Hukumu ya kesi ya Lissu kutolewa tarehe sita Novemba

Mahakama imesema itahitaji muda wa kutosha ili iweze kutoa maamuzi sababu hili ni shauri la namna yake.

Muhtasari

Moja kwa moja

Na Waandishi wa BBC Swahili

  1. Hakuna aliyewajibishwa mauaji ya wakati wa machafuko ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025 - Heche

    .

    Lissu: Waeleze majaji uwepo wa jambo lingine mlilozungumzia katika hiyo mikutano ya CCM, CHADEMA na serikali.

    Heche: Tulizungumzia pia vitendo vya utekaji nyara ubambikaji wa kesi kwa watu kurekebisha mfumo wote wa haki jinai na kurejesha demokrasia

    Lissu: Waeleze majaji kuhusu ratiba ya mazungumzo hayo mliyokuwa mnazungumzia

    Heche: Katika mapendekezo yetu yalikuwa na mchoro mzima wa namna kila kimoja kingefikiwa baaada ya nyingine na mazungumzo yalichukuwa takribani mwaka mzima

    Lissu: Mazungumzo hayo yaliishaje

    Heche: Wakati wote tulipokuwa tunazungumza tulipeleka mapendekezo yetu hayo kwa maandishi wajumbe wa CCM walikuwa wanatusikiliza wanayabeba wanasema wanakwenda kufanya mashauriano na rais aliyeteua hiyo timu. Kuna wakati wenyeviti mheshimiwa mbowe na mheshimiwa Kinana walikwenda kumuona rais kwa pamoja juu ya mazungumzo na mapendekezo yetu hata kufanya press confrence ya pamoja juu ya yale ambayo tulikuwa tumeafikiana

    Mazungumzo yaliisha pale tulipodai fupewe maandishi toka upande wa CCM juu ya tulivhoazimia tangu tuanze vikao

    Majibu waliyotuletea yalikataa mapemdekezo yetu yote na huo ndio ukawa mwisho wa viyao

    Lissu: Hayo mapendekezo waliyaleta lini

    Heche: Siwezi kukumbuka tarehe hii ilikuwa mwaka 2023 baada ya hapo sisi tuliendelea na siasa zetu kwenda kwa wananchi na mazungumzo yetu yakaishia pale

    Lissu: Nataka tuzungumze ya tarehe 29 october 2025 siku ya tarehe 29 october siku ya uchaguzi wewe ulikuwa wapi na waeleze majaji kama ulishiriki kwenye kupiga kura

    Heche: Siku hiyo nilikuwa mahabusu kwenye kituo cha polisi mtumba Dodoma ambapo nilikamatwa tangu tarehe 22/10/2025

    Lissu: Unafahamu nini kilitokea siku ya uchaguzi tarehe 29/10 na siku zilizofuata

    Heche: Nilipata habari watu wameuawa kwa wingi baada ya kutoka rumande watu zaidi ya 518 kwa mujibu wa ripoti ya Chande ambayo ilisema wanaweza kuongezeka zaidi. Mzee Warioba alisema ni zaidi ya waliouawa vita ya Kagera

    Katuga: Hili jIbu la mwisho la shahidi ni pure hearsay (taarifa zisizo rasmi) waheshimiwa ikiingia kwenye rekodi sidhani kama itakuwa sawa huu ni ushahidi wake.

    Lissu: Kuna mambo yanazungumzwa hapa hilo sio pingamizi ushahidi huu unahitaji kuthibitishwa na ushahidi mwingine kuna mashahidi watatu bado wanakuja lakini bado ana nafasi ya kucross examine (kumhoji kwa kina).

    Heche: Waheshimiwa majaji hakuna serikali imeua watu wengi kwa nchi yetu kiasi kile tangu watu waliuawa wakati wa vita ya maji mjaji

    Kwa taarifa ya jaji chande Dar zaidi ya watu 130, Mwanza 90 Arusha Mbeya Nako hakuna serikali imewahi kuua watu wengi kiasi hicho

    Lissu: Waeleze majaji kutokana na hayo mauaji makubwa unayosema waleeze kuhusu ufahamu wa muhusika yoyote kuwajibika kwa namna yoyote

    Heche: Sina taarifa ya mtu yeyote kuwajibika kutoka chombo chochote kutokana na vitendo vya kutisha na mauaji siku ya uchaguzi

    Lissu: Waeleze majaji kama kuna kiongozi yeyote wa serikali amewajibika kwa mauaji hayo

    Heche: Hakuna mtu yeyote amewajibika kutokana na mauaji hayo

    Lissu: Ulisema awali ulisikiliza hotuba ya Jaji chande yote ilitaja kiongozi yeyote aliyetoa amri ya kua watu wengi kiasi hiki

    Heche: Hakuna sehemu hotuba imetaja kiongozi aliyetoa amri ya kutekeleza mauaji haya

    Lissu: Je, kuna mtu yeyote amechukuliwa hatua

    Heche: Kwa ufahamu wangu sifahamu mtu hata mmoja

    Lissu: Walio uawa ni binadamu au ni wadudu waeleze majaji uhalali wa serikali kuua rai wake kwa wingi kiasi hicho

    Heche: Hakuna uhalali wowote tena kwa namba kubwa kiasi hicho

    Lissu: Hoja yetu ya kuahirishwa uchaguzi kama ingesikilizwa na kutekelezwa maafa makubwa kiasi hiki yasingetokea

    Lissu: Hoja yetu ya kutaka mabadiliko ya kufanyika kwa mabadiliko ya Katiba na Tume kuwa huru ingekuwaje.

    Heche: Naamini kama hoja yetu ingekubaliwa maafa yale yasingetokea.

    Lissu:Sasa Shahidi ulisema umesikiliza hotuba ya Jaji Mkuu Chande alisema kisababishi cha kwanza cha hayo mauaji kilikua nini

    Heche: Alisema madai ya muda mrefu ya Watanzania kutaka Katiba Mpya, Tume Huru ya Uchaguzi, Rushwa na Ufisadi, ukosefu wa ajira kwa vijana, watu kutekwa nyara na kupotezwa

    Lissu:Shahidi Waeleze Waheshimiwa majaji jaji mkuu chande alisema nini juu ya utekaji nyara na upotezaji watu kwa kumbukumbu zako

    Heche: Alisema watu wanatekwa nyara kwa sababu za kimapenzi, ushirikina na kibiashara

    Lissu: Shahidi kwenye ushahidi wako ulitaja utekaji mwingi wa wanasiasa umetaja wa CCM

    Heche: Hakusema kokote kwamba kuna viongozi wametekwa kwa sababu za kisiasa

    Unaweza kusoma;

  2. Lissu ahoji Ripoti ya Jaji Chande mahakamani

    Tundu Lissu

    NB: Lissu: Sasa shahidi Mimi nilikuwa garezani wakati haya yanatokea, nikishtakiwa kwa kosa la uhaini, sasa waeleze majaji kuhusu wewe na viongozi wenzako wa Chama kuitwa kwenda kutoa ushahidi mbele ya Tume ya Jaji Othman Chande.

    Shahidi: Mimi binafsi Sijawahi kuitwa na Sina ufahamu wowote wa viongozi wenzangu wa Chandema kama waliwahi kuitwa kwenda kutoa ushahidi katika tume ya Jaji Othman Chande

    NB:Lissu: Kwa ufahamu wako na haya uliyoyatolea ushahidi hapa mahakamani, Tume ya Jaji Othman Chande ilichunguza nini? wakati nyie hamkuitwa?

    Shahidi: Mimi sipo kwenye nafasi nzuri ya kueleza haya waliyochunguza

    Lissu: Kuna ushahidi Umetolewa mahakamani kwamba nilikuwa na Jitihada za chama kujadiliana na CCM pamoja na Serikali juu ya madai ya mabadiliko ya Katiba na Mfumo wa uchaguzi kabla ya Kauli mbiu ya No reforms no Elctionwaeleze majaji ufahamu wako Juu hili

    Shahidi: Nafahamu kuhusu hilo Suala kwa sababu mimi binafsi nimeshiriki nilikuwa kwenye timu ya chadema iliyokutana na Rais Samia Suluhu Hassan aliyekuwepo mwaka 2022 hadi mwaka 2025 Ikulu ya Chamwino Dodoma kuzungumza naye na ikakubaliwa kuunda timu ya watu watano watano.

    Shahidi: Mwaka 2021 tukwenda Mwanza kufanya kongamano kubwa la kudai Katiba Mpya na Sheria ya Uchaguzi ili kuwezesha Mabadiliko na siku hiyo Mbowe alikamatwa na mimi nilikamatwa na Mbowe alifunguliwa kesi ya ugaidi na babadae alifutiwa kesi

    Shahidi: Tulienda kwenye kikao Ikulu na baadae tukienda Chamwino.Dodoma kukutana na Rais, ambapo katika kikao hicho alikuwepo Mbowe, Said Issa alikuwa Makamu Mwenyekiti Chadema Zanzibari, Katibu Mkuu John Mnyika, na mimi mwenyewe, John Heche.

    Shahidi: Kwa upande wa Serikali alikuwepo Rais Samia Suluhu Hassan, Mwanasheria Mkuu wa Serikali( AG) Elieza Felishi, Waziri George Simbachawene , marehemu Jenister Muhagama na mawaziri wengine ambao siwakumbuki.

    Shahidi: Kwa upande wa Chama cha CCM, alikwemo Makamu Mwenyekiti kwa wakati huo Abdullahman Kinana na viongozi wengine.katika.kikao hicho Mbowe alieleza namna chama kilivyoonewa matatizo wakati wa Uchaguzi,

    Shahidi: Katika kikao hicho walikubaliana kuunda timu ya watu watano kwa upande wa Serikali na vyaama ambapo walienda kupitia kwa kinay matatizo ya Uchaguzi na malalamiko.ya Uchaguzi ili yafanyiwe kazi kabla ya Uchaguzi wa mwaka 2025

    Shahidi: Kwa upande wa Chande ailiundwa timu iliongozwa na Mwenyekiti kwa kipindi hicho, Freeman Mbowe, Katibu Mkuu John Mnyika, wakili wa Mahakama Kuu, Jeremiah Mtobesya, mjumbe wa Kamati Mkuu ya Chama kutoka Zanzibar, Zeyudi Mmbamba na mimi mwenyewe John Heche, pia kulikuwa Kuna timu kutoka Sekretarieti mdogo Reginald Munisi,

    Shahidi: Kwa upande wa CCM, timu ilikuwa na watu watano ambao ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Abdullahman Kinana, Endrew Chenge na wawakilishi wawili kutoka Zanzibar ambao siwakumbuki majina yao pamoja na Waziri Jenister Muhagama, ambaye kwa sasa ni marehemu

    Lissu: Waeleze majaji baada ya kuundwa timu hiyo kulitokea nini?

    Shahidi: Mazungumzo yalichukua mwaka mzima na sehemu, tuliandika na kupeleka mapendelezo yetu yanamna ya kukwamua mchakato wa katiba, mapendelezo ya sheria ya Uchaguzi, vyombo viliyoundwa kuhakikisha vinaandika maoni na mapendekezo ya Katiba, mapendelezo ya namna ya kuunda Tume huru ya uchaguzi, pia tulizungumza kuhusu watu wetu kubambikiwa kesi na kufungwa kwa kesi za uongo. Tulizungumza kuhusu viongizi wetu kukimbia nchi kwa kuhofia usalama wao ikiwemo Tundu Lissu, Godbless Lema, Ezekie Wenje, tulizungumza madai ya kuwaondoa wabunge 19 wanawaken maarufu kama Covid, ambao walienda bungeni kinyume na utaratibu wa Chama. Walizungumzia kuhusiana na kufungwa mikutano ya hadhara iliyokuwa imezuiliwa na Rais John Magufuli.

    Unaweza kusoma;

  3. Lissu hajatajwa popote katika ripoti ya Jaji Chande - Shahidi

    John Heche

    Lissu: Waeleze majaji kwa ufahamu wako iwepo Kuvuruga Uchaguzi kwenye sheria ya Kanuni ya Adhabu

    Shahidi: Sina ufahamu huo kuhusu kuvuruga Uchaguzi kama ni kosa kwenye Sheria ya Kanuni ya Adhabu.

    Lissu: Waeleze majaji kwa ufahamu wako iwepo kuzuia Uchaguzi kwenye sheria ya Kanuni ya Adhabu

    Shahidi: Sina ufahamu huo kuhusu kosa la kuzuia Uchaguzi katika Sheria ya Kanuni ya Adhabu.

    Lissu: Waeleze majaji kwa ufahamu wako iwepo kukinukisha ni kosa kwenye sheria ya Kanuni ya Adhabu

    Shahidi: Sina ufahamu huo kuhusu kukinukisha kama ni kosa kwenye Sheria yaKanuni ya Adhabu.

