiriki la Icarus hadi magari yanayoruka yaliyooneshwa katika filamu za sayansi ya kubuni kama Blade Runner.
Je, Wahouthi wameziunganisha Saudi Arabia na UAE kwa karibu zaidi?
Sheikh Mansour bin Zayed Al Nahyan, Makamu wa Rais wa Falme za Kiarabu (UAE), ambaye alikuwa katika ziara nchini Saudi Arabia kwa mwaliko wa nchi hiyo, alikutana na Mrithi wa Ufalme wa Saudi Arabia, Mohammed bin Salman
Mfanyabiashara maarufu wa Zimbabwe Wicknell Chivayo afariki dunia, rambirambi zamiminika
Polisi walisema ajali hiyo ilitokea karibu saa 11 jioni kwa saa za Zimbabwe, Mashariki mwa mji mkuu Harare na kuua watu wote waliokuwemo
Mfahamu rubani Smit Machhar, aliyeinusuru ndege ya Dubai kuelekea Israel
Rubani Smit Machhar sasa anasifiwa kote duniani kama 'shujaa' mwenye ujasiri wa safari ya ndege kati ya Dubai na Israel.
Unataka kupunguza gharama za data?
Soma mtandao wetu wa maandishi kwa gharama ndogo za data.
Gumzo mitandaoni
Miji bora zaidi duniani mwaka 2026 na siri za mafanikio yake
Ni nini kinachoufanya mji uwe wa kuvutia kiasi cha watu kutaka kuishi humo, kufanya kazi au hata kuutembelea?
Edward Rukidi Kijanangoma: Kutoka uwanahabari hadi ufalme wa Tooro Uganda
Mwanahabari Kijanangoma anapanda kwenye kiti cha ufalme wa Tooro huku mzozo wa kumrithi marehemu Mfalme Oyo ukiendelea.
Ajali 6 mbaya zaidi za majini zilizotikisa dunia
Kuzama kwa Le Joola nchini Senegal mwaka 2002 kulisababisha vifo vya watu 1,800. Hata hivyo, duniani kumewahi kutokea majanga mengine ya majini yaliyosababisha vifo vya maelfu na kuacha alama kubwa katika historia.
Hukumu ya kesi ya Lissu kutolewa tarehe sita Novemba
Mahakama imesema itahitaji muda wa kutosha ili iweze kutoa maamuzi sababu hili ni shauri la namna yake.
Harvard yafichua siri rahisi ya kuishi maisha marefu
Utafiti mkubwa wa Harvard unaonyesha kwamba, kuwa na mahusiano mazuri na watu kunaweza kusaidia kuongeza miaka ya kuishi ukiwa na afya njema. Badala ya kuwa na watu wengi, mahusiano machache lakini yenye kina, pamoja na kushiriki shughuli za kijamii, yanaweza kuwa na mchango mkubwa katika afya ya mwili na akili.
Mabilionea duniani wanavyopambana kuishi milele
Matajiri wakubwa wanaendelea kutumia mamilioni ya dola kutafuta njia ya kuishi milele kwa nini basi mafanikio halisi ya kisayansi hayapati ufadhili?
Kwa nini mtu tajiri zaidi Afrika anataka kuuza sehemu ya himaya yake?
Mfanyabiashara bilionea Aliko Dangote ameanzisha mauzo makubwa zaidi ya awali ya hisa kuwahi kufanyika barani Afrika, baada ya kampuni yake ya kusafisha mafuta kuorodheshwa katika Soko la Hisa la Nigeria.
Kwa nini mahasimu wa zamani Ethiopia sasa wameungana?
“Jambo hili limeathiri vibaya kisaikolojia mji wetu, na watu wetu wako katika hali ya hofu,” amesema Meya wa mji huo, Mogos Shiferaw.
Akili mnemba na nyakati za mwisho: Kwa nini baadhi ya watu wanaamini teknolojia hii ni Mpinga Kristo?
Baadhi ya Wakristo wanaamini akili mnemba inaweza kuhusishwa na matukio ya nyakati za mwisho. Huu hapa ni ufafanuzi zaidi kuhusu kwa nini teknolojia hiyo inahusishwa na Mpinga Kristo.
Mama Fatma Karume: Mwanamke aliyeipika Zanzibar jikoni na kibarazani
Mama Fatma Karume, mjane wa Rais wa kwanza wa Zanzibar, Sheikh Abeid Amani Karume, amefariki dunia Jumatatu, Septemba 21, 2026, akiwa na umri wa miaka 97.
Je, TikTok na Reels zinaharibu umakini na kumbukumbu za vijana?
Utafiti unaonyesha kuna uhusiano kati ya matumizi makubwa ya video fupi na matatizo ya umakini, kumbukumbu na kujidhibiti miongoni mwa vijana, ingawa bado hakuna ushahidi wa moja kwa moja kwamba video hizo husababisha uharibifu wa kumbukumbu.
Jinsi Mecca na maeneo mengine matakatifu yanavyolindwa
Mfumo wa Patriot ulipelekwa katika miji hiyo kwa ajili ya kulinda maeneo matakatifu kama Makka na Madina.
BBC News Swahili sasa ipo WhatsApp
Dira ya Dunia TV
Kipindi cha habari motomoto, kinachowaweka watazamaji karibu zaidi na yanayojiri duniani























































