Hukumu ya kesi ya Lissu kutolewa tarehe sita Novemba

Mahakama imesema itahitaji muda wa kutosha ili iweze kutoa maamuzi sababu hili ni shauri la namna yake.

Muhtasari

Moja kwa moja

Na Waandishi wa BBC Swahili

  1. Heche afafanua ushahidi wake kuhusu uchaguzi, utekaji na Tume ya Chande

    .

    Lissu: Uliulizwa kuhusu ripoti za waangalizi wa uchaguzi kama SADC kuhusu utekaji. Waeleze majaji ulichosema.

    Heche: Ukurasa wa 6 ulizungumzia masuala ya utekaji.

    (Akasimama Wakili Mkuu wa Serikali akasema hiki ni kipengele cha re-examination, siyo in-chief, akipinga Heche kuanza kusema mambo mapya ambayo hakuyasema mwanzo. Alisema swali aliloulizwa linahitaji jibu la kufafanua alichosema, siyo kueleza ripoti inasemaje, na kwamba wao wataiomba mahakama wapate nafasi ya kumuuliza maswali hayo. Lissu akasema kitu pekee anachokubaliana na Wakili Mkuu wa Serikali ni kutajwa kwa ukurasa wa 6, lakini mengine yote yalikuwa sahihi.)

    Lissu: Uliulizwa uonyeshe kwenye ripoti ya SADC kuhusu utekaji, ukaonesha uliposoma. Fafanua.

    Heche: Ni kweli, kwenye ripoti ya majaji kuna suala la utekaji.

    Lissu: Uliulizwa kuhusu nilichozungumza wakati wa mikutano na wadau, kwamba ueleze kama katika mikutano hiyo nilitumia maneno ya kuhamasisha uasi au kuvuruga uchaguzi. Ukajibu kwamba hakutumia maneno hayo, ila aliyasema kwa tofauti. Fafanua.

    Heche: Nilimaanisha maudhui yalikuwa yale yale ya kuzungumzia mfumo wa uchaguzi. Uchaguzi wa maneno ulibadilika, lakini ulikuwa unahusu mfumo wa uchaguzi.

    Lissu: Uliulizwa kuhusu ulivyokuwa Mbunge wa Tarime. Ukasema uchaguzi haukuwa huru na wa haki, na ukasema mlilazimisha kutangazwa kuwa mshindi. Pia ukasema hukuwa na mamlaka ya kutangaza kuwa uchaguzi haukuwa huru na wa haki. Ulikuwa na maana gani?

    (Akasimama Wakili Mkuu wa Serikali, Nassor Katuga, akapinga swali hilo akisema Heche hakuulizwa hivyo. Lissu akakubali kupata mwongozo wa mahakama kama alivyoomba Wakili Katuga. Jaji Ndunguru akarejea alichosema Heche katika ushahidi wake kwa kusoma kumbukumbu, kisha Lissu akamtaka afafanue.)

    Lissu: Uliulizwa kuhusu Mbunge wa Butiama. Ukasema mbunge wa sasa wa Butiama alikuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi miaka ya nyuma. Ukaulizwa kama ni makosa kwa mtumishi wa zamani wa serikali kugombea na kujiunga na chama cha siasa. Ukasema katika suala la Mbunge wa Butiama haikuwa sahihi kwake kugombea na kuwa mwanasiasa katika uchaguzi wa 2025. Fafanua.

    Heche: Nilisema kwamba kanuni za CCM zinataka mtu anayegombea awe amejiunga na chama kwa takribani miaka mitano. Kwa hiyo ninaamini bado alikuwa ni mkurugenzi.

    Lissu: Ulisikilizishwa audio clip iliyodaiwa kutoka kituo cha redio cha East Africa. Elezea ulichokisikia kwenye audio hiyo na ukifafanue.

    (Akasimama Wakili Mkuu wa Serikali, Nassor Katuga, akapinga tena Lissu kuuliza swali hilo, akisema halijalenga kufafanua. Lissu akaiomba mahakama sauti hiyo ichezwe tena ili aweze kuuliza swali la ufafanuzi au apewe maelezo ya kilichokuwemo kwenye sauti hiyo. Lissu akawauliza majaji rekodi ya mahakama inasema nini kuhusiana na sauti hiyo, akiwaomba wampe kumbukumbu husika. Majaji wakarejea kusoma alichosema Heche kuhusu suala hilo.)

    Lissu: Uliulizwa kuhusu kwenda kwenye Tume ya Chande. Uliulizwa kama tume hiyo ilikualika wewe na chama chako, ukasema tume hiyo haikukuita na hukumbuki kama ilikialika chama. Ukaulizwa kama ulijua tume hiyo ilitangaza kwamba kuna watu walikuwa wanawazuia wengine kwenda kutoa ushuhuda kwenye tume, ukasema hujui. Kisha ukaulizwa maswali mengine mengi, mpaka ukaoneshwa barua ya tume ya tarehe 22 Desemba mwaka jana ikikutaka kwenda kutoa maoni kwenye tume, ukaoneshwa barua nyingine ya tarehe 2 Januari na ya tatu ya tarehe 21 Januari, zote zikiwa zimeelekezwa kwako. Ukasema tume haikukushirikisha wala haikushirikisha chama. Naomba ufafanue majibu yako.

    Heche: Waheshimiwa majaji, chama chetu kilifungiwa kufanya kazi...

    (Akasimama Wakili Mkuu wa Serikali, Nassor Katuga, kupinga majibu ambayo Heche ameanza kuyatoa. Lissu akasema ni vyema shahidi akajibu swali kwani yeye si mwanasheria.)

    Heche: Sijawahi kupata mwaliko kwenye tume kwani chama chetu kilikuwa kimefungiwa.

    (Akasimama tena Wakili Nassor Katuga akapinga hilo na kuiomba mahakama wapewe tena muda wa kumuhoji shahidi huyo, akisema analeta mambo mapya kwani awali hakusema masuala ya kufungiwa kwa chama.)

    Lissu: Kuhusu chama?

    Heche: Hakikupokea mwaliko pia.

    (Wakili Katuga akasimama tena akisema Heche hakusema hivyo, kwani awali alijibu kuhusu kuitwa kwa chama kuwa "hakumbuki". Majaji wakarudia kusoma kumbukumbu ya majibu ya John Heche.)

    Lissu: Shahidi, umesikia ulichojibu? Ulisema barua siyo ya chama. Ulikuwa na maana gani? Fafanua.

    Heche: Ilikuwa addressed kwa chama.

    Lissu: Uliulizwa kuhusiana na chama kualikwa bungeni Dodoma kwenda kutoa maoni kuhusu mabadiliko ya sheria ya uchaguzi wa rais, wabunge na madiwani. Pia ukaulizwa kuhusu kifungu cha 6 cha sheria hiyo na kama kimewaweka wakurugenzi kusimamia uchaguzi. Ulikuwa na maana gani katika majibu yako?

    Heche: Waheshimiwa majaji, bado watumishi wa umma ndio wanasimamia uchaguzi. Mapendekezo yetu yalikuwa tume iwe na watumishi wake kuanzia ngazi ya juu hadi chini, siyo watumishi kutoka serikalini.

    Lissu: Uliulizwa kuhusu Thabo Mbeki Foundation. Ulisema ni taasisi ya kimataifa, ukasema ndiyo. Wafafanulie majaji hii habari ya Thabo Mbeki Foundation kuwa taasisi ya kimataifa.

    Heche: Kwa sababu inafanya kazi katika nchi zaidi ya moja, kwa hiyo ni taasisi ya kimataifa.

    Lissu: Waheshimiwa majaji, nimemaliza.

  2. Hujambo na karibu katika matangazo yetu mubashara kuhusu kesi ya uhaini inayomkabili kiongozi wa Chadema, Tundu Lissu.

  3. Lissu ataka kuteta na IGP, DCI na CDF kabla ya ushahidi

    Mashahidi

    Lissu: Jana uliulizwa na wakili ignas Mwinuka kama matukio ya fomu na kuenguliwa wewe ukasema haukuenguliwa, ukasema ujazajibwa fomu ni moja ya vigezo vyenye shida kwenye uchaguzi, fafanua.

    Heche: Hili suala la ujazaji fomu, ni sehemu inayotumika kuengua wagombea hasa wa upinzani.

    Lissu: Uliulizwa kuhusu masuala ya ujazaji fomu na kuenguliwa kwa wagombea.

    Heche: Uchaguzi niliochaguliwa haukuwa huru na wa haki sababu ulikuwa na mauaji pia kuenguliwa kwa wagombea wengine.

    Vilevile kubugudhiwa na polisi kama kawaida mawakala wetu walienguliwa.

    Lissu: Usiende mbali kaka.

    Heche: Sawa

    Lissu: Unakumbuka uliulizwa swali la mimi kushambuliwa na kupelekwa Nairobi kwa matibabu na kama unakumbuka makamu wa rais wakati huo aliwenda kuniona Nairobi ukasema aliwenda kwenye mkutano kisha hospitali fafanua.

    Heche: Ni kweli alikwenda kwenye mkutano na kisha kwenda hospitali kumuona mheshimiwa Lissu.

    Lissu: Uliulizwa suala la mafao yangu nikiwa hospitalini swali likawa kama nilikupa jukumu la kufuatilia mafao yangu na jibu lilikuwa ulikuwa kwenye kamati ya kufuatilia jambo hilo fafanua.

    Heche: Wakati mh Lissu anatibiwa nje waheshimiwa kulikuwa na kamati ya kufuatilia matibabu yake tuliongea na spika na katibu wa bunge wakati huo hawakuwahi kulipia matibabu yake.

    Lissu: Uliulizwa maswali juu ya Tume ya Chande na kama chadema tulikuwa na imani na Tume hiyo na ukasema hapana hatukuiamini ukasema mliamini italinda mauaji na wauaji.

    Heche: Hatukuwa na imani nayo sababu tuliamini itaficha ukweli na kusafisha watu waliohusika.

    Lissu: Katuga alikuuliza sana juu ya michango ya chama tone tone na michango mingine uliyopokea ya tone tone umepeleka wapi ukasema suala la michango kwa chama sio suala makamu mwenyekiti ulikuwa na maana gani?

