Karibu katika matangazo ya moja kwa moja ya kesi ya uhaini ya Tundu Lissu 04.09.2026.

Leo tunaendelea na maswali ya dodoso kwa shahidi namba tatu Aman Sam Golugwa ambaye jana alimaliza kutoa ushahidi wake sasa ni zamu ya Jamuhuri kumuhliza maswali.
Mahakama imesema itahitaji muda wa kutosha ili iweze kutoa maamuzi sababu hili ni shauri la namna yake.
Na Waandishi wa BBC Swahili

Leo tunaendelea na maswali ya dodoso kwa shahidi namba tatu Aman Sam Golugwa ambaye jana alimaliza kutoa ushahidi wake sasa ni zamu ya Jamuhuri kumuhliza maswali.

Lissu: Turudi kwenye Watazamaji walitumia muda wao Kimataifa, watazamaji wote hao walisemaje juu kufunguliwa kwangu kwa kwsi hii ya Uhaini.
Golugwa: Kwanza walisikitishwa na walisema kesi hii ya uongo na hawakuona mazingira ya Uhaini kwa kile walichokisikia katika maneno aliyoyazungumza Mh Tundu Lissu na hivyo wakataka na kuzisihi mamlaka zimwachilie huru bila masharti yoyote
Lissu: Waeleze waheshimiwa majaji baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa limesemaje juu ya kesi hii?
Golugwa: Limesema kukamatwa kwangu kwa Lissu haikua halali na kitendo cha kukamatwa kwake kinaminya uhuru na haki ya kujieleza na shtaka alilofunguliwa ni shtaka katili lenye lengo la kumuumiza na hivyo kutaka mamlaka zimwachilie kwa sababu kesi inaonekana ni ya kisiasa.
Lissu: Waeleze waheshimiwa majaji kikao cha Mawaziri wa Jumuiya ya Madola kinasemaje juu ya kesi hii.
Golugwa: Waheshimiwa majaji kikao cha mawaziri kimesema kwanza kesi hii inadhihirisha unyonyaji wa Demokrasia, kesi hii ni ya kisiasa, na ni batili na hivyo Tundu Lissu aachiliwe bila mashart yoyote.
Lissu: Sasa turudi kwenye mkutano wa tarehe 3 Aprili 2025.
Kwenye ushahidi wako jana ulisema Mkutano huu uliandaliwa na Sekretariet ya chama kwa wazo la Katibu Mkuu.
Lissu: Waeleze waheshimiwa majaji watu wengine waliohudhuria
Golugwa: Watu wengine waliohudhuria mkutano huo walikuwamo viongozi wa chama ambao hawakua watia nia na waandishi wa habari walioalikwa.
Lissu: Wafafanulie waheshimiwa majaji ukisema viongozi wa chama ambao hawakuwa watia nia una maana gani?
Golugwa: Ninamaanisha walikuwepo viongozi wa Chama kwenye ngazi ya Jimbo, Mkoa na Wilaya.
Lissu: Waeleze waheshimiwa majaji kama viongozi wa Chama ni hao tu.
Golugwa: Waheshimiwa majaji walikuwepo pia viongozi wakuu ambao sio watia nia nikiwemo mimi mwenyewe.
Lissu: Shahidi waeleze waheshimiwa majaji wote uliowataja walijuaje kuna mkutano?
Golugwa: Waheshimiwa majaji nianze na viongozi wakuu, mimi ndiye niliyefanya jukumu la kuwapigia simu viongozi wafuatao, Mwenyekiti Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti Bara John Heche, Makamu Mwenyekiti Zanzibar Said Mzee Saidi na Naibu Katibu Mkuu.
Hawa niliwapigia simu mimi mwenyewe na kuwaambia kuhusiana na uwepo wa mkutano huo. Wengine waliokuwepo ukumbuni walialikwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Chama Brenda Rupia ambaye ni mjumbe wa Sekretariet.
Lissu: Waeleze waheshimiwa majaji wakati yote hayo yanafanyika mimi nilikua wapi?
Golugwa: Waheshimiwa majaji wakati haya yote yanafanyika Tundu Lissu alikua kwenye Operesheni ya Chama iliyokuwa inaendelea Kanda ya Nyasa ya No Reforms No Elections.
Lissu: Waeleze Waheshimiwa majaji kama mimi nilishiriki kwa namna yoyote ile.
Golugwa: Waheshimiwa Majaji Tundu Lissu hakushiriki kuanzia kwenye maandalizi ya kikao hiki, na hata katika kuwasiliana na kutuma mialiko kwa hao watia nia.
Lissu: Waeleze waheshimiwa majaji ushiriki wangu katika kuwaalika waandishi wa habari
Golugwa :Tundu Lissu hakushiriki katika kuwaalika waandishi wa habari kuja katika mkutano huu
Lissu: Imedaiwa kwenye Mahakama hii kwamba mimi ndiye niliyeitisha hao watu kwenye mkutano.
Golugwa: Waheshimiwa majaji hayo madai yatakua ya uongo, ya upotoshaji.Tundu Lissu Hakuhusika.
Lissu :Waeleze waheshimiwa majaji uwepo wa Waandishi wa Habari katika mkutano huo
Golugwa: Walikuwepo waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali, wa Television, Magazeti, Online Television pamoja na Redio
Lissu: Waeleze waheshimiwa majaji vyombo vya habari vilivyowalikishwa.
Golugwa: Kwa kumbukumbu nakumbuka kulikua na Clouds Tv, nakumbuka uwepo wa Jambo Tv, nakumbuka uwepo wa Chanzo TV, ITV na ninakumbuka kuwaona Waandishi wa habari wa gazeti la Mwananchi.
Lissu: Waeleze waheshimiwa majaji, hao waandishi walialikwa na nani
Golugwa: Waheshimiwa majaji walialikwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi Brenda Rupia ambaye ni mjumbe wa Sekretariet.
Lissu: Waeleze waheshimiwa majaji kwa kumbukumbu zako uwepo wa masharti yoyote waliopewa hao waandishi wa Habari.
Golugwa: Hapakuwa na masharti yoyote ambayo wamepewa
Lissu: Waeleze waheshimiwa majaji kwa kumbukumbu zako uwepo wa maelekezo kutoka kwangu au kwa kiongozi yoyote juu ya waandishi wa habari juu ya namna ya kufanya kazi
Golugwa: Hapakuwa na maelekezo kutoka kwa Tundu Lissu au kiongozi yoyote yule kwenda kwa Waandishi wa habari kuhusiana na wao kufanya kazi zao.
Lissu: Waeleze waheshimiwa majaji uwepo wa matangzo ya moja kwa moja yaliyofanywa kwenye mkutano huo yaliyofanywa na vyombo vya habari.
Golugwa: Ni kweli kulikuwa na matangazo ya moja kwa moja
Lissu: Waeleze waheshimiwa majaji vyombo vya habari vilivyorusha matangazo ya moja kwa moja, kama unavikumbuka.
Golugwa: Kwa kumbukumbu zangu waliorusha matangazo ya moja kwa moja ni Jambo Tv na Chanzo Tv
Lissu: Inadaiwa mimi ndiye niliyerusha matangazo hayo kwenye Jambo Tv
Golugwa : Ni uongo, sio kweli huo ni upotoshaji.
