Kazi yangu ni kusema ukweli - Mnyika

Jaji: Shahidi unakumbushwa kwamba kiapo chako kinaendelea
Katuga: Unasema wewe ndio ulikiwakilisha chama kwenye kamati ya Bunge ya katiba na sheria?
Mnyika: Ndio
Katuga: Waambie waheshimiwa kama unakumbuka au hukumbuki moja ya pendekezo ulilotoa ni kushirikishwa wakurugenzi kwenye maswala ya uchaguzi
Mnyika: Ndio
Katuga: Waambie waheshimiwa kama unafahamu au hufahamu na mapendekezo yako yalipelekea wakurugenzi kuondolewa na kuwa maafisa wa uchaguzi
Mnyika: Sifahamu
Katuga: Waambie waheshimiwa kama chama mlipata nafasi ya kutoa maoni ya mbele ya kamati hiyo kufanya maboresho ya sheria
Mnyika: Kwa kuwa nilizimiwa mic sikutoa maoni
Katuga: Ulitoa maoni kwenye mabadiliko ya kikatiba kabla ya mabadiliko
Katuga: Mada ni jambo linalojadiliwa bado unasimama na msimamo mada na ajenda ni vitu viwili tofauti
Mnyika: Ndio ni vitu viwili tofauti Katuga kwa tafsiri hii unaimbia mahakama mkutano wa tarehe tatu haukuwa na agenda ulikuwa na Mada
Mnyika: Ndio hakukuwa na ajenda ni mada
Katuga: Kwa kuwa hakukuwa na agenda na ni mada kiongozi alikuwa na uhuru wa kuzungumza jambo lolote alilolipanga na kuamua kutekeleza
Mnyika: Mkutano ulikuwa na mada moja tu 'No reforms no election'
Katuga: Uliulizwa kama uasi ni kosa kisheria ukasema sio kosa na ukamnukuu Nyerere kuwa alisema vijana waasi dhidi ya Mifumo kandamizi
Mnyika: Sahihi
Katuga: Waambie majaji uelewa wako wa kisiasa neno uasi lina maana gani
Mnyika: Kupinga au kukataa kwa nguvu kubwa sana
Katuga: Kuhamasisha uasi dhidi ya uchaguzi tafsiri yake ni nini
Mnyika: Ni kukataaaa uchaguzi haramu kwa njia za kidemokrasia Katuga waambie waheshimiwa tafsiri yako ya uasi kama ndivyo ulivyowaambia waheshimiwa na kama kulikuwa na demokrasia
Mnyika: Nimesema na hayo maneno kidemokrasia yapo
Katuga: Mimi kazi yangu kuonesha ulivyo Muongo
Mnyika: Mimi kazi yangu kusema ukweli
Katuga: Hiyo tafsiri uliyoitoa ni kwa mujibu wa nani au nini?
Mnyika: Uelewa wangu kisiasa
Katuga: Mwaka Jana chama chako kilishiriki uchaguzi mkuu?
Mnyika: Tulizuiliwa kushiriki
Katuga: Waambie majaji kama unakumbuka ni kweli kwamba ulisikia mwenyekiti akiwaambia watia nia kama unategemea kuwa mbunge mwaka huu sahauni
Mnyika: Aliwaambia
Katuga: Mwenyekiti na yeye alisema yeye alikuwa na nia ya kugombea urais ila ame ahirisha
Mnyika: Hiyo sentensi siikumbuki
Katuga: Kama chama cha siasa na wewe ni mtendaji mkuu mlijiandaa kushiriki uchaguzi wa mwaka jana 2025?
Mnyika: Tulijiandaa vizuri sana
Katuga: Waambie majaji kama mlijiandaa kushiriki kwa mujibu wa katiba na marekebisho yaliyofanyika
Mnyika: Tulijiandaa kwa mujibu wa katiba iliyipo na mapungufu yake
Katuga: Unajua kuwa kwa haki hiyo waliyokuwa nayo CHADEMA na vyama vingine vilikuwa nayo?
Mnyika: Sahihi
Katuga: Mwenyekiti alisema tutazuia uchaguzi kwa njia ya kidemokrasia
Mnyika: Sikutumia moja kwa moja maneno unayoyasema ila nilieleza njia za kidemokrasia
Katuga: Sasa katika ushahidi wako waambie majaji kwamba njia zilizosemwa na mwenyekiti za kuzuia uchaguzi kidemoktasia ni njia moja, mbili, tatu,
Katuga: Waambie majaji kama kuhasisha uasi ni njia ya kidemokrasia kupinga uchaguzi usifanyike
Mnyika: Ndio ni njiaa ya kidemokrasia
Katuga: Umekubali kuwa vyama vingine vina haki ya kushiriki uchaguzi
Mnyika: Uchaguzi huru wa haki
Katuga: Waambie majaji ulikuwa wa aina gani
Mnyika: Haukuwa wa huru wala wa haki na jaji nyalali alisema…
Katuga: Sikilizaaaaa, Waambie majaji kwa maneno yako vilikuwa na haki ya kushiriki uchaguzi
Mnyika: Siwezi kuvitolea maoni vyama vingine
Katuga: Kwa elimu yako hiyo ni demokrasia gani itakayotumika kumzuia mtu anayeenda kupiga kura
Mnyika: Kuahirisha uchaguzi na njia nyingine za kidemokrasia
Katuga: Uliwahi kufungua kesi kupinga uchaguzi?