    Lissu: Waeleze majaji kwa ufahamu wako uwepo wa kosa la kuzuia Uchaguzi, kuvuruga Uchaguzi iwapo ni kosa kwenye Sheria ya Uchaguzi wa rais, wabunge na madiwani ya mwaka 2024

    Shahidi: Sio kosa kwenye Sheria ya Uchaguzi

    Lissu: Waeleze majaji kwa ufahamu wako uwepo wa kosa la kukinukisha iwapo ni kosa kwenye Sheria ya Uchaguzi wa rais, wabunge na madiwani ya mwaka 2024

    Shahidi: Sio kosa kwenye Sheria ya Uchaguzi ya mwaka 2024

    Lissu: Shahidi Waambie majaji iwapo mwa kosa la Nilitengeneza nia kwenye Sheria ya Kanuni ya Adhabu

    Shahidi: Kwa ufahamu wangu hakuna kosa kwenye Sheria hiyo

    Lissu: Shahidi Waambie majaji kwa ufahamu wako, iwapo nj kosa kutengeneza nia kwenye Sheria ya Uchaguzi.

    Shahidi: Kwa ufahamu wangu hakuna kosa kwenye Sheria hiyo.

    Lissu: Waleeleze majaji kuhusu uwepo wa neno Makamu wa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania niliyataja katika mkutano wangu

    Shahidi: Hakuna sehemu yoyote ambayo Lissu alitaka neno Makamu wa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwenye hotuba yake

    Lissu: Waeleze majaji kuhusu uwepo wa neno Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania niliyataja katika mkutano wangu

    Shahidi: Hakuna sehemu yoyote ambayo Lissu alitaka neno Wazri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwenye hotuba yake

    Lissu: Waeleze majaji kuhusu uwepo wa maneno Baraza la Waziri, manaibu mawaziri, wakuu wa mikoa, wilaya niliyataja katika mkutano wangu

    Shahidi: Hakuna sehemu yoyote ambayo Lissu alitaka maneno hayo , kwenye hotuba yake

    Lissu: Waeleze majaji kuhusu uwepo wa maneno Mwanasheria Mkuu wa Serikali, au Mkurugenzi wa Mashtaka niliyemtaja katika mkutano wangu wa Aprili 3, 2025

    Shahidi: Hakuna sehemu yoyote ambayo Lissu aliwataja Mkurugenzi wa Mashtaka nchini au Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwenye hotuba yake

    Lissu: Shahidi Waeleze majaji kwa kuwa ulikuwepo katika huo mkutano uwepo wa neno Halmashauri ya Jiji , Manispaa,Wilaya, Kijiji wala kitongoji niliyotaja katika hotuba yangu

    Shahidi : Waheshimiwa majaji hakuna sehemu yoyote ambayo Lissu alitaka taasisi hiyo

    Lissu: Kwa ufahamu wako shahisi, waleeze majaji uwepo wa maneno Wakurugenzi wa Jiji, Manispaa, Wilaya, Halmashauri, wala Watendaji wa Mitaa na Vijiji ambao niliwataja katika mkutano wangu wa Aprili 3, 2025

    Shahidi: Hakuna sehemu uliyowataja watendaji hao

    Lissu: wa kumbukumbu zako uwepo wa Jeshi la Polisi Jeshi wa Wananchi, Jeshi la Magereza, Jeshi la Akiba ambao niliwataja katika mkutano wangu

    Shahidi : Hakuna sehemu uliyowataja

    Lissu: Sasa shahidi hao wote niliyokutajia kuanzia raisi, Wakurugenzi vyombo vya usalama, wote ndio Serikali, Sasa swali langu ni hayo maneno niliyoyataja kwenye hati ya mashtaka ambayo ni uaisi, tutakinukisha, tutavuruga Uchaguzi yanamtishia nani?

    Shahidi: Hayamtishi mtu yoyote kati ya hawa.ulisowataja, maana ni maneno ya kawaida.

    Lissu:Shahidi, haya maneno yaliyopo katikahati ya mashtaka niliyokusomea hapa mahakamani yana kosa gani?

    Shahidi: Hayana kosa lolote

    Lissu: Waeleze majaji iwapo kuna maneno katika hotuba yangu kuwa tutachoma moto vituo vya kupigia kura, tutachoma moto vituo vya mwendokasi, magari ya watu binafsi, Magari ya Serikali na ofisi za CCM, iwapo nilisema katika mkutano wangu

    Shahidi : Hakuna sehemu uliyoisema maneno hayo

    Lissu: Waeleze majaji uwapo wa maneno katika hotuba yangu ya tutakata vidole watu watakao kwenda kupiga kura

    Shahidi: Hakuna sehemu ambayo Lissu ameseha hayo

    Lissu: Waeleze majaji uwapo wa maneno katika hotuba yangu kauwe Polisi au watumishi wa Tume au watu wengine wowote.

    Shahidi: Hakuna sehemu ambayo Lissu amesema hayo

    Lissu: Kwa kuwa hotuba ya Jaji Othman Chande uliyosikiliza, waeleze majaji uwepo wa maneno ya vurugu za Uchaguzi mwaka 2025 , zilisabaabishwa na Mwenyezwa Chadema Tundu Lissu

    Shahidi: Hakuna sehemu yote iliyoelezwa katika hotuba ya hiyo kuwa Lissu alisabanisha vurugu

    Lissu: Kwa kuwa hotuba ya Jaji Othman Chande uliyosikilia, waeleze majaji uwepo wa maneno yoyote alitaja jina Tundu Lissu amechochea vurugu za Uchaguzi mwaka 2025,

    Shahidi: Hakuna sehemu yote alipotajwa Lissu Katika ripoti ya Jaji Chande

    Lissu: Kwa kuwa hotuba ya Jaji Othman Chande uliyosikilia, waeleze majaji uwepo wa maneno yoyote alitaja ya chama chochote kuchochea vurugu za Uchaguzi mwaka 2025,

    Shahidi: Hakuna sehemu yote iliyotaja Chama cha siasa kuchochea vurugu za Uchaguzi Katika ripoti ya Jaji Chande

    Lissu: Kwa kuwa hotuba ya Jaji Othman Chande uliyosikilia, waeleze majaji uwepo wa maneno kukatwa vidole katuka vurugu za Uchaguzi mwaka 2025, kwenye ripoti ya Jaji Chande

    Shahidi: Hakuna sehemu yote alipotajwa watu kukatwa vidole kwenye Katika ripoti ya Jaji Chande

    Lissu: Kwa kuwa hotuba ya Jaji Othman Chande uliyosikilia, waeleze majaji uwepo wa sehemu inayoonyesha majina ya askari Polisi waliyouawa katika vurugu za Uchaguzi mwaka 2025,

    Shahidi: Hakuna sehemu iliyoonyesha majina ya askari polisi waliyouawa katika ripoti ya Jaji Chande

    Lissu: Kwa kuwa hotuba ya Jaji Othman Chande uliyosikilia, waeleze majaji uwepo wa majina ya watu waliouwa na majina ya watu waliyowaua vurugu za Uchaguzi mwaka 2025,

    Shahidi: Hakuna sehemu yote alipitajwa majina ya watu waliouwa na watu waliyowaua Katika ripoti ya Jaji Chande wakati wa Uchaguzi

    Lissu: Kwa kuwa hotuba ya Jaji Othman Chande uliyosikiliza, waeleze majaji uwepo wa maeneo yaliyotajwa kuharibu miundo mbinu ya CCM, orodha ya magari ya serikali na watu binafsi aina na namba zake yanayodaiwa kuchomwa moto katika vurugu za uchaguzi mwaka 2025,

    Shahidi: Hakuna orodha wala aina ya magari yanayodaiwa kuchomwa moto katika ripoti ya Jaji Chande.

  4. Lissu kwa shahidi: Kuna kosa la kuvuruga Uchaguzi katika Katiba ya Tanzania?

    Tundu Lissu

    Lissu: Walielekeza mamaji tofauti yoyote kati ya hotuba yangu katika mikutano ya hadhara na kikao cha wadau

    Shahidi: Hotuba ya Aprili 3, 2025 na hotuba aliyokutana na wadau mikoa ya Mbeya, Iringa, ni hotuba Ile Ile ambayo alikuwa anarudia masuala ya ubovu inatokana na Uchaguzi, matatizo ya Uchaguzi, mapendelezo na kusogeza mbele uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

    Lissu: Hapa Mahakamani umeletwa ushahidi kuwa mkutano huo ulirushwa live( mubashara) na kuhifadhiwa katika mitandao ya kijamii, Waeleze majaji ufahamu wako juu ya hilo

    Shahidi: Mimi binafsi nilikuwa katika mkutano ndani hivyo sijui kama mkutano huo ulirushwa live( Mubasha) au haukurushwa live

    Lissu: Waleeleze majaji kwa ufahamu wako kama Uliweza kuona hiyo hotuba ikiwa imehifadhiwa katika mitandao mbalimbali ikiwemo Jambo TV

    Shahidi: Nina ufahamu kuwa nimeiona hotuba hiyo kwenye Youtube katika mitandano mbalimbali ikiwemo The Chanzo, Mwanzo na Jambo TV

    Lissu: Waeleze hicho ulichokiona katika mitandao hiyo inaurefu wa muda gani

    Shahidi: Zinatofautiana muda,The Chanzo ni dakika 45, Mwanzo ni dakika 60 yaani saa moja na jambo Tv ni masaa mawili, kwa hiyo zinatifautiana muda

    Lissu: Walezi majaji katika YouTube channel hizo tatu kama kuna maneno ambayo yapo katika hati ya mashtaka

    Shahidi: Ndio ni miongoni mwa maneno ambayo yapo katika channel hizo

    Lissu: Waeleze majaji na maneno mengine niliyozungumza kuhusu Uchaguzi iwapo yapo katika channel hizo.

    Shahidi: Maneno hayo yapo kuhusu kuepusha maafa katika uchaguzi kuhusu kubadili Sheria za Uchaguzi, kuhusu kuengua wagombea, kuhusu kusogeza mbele uchaguzi ,

    Shtaka nililoshtakiwa nalo linasema mimi ndio niliyorusha hayo maneno katika mitandao ya Youtube Channel ya Jambo TV na nyingine, wewe unasemaje?

    Shahidi: Lissu hajarusha hayo maneno katika mitandao hiyo

    Lissu: Shahidi Waleeleze majaji kwa vile ulikuwepo pale kwenye mkutano juu ya mimi kufanya chochote zaidi ya kuzungumza

    Shahidi: Lissu hakufanya jambo lingine lolote zaidi ya kutoa hotuba, hakugusa kamera

    Lissu: Sasa shahidi tuzungumze kitu kimoja kwenye hati ya mashtaka, Waeleze majaji kwa ufahamu wako iwapo wa kosa la uasi katika Katiba hii

    Shahidi: Sina ufahamu wowote uwepo wa uais katika Katiba

    Lissu: Waelelze majaji, Kwa ufahamu wako uwepo wa kosa la kuhamasisha uasi katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

    Shahidi: Kwa ufahamu wangu hakuna kosa la kuhamasisha uasi katika Katiba ya nchi hii

    Lissu: Waeleze majaji kwa ufahamu wako uwepo wa kosa la kuvuruga Uchaguzi katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

    Shahidi: Hakuna kosa la kuvuruga Uchaguzi Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

    Lissu: Waeleze majaji kwa ufahamu wako uwepo wa kosa la kuvuruga Uchaguzi katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

    Kosa la kuzuia uchaguzi katika Katiba ya nchi hii ya mwaka 1977

    Lissu: Waeleze majaji iUwepo wa kosa la kuhamaisha watu kuzuia uchaguzi katika Katiba hii

    Shahidi: Kwa ufahamu wangu hakuna kosa kimahama watu kuzuia uchaguzi katika Katiba hii

    Lissu: Waeleze majaji kwa ufahamuw Ako ,uwepo wa kosa la kukinukisha katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano

    Shahidi: Kwa ufahamu wangu hakuna kosa la kukinukisha katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

    Lissu: Iwapo wa kosa la kuzuia watu kwenda kupiga kura katika Katiba hii

    Shahidi: Kwa ufahamu wangu Sijawahi kuona na sio kosa watu kwenda kupiga kura katika Katiba

    Lissu: Waeleze majaji kwa ufahamu wako, uwepo wa kosa la uasi kwenye Sheria ya Kanuni ya Adhabu

    Shahidi: Sina ufahamu huo wa kosa la uasi katika Sheria ya Kanuni ya Adhabu

    Lissu: Waeleze majaji uwepo wa kosa la kuhamaisha uasi Katika Sheria ya Kanuni ya Adhabu

    Shahidi: Sina ufahamu huo hilo kosa la kuhamaisha uasi Katika Sheria hizo

  5. Hakuna kosa la kukinukisha kwenye Katiba - Heche

    Lissu: Waeleze majaji iwapo unafahamu juu ya kosa la uasi kwenye katiba hii

    Heche: Sifahamu

    Lissu: Waeleze kuhusu kosa la kuhamasisha uasi

    Heche: Sina ufahamu juu ya kosa la kuhasisha uasi kwenye Katiba

    Lissu: Waleeze majaji juu kosa linaitwa kuvuruga uchaguzi kwenye katiba hiii?