Lissu: Waeleze waheshimiwa majaji uhusika wangu kwenye kuchapisha maneno yaliyopo kwenye hati ya mashtka kwenye Jambo Tv.
Golugwa: Hakuna uhusika wowote kwamba yeye ndiye aliyechapisha maneno hayo kwenye Jambo Tv.
Lissu: Kwa ufahamu wako maneno haya yalichapishwa na nani kwenye Jambo Tv.
Golugwa: Maneno hayo yamechapishwa na Mwandishi wa Habari ambaye tulimualika wa Jambo Tv
Lissu: Kwa hiyo Shahidi hii tuhuma kwamba mimi ndiye niliyechapisha maneno haya unaizungumziaje?
Golugwa: Hii tuhuma ni uongo ilikua na nia ya kuzorotesha Operesheni iliyokuwa inaendelea hakuchapisha Tundu Lissu.
Lissu: Inadaiwa kwamba nilichapisha hayo maneno kwenye mtandao wa Jambo Tv nikiwa na nia ya kuitishia Serikali ya Jamhuri ya Muungano, waeleze Waheshimiwa majaji kama kuna maneno Serikali ya Jamhuri ya Muungano
Golugwa: Nimeyasikia maneno hapo na mimi nimekuwepo kwenye huo mkutano hakuna neno Serikali ya Jamhuri ya Muungano
Lissu: Waeleze waheshimiwa majaji katika hayo maneno uwepo wa neno Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Golugwa: Waheshimiwa majaji hilo neno halipo
Lissu:Kwa ufahamu wako mtu akisema msimamo huu msimamo huu unaashiria uasi anakua ametenda kosa gani?
Golugwa: Hakuna kosa lolote ambalo atakuwa ametenda kwa ufahamu wangu.
Lissu: Kuna maneno yamezungumzwa kwamba tarehe 29 Oktoba vituo vimechomwa moto, tutaumiza watu, sasa katika maneno niliyokusomea waeleze waheshimiwa majaji uwepo wa maneno tutachoma vituo vya mwendokasi.
Golugwa: Katika maneno niliyosomewa hakuna neno lolote kwamba tutaenda kuchoma vituo vya mwendokasi, hakuna.
Lissu: Katika maneno niliyokusomea, waeleze waheshimiwa majaji uwepo wa maneno tutachoma vituo vya kupigia kura
Golugwa: Hakuna maneno hayo.
Lissu: Waeleze aheshimiwa majaji kwa kumbukumbu zako iwapo ulimsikia Jaji Chande alitaja waliosababisha hivyo vifo.
Golugwa : Waheshimiwa kwa kumbukumbu zangu sikumbuki iwapo aliwataja waliosababisha vifo.
Lissu: Waeleze waheshimiwa majaji juu ya sababu alizozitoa jaji mkuu kuhusu mauaji hayo.
Golugwa: Kwa kumbukumbu zangu sababu alizozitoa ni pamoja na madai ya Katiba Mpya, masuala ya utekaji na watu kupotea na manung’uniko ya muda mrefu ya wananchi ambayo hayajakua yametatuliwa.

Lissu: Sasa shahidi, kati ya waangalizi wote wa uchaguzi uliowataja, walizungumziaje matukio ya mauaji ya wananchi?
Golugwa: Kwa ujumla, waangalizi walisema kuwa vyombo vya dola, hasa polisi, waliwapiga waandamanaji na kuwazuia waangalizi kutimiza wajibu wao. Pia waliwapiga na kuwanyang’anya vifaa vyao.
Lissu: Walisema nini kuhusu mauaji ya wananchi?
Golugwa: Walisema kuwa vyombo vya dola vilihusika katika mauaji ya waandamanaji, na hivyo walitaka kuwe na uwajibikaji kwa mauaji yaliyofanyika.
Lissu: Uchaguzi huu uliendeshwa na kusimamiwa na chombo gani?
Golugwa: Uliendeshwa na kusimamiwa na Tume Huru ya Uchaguzi.
Lissu: Mwenyekiti na watendaji wa tume hiyo wanapatikanaje?
Golugwa: Wanapatikana kwa kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Lissu: Waeleze majaji mkurugenzi wa tume hiyo anapatikanaje.
Golugwa: Mkurugenzi wa tume hiyo huteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Lissu: Waeleze majaji wasimamizi wa uchaguzi wanapatikanaje.
Golugwa: Ni watumishi wa umma na huteuliwa kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa na mamlaka husika za uchaguzi.
Lissu: Waeleze majaji maafisa wasimamizi wa vituo vya kupigia kura (presiding officers) wanapatikanaje.
Golugwa: Wote huteuliwa na Tume Huru ya Uchaguzi.
Lissu: Waangalizi wote walisemaje kuhusu uchaguzi huo?
Soma zaidi:

Golugwa: Walisikitishwa na kuzimwa kwa mitandao ya mawasiliano, pamoja na taarifa za mauaji. Pia walieleza kuwa uchaguzi huo uligubikwa na matukio ya utekaji na kupotea kwa watu kabla ya kupigwa kwa kura.
Lissu: Watazamaji wa Jumuiya ya Madola walisemaje?
Golugwa: Waheshimiwa Majaji, sikuiona taarifa ya Jumuiya ya Madola, lakini nilisikia kauli ya Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola.
Lissu: Kauli hiyo ya Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola ilisemaje?
Golugwa: Alisema amesikitishwa na vurugu na mauaji yaliyotokea, na kwamba Jumuiya ya Madola itaendelea kufuatilia kwa karibu tukio hilo.
Lissu: Katika ushahidi wako wa jana kuhusu uchaguzi, waeleze majaji matokeo ya uchaguzi huo yalivyokuwa.
Golugwa: Mgombea urais wa CCM alitangazwa kupata kura milioni 31.6, sawa na asilimia 98.6.
Lissu: Na wagombea wengine walipata kiasi gani?
Golugwa: Waheshimiwa Majaji, waligawana asilimia 2.4 zilizobaki.
Lissu: Matokeo ya ubunge yalikuwaje?
Golugwa: Sifahamu.
Lissu: Ya udiwani yalikuwaje?
Golugwa: Sifahamu.
Lissu: Sasa waeleze majaji kuhusu Wakfu wa Thabo Mbeki. Walisemaje?
Golugwa: Waheshimiwa Majaji, Wakfu wa Thabo Mbeki ulizungumzia mambo manne:
Maelezo zaidi:

Lissu: Waeleze majaji, kwa ufahamu wako, waangalizi wa uchaguzi wa SADC walisema nini kuhusu uchaguzi huo?
Shahidi: Walisema uchaguzi wa Tanzania umeshindwa kukidhi vigezo vya uchaguzi wa kidemokrasia. Pia kulikuwa na vitisho dhidi ya viongozi wa vyama vya upinzani, hivyo mazingira ya ushindani hayakuwa sawa. Aidha, hakukuwa na uwazi katika mchakato mzima wa uchaguzi. Kulikuwa na udanganyifu katika mchakato wa uchaguzi na vurugu siku ya uchaguzi. Hivyo, uchaguzi wa Tanzania umekosa uhalali wa kuitwa uchaguzi wa kidemokrasia.
