Lissu: PW2 hakubadilika msimamo uleule wa PW1 kukinukisha ni uhaini kwa nini kwa sababu uchgauzi ni kwa mujibu wa sheria na katiba na unasimamiwa na serikali hivyo unatishia serikali
PW16 anasema hivi;
“Mshtakiwa alitaka kuitishia serikali kwa kufanya matendo ambayo alikuwa anayasema, kitendo cha kuitishia serikali kwa kutishia kuzuia uchaguzi na kuhamasisha uhaini kilikuwa ni uhaini kwa sababu ulipanga kuzuia uchaguzi kwa sababu uchaguzi unasimamiwa na serikali.
Waheshimiwa majaji PW16 akaelezea kwa nini haya maneno anadai ni uhaini “Maneno yakitumiwa na mshatakiwa kama ‘tutazuia uchgauzi, tutahamasiha uasi’ yalilenga kuitishia serikali ambayo imepewa mamlaka ya kulinda nchi” kwa hiyo kujaribu kuzuia uchaguzi ni uhaini haijalishi chochote kwa sababu gani, uchaguzi ni kwa mujibu wa sheria na katiba, na kuzuia ni kutishia serikali.
PW 16 wakati anahojiwa kufafanua kwenye maswali ya dodoso alisema hivi “Nilichomaanisha kwenye maneno hayo ni kwamba serikali ndiyo ina mamlaka ya kusimamia sheria za nchi kwa hiyo ukisema kwamba utazuia uchaguzi kitendo hicho ni kutishia serikali na kutishia amani na utulivu wa nchi” huo ndiyo ushahidi wa mapolisi waliotoa ushahidi kuhusu suala hilo.
Msimamo wao ndiyo huo ukitishia uchaguzi ni uhaini kwa sababu uchaguzi upo kwa mujibu wa sheria na katiba, na serikali ndiyo inayosimamia hivyo kufanya hivyo ni kuitishia serikali.
Sio kila shahidi wa upande wa mashataka alikuwa na msimamo huo PW17 ambaye ni shuhuda wa macho hakuunga mkono dhana hii ya polisi hivyo PW17 ndiyo shahidi pekee aliyepingana na msimamo huo.
Lissu azungumzia hoja ya "kuitishia serikali"
Lissu: Nasema hivyo kwa sababu uchaguzi unafanyika kwa mujibu wa sheria na katiba. Serikali ndiyo inayosimamia sheria, iliitisha serikali kwa kuikata sheria ambayo imewekwa, kuikaidi sheria iliyowekwa na serikali ni kosa.
Hapa ndipo kesi hii ipo, mtakumbuka kwamba PW1 alikiri kwamba kwenye hayo wanayolalamikia hakuna neno serikali wala hakuna neno Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wala hakuna neno Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, wala hakuna maneno rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , wala hakuna maneno Makamu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wala hakuna maneno Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na zaidi ya hapo hakuna Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam na kwa maneno yake ukurasa wa 157.
Hivyo hicho wanachodai kimetishiwa hakipo. Serikali yenyewe haipo na jina la kiongozi yeyote wa kiserikali lililotajwa huko ni kukiri kwake kwenye maswali ya dodoso.
Licha ya hayo PW1 aliendelea kusisitiza kuwa serikali ilipangwa kutishiwa akasema “mtu anaposema ‘kukinukisha sana’ umetenda uhaini, maneno kukinukisha sana, kukinukisha vibaya sana, hayapo kwenye sheria isipokuwa ukiyasema umefanya kosa la uhaini kwa sababu serikali ndiyo inayosimamia sheria kwa hiyo unakuwa umetenda uhaini” huo ndiyo ushahidi unawashawishi mtoe hukumu ya kunyonga mtu...hawana hata aibu.
Lissu: Ushahidi ulipo kwenye ushahidi wa PW1 kusema huu ni uhaini ukawa wimbo wa mapolisi wote na mawakili wote wa serikali waliopo mbele yenu…alipoamua tu kwamba huu ni uhaini hakuna kitu chochote kingebadili mawazo yake.
Alipoulizwa PW17 aliyekuwa shahidi wa kuona na kusikia kwenye mkutano wala hakuona shida yoyote alipoambiwa hivyo alisema “ni kweli.
Kwenye maelezo yake PW17 alisema ''mlikuwa mnazungumzia changamoto zinazowakabili na pia mlikuwa mnazungumzia sera yenu ya no reform no election nimesoma maelezo yake na nikaamua kufungua kesi ya uhaini ni mimi ndiye niliyeamua kufungua faili la uhaini''.
Baada ya kusoma maelezo yote” D16 ni maelezo ya PW17 ambayo PW1 anakiri anayasoma hayajasema kulikuwa na kosa lolote achilia mbali suala la uhaini, hivyo hakuna ambacho kingembadilisha.
Alipoulizwa na mawakili wa serikali. Unasema juu ya hayo maneno yanaweza kuihusu serikali ya Jamhuri ya Muungano?
Kumbuka amesema maneno serikali ya Jamhuri ya Muungano hayapo, je hayo maneno yakibaki yanaweza kuihusu serikali pia alisema “Hayo maneno yaliyonukuliwa kwenye maelezo yake kwa muktadha wake yanamaanisha serikali”.
Akaendelea kurudia maneno kwa vile uchgauzi unafanyika kwa sheria na katiba hivyo hayo maneno serikali yapo kwenye maneno ambayo tunalalamikia hayapo lakini yapo”.
Kisichokuwepo kinaingizwa huo ni ushahidi wa PW1 alipotoa ushahidi huohuo ndiyo ukawa msimamo wa kila polisi aliyekuja hapa kutoa ushahidi, yeye ndiye aliyewaweka polisi waseme nini kila polisi ushahidi wao unafanana kama sare wanazo vaa.
Lissu anaendelea kutoa majumuisho yake ya mwisho
Lissu: Waheshimiwa majaji nawashukuru naomba kwamba nikumbushwe jana niliishia wapi?
Jaji: Jana uliishia kwenye kesi ya Mbowe…ukasema umemaliza sehemu ya sheria kwa hiyo unaelekea kwenye ushahidi sasa.
Lissu: Nashukuru naomba kabla sijaanza kuzungumzia ushahidi naomba niseme kitu kimoja muhimu ambapo mahakama hii ilikisema kwenye kesi ya Freeman Mbowe, kuhusiana na madhara ya kutokufafanua kwenye hati ya mashtaka,sheria inatakiwa kutoa tahadhari muafaka kwa wale wanaotakiwa kuzifuata, sheria lazima zilinde raia dhidi ya mamlaka holela, sheria ilinde raia dhidi ya matumizi holela ya madaraka, na sheria ilinde haki ya kuzungumza kama si hivyo wote tutakuwa wafungwa, muhimu zaidi mahakama hii ilisema yafuatayo kuhusu sheria za namna hii:
Lissu: Kama sheria imeandikwa haina lindo na inanyima watu haki zao za kusema inasema mahakama inaweza ikafuta hata kama matendo inayokataza ni ya lazima sababu haki ya watu kusema lazima ilindwe, sasa mahakama ilimalizia hayo kwenye kesi ya Freeman Mbowe…. Je ushahidi?.