    Heche: Hakuna la kuvuruga uchaguzi kwenye Katiba hii

    Lissu: Waeleze majaji kuhusu kosa la kuzuia uchaguzi kwenye katiba hii

    Heche: Hapana sifahamu

    Lissu: Waeleze majaji iwapo unafahamu uwepo wa kosa la kuhamasisha watu kuzuia uchaguzi

    Heche: Sina ufahamu juu ya kosa hilo ndani ya katiba

    Lissu: Nikisema Katiba namaanisha katiba ya mwaka 1977 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Waeleze Waheshimiwa majaji iwapo ni kosa kuvuruga uchaguzi kwenye Katiba

    Heche: Waheshimiwa majaji hakuna kosa ka kuvuruga uchaguzi kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

    Lissu: Na Waeleze Waheshimiwa majaji kuhusu uwepo wa kosa la kuzuia uchaguzi kwenye Katiba

    Heche: Hakuna kosa la kuzuia uchaguzi kwenye Katiba ya 1977

    Lissu:Na waeleze waheshimiwa majaji uwepo wa kosa la kuhamasisha watu kuzuia uchaguzi kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

    Heche: Kwa ufahamu wangu hakuna kosa la kuzuia uchaguzi kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

    Lissu: Waeleze Waheshimiwa majaji uwapo wa kosa tutakinukisha kwenye Katiba

    Heche: Kwa ufahamu wangu hakuna kosa la kukinukisha kwenye Katiba

    Lissu: Kwa ufahamu wako uwapo wa kosa linaloitwa kuzuia watu kwenda kupiga kura kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

    Heche: Kwa ufahamu wangu sijawahi kuona kuzuia watu kupiga kura

    Lissu: Uwapo wa kosa la kuhamasisha uasi kwenye sheria ya Penal Code

    Heche: Sina ufahamu huo kweny sheria hiyo kuhusiana na kuhamasisha Uasi

    Lissu: Na Waeleze Waheshimiwa majaji ufahamu wako kuhusu uwapo wa kosa la kuvuruga uchaguzi kwenye sheria ya Kanuni ya adhabu

    Heche: Waheshimiwa majaji sina ufahamu wako uwepo wa kosa kwenye sheria hiyo kuhusiana na kuvuruga

    Lissu: Waeleze Waheshimiwa majaji uwapo wa kosa kukinukisha kwenye sheria ya kanuni ya adhabu

    Heche: Waheshimiwa sina ufahamu wa uwepo wa kosa kukinukisha kwenye sheria ya kanuni ya adhabu

    Lissu: Waeleze Waheshimiwa majaji kwa ufahamu wako kuhusu uwepo wa kosa linaloitwa kukinukisha kwenye sheria ya uchaguzi wa Wabunge, Rais na Madiwani ya 2024

    Heche: Waheshimiwa Majaji kwa ufahamu wangu hakuna kosa la kukinukisha, kwenye sheria za uchaguzi wa Udiwani, Rais na Ubunge ya mwaka 2024

  6. Lissu sio mtumishi wa Jambo TV, aliyerusha matangazoshahidi namba 17 - Heche

    Lissu: Waleze majaji huo mkutano ulifunguliwa na nani

    Heche: Ulifunguliwa na uongozi wa sekretarieti ambao ni Katibu mkuu

    Lissu: Baada ya Katibu mkuu kufungua aliwakaribusha kina nani

    Heche: Alinikaribusha mimi nikaongea kwa muda kidogo baadae Mimi nilimkaribusha Mwenyekiti wangu

    Lissu: UnavyoKumbuka kUanzia ufunguzi hadi mwisho ulichukua muda gani jumla Heche: Inaweza kuwa saa nne sababu kulikuwa na mambo mengi maombi nini

    Lissu: Ninashitakiwa kwa maneno ya kihaini wanasema kitu kimoja sahihi hapa wanasema mkutano huu unaashiria uasi……. sababu tunaenda kukinukisha vibaya sana hayo maneno niliyosoma yamechukua muda gani

    Heche: Hayajamaliza hata dakika moja

    Lissu: Kwemye hotuba yangu nilizungumza hayo tu

    Heche: Hapana waheshimiwa majaji alizungumza mambo mengi akifafanua na kutoa elimu kwa kina

    Lissu: Hayo mazungumzo marefu niliyofanya yalikuwa ya jambo gani

    Heche: Yalihusu mfumo wetu wa uchaguzi ulivyo haribika na hauwezeshi hauko huru na hauwezeshi wananchi kupata viongozi wanaowataka. Namna ambavyo ni vigumu kwa mgombea wa upinzani kufanikiwa hasa CHADEMA kushinda uchaguzi hata kama anakubalika, namna mfumo huu unavyosababusha maaafa na kuruhusu upendeleo wa wazi.

    Namna ambavyo vyombo vya dola vinatumika kuharibu uchaguzi.Kwa ujumla alieleza namna ambavyo huu mfumo sio huru na hautendi haki na unavyopaswa kubadilishwa kabla ya uchaguzi mwingine kuendelea.

    Lissu: Kwenye hayo uliyosema kwemye namna unavyopaswa kubadilishwa

    Heche: Alizungumza kuhusu mabadiliko ya kikatiba na kisheria yanaso simamia kanunu zetu, mabadiliko ya namna ya kupata wawakilishi hasa wabunge na mgawanyo wa majimbo

    Lissu: Nilisema nini juu ya jinsi ya kuondoa hayo maafa wakati wa uchaguzi

    Heche: Alisema ni kutengeneza mfuno huru kwa watu wote utakao tenda haki kwa wote

    Lissu: Tulisema nini juu ya mabadiliko yanayotakiwa

    Heche: Alisema kwamba mabadiliko yanayotakiwa kwenye tume nikutengeneza muundo mpya wa tume ambao haumpi mamlaka mwenyekiti wa CCM kuunda tume na unaotoa uhuru kwa wote kuanzia ngazi ya kitaifa mpaka kwenye kata tume iwe na wawakilishi wake isiwe inaazima watumishi wa serikali ambao wote wanachukua maelekezo toka kwa muajiri wao na hiyo tume ndio iwe na mamlaka ya kugawa majimbo kulingana na vigezo vinavyofaa na sio upendeleo.

    Lissu: Kwenye hotuba yangu pia nilizungumzia mikutano yetu ambayo tulikuwa tumeshafanya

    Heche: Alieleza namna mikutano yetu inavyorugwa na polisi, tume yenyewe mfano yeye mwenyewe alivyosimamishwa kufanya kampeni wakati wa uchaguzi mkuu 2020 na sio yeyetu na wagombea wengine pia.

    Lissu: Nilisema nini kuhusu wagombea wa upinzani kuenguliwa hasa CHADEMA.

    Heche: Waheshimiwa majaji alieleza kwa kirefu namna ambavyo wagombea wa upinzani wanavyoibiwa kwa sababu ambazo sio za kisheria wala kikatiba akaeleza kwamba kwenye uchaguzi wa mwaka 2020 ilivunja rekodi ya wagombea wengi kuenguliwa hivyo CCM kupita bila kupingwa, alitolea mfano namna wagombea kama Suzan Kiwanga alivyoenguliwa na akawa anatoa mfano kwenye chaguzi za serikali za mtaa ulivunja rekodi zote za engua engua hata kama tungekwenda kushiriki isingekuwa na maana sisi kushiriki sababu tumeshaenguliwa.

    Lissu: Nilisema nini kuhusu mawakala wa vyama na wagombea

    Heche: Kuhusu mawakala na wagombea alieleza kwamba wakala anapaswa kuwa muwakilishi wa mgombea na chama chake lakini sasa taratibu zimewekwa ngungu kwa namna ya mawakala kuingia kwenye vituo kuanzia namna ya kuwaapisha na kuingia kwenye vituo hivyo uwakilishi wao unakuwa ni wa shida na hivyo chama CHADEMA kinakosa wawakilishi kwenye vituo.

    Lissu: Waeleze waheshimiwa majaji nilisema nini kuhusu yanayotokea siku ya uchaguzi

    Heche; Alieza kuhusu usUmbufu unaokuwepo siku ya uchaguzi namna ya wapiga kura kupata majina yao, mara jina halionekani, kura zinaingizwa kwenye vituo namna wagombea na mawakala wananyimwa fomu kwenye vituo, namna ambavyo majumuisho yanafanyika na kura kutangazwa ambazo sio halali.

    Lissu: Waeleze majaji nilivyosema juu ya kupinga mambo yote haya Mahakamani

    Heche: Alieleza ni ngumu kupinga mambo yote haya Mahakamani na akaeleza attempts ambazo zimefanywa na watu mbali mbali kwa kutumia njia za Mahakama, alieleza namna ambavyo namna wagombea wananyimwa fomu za malalamiko fomu za matokeo, vitu ambavyo ungeweza kuvitumia Mahakamani kama ushahidi.

    Akaeleza pia gharama kubwa ambazo zinatakiwa kulipwa na wagombea katika kufungua mashauri ambazo wanakuwa hawaziwezi akaeleza wingi wa kesi mfano alitoa mfano wa vijiji 17,000 tungefungua kesi kwenye Mahakama zipi

    Na akamalizia kwa kusema kwamba matatizo haya ya kisiasa yanaweza kumalizika kisiasa na sio lazima yaende Mahakamani akitumia mfano wa kesi ile ya Mtikila. Alisema pia Mahakama kupitia kesi ya Walid Kaburu ilisema uchaguzi usio huru na wa haki sio uchaguzi.

    Lissu: Sasa shahidi waleze majaji nilisema nini juu ya hoja ya kuahirisha uchaguzi mwaka jana

    Heche: Alisema kwamba sisi kama chama tulikuwa tayari uchaguzi uahirishwe usogezwe mbele yafanyike kwanza mabadiliko ya kikatiba na kisheria yatakayoruhusu uchaguzi huru na wa haki yatakayo epusha madhila yanayotokea wakati wa uchaguzi ikiwemo watu kujeruhiwa, kuuawa kutekwa na mengineyo. Kwamba chaguzi hizi zilizopita kulikuwa na hayo madhila na uchaguzi ukisogezwa mbele tutapata viongozi tunaowataka.

    Lissu: Waeleze majaji tofauti ya hotuba yangu ya April 3 mwaka jana na mikutano yangu na wadau uliowataja na mikutano ya hadhara ulioitaja.

    Heche: Hotuba ileya tarehe tatu ilikuwa hotuba. Ile ila meneno huenda yalipishana ila ililenga kilekile kueleza ubovu wa mfumo wetu wa uchaguzi

    Lissu: Sasa shahidi ushahIdi umeletwa Mahakamani kwamba mkutano ule ulirushwa live kweNye televisheni na kuhifadhiwa kwenye mitandao ya kijamiii waeleze majaji juu ya ufahamu wako juu ya hilo.

    Heche: Sina hakika kama ulikuwa live au haukuwa live sababu mimi nilikuwa ndani kwenye mkutano ila waandishi wa habari najua walikuwepo.

    Lissu: Waambie majaji kuhusu kuhifadhiwa kwenye mitandao ya kijamii specifically Jambo Tv.

    Heche: Niloona kwenye mitandao mbali mbali ikiwembo Mwanzo, The Chanzo na hata Jambo TV nilifuatilia pia.

    Lissu: Waeleze majaji sasa hicho ulichokiona katika hiyo mitandao kina urefu wa muda gani.

    Heche: zinatofautiana tofautina, kwenye Jambo hotuba iko kama saa mbili hivi Chanzo kuna clip Dakika 45 na tano nyingine saa moja, kwa hiyo zinetofautiana tofautiana kwa namna walivyooona.