Lissu: Waeleze majaji, watazamaji wa uchaguzi wa Jumuiya ya Ulaya (EU) walisemaje kuhusu uchaguzi huo?
Shahidi: Watazamaji wa Jumuiya ya Ulaya, kwanza, walisema wamesikitishwa na matukio ya vurugu yaliyotokea siku ya uchaguzi na yaliyosababisha kuvurugika kwa mchakato wa uchaguzi. Pia wamesikitishwa na uharibifu wa mali, kuzimwa kwa mawasiliano ya mtandao, na taarifa za mauaji.
Soma zaidi:
Lissu: Unasema kwamba mkutano uliandaliwa na Sekretariet, waeleze waheshimiwa majaji hii Sekretariet ni akina nani?
Golugwa: Hii Sekretariet ninayoizungumzia ni Katibu Mkuu wa Chama, Manaibu Katibu wawili kwa maana ya Bara na Zanzibar, Makatibu wa Mabaraza matatu ya chama, BAWACHA, BAVICHA na BAZECHA.Pia Wakurugenzi wa Chama pamoja na wataalam wawili ambao wameteuliwa na Mwenyekiti kuwa sehemu ya Sekretariet ya chama.
Lissu: Jumla watu wangapi hapo kwa hesbau yako
Golugwa:14 Lissu: Kwa muundo wa Chama Sekretariet ya Chadema ni chombo cha aina gani?
Golugwa: Sekretariet ya Chadema ndicho chombo cha kiutendaji kinachofanya kazi kila siku za kichama kwa niaba ya Kamati Kuu ya Chama
Lissu:Sasa Shahidi umesema Katibu Miuu alikuja na wazo kwamba muandae mkutano muwaandae watia nia hao watia nia ni akina nani?
Golugwa: Hao watia nia ni wanachama wa Chadema ambao aidha walipitishwa kuwa wagombea kwenye uchaguzi wa 2020 katika nafasi za udiwani, ubunge na Urais na kwamba bado nia yao ya kutaka kugombea nafasi hizo bado walikuwa nayo. Na wengine katika kundi hilo la watia nia ni wale ambao hawajawahi kugombea wala kupitishwa kwenye nafasi hizo nilizozitaja kwa maana mwaka 2025 na wao wakataka kutia nia wapitishwe kugombea nafasi hizo. Hao ndio watia nia.
Lissu: Waeleze waheshimiwa majaji hao watia nia walikua wanatia nia ya kugombea nafasi gani
Golugwa:Waheshimiwa majaji hao watia nia walikuwa wanatia nia ya kugombea kwenye uchaguzi wa mwaka 2025.
Lissu:Waeleze waheshimiwa majaji lengo la kuwaita hao watia nia kwenye huo mkutano wa tarehe 3 Aprili lilikuwa lengo gani?
Golugwa: Lengo lilikuwa ni kuwaeleza na kuwafafanulia juu ya msimamo wa Chama uliopitishwa na mkutano kwa maana ya wazo la No Reforms No Elections, na msimamo huo ukawa umefafanuliwa na Kamati Kuu ya chama kwa kuazimiwa hilo ndilo lilikuwa lengo.
Lissu: Waeleze waheshimiwa majaji unaposema No Reform No Elections, huu msimamo ulikuwa unahusu nini hasa?
Golugwa: Msimamo huu ulianza au ulizaliwa baada ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa Mwaka 2024.
Nikiwa Katibu wa Kanda ya Kaskazini, Katibu Mkuu alituambia Makatibu wa Kanda atuandikie ripoti ya uchaguzi wa Serikali za mitaa jinsi ulivyofanyika, na mimi kama mtendaji ambaye nilikuwa sehemu ya uchaguzi huo kwa kusimamia kanda ya Kaskazini nilitoa ripoti kwa kuonesha madudu mengi ya hivyo yaliyojitokeza.
Na Katibu Mkuu alitutaka tuandike maoni yetu ya kuhusiana na nini chama kifanye kutokana na hayo yaliyojitokeza, kwa hivyo mimi kwenye ripoti niliandika na waheshimiwa majaji naomba nitumie maneno exactly maneno niliyoandika yalikuwa maneno makali “Kwa ushenzi huu niliouona chama kisishiriki uchaguzi mwingine wowote mpaka kushinikiza mabadiliko kwenye mifumo ya uchaguzi”.
Na Makatibu wenzangu kutoka katika kanda 9 kila mmoja kwa lugha yake wote tulitoa taarifa au ripoti yenye pendekezo zinazofanana na ndipo Kamati Kuu ikaketi ikayachakata mapendekezo ya Makatibu wa Kanda na wajumbe wenyewe wa Kamati Kuu ikatafakari kwa jinsi wanavyojua, basi nadhani tarehe 10 Desemba 2024, Mwenyekiti wa Chama wakati huo Mh. Freeman Mbowe akatoa tamko rasmi la chama, msimamo wa Kamati Kuu yaliyoazimiwa kwamba hatutakuwa tayari kwenda kwenye uchaguzi mwingine wowote bila mabadiliko kwenye mifumo ya uchaguzi.
Lissu: Shahidi hebu waeleze waheshimiwa majaji kwa kifupi ni ushenzi gani uliouona.
Golugwa: Waheshimiwa majaji ushenzi ni mwingi.
Lissu:Sasa umekuwa ndani ya hiki chama kwa miaka mingapi?
Golugwa: Nimeingia kwenye chama hiki toka 2007 mpaka leo nimekuwa mwanachama wa chama hiki.
Lissu: Naomba uwaeleze aheshimiwa majaji mtu anapataje nafasi ya Naibu Katibu wa Chadema Bara.
Golugwa: Ili mtu kuwa Naibu Ktibu Mkuu wa Chadema mbali na uanachama wake kuaminika jina lke litapendekezwa na Mwenyekiti, maana yake mwenyekiti atapendekeza mtu ambaye anaona ana uwezo na jina lake litapelekwa mbele ya Baraza la Chama, na kisha wajumbe wa Baraza Kuu watafanya wajibu wao wa kuthibitisha wasifu na uwezo huyo Mwanachama aliyependekezwa.
Lissu: Waeleze Waheshimiwa majaji majukumu ya Naibu Katibu Mkuu wa Chadema
Golugwa: Wajibu wa Naibu Katibu Mkuu Chadema kwanza ni Msaidizi wa Katibu Mkuu anamsaidia Katibu Mkuu, pili ndiye mwandishi wa kumbukumbu za vikao vya chama na tatu Naibu Katibu Mkuu amepewa mwongozo kwenye itifaki ya chama kwamba ndiye Mkuu na msimamizi wa itifaki ya chama katika vikao na mikutano ya chama
Lissu: Sasa Shahidi tuache hayo ya wasifu ya chama kidogo, waeleze Waheshimiwa majaji wasifu wako wa kitaaluma
Golugwa: Waheshimiwa Majaji, Elimu yangu ya chuo nimesoma masuala ya Uhasibu
Lissu:Umesoma Uhasibu katika chuo gani?