    Heche: Suala michango ya aina yoyote ya kichama inapita kwenye account rasmi za chama kwa hiyo haiwezekani makamu mwenyekiti akahusika na masuala ya fedha za chama.

    Lissuk: Kwenye masuala hayohayo ya chama ya pesa za michango uliulizwa juu ya mtu anaitwa Salman na mwingine anaitwa Nilesh ukaambiwa kwenye account yako umewekewa milioni 30 na hao watu hebu fafanua.

    Katuga: Sasa hapo si alishajibu siwajui anafafanua nini hauhitajiki ufafanuzi wa jibu sifahamu.

    Lissu: Waheshimiwa majaji wakili wa serikali mkuu hawezi kutabiri jibu la shahdi kabla shahidi hajajibu hiyo objection ni ya wakili anayeanza kazi jana na sio wakili wa serikali mkuu.

    Heche: Waheshimiwa majaji nilipewa karatasi imeandikwa miamala kwenye akaunti yangu mwaka 2024 hata sijawa makamu ni karatasi fabricated ya AI.

    Katuga: Alichoulizwa na yeye anachojibu kitu kingine.

    Jaji: Fafanua.

    Heche: Siwajui hao watu sijui na hizo pesa.

    Lissu: Ulionesha video fulani.

    Heche: Sahihi

    Lissu: Na ulipoulizwa kama inakuonesha wewe na yanayosikika ulisema sauti inaelekea kama ya kwako lakini hukumbuki kutoa hotuba ya hivyo.

    Heche: Nilikuwa na maana kwamba hotuba kama hizo zinaweza kutengenezwa kwa kutumia akili mnemba nafikiri ndio AI.

    Lissu: Unakumbuka uliulizwa juu ya magari yako ya bei mbaya ukasema una magari mawili baadaye zikatolewa karatasi una magari matano uliposema mawili ulifafanua.

    Heche: Nilimaanisha nina magari mawili Prado na Hilux ndizo ninazo tumia maana alimaanisha ndio ya bei mbaya.

    Lissu: Uliulzwa kuhusu kukamatwa kwako nje ya mahakama hii ukaambiwa unasafirishwa kwenda Tarime sababu tulitoka nje ya nchi bila utaratibu na badala yake ukapelekwa Mtumba Dodoma na hukushtakiwa na passport yako ukarudishiwa.

    Heche: Ndio.

    Lissu: Walikuuliza mawakili hapa ulikwenda Kenya ukasema hapana hebu fafanua nini kilitokea.

    Heche: Nilipokamatwa hapo nilikamtwa kwa kuvuka mpaka bila utaratibu ndicho nilichoambiwa central police baadaye nikapelekwa polisi Mtumba.

    Jaji: Umemuelewa mshtakiwa?

    Heche: Nilizuiliwa na uhamiaji mpakani waheshimiwa majaji.

    Lissu: Uliulizwa kwamba unajua asilimia sabini ya watu waliokamatwa kwa sababu ya vurugu za Oktoba walikutaja wewe kuhusu kuratibu ukasema hujui fafanua ulimaanisha nini.

    Heche: Nilikuwa ndani tangu tarehe 22/10 kwa vyovyote siwezi kuwa nimehusika.

    Lissu: Uliulizwa maswali mengi juu ya kuhusika kwenye matibabu yangu ukaulizwa kabla serikali ilipe si lazima ipate referal na ijiridhishe kabla ya kulipia matibabu kasema uko sahihi na hauko sahihi.

    Heche: Kuna mazingira yanaweza kusababisha mtu akatibiwa bila kufuata utaratibu wa kawaida.

    Lissu ukaulizwa mbunge lazima apate referal ndio atibiwe nje ukasema sio lazima.

    Heche: Mbunge yuko mahututi sio lazima apate referal.

    Kabla kesi kuahirishwa Lissu ameiomba mahakama kuzungumza na mashahidi wake, Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP) Camilius Wambura, Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI) Ramadhan Kingai, pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF) Jenerall Jacob John Mkunda.

    "Naomba wale mashahidi wangu kesho waje niongeeee nao tupange wanakuja kuongea nini maana ni lazima tuongee". Alisema

  4. Katuga v Heche: Kuchoma vituo vya kupigia kura ni njia ya kuzuia uchaguzi?

    Lissu

    Katuga: Waambie majaji kama kuchoma vituo vya kupigia kura ni njia ya kuzuia uchaguzi.

    Heche: Sio njia

    Katuga: Kwa hiyo kuchoma vituo hakuwezi kuzuia uchaguzi

    Heche: Sijui

    Katuga: Je kuchoma vituo kuchoma mwendokasi na kuharibu majengo kunaweza kuvunja amani

    Heche: Sijui

    Katuga: Waambie majaji siku ya kupiga kura kama kuna fujo inaweza kuzuia uchaguzi au la

    Heche: Unataka maoni yangu

    Jaji: Rudia Swali

    Katuga: Waambie majaji kama fujo siku ya uchaguzi inaweza kuzuia upigaji kura

    Heche: Sijui

    Katuga: Waambie majaji kama kukata watu vidole kunaweza kuwatisha watu wasiende kupiga kura

    Heche: Sijui

    Katuga: Katika ushahidi wako ulieleza hapa mahakamani umeeleza mlipanga nini kifanyike

    Heche: Nilieleza tulitembelea viongozi wa dini na Jaji Warioba

    Katuga: Waambie majaji tulipanga kuzuia uchaguzi kwa kumtembelea Jaji warioba.

    Heche: Sahihi

    Katuga: Waambie majaji mlipanga kuzuia uchaguzi kwa kumetembelea sheeihk Ponda

    Heche:Sahihi

    Katuga: Je ni kweli au sio kweli ni uasi sio uasi juu ya tume ya uchaguzi

    Heche: Sio kweli

    Katuga: Vituo vya kupigia kura vina zimamiwa na nani

    Heche: Sijui

    Katuga: Kwa hiyo ukichoma kituo cha kura unakuwa umefanya kisa dhidi ya nani

    Heche: Sijui

    Katuga: Ulisema tume ya jaji chande haikuwahi kukuita hata kidogo

    Heche: Nilisema Jana

    Katuga: Ulisema pia kwamba tume haijawHi kuita chama chenu Chadema

    Heche: Sina taarifa

    Katuga: Hujajua taarifa inaweza kutoka kupitia gazeti la serikali

    Heche: Sijui

    Katuga: Waambie majaji kwamba tume ya jaji chande ilitangaza kwenye gazeti la serikali kuna watu wanazuia wengine kutoa maoni mbele ya tume hiyo

    Heche:Sijui

    Katuga: Waambie majaji kwamba uliwahi kuitwa na uka kaidi

    Heche: Sijawahi kuitwa

    Katuga: Waambie majaji kama unajua au hujui tume ilitangaza kupitia mbao mbalimbali za matangazo kuhusiana na machafuko ya october 29

    Heche: Sijui

    Katuga: Unaishi kenya au Tanzania

    Heche: Tanzania

    Katuga: Kwa ridhaa ya mahakama naomba nikupe nyaraka hizi ambazo ni barua toka tume ya uchunguzi ya jaji chande kuelekea kwa bwana John Heche

    Jaji: Mmmmh

    Lissu: Huu sio utaratibu shahidi aoneshwe nyaraka inazodaiwa aliandikiwa utaratibu wa kuonesha shahidi nyaraka uko kwenye kifungu cha 165 cha sheria ya ushahidi naondoa waheshimiwa maji nimechaganya.

    Katuga: Angalia nakala hiyo ni nyaraka ya nini

    Heche: Ni Barua

    Katuga: Kwenda kwa nani?

    Heche: Imeandikwa John Heche

    Katuga: Waambie kichwa cha habari cha barua hiyo kinahusu nini

    Heche: Anasoma..,yahusu kuwasilisha taarifa kwenye tume ya uchunguzi mwa matukio ya october 29

    Katuga: Imeandikwa kwa nani.

    Heche: Sijui , Mimi Naitwa John Wegesa Heche

    Katuga: Waambie majaji kama sanduku hilo la posta ni la Chadema.

    Heche: Ni la Chadema.

    Katuga: Ni ya tarehe ngapi?

    Heche: Desemba 20/2025

    Katuga: Waambie majaji hiyo barua imesainiwa na nani?

    Heche: Anasoma inaonesha imesainiwa na mtu anaitwa honorious Njoya.

    Katuga: Ni kweli sio kweli ilikutaka kwenda kuwasilisha taarifa kwa tume?

    Heche: Ndivyo ilivyoandikwa.

    Katuga: Kwa ridhaa ya mahakama nikuoneshe hii barua ya pili, samahani waheshimiwa naomba nimuoneshe barua nyingine.

    Heche: Hii ni Barua.

    Katuga: Inatoka wapi?

    Heche: Kwenye tume ya kuchunguza matukio ya kabla na baada ya uchaguzi.

    Katuga: Hiyo Barua ilikuwa inaenda kwa nani

    Heche:John Wegesa Heche Makamo mwenyekiti Chadema

    Katuga: Hiyo barua ilimtaja Heche kufanya nini?

    Heche: Kukutana na Tume

    Katuga: Na yenyewe imesainiwa na nani?

    Heche: Honorious Katibu wa Tume

    Katuga: Naomba nimuoneshe shahidi barua nyingine, iangalie hii barua shahidi na uwaambie majajai inatoka wapi?

    Heche: Ya kuchunguza matukio ya baada ya uchaguzi.

    Katuga: Waambie majaji nani alikuwa anapokea hizi barua?

    Heche: Ulikuwa ni wito

    Katuga: Hizo barua mbili ungependa zitolewe hapa mahakamani sababu ndio wewe mshitakiwa

    Heche: hapana siko tayari.

    Katuga: Unajua kwamba kwa alikuwa anakabidhiwa nani hizo barua

    Heche: Katibu Mkuu

    Katuga:Waheshimiwa majaji naomba nimuoneshe barua ya mwisho,

    waambie majaji inahusu nini.

    Heche: Taarifa kwa umma tume ya uchunguzi.