Mnyika: Hapana sijawahi
Katuga: Ni njia gani ya kidemokrasia isiyokuwa ya mahakamani inayoweza kumzuia mtu kupiga kura
Mnyika: Njia zipo nyingi, kususia uchaguzi na njia nyingine sio vurugu sio fujo wala sio nini
Katuga: Waambie majaji mtu anayekwenda kupiga kura kama hakuna zuio mahakamani njia pekee ya kumzuia ni kwa kutumia njia ya nguvu zote za uasi
Mnyika: Sijui
Katuga: Kwa mujibu wa katiba ya CHADEMA, Je inaruhusu mtu kuamini anacho amini
Mnyika: Ndio inaruhusu
Katuga: Je katiba ya CHADEMA inaheshimu imani ya mtu ilimradi asivunje sheria?
Mnyika: Ndio
Katuga: Je kwa mujibu wa katiba ya CHADEMA inaelekeza mtu asiamini anachokiamini ilimradi asivunje sheria?
Mnyika: Inaelekeza
Katuga: Mwenyekiti aliposema tutakinukisha tutahamasisha uasi alilenga kufanyike mabadiliko ambayo nyie ndio mnaamini ni mabadiliko yanayofaa?
Mnyika: Sielewi umeuliza nini, rudia swali lako
Katuga: Mwenyekiti aliposema tutakunukisha, tutahamasisha uasi alilenga kufanyike mabadiliko ambayo nyie ndio mnaamini ni mabadiliko yanayofaaa?
Mnyika: Hapana
Katuga: Baada ya mwenyekiti kupata kesi hii nani aliendeleza hamasa ya no reforms no election
Mnyika: Kamati kuu ya Chama, viongozi wa kamati kuu
Katuga: Je kiongozi aliyeongoza hii nia ni pamoja na makamo mwemyekiti?
Mnyika: Ndio
Katuga: Makamo mwenyekiti anaitwa Nani?
Mnyika: John Wegesa Heche
Katuga: Waambie majaji kama na yeye ulikuwa unamuandalia press conference na mikutano
Mnyika: Hapana sikumuandalia
Katuga: Waambie majaji kama hao viongozi waliendelea kuhamasisha umma kuhusu nia hiyo ya kuzuia uchaguzi
Mnyika: Tarehe tisa mwezi wa sita ndio ilikuwa mwisho kabla ya kuzuiwa kufanyika shughuli za kisiasa
Katuga: Waambie majaji kama unajua makamo mwenyekiti bara aliwahikuongea na East Africa Radio kuhusu nia hiyo ya kuzuia uchaguzi
Mnyika: Sijui
Katuga: Unajua kupitia hiyo redio alitangaza uchaguzi wa 2025 hautokuepo na mko determined?
Mnyika: Sijui
Katuga: Waambie majaji kama unajua kwenye uchaguzi wa mwaka jana kulikuwa na jaribio la kuzuia uchaguzi kwa kufanya fujo
Mnyika: Kulikuwa na mauaji ndio ninachojua
Katuga: Kulikuwa na jaribio la kuzuai uchaguzi kwa kuchoma vituo na miundombinu mingine?
Mnyika: Sijui
Katuga: Siku ya uchaguzi mwaka jana ulikuwa nchini au nje ya nchi
Mnyika: Nilikuwa nchni
Katuga: Je ulijitokeza kupiga kura?
Mnyika: Sikujitokeaza
Katuga: Kwa imani hiyo imedhihirisha ile nia ya kuzuia uchaguzi
Mnyika: Sio sahihi
Katuga: Unajua au haujui kuna mali za watu zilichomwa moto?
Mnyika: Sijui nilisikia kwenye vyombo vya habari
Katuga: Unajua au haujui vituo vya mwendo kasi vilichomwa?
Mnyika: Nimeviona vimeungua
Katuga: Ni sahihi au sio sahihi kwa umma kutafsiri kauli zile na kufanya vitendo vya uvunjifu wa amani
Mnyika: Sifahamu
Katuga: Je, ni haki sio haki kwa umma kutafsiri waonavyo maneno ya mwenyekiti?
Mnyika: Ni haki
Katuga: Ni haki ya Jamii kuchochoke na kufanya vurugu
Mnyika: Sio haki
Katuga: Waambie majaji ni haki au sio haki
Mnyika: Sio haki
Katuga: Jaji chande alisema matukio ya 2025 yalipelekea vifo vya watu
Mnyika: Nilisikia
Katuga: Waeleze majaji kama ulisikia akisema matukio yale yalihamasishwa na kutokana na maneno ya wanasiasa
Mnyika: Sifahamu
Katuga: Kwa mujibu wa hotuba ya Jaji chande waambie majaji kama hotuba hii inafanana na kile kilichopelekea machafuko
Mnyika: Hapana
Katuga: Waeleze majaji kama Lissu alihamasisha uasi ili kuwa na uchaguzi huru na wa haki
Mnyika: Hapana
Katuga: Jaji chande aliposema vurugu zile zilitokana na maneno ya kudai sheria ya uchaguzi
Mnyika: Hapana hakuyasema na mwenyekiti hakuhusika na vurugu
Katuga: Uliwahi kuwa mbunge, je ni wakuteuliwa au kuchaguliwa?
Mnyika: Kuchaguliwa
Katuga: Kwa uzoefu wako kuhusu bunge unauelewa wa katiba na sheria?
Mnyika: Ndio ninauelewa
Katuga: Waambie majaji mahakama ni chombo cha mwisho kwa mujibu wa sheria
Mnyika: Ndio
Maelezo zaidi:






