Golugwa:Nimesoma Katika Chuo cha Uhasibu Arusha ngazi ya Diploma
Lissu:Sasa mimi naskia kuna makelele kwenye masuala ya chama nataka uwaeleze waheshimiwa majaji uzoefu wako katika kazi hiyo ya Uhasibu.
Golugwa: Nimefanya kazi ya Uhasibu nikianza na ngazi ya Account Assistant na nimefanya kazi ya Uhasibu toka 2011 mpaka 2015 kwenye maeneo tofauti tofauti.
Lissu: Nataka tuzungumzie kesi, hii kesi ya uhani inayonikabili, ninatuhumiwa kwamba kwenye mkutano uliofanyika tarehe 3 Aprili 2025 nilitoa maneno yenye nia ya kuitishia serikali ya Jamhuri ya Muungano yanasema hivi “wanasema kitu kimoja sahihi hapa, wanasema hivi msimamo huu unaashiria uasi ni kweli tutahamasisha Uasi…… Swali langu waeleze waheshimiwa majaji kama unaufahamu huu mkutano.
Golugwa: Huo mkutano ninaufahamu.
Lissu: Waeleze waheshimiwa majaji huo mkutano uliandaliwa na nani na ulifanyikia wapi.
Golugwa: Huu mkutano uliandaliwa na Sekretariet ya chama baada ya Katibu Mkuu kuleta wazo kwenye kwamba watia nia ni wadau muhimu hivyo tuandae mkutano tukutane nao na Sekretariet ikafanya maandalizi na mkutano ukafanyika kwenye ukumbi wa makao makuu ya chama mikocheni Dar es salaam.

Anakula kiapo na kuanza kutoa ushabihidi akiongozwa na mshtakiwa.
Aman Sam Golugwa Naibu katibu mkuu chadema bara tangu mwaka 2022.
Kabla ya hapo nilikuwa katibu mkuu Chadema kanda ya Kaskazini tangu February 2013.
Lissu: Unaposema kanda ya kaskazini una maanisha nini?
Golugwa: Unaposema kanda ya kaskazini unamaanisha mikoa minne Tanga, Arusha, Kilimanjaro na Manyara kwa muundo wetu wa kichama.
Lissu: Waeleze majaji kabla ya kuwa Katibu kanda ya Kaskazini ulikuwa nani?
Golugwa: Waheshimiwa majaji nimeshika pia nafasi ya mwenyekiti mkoa wa Arusha 2019 - 2019.Waheshimiwa majaji kabla ya hapo toka 2008 mpaka 2014 nilikuwa Katibu wa mkoa wa Arusha.
Lissu: Waeleze majaji kama kuna nafasi nyingine yoyote nje ya hizo
Golugwa: Mwaka 2020 niliteuliwa na chama kuwa campaign manager wa aliyekuwa mgombea urais kupitia chadema,mheshimiwa Tundu Lissu.

Katuga: Waheshimiwa hakukuwa na hilo swali akaulizwa shahidi hotuba ya mwenyekiti na vurugu za Oktoba zilikuwa zinafanana au la sasa hii ni re-examination
Lissu: Hizi notes nimeandika mwenyewe ila kama wakili anasema hivyo naomba nisomewe rekodi ya mahakama kwenye hilo na jana niliomba nipewe rekodi ya kesi
Jaji: Utapewa mapema sana leo.
Jaji anamsomea.
Lissu: Iko sawasawa sina haja ya kuuliza tena hilo swali.
Jaji: Tuendelee
Lissu: Uliulizwa maswali kuhusu mimi na wewe kukamatwa mbeya 2024 ukasema mimi nilipelekwa kusikojulikana kwanini ulisema hakujulikani?
Mnyika: Siku hiyo ya tarehe 11 mwezi wa kumi na mbili ulipochukuliwa mbele yangu Ma RPC wa mbeya hawakutoa taarifa unapelekwa wapi lakini baadaye nilisema ulipelekwa DSM na kisha central na hatua nyingine.
Lissu: Shahidi uliulizwa kuhusiana na hotuba yangu na lengo la hotuba yangu ilikuwa ni kushinikiza serikali kufanya hayo mabadiliko ya kisheria ukasema hapana hilo halikuwa lengo naomba ufafanue.
Mnyika: Lengo lilikuwa kuwaunganisha Watanzania na wadau wote wa demokrasia kuungana mpaka serikali ifanye mabadiliko.
Lissu: Uliulizwa kama kuhamasisha uasi ni njia ya kidemokrasia na ukasisitiza ni njia ya kidemokrasia
Mnyika: Uasi ni kupinga si kukataa kwa nguvu kubwa na kufanya hivyo kwa njia za kidemokrasia kwa kutumia haki za kisiasa kwa kufuata sheria za nchi na mikataba ya kimataifa ambayo nchi yetu imeridhia.
Lissu: Sasa shahidi uliulizwa na wakili Katuga unakubaliana naye kuhamasisha uasi ni kosa hujasema sio kosa mwalimu nyerere alisema vijana waasi mifumo kandamizi.
Mnyika: Kwa maneno hayo ya mwalimu nyerere kufanya uasi haikuwa kisa ndio muktadha niliotumia kwamba kupinga mifumo kandamizi sio kosa na kuasi dhidi ya mifumo hiyo sio kosa.
Lissu: Ulisema sio kila mkutano unakuwa na Ajenda hebu fafanua.
Mnyika: Mkutano wa chama huo maalumu ulilenga kuwaelimisha watia nia na uliitwa na Katibu Mkuu na kuusimamia mkutano kama huo hauandikwi muhtasari ambao kwa kawaida unakuwa na mahali pa kuidhinisha kikao kijacho mkutano kama huo unakuwa na taarifa kwa ajili ya maamuzi.
Lissu: Uliulizwa kama mliweka masharti namna ya kurusha huo mkutano na iwapo jambo tv walikiuka makubalisno ukasema hapana ukaulizwa kama waandishi walikuwa wanaonekana wazi yote ukasema ndio nataka ufafanue uliposema uamuzi wa kurusha matangazo yale haukua uamuzi wenu ulikuwa uamuzi wa waandishi wale.
Katuga: Mbona sielewi hilo swali.
Jaji: Ngoja arudie swali tusikie.
Lissu: Waheshimiwa majaji wala sio swali jipya alisema uamuzi wa kurusha ulikuwa wa waandishi wenyewe na hakukuwa na masharti ya chama.
Jaji: Na yeye alijibu ndio kwamba hawapangiwi ni utashi wao.
Lissu: Kama rekodi ya mahakama iko hivyo basi naedelea, naelekea kumaliza.
Jaji: Mawili ya mwisho.
Lissu: Hahaha sijasema hivyo ila naelekea kumaliza.
Lissu: Uliulizwa na wakili Katuga kama mlikuwa mnapinga wakurugenzi kutumika kwenye uchaguzi na marekebisho ya sheria yaliyofanya ukasema ni kweli kilichofanyika ni kibaya zaidi ulimaanisha nini?
Lissu: Ulipoulizwa kuhusu uhuru wa vyombo vya habari ulimaanisha nini?
Mnyika: Uhuru nilimaanisha vyombo vya habari ndio wamiliki wa habari walioichukua sababu wana uhuru wa kuchapisha au kutochapisha ila pia wana uhuru wa kuivichakata pia.