    Lissu: Katika video hizo ulizoona uwepo wa haya maneno ninayokusomea ….. (Lissu anasoma maneno ya kwemye hati ya mashitaka anayoshitakiwa nayo)

    Heche: Ni miongoni mwa maneno ambayo yapo

    Lissu: Waeleze majaji yale mengine uliyosema kwamba niliyazungumzia

    Heche: Nayo pia yapo kuhusu engua engua kuepusha maafa kwa hiyo ni hotuba ndefu

    Lissu: Shitaka nililoshitakiwa nalo linasema mimi ndio nimeweka hizo video kwenye mtandao wa Jambo Tv

    Heche: Sio kweli waheshimiwa majaji sababu Mwenyekiti Tundunlissu sio mtumishi wa Jambo TV na kuna shahidi wa kiboxi ndio alisema yeye amerusha hayo matangazo nafikiri ni shahidi namba 17

    Lissu: Waaleze majaji kama uliniona mim kugusa microphone au kamera za waandishi wa habari

    Heche: Hakuhusa chochote sababu sisi tulikuwa juu na waandishi walikuwa sehemu yao nyingine

    .
  7. Lissu hakuandaa mkutano uliomtia matatani - Heche

    Mahakama imeanza na wakili wa Serikali Nzengeli anasimama.

    Nzengeli: Naitwa Ajuae Nzengeli Nzengeli ikiwapendeza naomba tuendeleee na shahidi namba tano ushahidi wake wa in-chief

    Lissu: Naomba nikumbushwe tulipoishia jana

    Jaji: Tulikuabaliana leo amalize ushahidi wake in-chief

    Lissu: Atamaliza waheshimiwa Majaji

    Heche anatikisa kichwa kukubali huku Jaji akimkumbusha Lissu walipoishia jana

    Lissu: Shahidi habari ya asubuhi

    Heche: Salama Mwenyekiti

    Lissu: Sasa waeleze majaji kwemye simu aliyokupigia Amani Golugwa kuhusu kikao cha tarehe tatu Amani Golugwa alikuambia nini?

    Heche: Aliniambia kuna nia kukutana na watia nia

    Lissu: Alikuambia lengo la kukutana na watia nia ni ni

    Heche: Aliniambia lengo ni kuendelea kutoa elimu kwa watia nia juu ya no reforms no election

    Lissu: Alikuambia mkutano umeandaliwa na nani na utafanyika wapi

    Heche: Umeandaliwa na sekretarieti ya makao makuu na utafanyika ofisi kuu za chama Dar es salaam

    Jaji: Ndio

    Lissu: Sasa shahidi tuhuma inayonikabili Mahakamani hapa ya uhaini inadai mimi ndiye niliyeandaa huo mkutano wewe unalionaje?

    Heche: Hilo sio kweli mkutano uliandaliwa na Sekretarieti kama nilivyopewa taatifa mimi ndovyo alivyopewa na yeye

    Lissu: Amani Gugwa alikuambiaje juu ya waalikwa wengine

    Heche: Kwamba wao wameshafanya maandalizi yote

    Lissu: Waeleze majaji amani alikuambia hao waaalikwa wengine ni akina nani

    Heche: Hakufafanua kwa undani ila aliniambia kuhusua watia nia na wageni wengine wachache

    Lissu: Hiyo siku ya tarehe tatu Aprili mwaka jana ulikuwa wapi.

    Heche: Mimi nilikuwa miongoni mwa wageni viongozi kwenye huo mkutano uliofanyika Mikocheni makao makuu ya chama na nilipata nafasi ya kuzungumza kidogo

    Lissu: Waeleze majaji viongozi wengine waliokuweko kwenye mkutano huo kwa kumbukumbu zako

    Heche: Alikueko Mwemyekiti wa chama taifa Mheshimiwa Tundu Lissu, mimi makamu Mwenyekiti bara, alikuepo Katibu Mkuu John Mnyika, alikueko Amani Golugwa, Naibu Katibu Mkuu bara, alikueko Brenda Rupia, Mkurugenzi wa Habari pamoja na watua nia wenyewe toka maeneo mbalimbali

    Lissu: Waeleze majaji kwa kumbukumbu zako idadi ya watu wote waliokuwa kwenye huo ukumbi walikuwa wangapi

    Heche: Sina hakika ya namba lakini ni zaidi ya watu 200.

  8. KARIBU KATIKA MUENDELEZO WA KESI YA LISSU LEO SEPTEMBA 11 , 2026, Yaliyojiri jana Mahakamani

    .

    Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, iliendelea jana katika Mahakama Kuu ya Tanzania, huku Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Bara, John Heche, akiendelea kutoa ushahidi wake kama shahidi wa tano wa upande wa utetezi.

    Katika hatua nyingine muhimu, Mahakama ilikataa ombi la utetezi la kuwaita Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu mstaafu Kassim Majaliwa na Mkurugenzi Mkuu wa Usalama wa Taifa kutoa ushahidi katika kesi hiyo.

    Hata hivyo, Mahakama ilikubali kuitwa kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Camillus Wambura, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, DCI Ramadhani Kingai, na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali John Jacob Mkunda, kama mashahidi wa upande wa utetezi.

    Uamuzi huo ulitolewa baada ya Mahakama kusikiliza hoja za pande zote kuhusu umuhimu wa mashahidi hao katika kesi hiyo, huku upande wa utetezi ukisisitiza haki ya Lissu kuwaita mashahidi anaowaona kuwa muhimu kwa utetezi wake.

    Leo, kesi hiyo inaendelea huku hatua inayotarajiwa ikiwa ni kuendelea kwa ushahidi wa John Heche mbele ya jopo la majaji watatu linalosikiliza kesi hiyo.

  9. Heche afafanua ujumbe wa Lissu: "Tatizo ni mfumo wa Uchaguzi"

    LISSU: Waeleze Waheshimiwa Majaji nilisema nini juu ya harakati mbalimbali za kubadili mfumo huu wa uchaguzi.

    HECHE: Alieleza kwamba harakati za kubadili mfumo wa uchaguzi zimekuwepo tangu miaka ya 1990. Alitaja juhudi mbalimbali, ikiwemo Tume ya Jaji Nyalali, Tume ya Jaji Kisanga na Tume ya Jaji Joseph Warioba, ambazo zote zilitoa mapendekezo kuhusu mageuzi ya mfumo wa uchaguzi, kuimarisha demokrasia na kutoa nafasi kubwa zaidi kwa wananchi kuamua viongozi wao.

    LISSU: Ukisema kuondoa mfumo wa chama kimoja una maana gani?

    HECHE: Mfumo uliopo sasa, kwa maelezo yake, umekuwa ukitawaliwa na Chama Cha Mapinduzi kupitia viongozi wake. Alieleza kwamba Rais ndiye mwenye mamlaka ya kuteua viongozi wa Tume ya Uchaguzi kuanzia ngazi ya juu hadi ngazi nyingine za usimamizi wa uchaguzi.

    LISSU: Elezea hicho ulichosema kuhusu Mchungaji Christopher Mtikila kwenda mahakama ya Afrika.

    HECHE: Kwa uelewa wangu, Mwenyekiti alieleza kwamba Tanzania ni sehemu ya mikataba mbalimbali ya kimataifa na imewahi kukumbwa na mashauri mbalimbali yaliyoibua mjadala wa haki za kisiasa, ikiwemo kesi ya Christopher Mtikila na mashauri mengine yaliyohusu masuala ya uchaguzi.

    LISSU: Waeleze Waheshimiwa Majaji katika mazungumzo yangu na wadau nililizungumziaje suala la mahakama za nje au za kikanda.

    HECHE: Waheshimiwa Majaji, alieleza kwamba kumekuwa na majaribio mbalimbali ya kubadili mfumo wa uchaguzi kupitia mahakama za ndani na za kikanda, lakini baadhi ya maamuzi au mapendekezo hayo hayajatekelezwa kikamilifu.

    LISSU: Waeleze Waheshimiwa Majaji nilizungumza nini na wadau kuhusu suala la kuahirisha uchaguzi wa mwaka 2025.

    HECHE: Alisema kwamba kwa sababu mfumo uliopo una matatizo mengi yanayosababisha migogoro, vurugu na matokeo yanayobishaniwa, chama kilikuwa tayari uchaguzi usogezwe mbele ili kutoa nafasi ya kufanya mabadiliko yatakayowezesha uchaguzi kuwa huru na wa haki.

    LISSU: Waeleze Waheshimiwa Majaji kuhusu jitihada za kuwashirikisha wadau wa nje unazozifahamu.

    HECHE: Nakumbuka tulisafiri hadi Nairobi, Kenya, mimi pamoja na Tundu Lissu na Godbless Lema kwa lengo la kuzungumza na wadau mbalimbali.

    LISSU: Waeleze Waheshimiwa Majaji mkakati wa kuzungumza na wananchi ulikuwaje.

    HECHE: Mkakati ulikuwa kufanya mikutano ya hadhara katika maeneo mbalimbali ya nchi.

    LISSU: Waeleze Waheshimiwa Majaji kwamba katika ziara ya kanda mimi na wewe tulikuwa pamoja.

    HECHE: Ndiyo, tulikuwa pamoja katika mikutano ya Mbeya Mjini na Iringa Mjini.

    LISSU: Waeleze Waheshimiwa Majaji mkutano wa Mbeya ulikuwa tarehe ngapi.

    HECHE: Sikumbuki tarehe, lakini nakumbuka ulikuwa mkutano wa kwanza katika ratiba hiyo.

    LISSU: Waeleze Waheshimiwa Majaji kuhusu mkutano wa Iringa.

    HECHE: Nao sikumbuki tarehe yake, lakini nakumbuka ulikuwa mkutano wa mwisho.

    LISSU: Baada ya hapo ratiba ilikuwaje? Wewe ulienda wapi na mimi nilienda wapi?

    HECHE: Mimi nilikwenda Njombe pamoja na baadhi ya maeneo ya Iringa, wakati Tundu Lissu alikwenda Rukwa, Sumbawanga, Tunduma na Songwe.

    LISSU: Waeleze Waheshimiwa Majaji katika mikutano tuliyokuwa pamoja nilizungumza nini.

    HECHE: Kwa kiasi kikubwa mazungumzo yake yalijikita katika matatizo ya uchaguzi na historia ya uchaguzi nchini. Hoja zilizokuwa zikitolewa zilifanana kwa kiasi kikubwa katika mikutano yote.

    LISSU: Waeleze Waheshimiwa Majaji kuhusu mkutano wa mwisho wa Iringa. Kulikuwa na tofauti gani kati ya mkutano huo na mikutano mingine?

    HECHE: Kwa kumbukumbu yangu, hakukuwa na tofauti kubwa kati ya hotuba ya Iringa na hotuba zilizotolewa katika mikutano mingine.

    LISSU: Kuhusu mkutano wa tarehe 3 Aprili 2025, waeleze Waheshimiwa Majaji wewe ulipataje taarifa za mkutano huo?

  10. Heche: Sikumbuki Lissu akisema “Tutakinukisha”

    .

    LISSU: Waeleze Waheshimiwa Majaji kwamba katika vikao na wadau mbalimbali, kiongozi wa ujumbe wa CHADEMA alikuwa mimi na nilikuwa msemaji mkuu. Ufafanue kwa kina ujumbe wetu. Kote tulikokwenda na kukutana na wadau, waeleze Waheshimiwa Majaji mazungumzo yangu kuhusu suala la Tume ya Uchaguzi ya nchi hii kutawaliwa na Rais.

    HECHE: Waheshimiwa Majaji, kote tulikopita, ikiwemo kwa viongozi wastaafu kama Mzee Joseph Warioba, ujumbe wetu uliongozwa na Mwenyekiti Tundu Lissu. Alieleza kwa kina namna ambavyo Tume ya Taifa ya Uchaguzi, inayoteuliwa na Rais ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM, inavyovuruga uchaguzi, kuwaonea wapinzani hususan CHADEMA, kufanya upendeleo wa wazi kwa wagombea wa CCM, na kuvunja sheria za uchaguzi zilizopo kwa uwazi.

    LISSU: Waeleze Waheshimiwa Majaji mazungumzo yangu kwamba sisi CHADEMA hatuko tayari kuendelea kushiriki au kuruhusu chaguzi za namna hii. Waeleze wadau nilichosema kuhusu ushiriki wetu katika chaguzi hizo.

    HECHE: Kote tulikopita na kwa wote tuliokutana nao, Mwenyekiti Tundu Lissu aliweka wazi msimamo wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo kwamba hatuko tayari kushiriki tena chaguzi za namna hii, ambazo matokeo yake yamekuwa ni mauaji, kuenguliwa kwa wagombea na kukosekana kwa haki.

    LISSU: Waeleze Waheshimiwa Majaji tulichowaeleza wadau hao kuhusu kuhamasisha Watanzania kupinga uchaguzi ujao.

    HECHE: Mwenyekiti aliwaeleza wadau wote tuliokutana nao kwamba kila mmoja, kwa nafasi yake, alipaswa kushiriki kuhakikisha mfumo wa uchaguzi unabadilika. Aidha, aliwaeleza kwamba msimamo wa chama wa “No Reforms, No Elections” ungeendelea kuwasilishwa kwa wananchi kupitia mikutano ya hadhara ili kuwaelimisha.