  5. Heche anaendelea kujibu maswali ya dodoso

    Heche

    Katuga: Waambie majaji kama moja ya malalamiko yenu, kwamba tume ya uchaguzi ndiyo ina mamlaka ya kupanga majimbo.

    Heche: Tume huru siyo hiyo unayoitaja wewe.

    Katuga: Waambie majaji, unajua au hujui ni nani anayepanga majimbo ya uchaguzi?

    Heche: Ni waziri.

    Katuga: Kwa ridhaa ya mahakama hii tukufu tusomee ibara ya 75 (3) ya Katiba.

    Heche akasoma ibara hiyo ambayo inahusiana na ugawaji wa majimbo ya uchaguzi

    Katuga: Wasomee hiyohiyo 75 (4)

    Heche akasoma tena.

    Katuga: Ni kweli kwamba kwa mujibu wa ulichosoma tume inaangalia idadi ya watu ikitaka kugawa jimbo?

    Heche: Ibara ya 74

    Katuga: Tuambie, ni wewe au siyo wewe uliyeiambia mahakama tukufu kwamba hotuba ya mwenyekiti hakutoa njia ya kuzuia uchaguzi.

    Heche: sijui

    Katuga: Ni haki au si haki kwa aliyehamasika na hotuba hiyo kutumia njia yoyote kuuvurga uchaguzi?

    Heche: Sijui

    Katuga: Ni haki kwa yoyote kufanya lolote ili kuweza kukinukisha?

    Heche: Sijui

    Katuga: Waambie majaji kama kuchoma vituo vya kupigia kura ni njia mojawapo ya kuzuia uchaguzi au siyo njia moja wapo?

    Heche: Sijui

    Katuga: Waambie majaji, kama kuanzisha fujo, kuchoma vituo, majengo, mwendokasi, mafuta kunaweza kuvunja amani?

    Heche: Sijui.

    Katuga: Waambie majaji kama kuna fujo ambayo haiwezekani kuwa contained inaweza au haiwezi kuzuia kupiga kura?

    Heche: Sijui.

    Katuga: Waambie majaji kama kukata watu vidole waliopiga kura, kunaweza kuwatisha watu wengine wasiende kupiga kura.

    Heche: Sijui.

    Katuga: Waambie waheshimiwa majaji, kama katika ushahidi wako, ulieleza hapa mahakamani kwamba hii nia ya kuzuia uchaguzi tulikuwa tunafanya hivi...

    Heche: Nilieleza vizuri sana.

    Katuga: Kwamba mipango kufanya uchaguzi kwa kumtembelea jaji Warioba?

    Heche: Ni sahihi.

    Katuga: Mlipanga kuzuia uchaguzi kwa kumtembelea sheikh ponda?

    Heche: Ni sahihi.

    Katuga: ni kweli au si kweli, kuchoma vituo vya kupigia kura ni uasi dhidi ya tume ya uchaguzi?

    Heche: Siyo kweli.

    Katuga: Tupe tafsiri ya uasi

    Heche: Kukataa mfumo mbovu, kukataa wizi wa kura.

    Katuga: Vituo vya kupigia kura vinasimamiwa na nani?

    Heche: Sijui.

    Katuga: Vinasimamiwa na nani?

    Heche: Na tume.

    Katuga: Ukichoma kituo cha kupigia kura, unakuwa umefanya kosa dhidi ya nani?

    Heche: Dhidi ya Tume.

    Katuga: Ulisema kwenye ushahidi wa msingi kwamba tume ya chande haikuwahi kukuota hata kidogo?

    Heche: Nilisema jana.

    Katuga: Ulisema tume hiyo haijawahi kabisa kuita chama chenu?

    Heche: Sikusema hivyo, nilisema sina kumbukumbu ya kuitwa kwa chama chetu.

    Katuga: Unajua au hujui kama moja ya njia ya serikali kutangaza taarifa ni kupitia gazeti la aserikali

    Heche: Sijui.

    Katuga: Unajua au hujui kama tume ya jaji chande ilisema kwenye gazeti la serikali kwamba kuna watu wanawazuia wengine kwenda kutoa maoni kwenye tume hiyo?

    Heche: Sijui.

    Katuga: Unajua au hujui kama uliitwa na tume ya jaji chande ukafafanue baadhi ya kauli zako?

    Heche: Sikuwahi kuitwa?

    Katuga: Waambie majaji kama unajua au hujui kama tume ilitangaza kupitia platforms mbalimbali kwa watanzania wote kwenda kutoa maoni kuhusu matukio ya oktoba 29.

    Heche: Sijui.

    Katuga: na wewe unasema unaishi wapi?, Tanzania au Kenya?

  6. Wewe uliendeleza nia ya kuzuia uchaguzi mkuu, Wakili Katuga ambana Heche

    Heche

    Katuga: Ni kweli au si kweli, baada ya mshtakiwa kukamatwa kwa kesi hii, wewe uliendeleza nia ya kuzuia uchaguzi mkuu, ni kweli au siyo kweli?

    Heche: Niliendeleza msimamo wa no Reforms No Election

    Katuga: Ni kweli au si kweli wewe uliendeleza nia ya kuzuia uchaguzi

    Heche: Hicho unachouliza siyo kweli.

    Wakili Katuga: Unakumbuka au hukumbuki kupitia vyombo vya habari uliwahi kutangaza uchaguzi wa 2025 hautofanyika?

    Heche: Sikumbuki .

    Katuga: Unakumbuka au hukumbuki kwamba ulieleza katika kuzuia uchaguzi mlionana na watu mbali mbali wa dini?

    Heche:Sikumbuki

    Katuga: Sema kama ulieleza kwamba mliwatembelea viongozi wa dini.Nilieleza waeleze majaji kama kuna ufanano je ushahidi wa kuwatembelea viongozi wa dini na huu uliotoa hapa mahakamani unafanana au haufanani

    Heche: Mimi sikumbuki.

    Katuga:Unakumbuka au hukumbuki, uliutangazia umma wa watanzania kupitia EA radio kwamba siyo tu chadema hawatashiriki bali uchaguzi hautafanyika.

    Heche: Nilishakwenda pale maranyingi, sikumbuki.

    Katuga: Upo tayari kukumbushwa?

    Heche: Sipo tayari. (Wakili katuga akaomba mahakama imkumbushe Heche kwa ushahidi huo wa sauti akiwa East Africa Radio (EA radio)

    Lissu akasimama na kutaka wakili wa serikali asiruhusiwe kufanya anachotaka kufanya yaani kuthibitisha maneno yake kwa njia ya sauti. Huku Lissu akirejea kifungu husika cha 177 (1) na 2 cha sheria ya ushahidi) akisema jambo hilo haliwezekani.

    Majaji wakasema kwamba akumbushwe na asikilizishwe sauti hiyo.

    Katuga: Waambie majaji hiyo nyara, hicho ukichosikia, je kina ushahidi wowote unaofanana na ushahidi wa msingi ulioutoa?

    Heche: Sahihi.

    Katuga: Ni kweli hiyo nyaraka inastahili na kwamba mtaonana na watu waliowahi kuwa viongozi?

    Heche: Ni sahihi

    Katuga: Ni sahihi jana ulisema mlionana na Mzee Warioba?

    Heche: Nilisema.

    Katuga: Ni kweli au sio kweli kwamba uliwahi kuzungumza na EAradio?

    Heche: Sikumbuki.

    Katuga: Pamoja na kukumbushwa bado hukumbuki?

    Heche: Sijui sikumbuki.

    Katuga: Waambie majaji ni wewe ulieeleza kwamba ulisikiliza hotuba ya jaji chande yote.

    Heche: Nilieleza jana.

    Katuga: Ulieleza kwamba fujo za Oktoba 29 zililenga kuzuia uchaguzi?

    Heche: Eneo hilo sikumbuki.

    Katuga: Unakumbuka au hukumbuki kwamba hotuba ya jaji chande ilisema fujo zile zilisababishwa na viongozi wa vyama vya siasa waliokuwa na madai mengi ya mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi?

    Heche: Sikumbuki

    Katuga: Unakumbuka ulisema jaji chande alisema askari 16 waliuawa

    Heche: Sina kumbukumbu hiyo.

    Katuga: Unakumbuka jaji chande kama anasema matukio yale yalipangwa na kuratibiwa?

    Heche: Hiyo nakumbuka.

    Katuga: Waambie majaji kama unakumbuka ulisema mpo determined kupitia ushindi uliopewa?

    Heche: Maneno hayo yapo.

    Katuga: Ulisema hakuna makosa ya kuzuia uchaguzi?

    Heche: Nilisema

    Katuga: Kwa uelewa wako mdogo wa sheria, ni sheria ipi inasema hayakuwa makosa kuzuia uchaguzi?

    Heche: Kwa ufahamu wangu.

  7. Heche: Lissu hakutoa maelekezo ya kuhamasisha Uasi

    .

    Wakili Katuga: Waambie majaji, mbali na mwaliko, kama unafahamu au hufahamu kulikuwa na hotuba rasmi aliyoandaliwa mwenyekiti.

    Heche: Sifahamu.

    Wakili Katuga: Mikutano ya CHADEMA huwa inahifadhi kumbukumbu?

    Heche: Siyo yote.

    Wakili Katuga: Nani alikuwa mzungumzaji mkuu?

    Heche: Mwenyekiti wa Chama Taifa.

    Wakili Katuga: Waambie majaji wewe kama wewe ukiongea kwenye huo mkutano?

    Heche: Niliongea.

    Wakili Katuga: Muda gani?

    Heche: Nadhani kama nusu saa, sikumbuki.

    Wakili Katuga: Waambie majaji kama umeiambia Mahakama siku hiyo ya mkutano uliongea nini.

    Heche: Sikumbuki.

    Wakili Katuga: Ulimsikia mwenyekiti akisema tutazuia uchaguzi?

    Heche: Ndiyo.

    Wakili Katuga: Waambie majaji kama mwenyekiti alisema tutahamasisha uasi.

    Heche: Sijasikia.

    Wakili Katuga: Waambie kama alisema mahakamani hakuendeki?

    Heche: Alisema.

    Wakili Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji kama mwenyekiti alisema polisi wanaingiza kura feki.

    Heche: Alisema.