Lissu: Katika mashahidi wa mashtaka ni mmoja tu aliyekuwa kwenye mkutano ambaye ni PW17 na huyo PW17 sio tu alisikia bali alirusha matangazo, Majaji kesi ya upande wa mashtaka imejengwa kwenye nini?
Imejengwa kwenye ushahidi wa PW1, PW2 na PW16, hawa mapolisi ambao hakuwepo kwenye mkutano, dhana ya kesi hii ni kwamba mimi mshtakiwa nilichochea umma kwa kuzungumza maneno yale kwa lengo la kuitishia serikali kwa sababu moja tu ambayo wameelezea kwenye ushahidi wao.
Kwa sababu hii serikali ndiyo inasimamia sheria za nchi hii na hivyo kwakuwa ndiyo inayosimamia uchagauzi mkuu, hivyo ni kuitishia serikali ila inayosimamia huo uchaguzi hiyo ndiyo dhana yao kwakuwa uchaguzi unaendeshwa kwa katiba na sheria.
Nianze na shahidi PW1 alisema juu ya nia ya kushaiwishi umma kuzuia uchaguzi, maneno yake yapo kwenye ukurasa 146 kwenye rekodi za mahakama anazungumzia nini kilichomfanya aamini kuna kosa la uhaini ni maneno ya mshtakiwa “atahamasisha uasi, atazuia uchaguzi, atakinukisha sana, atakinukisha vibaya sana”.
Lissu amtaja Mbowe akijitetea na kifo
Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, jana aliendelea na mawasilisho yake ya mwisho katika kesi ya uhaini, akijikita katika hoja za kisheria na kuhoji kama maneno anayodaiwa kusema yanaweza kisheria kuunda kosa la uhaini.
Katika hoja zake, Lissu alisisitiza kuwa hakatai kusema maneno yanayotajwa na upande wa mashtaka, lakini hoja yake ni kama maneno hayo yanatimiza masharti yote yanayohitajika kisheria kuthibitisha kosa hilo.
“Kuchochea umma” si kosa lililotajwa kwenye sheria, Lissu aliiambia Mahakama
Moja ya hoja kuu za Lissu ilikuwa kuhusu lugha iliyotumika kwenye hati ya mashtaka. Alisema kifungu cha 39(2)(d) cha Kanuni ya Adhabu kinachotumika katika kesi hiyo kinahusu kutishia Serikali kupitia kuchochea mtu au kikundi cha watu, wakati hati ya mashtaka inatumia maneno “kuchochea umma.”
Kwa mtazamo wa Lissu, tofauti hiyo ni muhimu kwa sababu mahakama haiwezi kutengeneza kosa ambalo halijaainishwa na sheria.
Pia alihoji shtaka la kutishia “Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania”, akitaka kujua ni sehemu gani ya Serikali inayodaiwa kutishiwa na kauli zake.
Lissu pia alipinga ushahidi unaohusisha maandalizi ya mkutano wa CHADEMA wa Aprili 3, 2025. Alisema hakuuitisha wala kuuandaa mkutano huo, bali alikuwa mmoja wa watu walioalikwa. Kwa mujibu wa hoja zake, maandalizi ya mkutano yalifanywa na Sekretarieti ya CHADEMA.
Hivyo, alitaka mahakama izingatie ushahidi uliotolewa kuhusu nani aliyeandaa mkutano huo na nafasi yake binafsi katika maandalizi hayo.
Lissu pia alihoji ushahidi kuhusu kualika waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo, akipinga kuhusika na kualika, lakini pia kuchapisha maudhui ya video ya mkutano huo mtandaoni kupitia Jambo TV.
Wakati wa maswali yake kwa shahidi mkuu wa upelelezi, Lissu alihoji kama yeye ni mfanyakazi, mtangazaji au mpiga picha wa Jambo TV, na kama alikuwa na nywila ya kuingia kwenye mfumo wa chombo hicho.
Lissu pia alisisitiza kwamba kukiri kusema maneno yanayodaiwa hakumaanishi amekiri kosa la uhaini.
“Maneno pekee hayatoshi kuthibitisha uhaini”
Kwa mujibu wa hoja yake, mahakama inapaswa kuangalia maana ya maneno hayo, mazingira yalipotolewa na ushahidi mwingine wa kesi, kisha kuamua kama vipengele vya kosa linalomkabili vimethibitishwa.
Upande wa mashtaka, kwa upande mwingine, unasema maneno hayo na mazingira yalipotolewa yanaonyesha dhamira ya kutishia Serikali na kuzuia Uchaguzi Mkuu wa 2025.
Katika kuunga mkono hoja zake kuhusu namna sheria inavyopaswa kutumika katika kesi za jinai, Lissu pia alirejea kesi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe.
Lissu alitumia mfano huo katika kueleza hoja zake kuhusu namna mahakama inavyopaswa kufuata sheria na ushahidi uliowasilishwa badala ya kuunda kosa ambalo halijaainishwa kisheria.
Kingine Lissu alichosema jana ni kuhusu uamuzi katika kesi yake kwamba hautamhusu yeye pekee, bali unaweza kuweka msingi wa kisheria ambao mahakama zinaweza kuufuata katika miaka ijayo.
Alisema kesi yake ni tofauti na kesi mbili za uhaini alizotaja za Grey Likungu Mataka na wenzake ya mwaka 1970, na Hatibu Gandhi na wenzake ya mwaka 1983, ambazo alisema zilihusu madai ya kujaribu kuipindua Serikali au kumuua Rais.
Kwa mujibu wa Lissu, kesi yake chini ya kifungu cha 39(2)(d) inahusu madai ya kutishia Serikali kwa kuchochea umma kuzuia Uchaguzi Mkuu wa 2025.
Leo Alhamisi Septemba 24, anatarajiwa kuendelea na mawasilisho yake ya mwisho, safari hii akichambua ushahidi uliowasilishwa katika kesi hiyo. Iwapo atakutwa na hatia adhabu ya kosa la uhaini kwa sheria za Tanzania ni kifo.
KARIBU KATIKA MUENDELEZO WA KESI YA UHAINI YA LISSU LEO SEPTEMBA 24, 2026
Lissu: Kuanzia Rais hadi watendaji wa vijiji, ni nani niliyemtishia?