Lissu: Uliulizwa juu ya maneno ninayoshitakiwa kwayo yale maneno maarufu ukaulizwa huoni hayo maneno yanalingana na yaliyotokea tarehe 29 Oktoba ukasema hayana uhusiano naomba ufafanue hilo jibu.
Mnyika Maneno yalitolewa tarehe tatu kabla ya uchaguzi na mshtakiwa aliyetoa maneno alikamatwa tarehe 9 ya mwezi wa nne mwaka 2025 na akashikiliwa rumande kipindi chote mpaka sasa.
Lissu: Shahidi unakumbuka ulisomeshwa kamusi juu ya neno uasi uliambiwa usome maana ya neno uasi na ukaulizwa swali kwamba hiyo tafsiri pekee ya neno uasi nataka usome tena kisha ufafanue soma kwa makini soma kila kilichoandikwa
Mnyika: Uasi kitendo cha uvunjaji wa sheria kinachofanywa na kikundi cha watu kinachotaka kubadili mfumo wa kisiasa wa nchi yao
Lissu: Sasa fafanua hilo jibu
Mnyika: Uasi sio kupinga dola pekee hata kupinga mifumo ndani ya taasisi ni uasi.
Uliulizwa maswali mengi sana kuhusu uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025 na mawakili wote wa serikali na jibu lako haukuwa uchaguzi huru na wa haki elezea majibu yako elezea bila kutaja ripoti ya waziri wa serikali asipate presha
Katuga: Na kisukari pia
Lissu: hahaha na kisukari hahahahha
Mnyika: Sababu mazingira yake na uchaguzi wenyewe hayakuwa huru na haki
Lissu: Uliulizwa kuhusu kesi ya uhaini ya Mwenyekiti Mbowe ukasema ilikuwa ya uongo licha ya kupatikana na kesi ya kujibu hebu fafanua hilo jibu
Mnyika: Mahakama haikumkuta na hatia na mimi kama mtendaji mkuu wa chama sifahamu matukio ya kufanya ugaidi na kumekuwa na tabia ya. kubambikia watu kesi .
Lissu: Uliulizwa juu ya makomandoo wa JWTZ walikuwa walinzi wake mwenyekiti Mbowe na ulisema walikuwa pia wana harakati.
Mnyika: Walikuwa makomandoo walishamaliza utumishi wao jeshini hivyo mwenyekiti Mbowe akawatumia kama walinzi wake na pia sababu walikuwa wanashirki harakati za chama hivyo walikuwa wanaharakati.
Lissu: Uliulizwa kwamba mwenyekiti Mbowe alishtakiwa na watu wengine waliokuwa makomandoo wa jeshi na sio viongozi ukajibu wakati huo walikuwa ni walinzi wake na wanaharakati.
Mnyika: Niliposema walikuwa makomandoo nilimaanisha walikuwa makomandoo zamani na aliwachukua kuwa walinzi wake na sababu mwenyekiti anakuwa kwenye harakati za chama nao walikuwa sehemu ya harakati hizo
Lissu: Ukiulizwa maswali juu ya vyombo vya ulinzi kama una kubali au hukubali kwamba kutishia amani ni kumtishia rais na hivyo vyombo vya ulinzi wa amani
Myika: Kumtishia rais au vyombo inabidi hilo tishio lako liwalenge moja kwa moja hao unaowatishia.
Lissu: Uliulizwa kama unajua Tanzania ni nchi huru na kama unajua mahakama ndio ina kauli ya mwisho kuamua kesi ya jinai na kama kesi huamuliwa kwa ushahidi kwanini unasema kesi hizo ni za uongo fafanua hilo jibu.
Mnyika: Kesi zilikuwa za uongo sababu mahakama haikupokea ushahidi uliowatia hatiani washtakiwa ulifutwa tu hivyo zilikuwa ni kesi za uongo.
Lissu: Uliulizwa maswali juu ya hotuba ya Jaji Chande ukaulizwa kama ulimsikia jaji chande akisema matukio hayo yalichochewa na baadhi ya wanasiasa na jibu lako ilikuwa hotuba yangu haikuendana na matukio hayo fafanua hilo jibu
Mnyika: Hotuba yako ilitolewa kabla na wewe ulikamatwa kabla na hotuba yako ilikuwa kuhusu kupinga uchaguzi kwa msimamo wa no reforms no election
Job: Unakubaliana na mimi kitendo cha fedha za tone tone kulipa kwa watu wachache ni ukiukwaji wa katiba?
Myika: Kuna kipaumbele ambacho kipo wazi
Job: Kama hizo fedha chache zimeliwa kwa ubaguzi unapata wapi uahalali wa kuzungumzia uhuru na haki?
Mnyika: Mikono yetu ni safi sisi hatuna ubaguzi nyie serikali ndio mna ubaguzi kuzuia ruzuku yetu.
Job: Usipoaminika kwa dogo huwezi kuaminika kwa kubwa.
Mnyika: Tunaaminika kwa dogo na makubwa
Job: Una uzoefu wako wa kutunga sheria unaona hujakushauri vyema kwa kutofuata njia ya mahakama
Myika: Hapana tumejaribu kushauriana vyema kila hatua.
Job: Ulisema humfahamu Ishengoma Mutembei Barongo huyo bwana Mutembei ndio katibu wa kata wa mikocheni
Mnyika: Siwezi kukubaliana na mambo nisiyoyafahamu
Job: Utakubaliana video clip iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii bwana mutembei alieleza mipango ya kuvuruga uchaguzi ilitoka juu ndani ya chama?
Mnyika: Siwezi kusema sababu sijaona hiyo clip
Job: Ni hayo tu waheshimiwa majaji.
Nzengeli: Waheshimiwa majaji tumefikia mwisho kumuuliza maswali ya dososo kwa shahdi huyu.

Job: Katika muktadha huo, utakubaliana na mimi kwamba kwa mujibu wa kifungu cha saba, toleo la mwaka 2016, sura ya mia mbili na tisa, moja ya jukumu la waandishi wa habari ni kutafuta habari?
Mnyika: Siwezi kusema ni sahihi au si sahihi, umetaja kabisa kifungu mahususi.
Job: (Anarejea kusoma kifungu cha Sheria ya Habari ya mwaka 2016 na maboresho ya mwaka 2023.) Utakubaliana na mimi sasa kwamba moja ya jukumu la vyombo vya habari ni kutafuta taarifa?
Mnyika: Kwa mujibu wa majukumu yao.
Job: Kwa muktadha huo, mwandishi anapokuwa amepata habari ana uhuru wa kuipeleka habari hiyo?
Mnyika: Ana uhuru wa kuchapisha au kutokuchapisha. Freedom, uhuru.
Job: Utakubaliana na mimi kwamba katika msingi huo waandishi wa habari mliowaalika walitengeneza majibu yao kwa uhuru?
Mnyika: Sisi tuliwapa uhuru kwenye kutekeleza. Walikuwa huru kwa namna yao.
Job: Ulieleza mahakama kwamba yale makusanyo ya Tone Tone, kuna uamuzi ulipitishwa wachache wanufaike na wachache wasinufaike. Kikundi cha watu wachache kinufaike na wachache. Je, ni ubaguzi?