    LISSU: Waeleze Waheshimiwa Majaji kama nilitumia maneno kuhusu kuhamasisha uasi kwa Watanzania dhidi ya mfumo wetu wa uchaguzi.

    HECHE: Waheshimiwa Majaji, sina kumbukumbu ya Mwenyekiti kutumia neno “uasi”. Hakuna mahali alipolitumia. Maneno yake yalikuwa yakisisitiza kupinga mfumo mbovu wa uchaguzi na kudai mabadiliko ya mfumo huo.

    LISSU: Waeleze Waheshimiwa Majaji kama katika mazungumzo yangu nilisema tutahamasisha wananchi kuzuia uchaguzi.

    HECHE: Waheshimiwa Majaji, Mwenyekiti alieleza msimamo wa kupinga uchaguzi huo kutokana na kutokuwepo kwa mabadiliko yaliyokuwa yanahitajika.

    LISSU: Kwa ufahamu wako, mimi kusema tutavuruga uchaguzi huu ili kuhakikisha haufanyiki?

    HECHE: Waheshimiwa Majaji, nakumbuka alisema kwamba chama kingepinga uchaguzi huo kwa sababu ya kasoro zilizokuwepo kwenye mfumo wa uchaguzi.

    LISSU: Waeleze Waheshimiwa Majaji, kwa kumbukumbu zako, kama nilitumia neno “tutakinukisha”.

    HECHE: Sikumbuki mahali popote ambapo Mwenyekiti alitumia neno “tutakinukisha”.

    LISSU: Katika mazungumzo na wadau, waeleze Waheshimiwa Majaji kuhusu mimi kuzungumzia matatizo ya uundwaji wa majimbo ya uchaguzi nchini.

    HECHE: Nakumbuka Mwenyekiti alizungumzia mgawanyo wa majimbo kwa upendeleo na namna viongozi wanavyojigawia majimbo kwa maslahi yao.

    LISSU: Waeleze Waheshimiwa Majaji, kwa kumbukumbu zako, kuhusu mimi kuzungumzia matatizo ya uteuzi wa wagombea.

    HECHE: Tundu Lissu alieleza namna wagombea wa upinzani walivyoenguliwa kwa wingi. Alitolea mfano uchaguzi wa mwaka 2020 ambao uliweka rekodi ya kuenguliwa kwa wagombea wengi wa udiwani.

    LISSU: Waeleze Waheshimiwa Majaji nilisema nini juu ya yanayofanyika siku ya uchaguzi.

    HECHE: Alieleza kwa kina namna zoezi la upigaji kura linavyovurugwa, ikiwemo wasimamizi wa uchaguzi kufanya makosa, kutangazwa kwa matokeo yasiyo halali na baadhi ya wagombea ambao hawakushinda kutangazwa kuwa washindi.

    LISSU: Waeleze Waheshimiwa Majaji nilisema nini kwa wadau kuhusu utaratibu wa kupinga matokeo ya uchaguzi mahakamani.

    HECHE: Waheshimiwa Majaji, alieleza kwamba ni vigumu kupinga matokeo ya uchaguzi mahakamani. Alisema kwamba mgombea akiwania nafasi na akaenguliwa, hana fursa ya kwenda mahakamani kupinga hatua hiyo katika mazingira fulani.

    LISSU: Waeleze nilisema nini juu ya kupinga matokeo ya Uchaguzi wa Rais mahakamani.

    HECHE: Waheshimiwa Majaji, Tundu Lissu alieleza kuwa nchini Tanzania haiwezekani kupinga matokeo ya uchaguzi wa Rais katika vyombo vya ndani vya kisheria.

    LISSU: Waeleze Waheshimiwa Majaji nilisema nini juu ya haki ya wananchi wasiokuwa wanachama wa vyama vya siasa kugombea uongozi.

    HECHE: Alieleza kwamba nchini Tanzania mgombea huru haruhusiwi kugombea nafasi za kisiasa bila kuwa mwanachama wa chama cha siasa.

    Unaweza kusoma;

  11. Heche: Lissu hakuwahi kuhamasisha uasi, alisisitiza mageuzi ya uchaguzi

    .

    LISSU: Kote huko tulikoenda na kukutana na wadau mbalimbali, waeleze Waheshimiwa Majaji mazungumzo yangu kuhusu Tume ya Uchaguzi kutawaliwa na Rais.

    HECHE: Kote tulikopita, kwa viongozi wa dini na wadau wengine muhimu, ujumbe wetu uliongozwa na Mwenyekiti Tundu Lissu. Alieleza kwamba Tume ya Uchaguzi inateuliwa na Rais, ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM. Alieleza pia kuwepo kwa vitendo vya kuwaonea wapinzani na ukiukwaji wa sheria za uchaguzi.

    LISSU: Nashukuru. Inatosha.

    LISSU: Na, shahidi, kuhusiana na suala hilo la Tume kuwa ya namna hiyo, waeleze Waheshimiwa Majaji kwamba sisi CHADEMA hatuko tayari kuendelea kushiriki uchaguzi wa namna hii tena.

    HECHE: Kote tulikopita tulieleza kwamba sisi CHADEMA hatuko tayari kushiriki tena uchaguzi wa namna hiyo.

    LISSU: Tuliwaeleza nini kuhusu kupinga uchaguzi huo?

    HECHE: Mwenyekiti aliwaeleza wadau mbalimbali, kila mmoja kwa nafasi yake, kwamba tungepinga uchaguzi huo chini ya kaulimbiu ya “No Reforms, No Elections.”

    LISSU: Waeleze Waheshimiwa Majaji kama nilisema tutahamasisha uasi ili kupinga uchaguzi wa nchi hii.

    HECHE: Hakuna sehemu ambayo Mwenyekiti alitumia neno “uasi.” Maneno aliyotumia yalikuwa yakisisitiza haja ya mabadiliko katika mfumo wa uchaguzi. Alitumia maelezo mbalimbali, lakini ujumbe wake uliendelea kuwa wa kupinga uchaguzi bila kuwepo kwa mabadiliko hayo.

    LISSU: Waambie Waheshimiwa Majaji kama nilisema nitahamasisha wananchi kuzuia uchaguzi.

    HECHE: Waheshimiwa Majaji, kwa kadiri ya ninavyokumbuka, Mwenyekiti alieleza msimamo wa kupinga uchaguzi huo kwa sababu ya kutokuwepo kwa mabadiliko yaliyokuwa yanahitajika.

    LISSU: Waeleze Waheshimiwa Majaji kwamba nilisema tutavuruga uchaguzi huu ili kuhakikisha haufanyiki, na kwamba maneno hayo ndiyo yamenisababishia shtaka hili.

    HECHE: Waheshimiwa Majaji, Mwenyekiti alisema kwamba chama kingepinga uchaguzi huo kutokana na kutokuwepo kwa mabadiliko yaliyokuwa yanahitajika.

    LISSU: Shahidi, epuka majibu ya “ndiyo” pekee. Ukisema “ndiyo” tu, inakuwa vigumu kueleweka. Eleza kwa ufafanuzi.

  12. Heche aeleza mahakamani chanzo cha msimamo wa “No Reforms, No Elections”

    .

    LISSU: Waeleze Waheshimiwa Majaji, sasa kwa vile sikutibiwa kwa utaratibu wa kibunge, nilitibiwaje?

    HECHE: Waheshimiwa Majaji, sehemu kubwa ya gharama za matibabu ilitolewa na chama. Chama kilihusika katika kugharamia matibabu hayo, pamoja na michango kutoka kwa marafiki na Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), ambacho wakati huo Mheshimiwa Tundu Lissu alikuwa Rais wake. Pia kulikuwa na michango kutoka kwa wananchi; wengi walichangia kwa njia mbalimbali, ikiwemo kuchangia damu.

    LISSU: Sasa shahidi, kwa vile kwenye ushahidi wako ulisema ulikuwa mbunge, waeleze Waheshimiwa Majaji kitu gani kilitokea kwenye ubunge wangu baada ya kuelekea kwenye matibabu?

    HECHE: Waheshimiwa Majaji, Mheshimiwa Tundu Lissu alivuliwa ubunge kwa sababu zilizoelezwa kwamba alikuwa mtoro wa vikao vya Bunge.

    LISSU: Ilikuwa mwaka gani?

    HECHE: Waheshimiwa Majaji, nakumbuka Mheshimiwa Tundu Lissu alikuwa bado kwenye matibabu nje ya nchi. Nakumbuka pia jimbo lake liliitishiwa uchaguzi wa kuziba nafasi yake.

    LISSU: Shahidi, waeleze Waheshimiwa Majaji ufahamu wako kuhusu aliyekuwa Makamu wa Rais wa wakati huo, Samia Suluhu Hassan, kuja kunitembelea hospitalini Nairobi.

    HECHE: Nakumbuka aliyekuwa Makamu wa Rais wakati huo, Samia Suluhu Hassan, alikwenda Nairobi kwa ziara ya kiserikali, lakini pia alipata fursa ya kumtembelea Mheshimiwa Lissu hospitalini.

    LISSU: Kuhusu Tume ya Utumishi wa Bunge kuja kunitembelea hospitalini je?

    HECHE: Waheshimiwa Majaji, hilo sina kumbukumbu nalo.

    LISSU: Na waeleze Waheshimiwa Majaji ufahamu wako kuhusu aliyekuwa Rais mstaafu marehemu Mzee Ali Hassan Mwinyi na mke wake kuja kunitembelea.

    HECHE: Waheshimiwa Majaji, hilo nalikumbuka. Taarifa zilichapishwa kwenye vyombo vya habari zikieleza kwamba Mzee Ali Hassan Mwinyi pamoja na mke wake walikwenda kumtembelea Mheshimiwa Lissu.

    LISSU: Na waeleze Waheshimiwa Majaji ufahamu wako kuhusu mawaziri wakuu wastaafu Edward Lowassa, Frederick Sumaye na Joseph Warioba kuja kunitembelea hospitalini Nairobi.

    HECHE: Waheshimiwa Majaji, nina kumbukumbu ya Edward Lowassa kumtembelea Mheshimiwa Lissu Nairobi. Vilevile, nakumbuka Frederick Sumaye. Hata hivyo, sina kumbukumbu ya kutosha kuhusu Mzee Joseph Warioba.

    LISSU: Waeleze Waheshimiwa Majaji kuhusu Jaji Mkuu mstaafu Othman Chande kuja kunitembelea Nairobi.

    HECHE: Waheshimiwa Majaji, nina kumbukumbu ya Mheshimiwa Jaji Othman Chande kumtembelea Mheshimiwa Lissu hospitalini.

    LISSU: Waeleze Waheshimiwa Majaji ufahamu wako kuhusu Balozi wa Tanzania nchini Kenya wakati huo, Pindi Chana, kuja kunitembelea hospitalini Nairobi.

    HECHE: Waheshimiwa Majaji, nina kumbukumbu ya Mheshimiwa Pindi Chana kwenda kumtembelea Mheshimiwa Lissu alipokuwa Nairobi kwa matibabu.

    LISSU: Shahidi, nimekuuliza maswali yote haya kwa sababu nataka kukuuliza swali hili: wewe umetumia muda gani kuja kuniona?

    HECHE: Waheshimiwa Majaji, nimekwenda Nairobi mara kadhaa. Siwezi kuwa na kumbukumbu sahihi ya muda wote niliotumia huko, lakini wakati mwingine nilikaa kwa mwezi mmoja, na mara nyingine kwa wiki mbili. Aidha, watu wengi walikwenda kumtembelea.

    LISSU: Sasa shahidi, turudi kwenye tarehe 3 Aprili mwaka jana. Kwenye ushahidi wako wa awali umeiambia Mahakama kwamba nia ya kuwaita watia nia kwenye mkutano huo ilikuwa kuwafahamisha na kuwaelimisha kuhusu msimamo wa chama wa “No Reforms, No Elections.” Tuanzie hapo. Ni mabadiliko gani ambayo chama kilitaka yafanyike kabla ya uchaguzi?

    HECHE: Waheshimiwa Majaji, chama kilitaka mabadiliko ya kikatiba na kisheria. Mabadiliko hayo yalihusu sheria zinazoongoza uchaguzi, namna Tume ya Uchaguzi inavyopatikana, pamoja na Katiba, hususan Ibara ya 74 inayounda Tume hiyo, ili kuwepo kwa Tume Huru ya Uchaguzi inayotoa usawa kwa wote katika uchaguzi mkuu.

    LISSU: Shahidi, kama nilikusikia vizuri, ulisema kwamba msimamo huu wa “No Reforms, No Elections” ulifikiwa kwenye kikao cha Kamati Kuu ya chama kilichofanyika tarehe 3 Desemba 2024. Sasa nini kilifuata baada ya msimamo huo kutangazwa na Kamati Kuu?