Lissu: Kuna lengo la kuchochea ili
kuitishia serikali. Hakuna lengo la kuzuia uchaguzi wala lengo lingine lolote.
Kwa hiyo ni
wazi, kwa misingi hii tu, nimeshtakiwa kwa kitu ambacho hakipo kwenye sheria.
Tatizo la
tatu ni hili: hiki kinachoitwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano ni kitu gani
ambacho naambiwa nimechochea watu wakitishie?
Swali hili
ni muhimu kwa sababu nilizozieleza.
Hiki
kinachoitwa kuitishia Serikali ya Jamhuri ya Muungano ni kitu gani?
Hilo neno
"Serikali ya Jamhuri ya Muungano" si jambo rahisi kama walivyofikiri
wakati wanaandaa hati ya kesi hii.
Serikali ya
Muungano imefafanuliwa katika Katiba yetu.
Imeelezwa
katika Sura ya Pili ya Katiba. Sura nzima ya pili ya Katiba yetu inazungumzia
serikali.
Mosi, Rais
wa Jamhuri ya Muungano, huyo ni serikali.
Pili,
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano.
Tatu,
Waziri Mkuu na Baraza la Mawaziri. Sehemu hiyo ya Sura ya Pili nayo vilevile ni
serikali.
Mwanasheria
Mkuu wa Serikali ni serikali.
Mkurugenzi
wa Mashtaka ni serikali.
Kwa mujibu
wa Sura ya Nane ya Katiba, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ni sehemu ya Serikali
ya Jamhuri ya Muungano.
Baraza la
Mapinduzi Zanzibar nalo pia ni serikali.
Yote hayo
ni Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
Lissu: Ili kuonesha kwamba sizungumzi
kutoka kichwani, nawaalika muangalie tafsiri ya neno serikali katika
Katiba.
Kwa hiyo
upande wa mashtaka ulipaswa kuniambia, katika hicho kitu chote kinachoitwa
Serikali ya Jamhuri ya Muungano, kuanzia Rais hadi kwa watendaji wa vijiji,
waweke wazi hii serikali niliyoitishia ni ipi.
Je, ni
Rais? Waziri Mkuu? Makamu wa Rais? Polisi? Magereza? Watendaji wa vijiji? Ni
nani?
Sasa,
Waheshimiwa Majaji, katika mazingira haya, hati hii ya mashtaka inayozungumzia
kuchochea umma wakati sheria haitambui umma, na inayosema nimechochea umma ili
kuzuia Uchaguzi Mkuu wakati sheria inasema kuchochea mtu au kikundi cha watu
kuitishia serikali, hati hii ya mashtaka inakuwaje halali?
Natambua
kwamba kesi ya Freeman Mbowe ni uamuzi wa mahakama hii. Ni uamuzi wa jaji
mwingine, na hamfungwi nao.
Lissu: Sheria isipotaja kosa, Mahakama haiwezi kulibuni
Lissu: Nilisema PGO Order No. 1, aya ya
25, inasema:
"Makosa
ni matendo ambayo sheria imeyatamka kuwa ni makosa."
Kama sheria
haijaandika kwamba kuchochea umma ni kosa, basi hakiwezi kuwa kosa.
Nilisema
pia kuhusu uamuzi wa Mahakama ya Rufani katika kesi ya Bahame 6 na wenzake.
Mahakama ilizungumzia kanuni ya uhalali na ikasema kwamba:
"Mtu
asihukumiwe kwa kitendo ambacho hakikuwa kosa wakati anapokifanya."
Nimeshtakiwa
kwa kosa ambalo halipo.
Kwenye kesi
ya Bahame 6 na wenzake, washtakiwa walishtakiwa kwa kuingia kinyume cha sheria
katika hifadhi ya taifa. Wakati huo, sheria husika ilikuwa tayari
imebadilishwa. Walishtakiwa kwa kosa hilo na wakafungwa kwa kosa hilo, lakini
Mahakama ya Rufani ikakataa.
Mimi
nakabiliwa na kosa la jinai, kosa la uhaini, ambalo Ibara ya 28(4) imelifanya
kuwa miongoni mwa makosa makubwa zaidi katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Uhaini,
kama unavyofafanuliwa na sheria, ni ule uliofafanuliwa katika kifungu cha 39
cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu. Na kifungu cha 39(2), kilichotumika kunishtaki,
kimeeleza ni aina gani ya uhaini ninaoshtakiwa nao.
Lissu: Waheshimiwa majaji, nimezungumzia
kesi ya zamani kidogo.
Hapo zamani
kulikuwa na kodi ya kichwa.
Mwanamke
mmoja aitwaye Mwanangomeni alishtakiwa kwa kutolipa kodi ya kichwa, wakati
sheria haikueleza kwamba wanawake walikuwa na wajibu wa kulipa kodi hiyo.
Mahakama
Kuu ya Tanganyika ikasema kwamba kama sheria haijaelekeza wanawake kulipa kodi,
basi haitakuwa kosa kwa wanawake kutolipa kodi hiyo.
Hiyo
ilikuwa miaka 93 iliyopita, wakati wa ukoloni.
Na kwenye
kesi niliyoitaja ya Amin Salum Mrisho ya mwaka 1971, mshtakiwa alipatikana na
hatia ya kosa la kawaida la wizi na akahukumiwa kwa vifungo.
Mahakama
Kuu ikasema hapana, kwa sababu usipomshtaki mtu kwa kosa hilo huwezi kumhukumu
kwa kosa hilo.
Naomba
nipendekeze kwenu msome maamuzi ya Mahakama Kuu katika kesi iliyozungumzwa sana
hapa. Nimepewa hukumu yake tu, lakini imekuwa ikitajwa mara kwa mara.
Ni kesi ya
Freeman Mbowe na wenzake saba dhidi ya Jamhuri.
Kesi hiyo
ni muhimu kwa ushahidi wa kesi hii.
Nimeitaja
hapa kwa sababu ya umuhimu wake wa kisheria.
Lissu: Nimeshtakiwa kwa kosa ambalo halipo kwenye sheria
Lissu: Waheshimiwa majaji, kifungu cha 39(2)(d) cha
sheria iliyotumika kunishtaki kinasema: "Mtu yeyote anayechochea mtu au
kikundi cha watu..."
Shtaka
dhidi yangu linasema nimechochea umma. Kwenye kifungu hicho cha 39(2) hakuna
umma, kuna mtu au kikundi cha watu.
Sasa umma
ni nini? Hiki kitu kinachoitwa umma ni kitu gani?