    Wakili Katuga: Unajua au hujui kwamba pamoja na kesi hii, Tundu Lissu anashtakiwa kwa kutoa taarifa za uongo mtandaoni?

    Heche: Sijui.

    Wakili Katuga: Waambie majaji unajua au hujui kwamba mshtakiwa kwenye kesi ya Kisutu, katika hoja ya awali, alisema majaji ni ma-CCM?

    Heche: Sijui.

    Wakili Katuga: Unajua au hujui, ushahidi wako huu ulioutoa hapa unaweza kutumika kwenye hiyo kesi?

    Heche: Sijui.

    Wakili Katuga: Waambie majaji kama mwenyekiti aliwaambia au hakakuwaambia njia za kuchukua kuvuruga uchaguzi.

    Heche: Yes, hakutuambia.

    Wakili Katuga: Waambie majaji kama Lissu aliwaambia au hakukuwaambia njia za kuzuia uchaguzi.

    Heche: Hakutuambia.

    Wakili Katuga: Sema kama aliwaambia au hakuwaambia njia za kuhamasisha uasi.

    Heche: Hakutuambia.

    Wakili Katuga: Njia ya kukinukisha je?

    Heche: Hakusema.

    Wakili Katuga: Katika ushahidi wako, waambie majaji kama ulisema mwenyekiti alisema muhamasishe uasi dhidi ya nani?

    Heche: Nilieleza.

    Wakili Katuga: Ni ushahidi wako kwamba uasi ulikuwa uanzishwe dhidi ya Tume ya Uchaguzi?

    Unaweza Kusoma;

  8. Kesi ya Lissu: Heche atetea msimamo wa CHADEMA

    .

    Wakili Katuga: Waambie majaji, ni sheria ipi inayokulazimisha kwamba ukitangazwa mshindi huna uwezo wa kukataa?

    Heche: Wananchi, Waheshimiwa Majaji, siyo sheria. Siijui.

    Wakili Katuga: Wewe ukitangazwa kuwa mshindi, huo uchaguzi hauwi batili?

    Heche: Siyo kweli.

    Wakili Katuga: Ni kweli au siyo kweli uliingia bungeni kwa uchaguzi uliokuwa batili?

    John Heche: Ni sahihi.

    Wakili Katuga: Waambie majaji kama ni kosa au siyo kosa kama huyu mkurugenzi uliyesema alistaafu ukurugenzi wa Tume ya Uchaguzi akaenda kugombea kupitia CCM, je angekuja CHADEMA ingekuwa kosa au siyo kosa?

    Wakili Katuga: Mtu yoyote aliyekuwa mtumishi wa umma, nitakuwa sahihi nikisema ana haki ya kujiunga na chama cha CHADEMA?

    Heche: Ni sahihi.

    Wakili Katuga: The same pia, mtu yoyote aliyemaliza utumishi wake, anaweza kujiunga na chama kingine chochote?

    Heche: Hayo ni maneno yako.

    Wakili Katuga: Umetaja sheria yoyote inayomkataza mtumishi wa umma kutojiunga na CCM baada ya kustaafu?

    Heche: Sijataja.

    Wakili Katuga: Ulisema CHADEMA mlikuwa tayari uchaguzi usogezwe mbele.

    Heche: Sahihi.

    Wakili Katuga: Ulisema ni sheria gani inayoruhusu uchaguzi usogezwe mbele ili kupisha mabadiliko?

    Heche: Sikueleza.

    Wakili Katuga: Ulisema mlienda Nairobi kumuona Raila Odinga. Waambie majaji kama kule pia mlimwambia Raila Odinga mnaenda kuzuia uchaguzi, mnaenda kukinukisha, mnaenda kuzuia uchaguzi, waambie Waheshimiwa Majaji.

    Heche: Tulimwambia matatizo ya uchaguzi. Waheshimiwa Majaji, mambo tuliyoyazungumza ni yaleyale.

    Wakili Katuga: Taarifa zinazotolewa na Brenda Rupia zinakuwa ni maelekezo ya chama au utashi wake binafsi?

    Heche: Katibu Mkuu na ofisi yake ndiyo inamwelekeza kutoa taarifa.

    Wakili Katuga: Mpaka unakuja kutoa ushahidi hapa, ulifanikiwa kusoma mashtaka au hukusoma?

    Heche: Nilisoma.

    Wakili Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji kama kuna sehemu yoyote mshtakiwa anashtakiwa kwa kuandaa mkutano?

    Heche: Sijui.

    Wakili Katuga: Ulisema tuhuma za mshtakiwa za kuwaalika waandishi wa habari siyo za kweli.

    Heche: Sahihi.

    Wakili Katuga: Kuna sehemu mshtakiwa anashtakiwa kwa kuwaalika waandishi wa habari?

    Wakili Katuga: Waambie majaji kama mwenyekiti alitaka au hakutaka hotuba yake iwafikie umma?

    Heche: Siwezi kukumbuka.

    Wakili Katuga: Ni kweli au siyo kweli kwamba tarehe 3 Aprili 2025 kulikuwa na mkutano uliofanyika ndani huku waandishi wa habari wakiwepo?

    Heche: Sikumbuki.

    Wakili Katuga: Mwenyekiti alikuwa na uwezo au hakuwa na huo uwezo wa kuwaondoa au kutoongea mbele ya waandishi wa habari?

    Heche: Mkutano uliandaliwa na sekretarieti. Kwa hiyo sijui.

    Wakili Katuga: Ulimwona au ulimshuhudia akilazimishwa kuongea mbele ya waandishi wa habari?

    Heche: Nimesema sijui.

    Unaweza kusoma;

  9. Heche Akiri: Niliingia bungeni kwa uchaguzi uliokuwa na 'figisu'

    .

    Wakili Katuga: Waambie majaji kama ni ushahidi wako kwamba mshtakiwa alisema hatuko tayari kushiriki uchaguzi wa namna hii, mlipokuwa mkipita kwa wadau?

    Heche: Sahihi.

    Wakili Katuga: Nitakuwa sahihi, nikisema msimamo umekuwa ni kutoshiriki kwenye uchaguzi mpaka mabadiliko yafanyike?

    Heche: sahihi

    Wakili Katuga: Nakumbuka uliiambia Mahakama kwamba Lissu alipokuwa akipita kwa wadau hakuna sehemu alitumia neno kuhamasisha uasi?

    Heche: ni sahihi

    Wakili Katuga: Kama kutakuwa na shahidi alisema hata kwa wadau alitumia neno kuhamasisha uasi, ushahidi huo utakuwa wa uongo au ukweli?

    Heche: Inategemeana na context.

    Wakili Katuga: Hizo shahidi mbili haziko sawa au ziko sawa?

    Heche: Ziko sawa.

    Wakili Katuga: Kwa hiyo ni ushahidi wako kwamba alikuwa anatumia neno tutahamasisha uasi kwa wadau na wewe unasema hajatumia maneno tutahamasisha uasi, haya maneno yako sawa?

    Heche: Nilisema maneno ni hayo hayo lakini context ndizo zinatofautiana.

    Wakili Katuga: Ulisema vyombo vya habari havitoi nafasi sawa kwa wagombea?

    Heche: Ni sahihi.

    Wakili Katuga: Uliiambia Mahakama mengi kuhusu mapungufu ya uchaguzi.

    Heche: Sahihi.

    Wakili Katuga: Ulieleza ni aina gani ya mfumo wa uchaguzi unazuia vyombo vya habari visitoe nafasi sawa?

    Heche: Nilieleza.

    Wakili Katuga: Ulieleza ni sheria ipi inayowaambia waandishi wa habari toeni habari hii na hii msitoe?

    Heche: Kuna upendeleo.

    Wakili Katuga: Umesema kutokana na kutokuwa na usawa wa sheria za uchaguzi, kwamba kuna sehemu mawakala wamekuwa wakipata usumbufu wa viapo unakumbuka?

    Heche: Nilisema.

    Wakili Katuga: Waambie majaji kama ulitaja vituo ambavyo mawakala walizuiwa.

    Heche: Nilisema kwa nchi nzima.

    Wakili Katuga: Unajua au hujui kama ukiposhinda uchaguzi, pia ulituhumiwa kufanya fujo na kuingiza kura feki?

    Heche: Hilo unajua wewe, sijui.

    Wakili Katuga: Unajua au hujui kwamba mwanasiasa akishindwa hakubali kiurahisi?

    Heche: CHADEMA ukishindwa unarudi zako nyumbani.

    Wakili Katuga: Waambie majaji kama wewe ulivyoshindwa ulikubali?

    Heche: Uchaguzi haukuwa huru na haki, nilipoteza.

    Wakili Katuga: Ulishinda ubunge mwaka gani?

    Heche: 2015.

    Wakili Katuga: Uchaguzi wa 2015 ulikuwa huru na haki?

    Heche: Uchaguzi wa 2015 ulikuwa na figisu.

    Wakili Katuga: Uchaguzi wa 2015 uliochaguliwa uliukubali au uliukataa?

    Heche: Niliukubali kwa vita, japo ulikuwa na makosa mengi.

    Wakili Katuga: Ulikuwa wa uhuru na haki au haukuwa huru na haki jimboni kwako wewe?

    Heche: Haukuwa huru na haki.

    Wakili Katuga: Waambie majaji kama wewe ni mtu wa haki kama unavyojiita, waambie majaji ulikuwa na uwezo wa kuukataa ushindi wako au ulikuwa huna?

    Heche: (Heche akawa mbishi, majaji wakamweleza kwamba anaulizwa yeye kwa nafasi yake.)

    Wakili Katuga: (Wakili Katuga akarudia swali.)

    Heche: Nilikuwa sina uhuru.

    Unaweza kusoma;

  10. Hujambo. Haya ni matangazo yetu ya moja kwa moja ya leo, tarehe ni 15 Septemba 2026

    Hujambo. Haya ni matangazo yetu ya moja kwa moja ya leo, tarehe ni 15 Septemba 2026.

    Yaliyojiri jana kwa ufupi ni kwamba shahidi Godbless Heche aliendelea kuhojiwa na Wakili wa Serikali Simon Katuga katika kesi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu.