    HECHE: Baada ya msimamo huo kufikiwa, ulitangazwa hadharani na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama wakati huo, Freeman Mbowe. Alisema kwamba baada ya yaliyojitokeza kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa Novemba 2024, ambapo baadhi ya wagombea walienguliwa na hata baadhi ya walioshinda hawakutangazwa, Kamati Kuu ilifikia uamuzi kwamba bila mabadiliko hakutakuwa na uchaguzi. Alisema uchaguzi hauwezi kufanyika kwa haki kwa mfumo uliokuwepo.

    LISSU: Waeleze Waheshimiwa Majaji, tamko hilo la Mbowe lilikuwa la tarehe ngapi?

    HECHE: Tamko hilo lilitolewa tarehe 10 Desemba 2024.

    LISSU: Baada ya tamko la Mwenyekiti wa Chama wakati huo, Mheshimiwa Mbowe, nini kilifuata?

    HECHE: Waheshimiwa Majaji, wakati huo chama kilikuwa kinaelekea kwenye uchaguzi wa ndani. Kulikuwa na maandalizi ya Baraza Kuu na Mkutano Mkuu wa chama. Kamati Kuu ilikutana tarehe 19 Januari 2025.

    LISSU: Waeleze Waheshimiwa Majaji maamuzi gani yalifikiwa kwenye kikao hicho cha Kamati Kuu.

    HECHE: Waheshimiwa Majaji, miongoni mwa maamuzi yaliyofikiwa ni kupitishwa kwa tamko la “No Reforms, No Elections” na kupelekwa kwenye Baraza Kuu la chama kwa hatua zaidi.

    LISSU: Hicho kikao cha Baraza Kuu la Chama kilikuwa cha tarehe ngapi?

    HECHE: Tarehe 20 Januari 2025.

    LISSU: Waeleze Waheshimiwa Majaji kitu gani kilitokea kwenye Baraza Kuu hilo.

    HECHE: Waheshimiwa Majaji, Baraza Kuu lilipokea ajenda hiyo, likaiunga mkono na baadaye kuipeleka kwenye Mkutano Mkuu wa Chama uliofanyika tarehe 21 Januari 2025.

    LISSU: Na nini kilitokea kwenye Mkutano Mkuu?

    HECHE: Huo ulikuwa pia Mkutano Mkuu wa uchaguzi, ambao ulimchagua Mheshimiwa Tundu Lissu kuwa Mwenyekiti wa Chama, Saidi Mzee kuwa Makamu Mwenyekiti Zanzibar, na John Heche kuwa Makamu Mwenyekiti Bara.

    LISSU: Specifically, kuhusu ajenda ya “No Reforms, No Elections,” waeleze Waheshimiwa Majaji nini kiliazimwa.

    HECHE: Mkutano Mkuu uliazimia kwamba Kamati Kuu ya Chama iandae mpango wa kuwafikia wadau mbalimbali, viongozi wa dini na wanachama, kuwaelimisha na kuwaeleza sababu za chama kufikia msimamo huo.

    LISSU: Na waeleze Waheshimiwa Majaji baada ya Mkutano Mkuu kuamua hivyo, Kamati Kuu ilifanya nini?

    HECHE: Kamati Kuu ilikutana katika retreat iliyofanyika Bagamoyo na kuazimia kutekeleza maamuzi ya Mkutano Mkuu. Iliamuliwa kwamba viongozi wa chama, akiwemo Mwenyekiti wa Chama Mheshimiwa Tundu Lissu, Makamu Wenyeviti wa Bara na Zanzibar, Katibu Mkuu John Mnyika, Manaibu Katibu Wakuu wa Bara na Zanzibar pamoja na viongozi wa kanda, wakutane na taasisi mbalimbali. Tulikutana na viongozi wa dini, mabalozi, wazee mashuhuri na mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) kuwaeleza msimamo wa chama na kuomba waunge mkono mabadiliko ili uchaguzi uwe huru, wa haki na wa amani.

    LISSU: Sasa shahidi, shtaka linalonikabili linasema kwamba nilitoa maneno yenye maudhui ya kihaini na kuyachapisha kwenye mitandao ya kijamii. Naomba uwaeleze Waheshimiwa Majaji kuhusu hilo.

    HECHE: Miongoni mwa wadau tuliokutana nao ni Jukwaa la Wahariri. Tulizungumza nao kama tulivyofanya kwa viongozi wa dini na mashirika yasiyo ya kiserikali.

    LISSU: Katika wadau wote hao tuliokutana nao, nataka uwaeleze Waheshimiwa Majaji mikutano ambayo mimi na wewe tulikuwepo pamoja.

    HECHE: Tulitembelea Ubalozi wa Marekani, tulimtembelea Mzee Joseph Sinde Warioba, tulikutana na Mzee Joseph Butiku ambaye ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, tulizungumza na Jukwaa la Wahariri, tulimtembelea Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, Askofu Wolfgang Pisa, na vilevile tuliitembelea LHRC.

    LISSU: Sasa kwa sababu tulikuwa pamoja, nataka uwaeleze Waheshimiwa Majaji nani alikuwa kiongozi na msemaji mkuu wa ujumbe wetu.

    HECHE: Kiongozi na msemaji mkuu wa ujumbe huo alikuwa Mwenyekiti wa Chama, Mheshimiwa Tundu Lissu.

    Unaweza kusoma;

  13. Heche: Kwa nini waliomshambulia Lissu bado hawajakamatwa?

    .

    LISSU: Shahidi, waeleze Waheshimiwa Majaji kuhusu kinga dhidi ya kukamatwa aliyonayo kiongozi yeyote au mwanachama yeyote.

    HECHE: Kwa ninavyofahamu, hakuna kinga yoyote aliyonayo kiongozi au mwanachama yeyote dhidi ya kukamatwa.

    LISSU: Waeleze Waheshimiwa Majaji, kwa unavyofahamu wewe, iwapo kuna chama kingine chochote ambacho wanachama wake wamekamatwa, kushtakiwa na kuwekwa mahabusu.

    HECHE: Waheshimiwa Majaji, sina kumbukumbu ya chama kingine ambacho viongozi wake wamewahi kushtakiwa.

    LISSU: Nilikuuliza kwamba viongozi wa CHADEMA wana kinga dhidi ya kukamatwa, ukasema hapana. Swali langu ni hili: kukamatwa kwa wanachama na viongozi wa CHADEMA lengo lake hasa ni nini?

    HECHE: Lengo la kukamata wanachama na viongozi ni kuwatisha na kuwakatisha tamaa, na kuwarudisha nyuma kwenye misimamo mbalimbali ambayo chama kimekubaliana.

    LISSU: Waeleze Waheshimiwa Majaji uhalali wa maneno hayo ya kukamata viongozi kwa lengo la kuwatisha, kwa unavyofahamu.

    HECHE: Hakuna uhalali wowote wa kufanya hayo. Hakuna uhalali wa kisheria wala wa kiutu. Mimi ninachokiona ni kile alichokisema Katibu Mkuu wa wakati huo, Bashiru Ally, kwamba, "tutatumia dola kuendelea kubaki kwenye dola." Kwa hiyo, haya matendo yanalenga kutumia dola kuendelea kubaki kwenye dola kwa CCM.

    LISSU: Shahidi, umewaeleza Waheshimiwa Majaji kwamba ulikuwa na mimi bungeni kuanzia mwaka 2015 hadi 2020. Waeleze Waheshimiwa Majaji kitu gani kilitokea tarehe 7 Septemba 2017?

    HECHE: Alishambuliwa kwa risasi mchana wa tarehe 7 Septemba 2017 akiwa anaenda kula chakula cha mchana katika makazi yake, Dodoma.

    LISSU: Waeleze Waheshimiwa Majaji, siku hiyo ya tukio wewe ulikuwa wapi?

    HECHE: Waheshimiwa Majaji, siku hiyo mimi nilikuwa bungeni.

    LISSU: Waeleze Waheshimiwa Majaji kitu gani kilitokea kabla ya hilo shambulio na baada ya shambulio, kwa unachokifahamu.

    HECHE: Kabla ya hilo shambulio tulikuwa bungeni. Baadaye mchana alienda nyumbani kwake, ambapo alifuatiliwa na gari hadi kwenye eneo la makazi yake. Eneo hilo nalifahamu kwa sababu niliwahi kwenda pale. Katika eneo hilo viongozi kadhaa wa Serikali na wabunge walikuwa wanaishi.

    Mara zote ukienda pale hukutana na askari anayekuuliza unaenda wapi, na kulikuwa na kitabu cha kusaini wageni. Alifuatiliwa na kushambuliwa pale nyumbani kwake. Washambuliaji waliondoka kupitia getini, na mpaka leo hakuna aliyewahi kushtakiwa wala kukamatwa kuhusiana na tukio hilo.

    LISSU: Waeleze Waheshimiwa Majaji baada ya hilo shambulio kitu gani kilitokea.

    HECHE: Baada ya hilo shambulio alisafirishwa kwenda Nairobi, Kenya, kwa ajili ya matibabu, ambapo alitibiwa kwa muda mrefu na baadaye kupelekwa Ubelgiji.

    LISSU: Sasa waeleze Waheshimiwa Majaji hizi taarifa za kutibiwa kwangu kwenda Ubelgiji wewe ulizijuaje?

    HECHE: Waheshimiwa Majaji, nilizijua kwa sababu nilikuwa naye bungeni. Aidha, nilimtembelea hospitalini Nairobi mara kadhaa. Vilevile, Spika wa Bunge wa wakati huo, Job Ndugai, ambaye sasa ni marehemu, alitutangazia bungeni.

    LISSU: Waeleze Waheshimiwa Majaji, umesema umewahi kuwa mbunge. Waeleze Majaji utaratibu wa mbunge anapougua na kutibiwa nje ya nchi ukoje.

    HECHE: Mbunge anapopata matatizo ya afya ambayo yanaweza kutibiwa hapa nchini, hutibiwa hapa kwa kutumia bima ya afya ya wabunge. Lakini kama anatakiwa kutibiwa nje ya nchi na amepata rufaa, Ofisi ya Katibu wa Bunge huchukua jukumu la kulipia matibabu, gharama za makazi pamoja na gharama za msaidizi anayekuwa naye.

    LISSU: Sasa waeleze Waheshimiwa Majaji kama huo utaratibu ulitumika kwenye matibabu yangu.

    HECHE: Utaratibu huo haukutumika kwa Mheshimiwa Tundu Lissu. Hakulipiwa matibabu, wala msaidizi wake, wala gharama za sehemu aliyokuwa akiishi wakati wa matibabu yake.

    Unaweza kusoma;

  14. Heche: 'Sikukamatwa kwa ugaidi, tuhuma zilikuja baadaye'

    .

    LISSU: Hiyo tarehe 4 Novemba uliposafirishwa kuja Dar es Salaam ulifikia wapi?

    Heche: Nilipotolewa Dodoma na kufikishwa Dar es Salaam, nilipelekwa Kituo cha Polisi Oysterbay. Siku hiyo niliwakuta kina Wakili Nassoro Katuga, Wakili Job Mrema, Wakili Thawabu Issa na Wakili Cathbert Mbilinyi.

    LISSU: Waeleze Waheshimiwa Majaji kitu gani kilitokea.

    Heche: Waheshimiwa Majaji, niliwakuta hawa mawakili wa serikali wakuu. Siku hiyo kulikuwa na watu wengi sana pale kituoni ambao walikuwa wamekamatwa, wengine wakiwa wamejeruhiwa. Niliambiwa walikuwa wamekamatwa kwa sababu ya vurugu za uchaguzi. Waliwekwa kwenye selo zao hadi kwenye korido. Hawa mawakili walikuwa pamoja na Bwana George Bagemu.

    LISSU: Waeleze Waheshimiwa Majaji kilitokea nini ulipowakuta hawa mawakili wa serikali?

    Heche: Nilipelekwa kwenye chumba ghorofa ya kwanza na kusomewa kwamba ninakabiliwa na kosa la ugaidi, nikidaiwa kuhusika na kuchoma vituo vya Mwendokasi kuanzia Kimara hadi Ubungo.

    LISSU: Aliyekusomea shtaka la ugaidi alikuwa nani?

    Heche: Alikuwa askari, lakini simkumbuki.

    LISSU: Ikawaje baada ya kusomewa hayo mashtaka ya ugaidi?

    Heche: Waheshimiwa Majaji, sikuwa tayari kuandika maelezo yangu. Walichukua tu majina yangu na mahali ninapoishi, kisha baada ya hapo wakanipeleka Kituo cha Polisi Mburahati.

    LISSU: Ulikaa muda gani pale Oysterbay?

    Heche: Nilikaa kwa saa chache tu. Kwanza nilipelekwa kituo fulani Kijitonyama, lakini tukaambiwa kimejaa, hivyo nikapelekwa Mburahati.