Kanuni ya
Adhabu imetoa tafsiri ya neno umma. Tafsiri ya umma kwa mujibu wa sheria hii
ina maana ya watu wote wa Tanzania Bara bila kujali uraia wao. Kila mtu aliyeko
ndani ya mipaka ya Tanzania Bara, pamoja na watu wanaokaa mahali popote au
wanaotumia sehemu yoyote, mfano baa, gesti au vilabu. Ni idadi yoyote ya watu,
hata watu ambao hata ufanyeje huwezi kuwajua.
Huo ndio
umma ambao ninatuhumiwa kuuchochea ili uzuie uchaguzi.
Sheria
niliyoshitakiwa nayo inasema unachochea mtu au kikundi cha watu. Mtu
anajulikana. Lakini kikundi cha watu ni nini hasa?
Natumia Oxford Advanced Learner’s Dictionary. Kikundi
ni idadi ya watu au vitu ambavyo vipo pamoja katika sehemu moja au
vinaunganishwa kwa namna fulani.
Hiyo ndiyo maana ya kikundi.
Si watu wote. Watu wote hawawezi kuwa kikundi. Kikundi ni
sehemu ya watu wote.
Nimeshtakiwa kwa kitu ambacho hakipo kwenye sheria.
Sheria iko wazi kabisa.
Lissu: Waheshimiwa majaji, hili kosa lilivyoletwa,
hizi taarifa zilivyoletwa, haziwezi kujibika.
Hakuna mtu anayeweza kujitetea kwa hati kama hii, kuambiwa
umechochea watu wote, waliopo uwanja wa ndege na waliopo majumbani kwao.
Hilo halipo kwenye kifungu cha sheria ya Kanuni ya Adhabu
niliyoshitakiwa nayo.
Waheshimiwa majaji, kwa sababu ya upana wa hilo neno umma,
upande wa mashtaka ulikuwa na wajibu wa kisheria kueleza huo umma ni upi katika
hati yao ya mashtaka ili kumwezesha mshtakiwa kuandaa utetezi wake.
Upande wa mashtaka ulitakiwa kueleza huo umma unaodaiwa
kuchochewa.
Hawakufanya hivyo.
Wameleta kitu ambacho hakipo kwenye sheria.
Basi turudi kwenye misingi.
Nilisema kitu kinachoitwa kosa la jinai ni kile
kilichokatazwa na sheria. Ni kitendo.
Kifungu cha 39(2) kimetengeneza kosa la uhaini kwa mtu
yeyote anayechochea mtu au kikundi cha watu kuitishia serikali.
Sheria haijatengeneza kosa la mtu kuchochea watu wote, yaani
umma.
Hakuna sheria ya namna hiyo.
Hakuna sheria inayosema ukichochea watu wote ni kosa.
Sheria inasema ukichochea mtu au kikundi cha watu.
Nimeshtakiwa. Nipo gerezani kwa mwaka mmoja na nusu sasa kwa
kitu ambacho hakipo kwenye sheria za nchi hii.
Ibara ya 13(6)(c) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania inasema:
"Ni marufuku kwa mtu kuadhibiwa kwa kitendo chochote
ambacho alipokifanya hakikuwa kosa chini ya sheria."
Nimeshtakiwa kwa kuchochea umma.
Hakuna sheria inayoitwa kuchochea umma.
Kuna sheria inayosema kuchochea mtu au kikundi cha watu.
Tundu Lissu kuanza kujitetea baada ya kukutwa na kesi ya kujibu
Lissu: Ushahidi uliobaki mahakamani una jibu moja tu
Lissu: Hoja yangu ni kwamba, kwa sababu migongano
hiyo inahusu jambo kubwa linalohusu ushahidi wa kwamba mshtakiwa aliwaalika au
hakuwalika waandishi wa habari, inaonesha kwamba ushahidi huo hauna thamani
yoyote.
Vipi kuhusu ushahidi wa utetezi kwenye hoja hii? Unasemaje?
Ushahidi wa utetezi umefuta shaka yoyote kuhusu mshtakiwa
kuwaalika waandishi wa habari kwenye mkutano wa tarehe 3 Aprili 2025.
Kama kulikuwa na shaka kwamba mshtakiwa aliwaalika waandishi
wa habari, imeondolewa yote na ushahidi wa utetezi.
Sisi tunasema kwamba waandishi wa habari waliohudhuria
mkutano wa tarehe 3 Aprili 2025 walialikwa na Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa
CHADEMA, Brenda Rupia, bila shaka yoyote. Wote wamesema hivyo.
Ushahidi huu upo katika ukurasa wa 592. Ushahidi wa DW2 upo
katika ukurasa wa 621 hadi 622. Ushahidi wa DW3 upo katika ukurasa wa 693.
Ushahidi wa DW4 upo katika ukurasa wa 800.
Mashahidi hao wote wanne wamesema kwamba aliyewaalika
waandishi wa habari ni DW4, Brenda Rupia.
Waheshimiwa majaji, ushahidi huo haukuhojiwa hata mara moja.
Sasa, nini maana ya kutokuhojiwa kwa ushahidi huu?
Lissu: Kwa sababu hizi, jibu la swali la pili, je,
mshtakiwa aliwaalika waandishi wa habari kwenye mkutano wa tarehe 3 Aprili
2025, jibu lake ni hapana.
Hiyo ni kusema kwamba mshtakiwa hakuwalika waandishi wa
habari kwenye mkutano wa tarehe 3 Aprili 2025.
Swali la tatu ni hili: Je, mshtakiwa alitengeneza nia ya
kuchochea mtu yeyote au kikundi cha watu kuzuia Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 kwa
lengo la kuitishia Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?
Kwa kesi hii, hili ni suala la kufa au kupona, kwa sababu ni
moja ya mambo muhimu zaidi katika kesi nzima dhidi yangu.
Taarifa iliyopo mahakamani inayonishtaki inanituhumu kwamba
nilitengeneza nia ya kuhamasisha umma na kuchochea umma kuzuia Uchaguzi Mkuu wa
mwaka 2025 kwa lengo la kuitishia Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Lissu aibua migongano mikubwa kwenye ushahidi wa mashtaka
Lissu: PW16, mnakumbuka, ndiye aliyekuwa mpelelezi
mkuu wa kesi. PW16 alisema yafuatayo kuhusu nani aliyewaalika waandishi wa
habari. Anasema hivi wakati anaongozwa:
"P na P1 wamesema kuwa walipewa maelekezo na
mkurugenzi wao, John Marwa, kwenda kurekodi na kurusha mtandaoni taarifa
inayodaiwa... John
Marwa alialikwa na Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa CHADEMA."
Nilimuuliza:
Je, mimi ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa CHADEMA?
Kwenye
ukurasa huo huo mmeandika:
"Hapana,
Tundu Lissu si Mkurugenzi wa Mawasiliano wa CHADEMA."