    Leo usikilizwaji unaendelea kwa maswali ya Wakili Katuga kwa shahidi Godbless Heche. Karibu.

  11. Katuga ambana Heche kuhusu mipango ya matukio ya Oktoba 29

    .

    Wakili Katuga: Waambie majaji, ile Prado ni ya shingapi?

    Heche: Milioni 80.

    Wakili Katuga: Na trekta?

    Heche: Milioni 80.

    Wakili Katuga: Ile Mitsubishi?

    Heche: Milioni 60.

    Wakili Katuga: Ulinunua ukiwa nani?

    Heche: Makamu Mwenyekiti.

    Wakili Katuga: Ni kweli kwamba kwa kipindi chote tangu umekuwa Makamu Mwenyekiti, hakuna fedha yoyote ambayo umelipwa?

    Heche: Na nani?

    Wakili Katuga: Waambie majaji, ni kweli ulieleza kwamba mdogo wako anaitwa Suguta?

    Heche: Suguta.

    Wakili Katuga: Wakati anakamatwa na polisi ulikuwepo?

    Heche: Sikuwepo.

    Wakili Katuga: Wakati ulisema alichomwa na singe ulikuwepo?

    Heche: Alisema RPC.

    Wakili Katuga: Ulikuwepo hukuwepo? Kwahiyo ni ushahidi wa RPC?

    Heche: Sahihi.

    Wakili Katuga: Waambie majaji kama huyu mdogo wako alichomwa na singe eneo gani la mwili?

    Heche: Sikueleza.

    Wakili Katuga: Umesema polisi walijaribu kumtupa mdogo wako ila walinzi walimuona?

    Heche: Ni kweli.

    Wakili Katuga: Waambie majaji kama ulikuwepo.

    Heche: Sikuwepo.

    Wakili Katuga: Huo ushahidi ulinetoa wapi?

    Heche: RPC alieleza.

    Wakili Katuga: Ni ushahidi wa RPC?

    Heche: Wakwangu.

    Wakili Katuga: Uliwahi kuhojiana na huyo polisi aliyemuua mdogo wako?

    Heche: Ni sahihi.

    Wakili Katuga: Alikueleza sababu za kufanya hilo tukio la kinyama? Kama alilenga kukuzuia wewe kwenye harakati za kisiasa.

    Heche: Hakusema hivyo.

    Wakili Katuga: Sababu za huyu bwana kutuhumiwa kufanya huo ukatili zimebaki kwa huyo mtuhumiwa, hapa Mahakamani hakuna?

    Heche: Ni sahihi.

    Wakili Katuga: Unajua au hujui, kwenye jinai, sababu za kumfanya mtu aachiliwe ni ushahidi?

    Heche: Kuna rushwa, upendeleo, sababu ni nyingi.

    Wakili Katuga: Umeiambia Mahakama hii tukufu kati ya hayo uliyosema ni sababu ipi ilipelekea huyu bwana polisi aachiliwe?

    Heche: Ni upendeleo ndiyo uliyemwachia.

    Wakili Katuga: Ulisema wewe unaamini kwamba waliomfanyia ukatili mdogo wako kwa kumuua, walikukomoa na kukuonyesha kwamba wanaweza kukufanyia chochote na wasifanywe chochote, huu ni ushahidi wa kuona, kusikia au imani?

    Heche: (Hajajibu)

    Wakili Katuga: Ana wazazi?

    Heche: Ndiyo.

    Wakili Katuga: Ni kweli kwamba uchungu wa mwana aijuaye mzazi?

    Heche: Ndiyo.

    Wakili Katuga: Kati ya wewe na mama yako aliyebeba ujauzito miezi tisa, nani anauchungu zaidi?

    Heche: Hilo la mama kumuuliza yeye.

    Wakili Katuga: Kwanini hukuiambia Mahakama kwamba huyu muuaji alitaka kumkomoa mama yako ila akataka kukukomoa wewe?

    Heche: Alitaka kunikomoa.

    Wakili Katuga: Kwahiyo wewe ndiye ulimsababishia kifo kwa sababu aliuliwa ili wewe utishike?

    Heche: Alitaka niache siasa ndiyo maana akauliwa.

    Wakili Katuga: Ulitokea mwaka gani?

    Heche: 2018.

    Wakili Katuga: Mwaka 2018 unakumbuka mambo ya siasa yalikuwa yamefungwa?

    Heche: Nilikuwa mbunge, zilikuwa zinaendelea.

    Wakili Katuga: Unakumbuka Magufuli alizuia siasa?

    Heche: Alizuia mikutano ya hadhara, siyo siasa.

    Wakili Katuga: Kwahiyo huyu polisi alimuua mdogo wako kukuzuia wewe kufanya siasa bungeni?

    Heche: Popote.

    Wakili Katuga: Wewe ni mjumbe wa Kamati Kuu?

    Heche: Sahihi.

    Wakili Katuga: Kikao cha tarehe 29/08/2026 ulihudhuria au hukuhudhuria?

    Heche: Mpaka nilifresh.

    Wakili Katuga: Kwahiyo unakumbuka vitu vya mwaka 2015 lakini vya 2026 haukumbuki? Heche: Baadhi nakumbuka baadhi sikumbuki, siyo vyote.

    Wakili Katuga: Naibu Katibu Mkuu alisema tarehe 29/08/2026 kwamba kulikuwa na kikao cha Kamati Kuu na kilikusanya tonetone, ni kweli Kamati Kuu ilikaa?

    Heche: Mwulize yeye, sikumbuki.

    Wakili Katuga: Kuna kikao kilichokaa kikamueleza Golugwa aseme tonetone imefika milioni 302?

    Heche: Sijui.

    Wakili Katuga: Unakumbuka au hukumbuki the same day unaletewa taarifa ya makusanyo ya tonetone na Naibu Katibu Mkuu alitoa maazimio, unakumbuka?

    Heche: Wewe ni mjumbe wa Kamati Kuu? Si kweli.

    Wakili Katuga: Kwahiyo taarifa ya Naibu Katibu Mkuu siyo taarifa ya Kamati Kuu?

    Heche: Si kweli.

    Wakili Katuga: Taarifa ya Naibu Katibu Mkuu ya kumtetea mwenyekiti wa chama kwa nguvu zote ni sahihi au siyo sahihi?

    Heche: Siikumbuki hiyo taarifa.

    Wakili Katuga: Uliwaambia majaji Ezekiel Wenje alinusurika kuuawa na akakimbilia Kenya?

    Heche: Ni kweli.

    Wakili Katuga: Wakati ananusurika ulikuwepo?

    Heche: Sikuwepo.

    Wakili Katuga: Ni aina gani sasa ya ushahidi huo?

    Heche: Nilielezwa.

    Wakili Katuga: Uliieleza mahakama ili ione huo ni ushahidi wa kweli?

    Heche: Sikuieleza.

    Wakili Katuga: Tunapomwita mtu mzalendo, ni yule ambaye anafanya kitu cha kizalendo kwenye nchi yake mama?

    Heche: Sahihi.

    Wakili Katuga: Mzalendo siyo mtu ambaye atahamasisha kuharibu nchi yake?

    Heche: Upo sahihi.

    Wakili Katuga: Mzalendo siyo mtu anayehamasisha uharibifu wa mali za umma?

    Heche: Ni sahihi.

    Wakili Katuga: Mzalendo wa kweli ni yule anayehamasisha shughuli za ujenzi wa taifa lake?

    Heche: Wapo wanaofanya hivyo halafu siyo wazalendo.

    Wakili Katuga: Mtu mzalendo ni yule anayehamasisha familia kufanya shughuli za maendeleo ya nchi yake?

    Heche: Siyo lazima.

    Wakili Katuga: Unajua au hujui Tanzania hatuna uraia pacha?

    Heche: Naelewa.

    Wakili Katuga: Unajua au hujui Mwenyekiti wako familia yake (watoto) siyo raia wa Tanzania?

    Heche: Sijui.

    Wakili Katuga: Unajua mke wake si raia wa Tanzania?

    Heche: Sijui.

    Wakili Katuga: Ulisema ulikamatwa nje ya Mahakama kwa tuhuma za kuvuka mpaka kwenda Kenya?

    Heche: Ndiyo.

    Wakili Katuga: Waambie majaji, je ni kweli ulivuka kwenda Kenya au hukuvuka?

    Heche: Sikutaka.

    Wakili Katuga: Ulitaka au hukutaka kwenda Kenya kupitia Sirali?

    Heche: Nilitaka.

    Wakili Katuga: Umeeleza hapa Mahakamani kwanini ulizuiliwa?

    Heche: Sikueleza.

    Wakili Katuga: Ulisema ulisafirishwa hadi Dodoma Kituo cha Polisi Mtumba selo ya peke yako, waambie majaji ulitaka uwekwe na nani? Na wewe ni mwanaume?

    Heche: Ukisema kuwekwa na nani una maana gani?

    Wakili Katuga: Katika kukamatwa kwako, uliwahi kuchukuliwa paspoti yako au hukuwahi?

    Heche: Niliwahi.

    Wakili Katuga: Lini ulichukuliwa?

    Heche: Tarehe 18/10.

    Wakili Katuga: Mwaka gani?

    Heche: Mwaka jana.

    Wakili Katuga: Ulirudishiwa?

    Heche: Ndiyo.

    Wakili Katuga: Ilikuwaje?

    Heche: Niliandika barua kwa Kamishna Jenerali, wakanirudishia.

    Wakili Katuga: Unajua au hujui DPP na Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai wanasimamia jukumu la kuratibu upelelezi wa makosa ya jinai?

    Heche: Sijui.

    Wakili Katuga: Kama hujui, ni kosa gani kisheria kuwakutanisha mawakili wa serikali na polisi?

    Heche: Sijui.

    Wakili Katuga: Unajua au hujui, ulisema ulikutana nao Kituo cha Polisi Oysterbay?

    Heche: Sahihi.

    Wakili Katuga: Waambie majaji, unajua au hujui kwamba kesi ya jinai haina ukomo?

    Heche: Sijui.