Mnyika: Ni ubaguzi. Wewe si mwanasheria wa serikali? Waambie walipe pesa zetu zaidi ya milioni mia 400.
Job: Nitakuwa sahihi kusema zaidi ya milioni 39 zinazotokana na michango ya Tone Tone zimetolewa kati ya tarehe 19 hadi 28 mwezi wa nane, 2026?
Mnyika: Sio sahihi.
Job: Ikitokea wanachadema wameupata ushahidi kuwa kuna pesa zilitoka, huoni utakuwa unaweka kiti chako rehani?
Mnyika: Hapana.
Job: Unakubaliana na mimi kwamba kitendo cha fedha za Tone Tone kulipa kwa watu wachache ni ukiukwaji wa katiba?
Mnyika: Kuna kipaumbele ambacho kipo wazi.
Job: Kama hizo fedha chache zimelipwa kwa ubaguzi, unaona wapi uhalali wa kuzungumzia uhuru na haki?
Mnyika: Mikono yetu ni safi. Sisi hatuna ubaguzi. Nyie serikali ndio mna ubaguzi kwa kuzuia ruzuku yetu.
Job: Usipoaminika kwa dogo, huwezi kuaminika kwa kubwa.
Mnyika: Tunaaminika kwa dogo na makubwa.
Job: Una uzoefu wako wa kutunga sheria. Unaona hujakushauriwa vyema kwa kutofuata njia ya mahakama?
Mnyika: Hapana. Tumejaribu kushauriana vyema kila hatua.
Job: Ulisema humfahamu Ishengoma Mutembei Barongo. Huyo bwana Mutembei ndiye Katibu wa Kata wa Mikocheni.
Mnyika: Siwezi kukubaliana na mambo nisiyoyafahamu.
Job: Utakubaliana kwamba video clip iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii, bwana Mutembei alieleza mipango ya kuvuruga uchaguzi ilitoka juu ndani ya chama?
Mnyika: Siwezi kusema kwa sababu sijaona hiyo clip.
Job: Ni hayo tu, Waheshimiwa Majaji.
Nzengelei: Waheshimiwa Majaji, tumefikia mwisho wa kumuuliza maswali ya dodoso shahidi huyu.
Job: Je, Tundu Antipas Lissu amewahi kufungua kesi ya kikatiba kwa jina lake binafsi?
Mnyika: Kwa mujibu wa ufahamu wangu, sifahamu.
Job: Utakubaliana na mimi sasa, shahidi, kwamba kwa mujibu wa sheria mahakama imepewa mamlaka ya kusikiliza mashauri ya kikatiba?
Mnyika: Ni kweli.
Job: Utakubaliana na mimi kwamba njia bora ya kupata utatuzi, usiporidhishwa na jambo, ni kwenda mahakamani?
Mnyika: Sikubaliani na wewe.
Job: Mshitakiwa kabla ya kutoa ushahidi alisema anataka kukuandaa. Alikuambia nini?
Mnyika: Aliniambia taratibu za kufuata tu ninapokuwa kizimbani.
Job: Nitamuomba shahidi. Waheshimiwa Majaji, ukiwa kama Katibu Mkuu, unamfahamu Ishengoma Mtembey Barongo?
Mnyika: Sijui.
Job: Je, unafahamu huyu ni Katibu wa Mikocheni?
Mnyika: Simfahamu.
Job: Je, unafahamu huyu bwana Ishengoma ni mwanachama wa Chadema?
Mnyika: Hayo yatakuwa ni maoni yako.
Job: Hawa makatibu wa kata, utaratibu wa kufanya kazi ukoje?
Mnyika: Wao ndio wasimamizi wa shughuli za chama kwenye kata na wanaripoti kwenye jimbo, hivyo Katibu Mkuu hahusiki moja kwa moja.
Job: Ikitokea kuna ushahidi kuwa huyu ni mwanachama wa Chadema na mnamkana?
Mnyika: Ngazi ya kata inahudumiwa na jimbo. Muite Katibu wa Jimbo umuulize swali hilo.
Job: Hebu wajibu Waheshimiwa Majaji, maelekezo yakitoka ngazi ya taifa yanafikaje kwenye ngazi ya kata?
Mnyika: Chama taifa kinawasiliana na makatibu wa kanda. Wao wanashusha kwenye mikoa, mikoa inashusha kwenye wilaya, kisha majimbo na kata.
Job: Kwa mujibu wa Katiba ya Chadema, kinaamini katika matumizi ya TEHAMA katika kuhabarisha umma?
Mnyika: (Anasoma katiba) kuhakikisha chama kinatumia TEHAMA kukiunga mkono, hivyo jibu ni sahihi.
Job: Shahidi, utakubaliana na mimi kwamba, kama inavyosomeka kwenye hati ya mashtaka, maneno haya niliyokusomea yanamaanisha matukio ya vurugu na fujo yaliyotokea tarehe 29 Oktoba 2025 yalisababishwa na mshitakiwa?
Mnyika: Mshitakiwa hahusiki. Wakati huo alikuwa ndani, na hayo aliyoyazungumza yalikuwa katika muktadha wa uchaguzi ndani ya chama.
Job: Chadema inaamini katika demokrasia?
Mnyika: Ndio. Wengi waamue, wachache wasikilize.
Job: Ni kweli kwamba, kwa nafasi yako, wewe ni mshauri wa mwenyekiti na kwamba ni wewe uliyemshauri mwenyekiti kutoa hotuba zake bila kukuhusisha?
Mnyika: Hakukuwa na haja ya kushauriana, kwa sababu huo ulikuwa msimamo wa chama.
Job: Shahidi, waeleze majaji: wakati unadai haki zako, si sawa kukanyaga haki za watu wengine, sivyo?
Mnyika: Ndio.
Job: Umewahi kufungua shauri lolote, au mwenyekiti wa sasa amewahi kufungua shauri kudai mabadiliko hayo?
Mnyika: Hapana.
Job: Wewe kama Katibu Mkuu wa Chadema, unauamini mhimili wa mahakama katika utoaji wa haki?
Mnyika: Ndio.
Job: Utakubaliana na mimi kwamba, kutokana na ushahidi ulioutoa hapa mahakamani, ili sheria itamkwe kuwa kandamizi ni lazima kwanza mahakama itoe uamuzi?
Mnyika: Sikubaliani na wewe.
Shahidi Mnyika anaendelea kuulizwa maswali ya Dodoso na wakili wa serikali Job Mrema

Nzengeli: Na ni kweli mlitoa elimu pale pale kwenye ufunguzi
Mnyika: Ni kweli elimu ilianza kutoka kwenye ufunguzi
Nzengeli: Wewe ni mtaalamu wa sheria au hujui sheria?