Lissu: Ni shahidi gani wa upande wa
mashtaka ambaye ushahidi wake uaminiwe na mahakama hii kwenye suala muhimu
ambalo upande wa mashtaka umeleta?
Majibu yapo
kwenye msimamo wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania katika kesi ya Khamis Said
Hassan. Nilishatoa mfano wake. Mahakama ikisema:
"Imeamuliwa
sasa kwamba migongano na mikwaruzano kwenye ushahidi ni msingi wa kujua ukosefu
wa uaminifu."
Hii
mikanganyiko kwenye ushahidi si midogo. Inahusu jambo muhimu. Kwa hiyo,
mkanganyiko kuhusu jambo lililotolewa ushahidi, kwamba mshtakiwa ndiye
aliyewaalika waandishi wa habari, si mkanganyiko mdogo.
Lissu ahoji ushahidi wa mashtaka kuhusu waandishi wa habari
Lissu: Ushahidi wa DW2 umeungwa mkono na DW3, Naibu
Katibu Mkuu wa CHADEMA, na DW4, Mkurugenzi wa Mawasiliano na Habari wa CHADEMA.
Maafisa wa chama ndio waliandaa huo mkutano.
Hii tuhuma kwamba ni mimi ndiye niliyeandaa mkutano ni
tuhuma ya uongo. Ninachoweza kusema kwa upole kabisa ni kwamba haijathibitishwa
kabisa. Nikisema hivyo, nasema kwa upole.
Upande wa mashtaka haujathibitisha kuwa mshtakiwa ndiye
aliyeitisha mkutano wa tarehe 3 Aprili 2025.
Kwa ruhusa
yenu, naomba niende kwenye suala la pili. Je, ni mtuhumiwa ndiye aliyewaalika
waandishi wa habari kwenye huo mkutano wa tarehe 3 Aprili 2025?
Swali hilo
ni muhimu. Kama lengo la mkutano lilikuwa la kihaini, kuwaalika waandishi wa
habari ni kitendo cha wazi, na waandishi wa habari waliokuja kwa mwaliko wangu
wanakuwa washirika wa kosa hilo. Kosa la uhaini litakuwa linawahusu pia.
Kwa hiyo,
tuhuma hii si ya bahati mbaya wala haijaletwa bure. Ina lengo la
kuthibitisha kitendo cha wazi. Wakithibitisha hilo, wanathibitisha uhaini.
Lissu: Kwenye maelezo ya ziada ya tarehe 22 Septemba
2025 hawakusema waziwazi. Walisema tu kwamba waandishi wa habari walialikwa,
lakini hawakusema walialikwa na nani.
Kwangu mimi, kutokumtaja aliyewaalika waandishi wa habari
hakukuwa bahati mbaya. Kulikuwa na nia mbaya kwa sababu, kwenye ushahidi,
walileta mashahidi waliosema mimi ndiye niliyewaalika waandishi wa habari.
PW1, ACP George Bagyemu, alisema hivi wakati anaongozwa
kutoa ushahidi wake kuhusu suala hili. PW1 alisema:
"Ni mtuhumiwa aliwaalika waandishi wa habari ili
hotuba yake iweze kusikilizwa na Watanzania, na wasio Watanzania waweze kuiona
kupitia Jambo TV."
Ushahidi wa PW1 uliungwa mkono na PW2, Inspekta John.
Ushahidi wake kuhusu hoja hii upo kwenye kurasa za 210 na 221 za kumbukumbu za
mahakama.
Mtakumbuka nilimhoji sana PW1 kuhusu suala hilo. Baada ya
maswali, PW1 alisema hivi, katika ukurasa wa 161:
"Ni kweli kwamba ni wewe ndiye uliyewaalika
waandishi wa habari. Sijui ni njia gani ulitumia kuwaalika, lakini ninachojua
ni kwamba uliwaalika."
Na ushahidi
huu, kama nilivyoeleza majaji, uliungwa mkono na PW2.
Sasa,
ushahidi huu ulipingwa moja kwa moja na PW16 na PW17.
Lissu: Umeitisha mkutano, umezungumza maneno ya
uhaini, tumethibitisha matendo ya wazi. Kwa mujibu wa Khatibu Ghadi, kwenye
mashtaka ya uhaini lazima uthibitishe bila wasi wasi. Kwa hiyo, jambo hili
limeletwa kwa lengo la kuthibitisha hilo.
Kama mkutano ulikuwa wa kihaini, walioshiriki kuandaa pamoja
na mimi wanakuwa washirika katika kosa hilo la uhaini. Kwa hiyo, kama kweli
niliandaa mimi, wale wote waliokuja hapa na wakasema wamefanya hivi au vile,
hao ni washirika. Na kama wao
ni washirika, basi tayari inakuwa kitendo.
Na
kumbukeni, bila matendo hakuna uhaini. Kama mkutano uliitishwa kwa lengo la
uhaini, basi walishirikiana na mimi. Na waliorusha matangazo hayo nao
wameshirikiana kuhamasisha uhaini.
Lissu: Kwa hiyo hoja yangu ni kwamba suala
la kama niliitisha mkutano au la ni suala muhimu kweli kweli.
Sasa
ushahidi uliopo mahakamani unasemaje kuhusiana na suala hili?
Kuhusu
tuhuma kwamba mimi ndiye niliyeitisha mkutano huo, katika mashahidi wote 17 wa
upande wa mashtaka hakuna shahidi hata mmoja aliyetoa ushahidi wa namna mkutano
huo ulivyoitishwa.
Upande wa
mashtaka waliiambia mahakama hii kwamba wangeleta vielelezo vya kuthibitisha
mashtaka yao. Hakuna ushahidi wa maneno, hakuna ushahidi wa nyaraka.
Ushahidi
pekee uliopo kwenye kumbukumbu za mahakama ni ushahidi wa utetezi.
Na ushahidi
wa utetezi unasema hivi: katika ukurasa wa 660, DW2, John Mnyika, ameiambia
mahakama kwamba mkutano ule uliitishwa na kuandaliwa na Sekretarieti ya CHADEMA
Makao Makuu. Amewaambia kwamba ilikuwa ni wazo lake mwenyewe.
DW2
ameiambia mahakama kwamba yeye ndiye aliyewaelekeza wasaidizi wa DW3 na DW4
kuandaa mkutano huo.
Pia DW2
ameiambia mahakama hii kwamba mimi na DW5, John Heche, tulikuwa waalikwa tu.
Lissu: Kanuni kuu tatu ninazoziongoza ni za uhaini.
Ya kwanza inahusu uchapishaji, na inasema uchapishaji chini ya kifungu cha
39(2)(d) una maana ya kitendo cha kutuma au kubadilishana maandishi
yaliyochapishwa na watu wengi. Picha au video hiyo si uchapishaji. Hii ipo
kwenye kesi ya Grey Likungu, ukurasa wa 509 mpaka 510. Kuchapisha maana yake ni
kubadilishana makaratasi, si kitu kingine.