    Wakili Katuga: Pamoja na yote hakuwahi kushtakiwa, uliulizwa kushtakiwa kwenye matukio ya Oktoba 29 na matukio mengine ukajibu hakuwahi kushtakiwa, sasa unajua au hujui hawa mawakili walikuwa wanaratibu matukio ya Oktoba 29?

    Heche: Sijui.

    Wakili Katuga: Unajua ama hujui watuhumiwa uliowaona pale walikuwa na makosa gani?

    Heche: Sijui.

    Wakili Katuga: Unajua au hujui kama watuhumiwa wengine walikutana na wewe na viongozi wa CHADEMA kama waratibu wa matukio ya Oktoba 29?

    Heche: Sijui.

    Wakili Katuga: Unajua au hujui, ushahidi uliokusanywa unaeleza ni wapi mlikaa vikao, wapi mipango ili kuratibu matukio ya Oktoba 29, 2025?

    Heche: Sijui.

    Wakili Katuga: Ni ushahidi wako kwamba baada ya kuhojiwa kuhusiana na matendo ya kigaidi ulikataa?

    Heche: Sikukataa.

    Wakili Katuga: Maana ya nini?

    Heche: Sikutoa maelezo.

    Wakili Katuga: Ulikataa au hukakataa? Heche: Nilikataa.

    Wakili Katuga: Ulisema ulisikia hotuba ya Jaji Chande, ulisikia kauli kwamba matukio yale yalipangwa na kuratibiwa?

    Heche: Nilisikia.

    Wakili Katuga: Unajua au hujui kwenye ushahidi uliokusanywa kama wewe ni mtuhumiwa wa uratibu wa matukio yale?

    Heche: Mimi ni mshtakiwa au mtuhumiwa?

    Wakili Katuga: Ulipatikana ushahidi kwamba wewe ulihusika kupanga na kuratibu matukio ya Oktoba 29, hotuba ya Chande ilisema yalipangwa na kuratibiwa sasa hivi vitu ni sawa au tofauti?

    Heche: Sijui.

    Wakili Katuga: Nilikusikia ukisema hujui au huna kumbukumbu kama kuna viongozi wengine wa vyama vya siasa waliwahi kushtakiwa?

    Heche: Ndiyo.

    Wakili Katuga: Unamfahamu Zitto Kabwe?

    Heche: Ndiyo.

    Wakili Katuga: Ni wa chama gani?

    Heche: ACT Wazalendo.

    Wakili Katuga: Unajua au hujui kama Zitto Kabwe aliwahi kushtakiwa kwa kuchapisha taarifa za uongo?

    Heche: Sijui.

    Wakili Katuga: Kwahiyo uliamua tu kusema?

    Heche: Nilisema viongozi wa CCM.

    Wakili Katuga: Basili Pesambili unamfahamu humfahamu?

    Heche: Basili namfahamu.

    Wakili Katuga: Unajua kama aliwahi kuwa waziri?

    Heche: Sifahamu.

    Wakili Katuga: Alafu unasema umewahi kuwa mbunge, tuambie kama unafahamu amewahi kushtakiwa?

    Heche: Sifahamu hilo.

    Wakili Katuga: Waambie majaji ile Hotel Dubai ulilala kwa shilingi ngapi?

    Heche: Ipi? Dubai nimeenda mara nyingi.

    Wakili Katuga: Waambie majaji, hapa nchini kwetu ili uende kutibiwa nje lazima uwe na referral ya hospitali zetu?

    Heche: Kuna mtu anaamua tu kwenda nje.

    Wakili Katuga: Waambie majaji kwa anayelipwa na serikali, ni lazima atimize wajibu au anaamua tu kwenda nje?

    Heche: Lazima atimize yanayotakiwa.

    Wakili Katuga: Kwahiyo mlipaji wa gharama za serikali, lazima ajiridhishe kwamba mtu huyo anakidhi vigezo vya referral ili aende nje? Kweli si kweli?

    Heche: Nchi hii kuna upendeleo, siyo lazima.

    Wakili Katuga: Unajua au hujui Mwenyekiti alipata referral kwenda nje au hujui?

    Heche: Sijui.

    Wakili Katuga: Ulisema Lissu alivuliwa ubunge.

    Heche: Ndiyo.

    Wakili Katuga: Unajua au hujui kama Lissu hakuridhika na maamuzi ya Spika, anaweza kwenda kupeleka shauri Mahakamani kwenda kupeleka pingamizi?

    Heche: Najua.

    Wakili Katuga: Unajua au hujui kama Lissu alipeleka shauri Mahakamani?

    Heche: Sijui

    Wakili Katuga: umesema no reforms no election ilitangazwa na Mbowe

    Heche: Sahihi

    Wakili Katuga: Waambie majaji kama, katika ushahidi wako,ulieleza au hukueleza kama mbowe alieleza kwamba tutazuia uchaguzi wa 2025

    Heche: Sikueleza

    Wakili Katuga: Kama alisema watahamasisha uasi

    Heche: Hakusema

    Wakili Katuga: Waambie majaji kama mbowe alielezea suala la kukinukisha?

    Heche: Hakusema

    Wakili Katuga: Waambie majaji kama kwenye huo msimamo kuna maneno kwamba tutazuia uchaguzi

    Heche: Hakuna

    Wakili Katuga: Waambie kama kwenye maneno no reforms no kuna maneno kwamba tunaenda kuhamasisha uasi

    Heche: Hapana

    Wakili Katuga: Je, tunaenda kukinukisha vibaya sana?

    Heche: Inategemeana na context yako na mtu anavyoelewa

  12. Vifo vya Mawazo, Akwilina na Mbwambo vyaibuka kwenye ushahidi wa Heche

    .

    Katuga: Unajua ama hujui Tanzania ni nchi huru

    Heche: Najua

    Katuga Unajua hujui kwa mujibu wa Katiba ya 77 Mahakama ndio chombo kinachotoa haki

    Heche: Najua

    Katuga: Unajua Mahakama haitakiwi kuingiliwa

    Heche: Najua

    Katuga: Unaimani na hii Mahakama

    Heche: Kesi haijaamulIwa siwezi sema nina imani

    Katuga: Waambie Majaji unaiaminini huiamini

    Heche: Naimini

    Katuga: Je ni sahihi kisheria mtu anayekuja kuwa shahidi akamapima dimina ya majaji

    Heche: Sijui

    Katuga: Waambie majaji kama uko hapa baada ya Lissu kuonekakana na kesi ya kujibu

    Heche: Najua

    Katuga: Unajua kwamba ushahidi wa kielectromic ni sawa na document

    Heche: Sifahamu

    Katuga: Waambie majaji kama hotuba zako nyingi ziko mtandaoni

    Heche: Najua

    Katuga: Waambie majaji kama uliwahi kuongelea kesi hii baada ya mshitakiwa kupatikana na kesi ya kujibu

    Heche: Sikumbuki

    Katuga: Waambie majaji kama ulisema dimina ya jaji haiko sawa hata ukimuangalia

    Heche: Sikumbuki

    Katuga: Uko tayari tukusikilizishe

    Heche: Sikuamini kuna AI siku hizi

    Katuga: Waheshimiwa Majaji naomba tumuoneshe fresh memory ili atusaidie kujibu baada ya maswali

    Jaji: Endelea

    Lissu: Huu utaratibu sijaelewa uko kwa sheria gani

    Jaji: Utamfanyia re-examination

    Heche: Siwezi kuamini kompyuta ni Katuga zama hizi za AI waheshimiwa majaji

    Jaji: Wewe sikiliza kisha utafafanua

    Katuga: Hii hotuba unaikumbuka

    Heche: Kwa mbaali sauti kama ni yangu

    Katuga: Unaikumbuka huiumbuki

    Heche: Siiikumbuki

    Katuga: Unakumbuka ulisema shahidi wa 17 yeye ndio amepublish

    Heche: Ndio

    Katuga: Je hilo swala shahidi ya 17 limezungumziwa hapo kwenye video

    Heche: Hiyo video sio yangu

    Katuga: Walau jibu kidogo hayo maneno P17 alisema ndiye alipublish yanafanana ya ushahdi wako hayafanani

    Heche: Nimeyasikia yanafanana kwenye hiyo AI yako

    Katuga: Kuthibitisha na ku-establish premafasheee kesi nini maana yake

    Heche: Sijui maana yake

    Katuga: Waambie majaji kama uliridhika Mahakama Ilipoamua Lissu anakesi ya kujibu uliridhika au hukuridhika

    Heche: Sikuridhika

    Katuga: Uliwahi kuita press kuwasema mashahidi waongo hapo nje

    Heche: Hapana

    Katuga: Tukikuonesha tena utakubali au utaita AI

    Heche: Siwezi kukataa kama ni kitu cha kweli

    Katuga: Lissu anachombo cha habari

    Heche: Hapana

    Katuga: Lissu akitaka kupeleka ujumbe kwa uma anatumia njia gani

    Heche: Anatumia mikutano

    Katuga: Mh Lissu akitaka kupeleka ujumbe kwa watanzania wote anatumia vyombo vya habari

    Heche: Anahutubia mikutano

    Katuga: Kwenye ushahdi wako ulisema mapolisi walikuwa wanaingiza kura feki kwenye vibegi vyao embu waambie majaji kama uliwahi kumkamata

    Heche: Niliwahi kuona askari shule ya Msingi Nyanungu

    Katuga: Ulileta huo ushahidi hapa mahakamani

    Heche: Niliongea general

    Katuga: Na unataka Mahakama ikuamini

    Heche: Ndio

    Katuga: Unajua watu wanatuhuma za mauaji kwa sababu mbali mbali

    Heche: Najua

    Katuga: Katika ushahiri wako umeiambia Mahakama hii Msafiri Mbwambo alichinjwa kwa kulalamikia sheria za uchaguzi

    Heche: Aliuawa sababu ya siasa

    Katuga: Uliwaambia majaji ameuawa sababu ya moja mbili tatu

    Heche: Nilisema sababu ya sababu za kisiasa

    Katuga: Umeeleza ile sababu ya msingi, waambie majaji kama umeelezea sababu yake ya kuchinjwa