Mnyika: Mimi sio mtaalamu wa sheria
Nzengeli: Nitakuwa sahihi nikisema huna utaalamu wowote wa kuchambua hati yoyote ya mshitaka
Mnyika: Ninaweza kuchambua kile iman ila nina uzoefu wa kutosha wa siasa
Nzengeli :Kama huna sema kama unao sema
Mnyika: Sina
Nzengeli : Kama mtu anauona uchaguzi ni wa haki na uhuru na unageuka kuwa sio wa haki kwa kuwa nyie chadema mmeamua
Mnyika: akikubaliana na msimamo wetu
Nzengeli: Kama hajakubaliana
Mnyika; Hayo ni maoni yake
Nzengeli: Nimemaliza namualika Job Mrema amalizie waheshimiwa majaji Ahsante
Job : Waambie majaji hii kamusi hii inasemaje hapo juu kwenye kichwa cha habari
Mnyika: Kamusi kuu ya kiswahili Job Toleo la ngapi Mnyika toleo la tatu mwaka 2022
Job : Kwa mujibu wa lichosoma utafiti ulifanywa na nani kuandaa hiyo kammusi
Mnyika : Baraza la kiswahili la taifa
Job: Bakita ndio wamepewa mamlaka ya kufanya utafiti huo
Mnyika: Kwa Tanganyika
Job: Umeulizwa maswali mengi ukawa unasoma kwenye kamusi je ni hiyo uliyoishika hapo toleo la tatu
Mnyiaka: Ndio ndio hii
Job: Unakubaliana mimi kamusi hiyo ndio chombo rasmi cha kutoa tafsiri sahihi ya lugha ya kiswahili
Mnyika: Ni Rasmi ila sio nakala pekee
Job :Mimi sijakuuliza pekee
Mnyika :Hapana
Job: Ni sahihi umeiuizwa kuhusu michango ya tone tone ukasema mmekusanya milioni 302 pesa za Tanzania kuna michango mingine?
Mnyika sina takwimu kamili
Job : Ni kweli kwamba mshaanza kutumia michango ya tone tone na inetumika kiasi gani
Mnyika: Michango hiyo inatumika kwa lengo mahususi na ni michango ya baraza kuu la chama
Job: kama nimekusikia vizuri uliulizwa majukumu yako kama katibu mkuu wa chadema ulishindwa kuyataja ni kweli
Mnyika: hapana sio kweli
Job: Wewe kama mlioaji wa chama una majukumu gani
Mnyika: Msimaizi shughuli zote za kila siku za chama
Job : Kama ndio hivyo ndugu shahidi kama ndio ukweli ni sahihi kwamba umeulizwa maswali mengi ya kiutendaji na unasema hujui
Mnyika: Sio kweli mengi nimejibu ndio isipokuwa machache ambayo ninahitaji uelewa zaidi
Job: Unafikiri ni sahihi chadema kuwa na mtendaji mkuu asiyejua makukumu yake
Mnyika: Ninajua ninachofanya
Job :Nitakuwa sahihi nikesema ukatibu wako mkuu umekuwa wa kusaidiwa saidiwa na ni kama ahsante kwa mwenyekiti wa chadema
Mnyika : Sio sahihi
Job: Je ni sahihi katika utendaji wako umekuwa ukibebwa na mwenyekiti
Mnyika :Hapana
Job :Je ni sahahi hata kizimbani umeshindwa kujieleza mwenyekiti akaja kukunongoneza
Mnyika sio kweli
Job: Ndugu shahidi utakubaliana na mimi kwamba vyama vya siasa vilivyisajiliwa vinatakiwa kufuata sheria za nchi hii kanuni katiba za vyama husika
Myika: Ni sahihi Job sasa waambie waheshimiwa majaji nini maana ya fujo ni nini
Mnyika: Fujo ni Fujo
Job; Haya waambie waheshimiwa kwa mujibu wa kamusi uliyo nayo hapo
Mnyika: Bila kuwepo kwa utaratibu mzuri au mpango, hovyo hali ya ghasia na machafuko
Job: Waheshimiwa majaji yako mambo ya kuendelea kufafanua shahidi ni anaendelea kutanua goli lakini sababu ya muda Jaji nakuruhusu malizia hilo swali
Job: Waambie waheshimiwa majaji utakubaliana na mimi sasa mwenyekiti ambaye ni mshitakiwa kwenye kesi hii mnamo tarehe tatu mwezi wa nne 2025 aliposema ataleta fujo atakinukisha si ndio fujo yenyewe
Job: Sasa hii Jaji hili swali tuna lishikilia mpaka. kesho shahidi ataendelea.
Baada ya kauli hiyo Tundu Lissu ameomba mwenendo wa kesi ili aweze kusoma huko aliko.

Katuga: Unajua kesi ya uhaini ya Khatib Gandye na wenzie
Mnyika: Niliwahi kusikia kuna kesi ya uhaini ya namna hiyo
Katuga: Uliwahi kusikia kuwa Jaji alisema kesi sio kama mpira wa miguu ni ushahidi na sio hisia
Mnyika: Najua
Katuga: Unajua kwamba kesi ya jinai sio mapemzi ni ushahidi Mnyika Najua
Katuga: Waambie majaji kuwa Katibu Mkuu kwamba wewe ni muhusika wa kujua idadi ya wanachama wa CHADEMA
Mnyika: Wasaidizi ndio wanafanya hiyo kazi kwa niaba ya katibu mkuu Katuga: Hizo kazi zinakuwa za Mwenyekiti au Katibu Mkuu
Mnyika: Katibu mkuu
Katuga: Uliwahi kufuatilia malalamiko ya wana-CHADEMA mtandaoni kuhusiana na posho
Mnyika: Hapana
Katuga: Una fahamu au hufahamu kuhusiana na wanachama walioita waandishi wa habari kueleza juu ya kilichopangwa na chama.
Mnyika: Hapana
Katuga: Unafahamu mwanachama huyu aliuambia umma kuwa mipango ile ilipangwa na kuratibiwa.
Myika: Hapana sifahamu
Katuga: Mwanachama huyu alisema kuna mifumo maalumu ya mawasiliano ya simu itakapozimwa ili kufanikisha nia hiyo
Mnyika: Sifahamu
Katuga: Unafahamu au hufahamu kwamba kumekuwa na mipango ya kusimamia vurugu sehemu tofauti tofauti
Mnyika: Sifahamu
Katuga: Mtibu mkuu mliwahi kujitokeza kwa namna yoyote kumpinga huyu mwananchama anayeitwa Ishengoma
Mnyika: Simfahamu unamjua wewe
Katuga: Waaambie majaji unafahamu kuwa vurugu za uchaguzi zilikuwa vurugu za siku ya uchaguzi zilipangwa na kuratibiwa kwa mujibu wa Jaji Chande
Mnyika: Nilisikia
Katuga: Baada ya vurugu za siku ya uchaguzi kuna watu walikamatwa kuhusiana na vurugu hizo
Mnyika: Nina fahamu walikamatwa na wakaaachiwa
Katuga: Waambie majaji kwamba watuhumiwa wakati wakihojiwa kituo cha polisi walifanya fujo sababu ya kauli ya kiongozi wao Tundu Lissu
Mnyika: Sifahamu
Katuga: Ikumbushe Mahakama ni kweli ushahidi uliosema
Mnyika: Ni tafsiri halali kisheria
Katuga: Ni ushahidi wako kuwa mtu yeyote anaweza kutenda matendo sababu ya kauli za Mwenye kiti
Mnyika: Hapana inategemeana
Katuga: Demokrasia ni nini?