Kanuni ya pili inayohusu uhaini inasema hivi: hatia ya
uhaini inahitaji uthibitisho wa kitendo cha wazi, si maneno. Lazima kuwe na
uthibitisho wa wazi wa matendo. Hiyo ipo kwenye kesi ya Khatibu Ghadi na
wenzake ya mwaka 1996.
Kanuni kuu ya tatu, na ya mwisho, inayohusu uhaini inahusu
maneno. Inasema maneno matupu hayatengenezi matendo ya wazi katika kesi ya
uhaini isipokuwa tu hayo maneno yanaelezea matendo ya uhaini.
Na ya nne,
ya mwisho, inahusu maneno vilevile. Inasema msimamo wa kuwa maneno
hayatengenezi matendo ya wazi ya uhaini unahusu tu uhaini unaodaiwa kufanywa na
mtu mmoja mmoja.
Lissu: Hizo ndizo kanuni kuu za sheria
ambazo nawaalikeni majaji ziwaongoze mtakapokuwa mnatafakari ushahidi pamoja na
sheria kwenye kesi hii.
Kwa ruhusa
yenu, sasa naomba nijielekeze kwenye yale niliyosema. Kwa kanuni hizi
nilizozisema, nifanye tathmini: je, mshtakiwa ndiye aliyeitisha huo mkutano
anapodaiwa kutamka hayo maneno ya kiahaini?
Suala la
nani aliyeitisha huo mkutano, kwenye ukurasa wa 131 wa kumbukumbu za mahakama,
limedaiwa na upande wa mashtaka kwamba mnamo tarehe 3 Aprili 2025, kwa nafasi
yangu kama Mwenyekiti wa CHADEMA, niliitisha mkutano na kuzungumza na wanachama
walioonesha nia zao za kugombea uchaguzi mkuu wa 2025 katika makao makuu ya
chama, Mikocheni.
Kwanza, kwa
nini jambo hili ni muhimu kwenye kesi hii? Kifungu cha 49 cha Kanuni ya Adhabu
kinasema kila kitendo kinachofanyika ili kuwezesha lengo la kufanya kosa
kinahesabika kuwa ni tendo la wazi linalothibitisha hiyo nia. Kwa hiyo,
ukiitisha mkutano maana yake ni kwamba watakuja kusema ni tendo la wazi la
kuthibitisha nia yake ya kutenda uhaini.
Lissu atoa mapendekezo ya kanuni ambazo zinatakiwa kufuatwa kwenye kutoa hukumu
Lissu: Hii sheria ya uhaini ikoje na inataka nini kama nilivyosema shtaka lilipo mbele yenu limeletwa chini ya kifungu cha 39 2 D ya kanuni za adhabu, kifungi cha 39 2 D kinasema hivi;
“Mtu yoyote ambaye akiwa chini ya utii wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwingineko anayetengeneza nia ya kuwezesha au nia ya kuchochea, kushawishi mtu yoyote au kikundi cha watu wakifanikiwa kuwezeshwa kwa matendo au malengo yafuatayo yaani kutishia serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bunge au Mahakama na anahamasisha nia hiyo kwa kuchapisha atakuwa ametenda kosa la uhaini na akipatikana na hatia anaweza kuhukumiwa adhabu ya kifo sasa ni mambo gani muhimu yanayotakiwa kwenye hicho kifungu cha 39 2 D ni mambo gani ambayo yasipothibithishwa yana uhaini na jambo la kwanza ni utiifu kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Jambo la pili ambalo ni lazima lithibitishwe ni kuwa limefanywa ndani ya nchi au kwingineko.
Jambo la tatu ambalo lazima lithibitishwe ni kutengenezwa kwa nia ya kutenda kosa la uhaini haiwezi kuwa nia ya kufanya kitu kingine lazima iwe nia ya kufanya kosa la uhaini na kama ni la kuchochea lazima huo uchochezi uwe wa kufanya kosa la uhaini lazima iwe nia ya kuchochea watu wafanye kosa la uhaini,
Nne kama ni kosa la kuchochea au kuhamasiha watu kufanya kosa la uhaini lazima wanaochochewa awe mtu mmoja au kikundi cha watu.
Lissu: Mtu mmoja au kikundi cha watu ndiyo wanaochochewa. Sharti la tano ni kwamba hiyo nia ya kutenda kosa la uhaini lazima idhihirishwe kwa kuchapisha maandishi au machapisho au kwa njia yoyote ile.
Sharti la 6 halipo kwenye cha 39 2 D bali lipo kwenye kifungu cha 10 D kwenye kanuni ya adhabu, hilo sharti ni kwamba lazima matokeo yaliyotakiwa kutoka kwenye hiyo nia lazima kuwe na matokeo yaliyolengwa kutokana na hicho kitendo.
Lissu: Maana yake ni kwamba kama nia ni kuchochea kosa la uhaini lazima matokeo ya nia yaonekane section 10: 2 ni jambo la lazima upande wa mashataka uoneshe matokeo ya nia hiyo.
Hili ambalo nimelisema sasa hivi hayakuzungumzwa kabisa katika kesi nyingine mbili za uhaini, kesi hii kwa mara ya kwanza inabidi ilitolee hili uamuzi ndiyo maana nilisema chochote mtakchoamua mnaweka msingi na vilevile mtaona kwamba kesi mbili za uhaini zilizopita, mahakama haikujadili inakuwaje watu wengine wanapochochewa kwa vyovyote baada ya hiki kivumbi kutulia tutakuwa tunatengeneza sheria mpya au muongozo ambao haukuwahi kutolewa, ndiyo maana nasema uzito wake sio hatma ya mtu mmoja bali mnaweka msingi baada ya kuwa nimeweka hayo kutoka kifungu cha 39 2 D nipendekeze kwenye masuala ambayo yataamuliwa na mahakama hii na yote hayo yanatokana na haya niliyoyasema.
Lissu: Maneno ya kuzuia Uchaguzi Mkuu 2025 yanatengeneza kosa la uhaini?
Lissu: Sijawahi kuficha wala kukana kwamba nilisema maneno haya, ukiangalia ukurasa wa 97 wa rekodi ya mahakama ya Kisutu tarehe 18-8-2025 niliambia mahakama yakabidhi maneno yafuatayo yapo ukurasa wa 97 kwa kumbukumbu nilisema:
“Ni kweli nilisema maneno hayo kwenye vyombo vya habari wazi suala ni je hayo maneno yanatengeneza kosa la uhaini?”