    LISSU: Ulipofika Mburahati kitu gani kilitokea?

    Heche: Waheshimiwa Majaji, niliwekwa hapo kuanzia tarehe 4 Novemba hadi tarehe 10 Novemba 2025.

    LISSU: Nini kilitokea baada ya kufikishwa Oysterbay?

    Heche: Nilichukuliwa pale na kurudishwa Kituo cha Polisi Oysterbay. Nilimkuta Naibu Katibu Mkuu, Ndugu Aman Golugwa, ambaye naye alikuwa amekamatwa wakati akitaka kusafiri. Pia nilikutana na Bwana Godbless Lema, Mjumbe wa Kamati Kuu, pamoja na Boniface Jacob na viongozi wengine wa Kamati Kuu. Wote hawa walikuwa wamekamatwa. Tulipokutana hapo tulimkuta ZCO Mafwele ambaye alituambia tudhaminiwe na tuondoke, kisha turipoti tena tarehe 12 Novemba 2025. Siku hiyo tulienda kuripoti.

    LISSU: Mlivyoenda kuripoti nini kilitokea?

    Heche: Tulienda kuripoti katika ofisi ya ZCO Mafwele pale Central, akatuambia tuendelee na shughuli zetu.

    LISSU: Hii tuhuma ya ugaidi waambie Waheshimiwa Majaji iliishia wapi?

    Heche: Waheshimiwa Majaji, mimi sikukamatwa kwa tuhuma ya ugaidi. Nilikamatwa kwa tuhuma ya kuvuka mpaka wakati naenda kuhudhuria mazishi ya Raila Odinga. Hii tuhuma ya ugaidi nilipewa baada ya kufikishwa Polisi Dodoma. Tuhuma hizo ziliishia hapo tu.

    LISSU: Kama nilikusikia sawasawa, ulisema katika ushahidi wako wa awali kwamba tangu ulichaguliwa kuwa Diwani mwaka 2008 hadi leo, kwa ufahamu wako, kuna kiongozi yeyote wa ngazi za juu wa chama ambaye hakukamatwa kwa sababu mbalimbali na kesi zake zikafutika tu kama hii?

    Heche: Waheshimiwa Majaji, sina kumbukumbu ya kiongozi ambaye hajakamatwa.

    LISSU: Sasa shahidi, katika kesi hii mimi nimekamatwa, kwa kadri ya taarifa zilizoletwa mahakamani na waendesha mashtaka. Waeleze Waheshimiwa Majaji kama hii ni kesi yangu ya kwanza tangu unifahamu.

    Heche: Hii si kesi ya kwanza kwa Mheshimiwa Tundu Lissu. Nakumbuka alikamatwa mwaka 2014 maeneo ya Nyamongo. Nakumbuka pia alikamatwa mara kadhaa kwa kesi mbalimbali, ikiwemo za uchochezi.

    LISSU: Kama unakumbuka nilipokamatwa, nilikamatwa kwa kesi gani?

    Heche: Nakumbuka tukio lenyewe. Kulikuwa na watu waliouawa pale mgodini. Mheshimiwa Tundu Lissu alifika eneo hilo kwa sababu kulikuwa na msuguano kati ya wananchi na walioua. Alifika kama mtetezi wa wananchi wa Nyamongo na alikamatwa kwa kesi ya uchochezi.

    LISSU: Waeleze Waheshimiwa Majaji, kipindi hicho nilikuwa na cheo gani ndani ya chama?

    Heche: Waheshimiwa Majaji, wakati huo Tundu Lissu alikuwa Mbunge na Mkurugenzi wa Haki na Sheria wa chama.

    LISSU: Waeleze Waheshimiwa Majaji hiyo kesi ya uchochezi iliishia wapi?

    Heche: Waheshimiwa Majaji, kama ilivyokuwa kwa kesi nyingine, nayo iliisha tu.

    LISSU: Na waeleze Waheshimiwa Majaji hizo kesi nyingine za uchochezi ziliishaje?

    Heche: Waheshimiwa Majaji, kesi za uchochezi ambazo Tundu Lissu alifunguliwa kuanzia mwaka 2015 hadi 2020 nazo ziliisha tu. Kwa baadhi yake ilisemekana serikali haikuwa na nia ya kuziendeleza.

    LISSU: Sasa shahidi, kwa hizi kesi ambazo umesema nimekamatwa nazo, waeleze Waheshimiwa Majaji kama ipo hata moja ambayo nimekutwa na hatia.

    Heche: Hakuna hata moja.

    LISSU: Na hivyo hivyo kwa viongozi na wanachama wa CHADEMA waliokamatwa na kufunguliwa kesi, je, yupo hata mmoja aliyekutwa na hatia akafungwa au kulipa faini?

    Heche: Waheshimiwa Majaji, kwa ninavyofahamu, ukiacha kesi ile tuliyokamatwa na kushtakiwa nayo pale Kisutu, sina kumbukumbu ya mtu yeyote aliyetiwa hatiani.

  15. Heche aieleza mahakama sakata la watu waliotekwa na kupotea Tanzania

    .

    LISSU: Waeleze Waheshimiwa Majaji matukio ya utekaji unayoyafahamu.

    HECHE: Matukio ya kutekwa na kupotea kwa watu mwaka 2016 ni pamoja na kupotea kwa Ben Saanane, Azory Gwanda, mwandishi wa Mwananchi, na Kanguye aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya CCM Kigoma.

    LISSU: Waeleze Waheshimiwa Majaji, kwa ufahamu wako, hao watu walipatikana au vipi?

    HECHE: Mpaka leo familia ya Ben Saanane haijawahi kujua ndugu yao yuko wapi. Hali kadhalika kwa familia ya Azory Gwanda.

    LISSU: Waeleze Waheshimiwa Majaji matukio mengine ya utekwaji kama yapo.

    HECHE: Waheshimiwa Majaji, kuna matukio ya kutekwa kwa Balozi Humphrey Polepole wa CCM, ambaye amewahi kuwa Mbunge, Balozi na Mkuu wa Wilaya. Kuna pia tukio la kutekwa kwa Mdude Nyagali, mwanachama wa CHADEMA, ambaye mpaka sasa hajulikani alipo tangu mwaka 2024.

    Pia yupo Deusdedit Soka, aliyekuwa Mwenyekiti wa Vijana wa CHADEMA kutoka Temeke; Jacob Mlaya, aliyekuwa Katibu wa CHADEMA Temeke; Daniel Chonchori, aliyepotea Tarime na ambaye alikuwa mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa; na Sinda Geteba, aliyekuwa mgombea wa udiwani wa CCM katika Kata ya Sirari. Familia yake inadai alichukuliwa na RCO na mpaka leo hajarudi.

    Kuna pia Bhurure Tall, aliyekuwa mwanachama wa CHADEMA; Amani Manengero kutoka Mwanza, aliyekuwa Mwenyekiti wa Vijana wa BAVICHA Mkoa wa Mwanza; Nyangoko Kina, mwananchi aliyepotea Tarime, Sirari; Deus Kipanya, aliyekuwa kiongozi wa CHADEMA Sumbawanga; pamoja na Siza Kiheta kutoka Tarime. Kwa sasa niseme hao tu kati ya watu wengi ambao wameweza kutekwa.

    LISSU: Jana wakati unatoa ushahidi ulielezea kesi iliyokuhusu wewe, Freeman Mbowe na wengine ambao walikuwa viongozi wa chama. Naomba uwaeleze Waheshimiwa Majaji, ukiacha hiyo kesi ya mwaka 2018, eleza kesi nyingine za kisiasa zinazokuhusu wewe na zinazowahusu viongozi wenzako wa chama.

    HECHE: Waheshimiwa Majaji, kuna kesi iliyomhusu Mwenyekiti Mbowe, kesi ya ugaidi ya mwaka 2021. Baadaye aliachiwa na tukaona picha yake ya kwanza Ikulu akiwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

    LISSU: Waeleze Waheshimiwa Majaji, hiyo kesi ya ugaidi ilimweka Mwenyekiti gerezani kwa muda gani?

    HECHE: Kwa miezi minane. Waheshimiwa Majaji, siku Mwenyekiti alipokamatwa Mwanza, nilikamatwa naye pamoja na wanachama wengine na baadhi ya viongozi wa dini tuliokuwa nao siku hiyo. Nakumbuka tulikamatwa pia na Mzee Azavery Lwaitama.

    LISSU: Waeleze Waheshimiwa Majaji, huyu Azavery Lwaitama ni nani?

    HECHE: Dk. Azavery Lwaitama kwa sasa ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa chama na mshauri wa chama. Tulikamatwa pia na Mzee Masinde ambaye sasa ni marehemu, John Pambalu aliyekuwa Mwenyekiti wa BAVICHA wakati huo na ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa Oganaizesheni na Mafunzo wa CHADEMA, Baba Askofu Mwamakula, pamoja na Rose Mayemba aliyekuwa Mwenyekiti wa Mkoa wa Njombe na ambaye sasa ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA.

    LISSU: Shahidi, umesema mlikamatwa wote pamoja na Mwenyekiti, halafu ukasema Mwenyekiti akafunguliwa kesi ya ugaidi.

    HECHE: Tulishikiliwa katika vituo mbalimbali vya polisi. Wengine walikuwa Nyakato, wengine Kirumba, na mimi nilikuwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Mwanza. Tulikaa siku mbalimbali; mimi nilikaa siku tano na nikafanyiwa upekuzi. Wengine walisafirishwa kwenda maeneo wanakotokea. Kwa mfano, Rose alipelekwa Njombe, huku Pambalu na Mzee Lwaitama wakipelekwa Dar es Salaam. Baadaye walifikishwa nyumbani kwao na kuachiwa.

    LISSU: Shahidi, endelea kueleza kuhusu kesi nyingine za aina hii.

    HECHE: Mwaka jana nilikamatwa hapa hapa nje ya Mahakama Kuu tarehe 22 Oktoba 2025. Tuhuma niliyopewa nilipofikishwa Central kwa Bw. Mafwele ni kwamba nilikuwa nimevuka mpaka kwenda Kenya bila kufuata taratibu.

    Kwa hiyo nilichukuliwa hapo na kuambiwa napelekwa sehemu nilipofanyia kosa, yaani Tarime. Tulianza safari na kufika Dodoma usiku wa siku hiyo hiyo. Nikapelekwa Kituo cha Polisi Mtumba, Dodoma, karibu na Mji wa Serikali, na kuwekwa selo peke yangu mpaka nilipotolewa tarehe 4 Novemba na kusafirishwa kurudishwa Dar es Salaam.

    Waheshimiwa Majaji, nilipokuwa huko ndugu zangu hawakuruhusiwa kuja kuniona mpaka nilipogomea kula wala kunywa kwa siku tatu. Baada ya hapo ndipo ndugu yangu aliruhusiwa kuja kuniona.

    Soma Zaidi:

  16. Kesi ya Lissu: Matukio ya kutekwa ni ya muda mrefu - Heche

    Majaji wameingia na kesi inaendelea, Heche akiulizwa na Lissu maswali ya ufafanuzi

    Jaji: Tuendelee

    Lissu: Tuendelee tulipoishia jana, ulitoa mifano ya mauaji wakati wa chaguzi mbalimbali, waeleze Majaji,mauaji mengine unayofahamu nyakati za uchaguzi

    Heche: Nakumbuka aliuawa mwanachama wetu mmoja Igunga, Mbwana Massod mwaka 2011

    Lissu: Huyu alikuwa na nani na nani alihusika?

    Heche: Mbwana Massod alikuwa kiongozi wa CHADEMA, alikuwa natokea Jimbo la Ubungo ambapo alienda kushiriki kampeni jimbo la Igunga, aliuawa na viongozi na wanachama wa CCM na hakuna hatua zozote za kisheria zilizo chukuliwa.

    Lissu: Waeleze majaji kama kuna watu wa CHADEMA walikamatwa wakati wa uchaguzi huo.

    Heche: Ndiyo, viongozi wa CHADEMA walikamatwa kuna Mwenyekiti wa Kinondoni kichama, Henry Kileo alikamatwa Pamoja na Mkurugenzi wa ulinzi wakati huo, Wilfred Rwakatare. Walishitakiwa wote kwa kesi kubwa za ugaidi. Henry alishitakiwa Tabora, Mahakam baadae ikatupilia mbali na kuachiwa huru na Wilfred Rwakatare alishitakiwa hapa Dar esa Salaam na baadaye Mahakamma ikamuachia huru, hiyo ni baada ya kuwa wamekaaa magerezani kwa muda mrefu.

    Lissu: Waeleze majaji kama kumekuwa na mauaji ya wananchi wengine wasio wanachama wa CHADEMA.