    Heche: Nilieleza sababu za kiuchaguzi

    Katuga: Unajua au hujui kuna kesi kwa viongozi wa CHADEMA iko Arusha ya kuteka mtu anaitwa Bariki na Paul Mafie na kuwapandisha mlimani kwa nia ya kuwatesa na kuwatishia unajua au hujui

    Heche: Sifahamu

    Katuga: Unajua mtu yoyote anaweza kushitakiwa kwa jinai

    Heche: Najua

    Katuga: Unajua kusadikika ni hisia

    Heche: Ndio

    Katuga: Ushahadi wako Katibu wenu aliuawa na watu wanaosadikika ni wa CCM

    Heche: Nilisema sababu za kiuchaguzi

    Katuga: Nani anafuatilia viapo vya mawakala Chadema

    Heche: Kila eneo linafuatiliaji wake, mgombea, kiongozi wa chama kulingana na eneo husika

    Katuga: Mwaka 2018 wakati wa kampeni za Jimbo la Kinondoni, alikuwa mgombea ni nani

    Heche: Salum Mwalimu

    Katuga: Ni kweli kwamba siku Akwilina ameuawa mlikuwa mnafunga kampeni

    Heche: Ni kweli

    Katuga: Waambie majaji kama sio kweli jioni baada ya mkutano ilitoka hamasa ya kwenda kwa Mkurugenzi kwa maandamano

    Heche: Sio kweli

    Katuga: Waambie majaji kama uliwaambia majaji mlikuwa watu wa ngapi mkifuata kwenda Magomeni

    Heche: Hapana

    Katuga: Ni kweli kwamba mlikuwa Kundi, ikabidi polisi wa wawatawanye

    Heche: Ndio ni kweli

    Katuga: Wakati mnashitakiwa 2018 ulisema Mwenyekiti alikuwa ameshambuliwa

    Heche: Nilisema Mwenyekiti wetu wa sasa

    Katuga: Ulisema angekuwa ameshambuliwa kwa risasi tungekuwa naye huu ni ushahidi wa aina gani ni ku- assune, kuona au kusikikiii

    Heche: Kuamini

    Katuga: Ulijua muaji wa Alphonce Mawazo

    Heche: Hapana

    Katuga: Waambie Mahakama kama ulijua sababu

    Heche: Ilikuwa uchaguzi

    Katuga: Sasa ulijuaje hizo sababu

    Heche: Sababu ya uchaguzi alikuwa kwenye kampeni

    Katuga: Mtu mwenye ugomvi na Mawazo anaruhusiwa kuua wakati wa uchaguzi

    Heche: Sheria inakuzuia wakati wote

    Katuga: Kwa hiyo huu ushahidi wa Mawazo ni wako au wa kusoma

    Heche: NIlisoma na iljadiliwa Bungeni

    Katuga: Unaawaambia Majaji ushahidi wako ni sababu za Bungeni

    Heche: Ni ushahidi wangu ni sababu za uchaguzi

    Katuga: Waambie majaji hizo sababu za hayo mauaji umetoa wapi

    Heche: Ilijadiliwa kila mahali na hata kuandikwa kwenye vyombo vya habari

  13. "Uliona watu waliomteka? - Katuga Amuhoji Heche kuhusu utekaji

    Katuga: Unaimanini taarifa ya TLS

    Heche: Ndio nina imamini

    Katuga: Taarifa yetu inasema huyu bwana alitoweka tuambie uliona watu watu waliomteka

    Heche: Mtuambie nyie watu wa serikali

    Katuga: Nilikusikia umejitapa utasoma sheria

    Heche: Ndio naanza

    Katuga: Umewataja wengi sana ukiwaunganisha na mambo ya uchaguzi unakumbuka

    Heche: Ndio

    Katuga: Umewaambia majaji kwamba huyu kapotea sababu ya sheria za uchaguzi

    Heche: Hapana

    Katuga: Kila anayepotea anakuwa ametekwa

    Heche: Niliozungumzia mimi ni waliotekwa

    Katuga: Kila ambaye haonekani maetekwa

    Heche: Sikuelewi

    Katuga: Mke wa saimon anaitwa nani

    Heche: Sikumbuki

    Katuga: Iambie Mahakama kuwa ushahidi wa Bwana Simon kutekwa ni wa mke wake umeamiwa na mke wake

    Heche: Sahihi

    Katuga: Waambie majaji kama unajua ushahidi wa kuambiwa haukubaliki Mahakamani

    Heche: Ndio

    Katuga: Uanajua au hujui hata kusoma pia bado inakuwa hear say

    Heche: Sijui

    Katuga: Unajua hujui ushahdi wako lazima ulingane na facts

    Heche: Najua

    Katuga: Waambie majaji kama umetaja ya kesi ya mzee sasi.

    Heche: Sikutaja

    Katuga: Bwana mdogo nani alikupa zawadi ya jezi ya Arsenal yenye jina lako

    Heche: Nmenunua mwenyewe

    Katuga: Hiyo jezi umenunua wapi

    Heche: Ya lini

    Katuga: Na hiii

    Heche: Nimekuambia tuko wengi baba yangu ana wake nane na tuko wengi

    Katuga: Kuna mtu anaitwa Salman una mfahamu

    Heche: Simfahamu

    Katuga: Baada ya kupewa hela kwa ajili ya chama ulipeleka wapi

    Heche: Sifahamu

    Katuga: Ulisema mwaka 2024 Kamati Kuu ilikaa na kujadili bila mabadiliko hamtashiriki uchaguzi

    Heche: Sahihi

    Katuga: Mkurugenzi wa habari aliposema “No Reforms No Election” ilimaanisha kuzuia uchaguzi

    Heche: Naweza kusema kinachonihusu

    Jaji: Naomba usikilize kwa makini ujibu swali

    Katuga:Wewe unaimbia Mahakama No Reforms No Election ni hakuna uchaguzi mpaka mabadiliko na Brenda alisema ilimaanisha kuzuia uchaguzi je kauli hizi ziko sawa au sio sawa.

    Heche: Haziko sawa

  14. Katuga amuhoji Heche kuhusu magari yake

    .

    Katuga: Kwa maneno rahisi wewe ni mwalimu

    Heche: Sahihi

    Katuga: Ulienda moja kwa moja

    Heche: Nilienda chuo cha ualimu diploma kisha nienda tena digrii

    Katuga: Umesoma kwa jina la wegesa chacha suguta

    Heche: Sahihi

    Katuga: Ulipata four form four (Division 4 kidato cha 4)

    Heche: Uongo nilipata 1.11

    Katuga: Mbali ya kuwa makamo mwenyekiti

    Katuga: Umeiambia mahakama kama una kitu kingine cha kuingiza kipato

    Heche: Sikuiambia

    Katuga: Umeiamba Mahakama kama unalipa posho au mshahara

    Heche: Sikuulizwa

    Katuga: Umeiambia

    Heche: Sikuiambia

    Katuga: Una Malori yanafanya kazi Kenya

    Hecha: Sina mimi ni mkulima

    Katuga: Una magari manne ya bei mbaya

    Heche: Nina magari mawili bei mbaya sijui ni kitu gani

    Katuga: Unajua taarifa za umiliki wa magari zinahifadhiwa TRA

    Heche: Ndio

    Katuga: Hizi kadi ni ngapi

    Heche: Tano

    Katuga: Zimesajiliwa kwa majina gani

    Heche: Majina yangu

    Katuga: Mfumo wa TRA unakusoma una vitu vitano

    Heche: Ndio

    Katuga: Kiutaratibu wa chama zile tone tone kiongozi akipokea michango anafanya nini

    Heche: Masuala ya fedha yako chini ya Katibu Mkuu

    Katuga: Unafanya nini

    Heche: Napokeaje pesa

    Katuga: Pesa ulizopokea kwa Nilesh ulifanya nini

    Heche: Simjui huyo mtu

    Katuga: Uliwaaambia majaji ulisoma taarifa ya TLS

    Heche: Ndio

    Katuga: Waambie majaji ilikuwa ya lini

    Heche: Nilisema ya 2026 sikumbuki tarehe

    Katuga: Nimekusikia ukisema taarifa nyinge iliandikwa kwa kingereza

    Heche: Ndio

    Katuga: Na ya TLS iliandikwa kwa kingereza

    Katuga: Ripoti ya TLS

    Katuga: Kuna mtu ulimtaja anaitwa Saimon Kanguye

    Heche: Ndio

    Katuga: Alitekwa lini

    Heche: Kati ya mwaka 2017 hapo

    Katuga: Una fahamu kama kuna matukio ya kijinai ya watu kuwaua watu kwa visasi

    Heche: Sifahamu

    Katuga: Hii taarifa ya TLS ya mwaka 2024 jina la mwisho ni la nani

    Heche: Saimon Kanguye

    Katuga: Umesema ulipata taarifa ya kutekwa kwakwe kwenye vyombo vya Habari. Chombo gani

    Heche: Sikumbuki

    Katuga: Uliwahi kuchunguza Kanguye

    Heche: Familia yake ilisema ametoweka ametekwa

    Unaweza kusoma;

  15. Katuga ahoji wasifu na elimu ya John Heche

    Wakili Nassor Katuga aendelea

    Wakili Katuga: Unajua au hujui kwamba lengo la kukuuliza maswali haya ni kuifanya mahakama ipime uaminifu wa ushahidi wako?

    Heche: Wa uongo au wa ukweli?

    Wakili Katuga: Waambie majaji, ni kweli baba yako anaitwa Charles Heche Suguye?

    Heche: Ndiyo.

    Wakili Katuga: Una elimu gani?

    Heche: Shahada ya Elimu na Sanaa (Bachelor of Arts with Education).

    Wakili Katuga: Wewe ni mwalimu?

    Heche: Ndiyo.

    Wakili Katuga: Uliendaje kusoma shahada hiyo?

    Heche: Nilimaliza A-Level, nikaenda chuo cha ualimu kusoma diploma, kisha baadaye nikaenda chuo kikuu.

    Wakili Katuga: Ni kweli kwamba kuanzia shule ya msingi hadi sekondari ulisoma kwa jina la Wegesa Charles Suguti?

    Heche: Ni kweli.

    Wakili Katuga: Ni kweli kidato cha nne ulipata Division Four ya alama 27?

    Heche: Siyo kweli.