Kuna kitu kingine muhimu nilikisema kipo ukirasa wa 97 wa kumbukumbu za mahakama yanasema “sikusema maneo hayo mara moja nilisema mara nyingi, Mbeya, Songwe, Iringa, Songea, Njombe, Lindi na Mtwara.
Haya maneno ya kuzuia uchaguzi mkuu 2025 hayajawahi kuwa siri, swali ni maneno haya yanatengeneza kosa uhaini au kosa lingine lolote la jinai?”
Mashahidi wangu wote ambao wametoa ushahidi mahakamni hapa pamoja na mimi mwenyewe vilevile wamesema kwa kiapo mbele yenu kwamba maneno haya yametolewa kwa nyakati mbalimbali, maeneo mbalimbli ndani ya Tanzania haijawahi kuwa siri, kauli yangu ya pili ya awali ni kwamba utetezi wangu haujawahi kuwa ninaona aibu kwa nilichokisema, huo haujawahi kuwa utetezi wangu, utetezi wangu umekuwa siku zote kwamba nilichokisema sio uhaini na sio kosa lolote la jinai kwa mujibu wa sheria za Tanzania huo ndiyo umekuwa utetezi wangu.
Kauli yangu ya Tatu ni kwamba baada ya kusikiliza mashahidi 17 wa upande wa mashtaka baada ya kuangalia vielelezo 16 vya utetezi na hakuna kielelezo hata kimoja cha mashataka, kesi ya upande wa mashtaka leo ni dhaifu kuliko walivyoileta mahakama kuu, kauli yangu ya nne ya awali iko hivi hii ni kesi ya 3 ya uhaini, katika hii ambayo tunaipenda angalu mimi naipenda nimeitolea damu hii ni kesi ya 3 ya uhaini kufunguliwa chini ya kifungu cha 89 (2) cha kanuni ya adhabu.
Lissu: Katika Kesi mbili za kwanza za uhaini mwaka 1970 na 1983 zilifunguliwa chini ya kifungu cha 39 2 a, b, na c cha sheria ya kosa kanuni za adhabu zote zilihusu jaribio la kupindua serikali na kumuua Rais tofauti na nyingine, kesi hii imefunguliwa chini ya kufungu cha 89 b hakuna habari ya kupindua serikali wala kumuua Rais.
Uhaini unaodaiwa hapa ni wa kutishia serikali na hii ni kesi ya kwanza katika historia ya nchi ambayo inahusu uhaini lakini haihusu kutaka kuipindua serikali wala kumuua Rais kwa sababu hiyo waheshimiwa majaji uamuzi wowote mtakaoufanya mnakwenda kuweka msingi wa kisheria kuhusu uhaini wa kuitishia serikali.
Vyovyote mtakavyoamua, mtaweka msingi ambao utaongoza mahakama zetu kwa miaka mingi ijayo kama alivyofanya Grey Likungu mwaka 1971, hivyo vyovyote mtakvyofanya mnatengeza msingi, hivyo hamtahukumu mtu mmoja mtaweka utaratibu wa sheria utakaofuatwa kwa miaka mingi ijayo,sihitaji kuwakumbusha uzito wa jukumu hilo mlilopewa, sio tu kuamua juu ya mtu mmoja bali mzigo wa kuongoza nchi hii kwa miaka ijayo.
Tumaini langu kwenu ni kwamba mtabeba huo mzigo wa kihistoria bila upendeleo na kwa ujasiri kwa hesima mliyopewa na viapo vyenu.
Lissu; Haya maneno ninayodaiwa kusema ya kile tuki kwa kiingereza elpsis (:) zipo nne kuna elpsis kabla ya maneno wanasema na kuna elpsis baada ya neno la mwisho na katikati ya maneno hayo kuna elpsis kwenye maneo mawili, hizo elpsis maana yake kuna maneno yameondolewa na hilo ni jambo la muhimu sana kama tutakavyoona kwenye hoja zangu za mahitimisho na proof kwamba kuna maneno yameondolewa ni hizo elpsis sasa mashataka dhidi yangu yanasema nilifanya kosa hilo katika wilaya ya Kinondoni ya mkoa wa Dar es salaam.
Tarehe 3, April 2025, wakati wa usikilizwaji wa awali wa kesi hii mnamo September 22, 2025 upande wa mashtaka ulitoa maelezo ya ziada in support of the charge kwenye maelezo ya ziada yaliyotolewa wakati wa uwasilishwaji wa awali upande wa mashataka ulidai kwamba mimi ndiye niliyeitisha mkutano wa watia nia wa chama changu mnano tarehe 3 April ambako nilisema hayo maneo hivyo huo mkutano wa April 3 kwa madai ya mashtaka uliitishwa na mimi.
Maelezo haya yapo ukurasa wa 131 wa rekodi ya mahakama , upande wa mashatka pia ulidai mimi ndiye niliyealika waandishi wa habari waliohudhuria kwenye mkutano huo na waandishi wa habari ninaodaiwa kuwaalika walidaiwa kutokea katika vyombo vya habari vifuatavyo; Mwananchi communication limited, Jambo TV na Clouds Media hayo vilevile yapo ukurasa wa 131 wa rekodi za mahakama.
Lissu: Inadaiwa vilevile kwenye hayo maelezo ya ziada inadaiwa kwamba hiyo kauli niliyoitoa kwenye mkutano huo ukiwachochea baadhi ya watu kwenye huo umma ambao walianza kuhamasishana katika maeneo mbalimbali yaliyotajwa kama vile Arusha, Kilimanjaro, Ruvuma, Dar ea salaam na Mbeya na walianza kuhamasishana ili kuzuia uchgauzi mkuu wa Oktoba 2025 kwa kutumia nguvu na baadhi yao inadaiwa walikamatwa askari polisi wakati wakitekeleza maelekezo yangu, maneno hayo yapo ukurasa 132 wa rekodi za mahakama, maelezo ya ziada ya mwisho yanasema hiyo kauli niliyotoa kwenye mkutano April 3 ilikuwa ni kitendo cha uhalifu na hayo maneno yaliripotiwa kwa afisa mkuu wa upelelezi wa kanda maalum ya Dar es salaam.
Lissu: Kuna kitu nimekisahau kwenye hayo maelezo ya ziada inadaiwa pia hayo maneno niliyosema kwenye mkutano niliyachapisha mwenyewe kwenye chombo cha habari kinachoitwa Jambo TV na yalirushwa moja kwa moja kwa umma, nilichapisha mwenyewe, taarifa iliyowasilishwa mahakamani pamoja na maelezo ya ziada ya mashtaka niliyoyasema ndiyo kiini cha kesi hii..hayo madai ya kwenye taarifa na madai ya taarifa katika usikilizwaji wa kesi hii ndiyo kiini cha kesi hii, kwa vile yapo katikati ya huu mgogoro hoja zangu za leo na pengine kesho zinahusu hayo.