    Heche: Waheshimiwa majaji kuna mauaji ambayo yana husisha wananchi wakati wa uchaguzi wa serikali za mtaa kuna maeneo ambayo yalitokea mauaji kama Shinyanga, Tunduma yenyewe pia

    Lissu: Waeleze majaji ufahamu wowote ulionao juu ya mauaji Pemba na Zanzibar

    Heche: Waheshimiwa majaji wakati …..

    Katuga: Hii aina ya uulizaji maswali waheshimiwa majaji ni kama mshitakiwa anatoa ushahidi

    Jaji: Sawa

    Lissu: Hilo swali sioni kama linashida yoyote

    Jaji: Nadhani upande wa Jamuhuri wako sahihi ungemuuliza tu maeneo mengine kama yapo na sio kumuelekeza kwa kumtajia maeneo

    Lissu: Sawa……Sasa waeleze majiji iwapo unakumbuka mauaji nje ya CHADEMA maeneo mengine.

    Heche: Nakumbuka mauji ya mwaka jana wakati wa uchaguzi mkuu ambapo mamia ya watu waliuawa mauaji hayo yalifanywa na vyombo vya dola- polisi. Mauaji makubwa yalifanyika Dar es Salaam, Mwanza, Mbeya, Arusha, Tarime, Geita na maeneo mengine mengi.

    Mauaji ambayo kwa kweli……..

    Lissu: Usitangulie peke yako

    Lissu: Waeleze majaji juu ya utekwaji na upetezaji wa watu

    Katuga: Huu ulizaji wa maswali nachoka kusimama waheshimiwa majaji haya maswali ni leading yana pendekeza majibu

    Lissu: Nimeshaondoka kwenye swala mauaji wakili wa serikali anasema lina sugest jibu, Jibu gani kama lipo shahidi atasema kama hajui atasema sijui. Suala la watu kupotezwa ni mjadala mzito nchi hiii na ni topic (mada) mpya kabisa na mlead (namuongoza) vipi shahidi?

    Vinginevyo nitaintroduce vip new topic (nitatambulisha vipi hoja mpya) waheshimiwa majaji

    Jaji: Tuna sisitiza tu tujikite kwenye taratibu za examination in chief tunaomba usiulize maswali yanayo suggest(pendekeza) majibu

    Lissu: Naomba nilirejee swali waheshimiwa majiji waambie majaji matukio mengine ya uonevu nje ya mauaji

    Heche: Matukio ya uonevu ni mengi ikiwemo watu kutekwa na kupotezwa. Katika hilo nitazungumza matukio kadhaa ninayo yafahamu

    Ripoti ya TLS inasema kuna watu 718 waliotekwa na kupotezwa kati ya hao kuna viongozi wa CHADEMA, wanachama wa CHADEMA, viongozi wa vyama vingine vya siasa kama CCM ambao wameonesha msimamo wao wa wazi wa kupinga matendo ya serikali hii.

    Lissu: Simama hapo hapo shahidi

    Jaji: Ndio

    Lissu: Hujatuambia hiyo ripoti ya TLS ni ya mwaka gani tupe taarifa kamili

    Heche: Waheshimiwa majiji ripoti ya TLS mwaka 2026 imeeleza matukio ya mwaka jana. Mwaka 2016/2017 ni ya muda mrefu waheshimiwa.

    Lissu: Tuaanze na ya 2016/20217

    Heche: Mwaka 2016/2017 ni ya Ben Sanane kutekwa na kupotea, Azory Gwanda alikuwa mwandishi, Kanguye aliyekuwa Mwenyeki wa CCM huko Kigoma.

  17. Kesi ya Lissu: Mahakama kuamua kuhusu mashahidi 7 akiwemo Rais Samia

    .

    Mwandishi wetu anaripoti kutoka Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar Es Salaaam kwamba Mahakama itatoa uamuzi mdogo kuhusu Mashahidi 7 waliotajwa na Tundu Lissu, anayetuhumiwa kwa kesi ya uhaini.

    Baada ya mwezi uliopita Mahakama kuamua kwamba Tundu Lissu ana kesi ya kujibu, mshtakiwa huyo alieeleza kwamba amepokea uamuzi huo na yupo tayari kujitetea yeye mwenyewe kama shahidi wa kwanza na kuwaleta mashahidi wengine mahakamani hapo.Aliwataja mashahidi hao, Lissu amesema mashahidi wake katika kesi hiyo watakuwa ni Rais Samia Suluhu Hassan, ambaye ndiye kiongozi Mkuu wa Serikali inayodaiwa kutishiwa.Mashahidi wengine ni aliyekuwa Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango, aliyekuwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, IGP Camilius Wambura, Mkuu wa Majeshi General Mkunda, Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) na Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai, CP Ramadhan Kingai.Wengine ambao wametoa ushahidi wao ni Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika, Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Amani Golugwa, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA - Bara, John Heche pamoja na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa chama hicho, Brenda Rupia.

    Upande wa mashtaka ukiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Nassoro Katuga ulipinga baadhi ya mashahidi waliotajwa na mtuhumiwa hasa wale 7 wanaotoka Serikalini, na wastaafu akiwemo Rais.

    Mahakama ilisema wale ambao hawabishaniwi mashahidi kutoka CHADEMA wangeendelea kutoa ushahidi na kwamba ingetoa uamuzi kuhusu vigogo 7 wakiongozwa na Rais.

    Lakini kwa sasa ushahidi wa Heche unaendelea.

  18. KARIBU TENA SEPTEMBA 10 LEO KESI YA LISSU INAENDELEA

    s
    Maelezo ya picha, Heche akiteta jambo na wenzake waliofika Mahakamani leo kuendelea na kesi ya uhaini ya Lissu
    .
    Maelezo ya picha, Profesa Azaveli Lwaitama (kushoto) akiwa na Sheikh Issa Ponda Mahakamani leo, anayesoma gazeti
    .
    Maelezo ya picha, Mawakili wa Serikali wakiwa Mahakamani
  19. Heche: Polisi walituzuia kwa mabomu kampeni za Lissu Tarime

    Mahakamani

    Lissu: Waeleze majaji, nilipokuja jimboni kwako mwaka 2020 nini kilitokea?

    Heche: Waheshimiwa majaji, Lissu alikuwa mgombea urais wa CHADEMA mwaka 2020. Alifika jimboni kwetu, tukafanya mikutano maeneo kadhaa. Siku ya kwanza, kesho yake tulitarajia kufanya mikutano katika kata inayoitwa Matongo. Hili eneo linaitwa Kewanja. Polisi walituzuia kwa mabomu katika eneo ambalo mgombea alipaswa kusalimia wananchi. Kukatokea vurugu kubwa sana kati ya raia na polisi. Kulikuwa na maji ya washawasha, risasi na mabomu. Lakini vurugu zilipokuwa kubwa sana na polisi wakazidiwa, walituruhusu kufanya mkutano.

    Heche: Lengo lilikuwa kutawanya watu wasije kutusikiliza. Kwa imani yao, tungekosa watu wa kutusikiliza. Bahati nzuri ilikuwa ni Tarime, Waheshimiwa Majaji, ambako si rahisi vitisho hivyo vikawakimbiza watu waliokuwa na hamu ya kumsikiliza mgombea urais.

    Heche: Wakati mgombea wetu anafanyiwa hivi, hakuna mgombea wa CCM aliyewahi kufanyiwa hivyo. Si Magufuli wakati ule wala Samia sasa, ambaye mikutano yao imewahi kuharibiwa kwa mabomu, risasi na maji ya washawasha.

    Lissu: Waeleze majaji, hili ni swali langu la mwisho kwa leo. Siku ya uchaguzi wa mwaka 2020 katika Jimbo la Rorya kulikuwa na nini?

    Heche: Waheshimiwa majaji, siku ya uchaguzi mkuu katika Jimbo la Rorya, ambako alikuwa anagombea Ezekia Biogot Wenje ubunge kupitia CHADEMA, walivamiwa nyumbani kwao na polisi. Katika tukio hilo, ndugu Nyatenda Wenje aliuawa nyumbani kwao pamoja na kuwepo kwa Wenje.

    Lissu: Huyu Nyatenda Wenje alikuwa nani?

    Heche: Alikuwa ndugu yake wa Ezekia Wenje.

    Lissu: Je, Ezekia Wenje kitu gani kilimtokea?

    Heche: Katika tukio hilo, Bwana Ezekia Wenje alinusurika kuuawa. Alikimbilia Kenya na baadaye akaenda uhamishoni nchini Canada.

    Lissu: Waeleze majaji, hatua zozote zilichukuliwa dhidi ya wauaji wa Nyatenda Wenje?

    Heche: Waheshimiwa majaji, sina kumbukumbu yoyote juu ya hatua zilizochukuliwa dhidi yao.

    Lissu: Waheshimiwa majaji, nimemaliza kwa leo.

    Lissu: Naomba tuahirishe mpaka kesho ili tuendelee na examination-in-chief, Waheshimiwa Majaji.

    Jaji: Upande wa mashitaka mnasemaje?

    Nzengeli: Ni sawa, tuahirishe mpaka kesho.

    Jaji: Shauri limeahirishwa. Uamuzi utatolewa kesho.

    Unaweza kusoma;

  20. Mdogo wangu aliuawa akiwa amefungwa pingu mikono yote nyuma - Heche

    John Heche

    Lissu: Matukio mengine?

    Heche: Wakati nagombea ubunge mwaka 2015, nilipokuwa naenda kufanya kampeni Kata ya Nyanungu, Tarime, tulishambuliwa na akauawa Bwana Bokhe Mwita Waitiei.

    Lissu: Alishambuliwa na watu gani?

    Heche: Alishambuliwa na wafuasi wa CCM. Walikamatwa na baadaye kuachiwa, kisha kesi ikaisha hivyo.

    Lissu: Unamaanisha nini unaposema kesi ilifunguliwa?

    Heche: Walikamatwa kwa sababu walifahamika, lakini baadaye waliachiwa huru.

    Lissu: Nini kilitokea kwenye uchaguzi wa Busanda?

    Heche: Aliuawa kiongozi Alphonce Mawazo, ambaye alikuwa mgombea wa Jimbo la Busanda. Hata kumzika ilibidi tuombe amri ya mahakama kwa sababu tulizuiwa kumuaga huku mwili wake ukiwa bado hospitalini.

    Lissu: Alphonce Mawazo alikuwa na nafasi gani kwenye chama?

    Heche: Alikuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Geita na mjumbe wa Baraza Kuu la chama.

    Lissu: Kuna hatua zozote zilichukuliwa dhidi ya waliomuua Alphonce Mawazo?

    Heche: Sikumbuki vizuri mwisho wa kesi hiyo, hivyo siwezi kueleza kwa uhakika.

    Lissu: Waeleze majaji nini kilitokea jimboni kwako Tarime mwaka 2020.

    Heche: Mwaka 2020, wakati nafunga kampeni Nyamongo, tulivamiwa kwa risasi. Watu wawili waliuawa na wengine kujeruhiwa. Waliouawa ni Chacha Isangora na Chacha Gabir.

    Watu waliowashambulia wanafahamika. Maganda ya risasi yalikutwa eneo la tukio. Baadhi yao walikuwa viongozi wa CCM. Polisi walichukua maganda hayo, waliwashikilia kwa muda, lakini baadaye wakawaachia. Familia zimebaki na yatima na wajane kutokana na matukio yanayohusishwa na uchaguzi.

    Lissu: Waeleze majaji kama kuna tukio lingine la wakati wa uchaguzi.

    Heche: Kwenye uchaguzi hapana, lakini katika shughuli za siasa zipo nyingine. Polisi walimuua mdogo wangu.

    Waheshimiwa majaji, mdogo wangu aliitwa Suguta Heche. Alikamatwa Sirari mwaka 2018, akafungwa pingu mikono nyuma na kuchomwa sindano akiwa katika hali hiyo.

    Sirari ipo Tarime Vijijini. Baadaye kulikuwa na madai ya jaribio la kumtupa ili ionekane amepata ajali au ameshambuliwa na watu wasiojulikana. Walinzi wa eneo waliona kilichokuwa kinaendelea, hivyo akarudishwa kituo cha polisi.

    RPC wa wakati huo alitoa taarifa kwa umma kwamba mdogo wangu ameuawa kikatili na polisi na kwamba hatua zingechukuliwa. Askari aliyekuwa anahusishwa na tukio hilo aliachiliwa na kuhamishwa kituo, na mpaka sasa ni mtumishi wa Jeshi la Polisi.

    Ninaamini mdogo wangu aliuawa kutokana na msimamo wangu wa kisiasa na kupinga maovu ya nchi hii, na kwamba tukio hilo lilikuwa ujumbe kwamba wanaweza kufanya lolote bila hatua za kisheria kuchukuliwa.

    Unaweza kusoma;