    Wakili Katuga: Ulipata Division ngapi?

    Heche: Division One.

    Wakili Katuga: Ya pointi ngapi?

    Heche: Pointi 11.

    Wakili Katuga: Mbali na kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chadema, umeiambia mahakama kwamba unajiingizia kipato kupitia shughuli gani?

    Heche: Sijaiambia.

    Unaweza kusoma;

    .
  16. Mwinuka ahoji msingi wa madai ya utekaji na tafsiri za ripoti za uchaguzi

    .

    Madai ya kutekwa na kupotea

    Wakili Mwinuka: Wewe binafsi umewahi kushuhudia mtu akitekwa kwa macho yako?

    Heche: Kwa macho yangu sijawahi kushuhudia.

    Wakili Mwinuka: Umewahi kushuhudia mtu akipotea kati ya hao uliowataja?

    Heche: Hapana.

    Wakili Mwinuka: Kuhusu Tume ya Chande ya Oktoba 29, msimamo wa Chadema ulikuwa upi?

    Heche: Msimamo wetu ulikuwa kwamba tume hiyo haikuaminika kwa sababu iliundwa katika mazingira ya kuficha ukweli kuhusu waliohusika.

    Wakili Mwinuka: Kwa msimamo huo, hamkutoa ushirikiano kwa tume hiyo?

    Heche: Sahihi.

    Ripoti za uchaguzi

    Wakili Mwinuka: Katika ripoti ulizozitaja kuhusu uchaguzi mkuu wa mwaka jana, ripoti ya Afrika Mashariki ilisema nini?

    Heche: Ilisema uchaguzi ulikuwa mzuri, wa haki na haukuwa na tatizo lolote.

    Wakili Mwinuka: Kuhusu ripoti nyingine za kikanda na kimataifa, hukueleza ulizipata wapi, ni kweli?

    Heche: Nilieleza kwamba nilizipata kupitia vyombo vya habari.

    Wakili Mwinuka: Kwa hiyo ulizipata kupitia Google?

    Heche: Nilieleza nilikozipata.

    Wakili Mwinuka: Ripoti ya Thabo Mbeki Foundation iliandikwa kwa lugha gani?

    Heche: Kiingereza.

    Wakili Mwinuka: Hii ya UN je?

    Heche: Kiingereza, lakini pia waliandika kwa lugha nyingine.

    Wakili Mwinuka: Human Rights Watch?

    Heche: Kiingereza.

    Wakili Mwinuka: Jumuiya ya Madola?

    Heche: Kiingereza pia.

    Wakili Mwinuka: Taarifa ya AU?

    Heche: Kiingereza.

    Wakili Mwinuka: Waangalizi wa SADC?

    Heche: Kiingereza pia.

    Wakili Mwinuka: Utakubaliana kwamba wewe ndiye ulifasili taarifa hizi kutoka Kiingereza kwenda Kiswahili hapa mahakamani?

    Heche: Sahihi.

    Wakili Mwinuka: Hukueleza umahiri wako wa lugha uliokuwezesha kufanya tafsiri hizo?

    Heche: Sikueleza.

    Wakili Mwinuka: Unakubaliana kwamba tafsiri inaweza kubadili maana kulingana na umahiri wa mfasiri?

    Heche: Sijui.

    Wakili Mwinuka ameishia hapo.

    Unaweza kusoma;

  17. Heche ahojiwa kuhusu madai ya mauaji na ushahidi wake

    .

    Madai ya mauaji

    Wakili Mwinuka: Kuhusu madai ya mauaji, umetaja orodha ya waliouawa. Je, wewe uliwahi kushuhudia kwa macho yako?

    Heche: Nilikuwepo Nyamongo siku ya kufunga kampeni...

    Wakili Mwinuka: Ni mauaji mangapi uliyashuhudia kwa macho yako?

    Heche: Hadi niorodheshe? Ndiyo maana nimeanza kueleza.

    Wakili Mwinuka: Ni mauaji mangapi uliyashuhudia kwa macho yako?

    Heche: Sijui ni mangapi.

    Wakili Mwinuka: Kuhusu mauaji ya Arumeru, ulimtaja nani?

    Heche: Msafiri Mbwembwe.

    Wakili Mwinuka: Wewe ulikuwepo wakati tukio hilo linatokea?

    Heche: Sikuwepo.

    Wakili Mwinuka: Kuhusu tukio la Ezekiel Wenje, ulisema nani alipata tukio?

    Heche: Nyatega Wenje.

    Wakili Mwinuka: Katika hayo mauaji uliyoyaeleza, ulikuwepo eneo la tukio?

    Heche: Sikuwepo.

    Wakili Mwinuka: Unatambua kwamba chanzo cha kifo kisheria lazima kithibitishwe na taarifa ya kitaalamu?

    Heche: Ni sahihi.

    Wakili Mwinuka: Kwa mauaji yote uliyoyaeleza hapa mahakamani, umeeleza chanzo cha kifo kwa mujibu wa taarifa za kitabibu?

    Heche: Sikueleza taarifa za kitabibu.

    Wakili Mwinuka: Umewahi kushiriki kama shahidi katika uchunguzi wa miili ya watu hao?

    Heche: Sikushiriki.

    Unaweza kusoma;

  18. Heche ahojiwa kuhusu madai ya mashambulizi na uchaguzi

    .

    Kikao cha leo kimeanza kwa dodoso la Shahidi makamu mwenyekiti wa Chadema, John Heche ambaye anahojiwa na Wakili Ignas Mwinuka wa serikali kuhusu madai mbalimbali aliyoyatoa katika ushahidi wake

    Wakili Mwinuka: Iambie mahakama, umeshiriki chaguzi ngapi zinazosimamiwa na NEC ukiwa mgombea?

    Heche: Nimeshiriki chaguzi tatu.

    Wakili Mwinuka: Kati ya hizo, mara mbili ulitangazwa mshindi?

    Heche: Kweli.

    Wakili Mwinuka: Katika chaguzi hizo ulizoshinda, polisi walishiriki kuweka kura kwenye masanduku ya kura ili ushinde?

    Heche: ...

    Wakili Mwinuka: Katika chaguzi hizo ulizoshinda, mawakala walizuiliwa ili wewe ushinde?

    Heche: Hapana.

    Wakili Mwinuka: Unatambua kwamba matokeo ya uchaguzi wa ubunge hupingwa Mahakama Kuu?

    Heche: Natambua.

    Wakili Mwinuka: Uliwasilisha malalamiko Mahakama Kuu kutokana na kutoridhishwa na matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2020?

    Heche: Hapana.

    Wakili Mwinuka: Tuambie kuhusu kujaza fomu. Nitakuwa sahihi kusema kwamba kufanikiwa kugombea kunategemea pia kujaza fomu sahihi?

    Heche: Siyo fomu pekee, kuna mambo mengi yanayowezesha mtu kugombea.

    Wakili Mwinuka: Lakini kujaza fomu ni moja ya vigezo?

    Heche: Ni moja ya vigezo.

    Wakili Mwinuka: Ambacho wewe ulitekeleza?

    Heche: Sahihi.

    Wakili Mwinuka: Ulimtaja Suzan Kiwanga kwamba alizuiliwa kugombea ubunge. Je, wewe binafsi ulijaza fomu ya Suzan Kiwanga?

    Heche: Hapana. Sikuzungumzia kuhusu fomu.

    Wakili Mwinuka: Malalamiko kuhusu kuenguliwa kwao ulipata kwa kusikia kutoka kwa wagombea hao?

    Heche: Sikuyasikia. Niliona na nilishiriki.

    Wakili Mwinuka: Mlijazaje kwa pamoja fomu moja?

    Heche: Hapana. Nilishiriki katika utaratibu wa kushughulikia fomu hizo.

    Wakili Mwinuka: Ulisema hivyo kwenye ushahidi wako wa msingi?

    Heche: Hapana.

    Tukio la kushambuliwa Septemba 7, 2017

    Wakili Mwinuka: Katika tukio la kushambuliwa kwa mshtakiwa Septemba 7, 2017, unakumbuka kama Rais wa wakati huo, John Magufuli, alitangaza kusikitishwa?

    Heche: Sikumbuki.

    Wakili Mwinuka: Unakumbuka kama Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM wakati huo, Humphrey Polepole, alitoa taarifa ya kulaani na kusikitishwa?

    Heche: Sikumbuki.

    Wakili Mwinuka: Unakumbuka Spika wa Bunge alitoa taarifa ya kulaani na kusikitishwa?

    Heche: Nakumbuka.

    Wakili Mwinuka: Unakumbuka Makamu wa Rais wa wakati huo alimtembelea Nairobi alipokuwa akipata matibabu?

    Heche: Nakumbuka alienda kwenye kikao na pia akapita hospitalini.

    Wakili Mwinuka: Wakati tukio hilo linatokea, wewe ulikuwa eneo la tukio?

    Heche: Sikuwa eneo la tukio.

    Wakili Mwinuka: Wakati gari la mshtakiwa liliposhambuliwa, wewe ulishuhudia kwa macho yako?

    Heche: Hayo alieleza mshtakiwa mwenyewe.

    Wakili Mwinuka: Kwa hiyo unachokieleza ni taarifa ulizozisikia kutoka kwa mshtakiwa?

    Heche: Sahihi.

    Unaweza kusoma;

  19. Karibu katika matangazo yetu mubashara kwenye kesi ya Lissu inayoendelea kusikilizwa mahakamani ya tarehe 14.09.2026.

    Usikilizaji wa kesi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu, unaendelea leo huku upande wa utetezi ukiendelea kutoa ushahidi wake mbele ya mahakama.

    Kikao cha leo kimeanza kwa dodoso la Shahidi makamu mwenyekiti wa Chadema, John Heche ambaye anahojiwa na wakili wa serikali kuhusu madai mbalimbali aliyoyatoa katika ushahidi wake wa msingi, ikiwemo uchaguzi, matukio ya mashambulizi, madai ya utekaji, mauaji pamoja na ripoti za waangalizi wa kimataifa.

    Karibu.

  20. Kesi ya Lissu: Mahakama yaahirishwa mpaka Jumatatu saa tatu asubuhi. Kwaheri.