Baada ya upande wa jamhuri kukuri kuendelea na shauri, Lissu anasimama na kusema.
Lissu: Waheshimiwa majaji mnamo tarehe 8 Septemba mwaka jana 2025 ,niliambiwa na mahakama hii kwamba kesi hii itaamua kama kwa sheria za nchi hii inawezekana kwa kiongozi wa kisiasa au kwa mtu mwingine yoyote kuhumumiwa kifo kwa kuzungumza maneno ya kisiasa kwenye mkutano wa kisiasa, waheshimiwa majaji leo takribani mwaka mmoja baadaye, nimesimama mbele yenu majaji kuwaambia kwamba kwa sheria za Tanzania na kwa ushahidi uliotolewa mahakamani hapa jambo hilo haliwezekani.
Ninaomba nirudie nimesimama mbele yenu majaji kuwaambia kwamba kwa sheria za Tanzania na kwa ushahidi uliotolewa mahakamani niko hapa kuwaonesha kwamba hilo jambo haliwezekani.
Nilikamatwa katika mji wa Mbinga mkoa wa Ruvuma jioni ya siku ya tarehe 9 April ya mwaka jana 2025, na nilikamatwa nikizungumza kwenye mkutano halali wa hadhara wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA, Chama ambacho nimekiongoza tangu tarehe 22 January 2025… baada ya kukamatwa huko nilisafirishwa usiku huo huo hadi hapa Dar es salaam ambapo waheshimiwa majaji mchana wa kesho yake 10, April 2025 nilisomewa mashtaka kwenye kesi mbili zilizofunguliwa dhidi yangu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Lissu:Waheshimwa majaji katika kesi ya kwanza nilisomewa shtaka la uhaini kinyume na kifungu cha sheria ya kanuni ya adhabu kifungu 82 b, katika kesi ya pili nilisomewa shtaka la kutoa taarifa za uongo kinyume na kifungu cha 16 ya sheria ya makosa ya mtandao, kesi ambayo imenileta mbele yenu leo.
Hii inatokana na kesi ya kwanza niliyosomewa mahakama ya Kisutu yaani Uhaini, baada ya takribani miezi 4 na nusu ya mashauri katika mahamaka ya hakimu mkazi Kisutu, Mkurugenzi wa Mashtaka DDP aliwasilisha taarifa kwenye mahakama hii kuhusiana na hilo shtaka la uhaini, taarifa yenyewe ni ya tarehe 12, Agosti 2025.
Taarifa hii inanituhumu kwa mambo yafuatayo;
Kwamba nikiwa chini ya utiifu kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, nilitengeneza nia ya kuhamasisha Umma kuwezesha kuzuia uchaguzi mkuu wa 2025 kwa lengo la kuitishia serikali ya Jamhuri ya Muungani wa Tanzania, na nilidhihirisha nia hiyo kwa kitendo changu cha kutamka au kusema na kuchapisha maneno yafuatayo;
“Wanasema kitu kimoja sahihi hapa wanasema hivi msimamo huu unaashiria uasi, ni kweli kwa sababu tunasema tutazuia uchaguzi, tutahamasisha uasi, hii ndiyo namna ya kupata mabadiliko kwa hiyo tunaenda kukinukisha sana sana huu uchaguzi tutauvuruga, tutauvuruga huu uchaguzi kwa sababu tunaenda kukinukisha vibaya sana.”
Habari za asubuhi, karibu tena leo Septemba 23, kesi ya Lissu inaendelea
Kesi ya Lissu yaahirishwa, kusubiri Kingai
Lissu: Baada ya maelekezo ya mahakama, msajili
amekuja kuniona na kuniarifu kuhusu utekelezaji wa amri ya mahakama ya wito kwa
mashahidi.
Msajili amenieleza kuwa mashahidi wote watatu walipelekewa
wito Dodoma, lakini haikuwezekana kuwaserve kwa sababu inadaiwa wote watatu
wako nje ya nchi.
Msajili amesema kuwa kati ya hao watatu, mmoja ambaye ni
Kamishna wa Polisi Ramadhani Kingai, Mkurugenzi wa Upelelezi nchini Tanzania,
anatarajiwa kurejea nchini leo. Kwa hiyo, siku ya Ijumaa anatarajiwa kuwapo
mahakamani ili kutekeleza wito wa mahakama.
Kuhusu mashahidi wengine wawili, waheshimiwa majaji,
haijulikani watarudi nchini lini.
Katika mazingira hayo, napendekeza mahakama iahirishe shauri
hadi siku ya Ijumaa saa nane na nusu mchana, ili kipindi cha asubuhi niweze
kukitumia kushauriana na shahidi huyo niliyeelezwa atafika, ikiwa ni pamoja na
kuchukua maelezo yake.
Kuhusu waliobaki, tutamalizana na shahidi atakayekuwapo,
kisha mahakama itafanya maamuzi kuhusu hao wengine.
La mwisho, waheshimiwa majaji, ninafahamu jinsi ratiba ya
shauri hili ilivyo. Ninaomba na mimi twende kwenye final submissions vyovyote
itakavyokuwa. Kama mashahidi hao watakuja, naamini hatutachukua muda mrefu. Na kama tutamalizana na shahidi
atakayekuwapo, nitaeleza kama tusubiri wengine au la. Wasipokuja kabisa, suala
hilo litakuwa mikononi mwenu kwa sababu nyinyi ndio mmetoa amri ya wito.
Katuga: Kwa masikitiko, hatuna pingamizi.
Nakumbuka mahakama ilipoongeza muda ilisema wazi kuhusu suala hilo. Hata hivyo,
namwomba mshitakiwa ahakikishe mashahidi wake wanafika mahakamani.
Pia,
wasipofika mahakamani, asiseme kwamba atalizia suala hilo mahakama. Ni yeye
ndiye atakayeieleza mahakama anaomba nini katika mazingira hayo.
Jaji: Shauri limeahirishwa mpaka Ijumaa
saa nane kamili mchana.
Lissu aomba kukutana na mashahidi kabla ya kuwaita kizimbani
Lissu: Niliomba jana kuongea na wale mashahidi
wengine. Sitakuwa tayari kuleta shahidi kizimbani bila kuonana na kuzungumza
naye. Ninaleta ombi hili hapa kwa sababu haya ndiyo mazingira pekee ninayoweza
kukutana nao. Waheshimiwa majaji, naomba mwongozo wenu.
Jaji: Tumesikia. Kimsingi, tulitegemea utuambie una
mashahidi, lakini kwa sababu huna mawasiliano nao, na kwa kuwa tulishatoa amri
ya wito kwa mashahidi hao, tutalifanyia kazi suala hilo.