Mnyika: Demokrasia ni utawala unaoundwa na watu kwa ajili ya watu

Katuga: Waambie Waheshimiwa majaji hiyo mikutano isiyokuwa na Mwenyekiti kama inakua na ajenda
Mnyika: Inategemea na mikutano
Katuga: Waambie Waheshimiwa kama mkutano wa tarehe 3 Aprili kama ulikua na ajenda
Mnyika: Ulikua na Mada
Katuga: Waambie kama huo mkutano ulikuwa wa kichama au ni training (mafunzo)
Mnyika: Ulikuwa wa kichama wa kuelemisha watia nia
Katuga: Waambie Waheshimiwa tofauti ya Ajenda na Mada
Mnyika: Mada ni jambo linalozungumzwa
Katuga: Hiyo tafsiri ya ajenda ni kwa mujibu wa ufahamu wako au
Mnyika: Nimejibu kwa tafsiri yangu
Katuga: Nitakua sahihi kwamba kwakua hakukua na mada maalum basi kiongozi alikua na nafasi ya kuzungumza chochote alichokifikiria
Mnyika: Hapana mkutano ulikua na mada
Katuga: Sasa kama nilikusikia na kukuelewa vyema kwenye neno uasi ukasema neno uasi si kosa
Mnyika: Sahihi
Katuga: Ni kweli au si kweli kwamba tafsiri yako ya neno uasi inatokana na kauli ya Mwl Nyerere
Mnyika:….
Katuga: Kwa uelewa wako wa kisiasa waambie maana ya neno uasi
Mnyika: Ni kupinga au kukataa kwa nguvu kubwa sana
Katuga: Kuhamasisha uasi kupinga uchaguzi maana yake nini
Mnyika: Ni kukataa au kupinga uchaguzi kwa njia halali za Kidemokrasia
Katuga: Hiyo tafsiri ya uasi uliyoitoa ni kwa mujibu wa Kamusi au uelewa wako wa kisiasa
Mnyika: Uelewa wangu wa kisiasa
Katuga: Mwaka jana chama chako kilishiriki uchaguzi mkuu
Mnyika: Hakijashiriki
Katuga: Kama unakumbuka kwenye Hotuba ya Mwenyekiti je ni kweli aliwaambia watia nia kwamba “kama unategemea kuwa mbunge mwaka huu sahau”
Mnyika: Aliwaambia
Katuga: Waambie Waheshimiwa majaji kama unakumbuka kwamba Mwenyekiti aliwaambia watia nia kwamba na mimi nilitaka nigombee cheo fulani lakini nimesahau
Mnyika: Hilo neno nimesahau Sikumbuki
Katuga: Waambie Waheshimiwa majaji kama mlijiandaa kushiriki uchaguzi Mkuu
Mnyika: Tulijiandaa vizuri
Katuga:Waambie Waheshimiwa Majaji kama mlijiandaa kushiriki uchaguzi wa 2025
Mnyika:Tulijiandaa kwa mujibu wa Katiba pamoja mapungufu yake
Katuga:Waambie kama nimekusikia vizuri unasema kwenye hotuba yake Mwenyekiti alisema tutazuia uchaguzi kwa njia za Kidemokrasia
Mnyika: Sahihi
Katuga: Waambie kama kwenye ushahidi wako ulisema mwenyekiti tutazuia uchaguzi kwa njia za Kidemokrasia
Mnyika: Sikusema moja kwa moja
Katuga: Katika ushahidi wako kama kuna sehemu uliwaambia Waheshimiwa majaji kwamba njia za kuzuia uchaguzi alizozisema Mwenyekiti ni njia moja, mbili, tatu ulizitaja hizo njia alizosema
Mnyika: Niliwaambia
Katuga: Waambie Waheshimiwa majaji kama kuhamasisha uasi ni njia ya Kidemokrasia
Mnyika: Njia ya Kidemokrasia
Katuga:Waambie kama kuzuia uchaguzi kwa njia ya uasi ni njia ya Kidemokrasia
Mnyika: Ni njia ya Kidemokrasia
Katuga: Umekubali kwamba vyama vingine vina haki ya kushiriki uchaguzi mkuu
Mnyika: Uchaguzi Mkuu Huru, Haki na Halali
Katuga: Ule uchaguzi wa mwaka jana ulikua ni uchaguzi wa aina gani
Mnyika: Haukua uchaguzi huru, halali na Haki
Katuga: Je kwa mujibu wa Katiba ya Chadema inaruhusu mtu kuamini anachoamini
Mnyika: Inaruhusu
Katuga: Je katiba ya Chadema inaelekeza mtu asiamini anachoamini ili mradi asivunje sheria
Mnyika: Inaelekeza
Katuga: Je Mwenyekiti katika hotuba yake kauli yake aliyosema tutavuruga uchaguzi, tutakinukisha, tutahamasisha uasi alilenga kuhamasisha kufanyike mabadiliko ambayo mliyoamini nyinyi kwamba ndio yatakayofaa
Mnyika: Ni kweli
Katuga: Hivi baada ya Mwenyekiti kuwa amepata kesi hii ni nani aliyeendeleza hiyo hamasa ya No Reform No Election
Mnyika: Viongozi wa Kamati Kuu ya Chama akiwemo Makamu Mwenyekiti wa Chama John Heche
Katuga: Ulikua unamuandalia hotuba
Mnyika: Hapana
Katuga: Ni kweli kwamba huyu John Heche katika kuendeleza nia aliweza kuongea na EAST AFRICA RADIO kuhusiana na nia hiyo ya kuzuia uchaguzi?
Mnyika: Sijui
Katuga: Waambie kama unajua kwamba kupitia hiyo redio alitangaza kwamba huo uchaguzi wa 2025 hautakuwepo
Mnyika:Sijui
Katuga: Waambie kama unajua au hujui kwamba katika uchaguzi wa mwaka jana kulikua na jaribio la kuzuia uchaguzi wa mwaka jana kwa kuchoma vituo vya kura
Mnyika: Sijui
Katuga: Waambie kama tarehe 29 Oktoba mwaka jana ulikua nchini au haukua nchini
Mnyika: Nilikua nchini
Katuga: Waambie Waheshimiwa majaji kama wewe binafsi ulijitokeza kupiga kura au hukujitokeza
Mnyika: Sikujitokeza
Katuga: Kwa msimamo wenu mwaka jana hakukua na uchaguzi
Mnyika: Hakukua na uchaguzi
Katuga: Kwa imani yako ile nia ya kuzuia uchaguzi ilidhihirika
Mnyika:Sio sahihi
Katuga: Unajua kwamba katika uchaguzi ule kulikua na mali za watu zilichomwa
Mnyika: Sijui, nilisikia
Katuga: Waambie Waheshimiwa majaji ni sahihi au sio sahihi Kwa umma walivyotafsiri wao yale maneno aliyosema Mwenyekiti wako katika hotuba yake ya Aprili 3
Mnyika: Ni haki
Katuga: Kwa tafsiri hiyo hiyo kwamba ni haki nitakua sahihi kwamba ni haki kwa umma kuchochea kuchoma vituo vya kura, kupiga watu, kukata vidole
Mnyika: Sio haki
Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji kama tarehe 3 Aprili 2025 Mwenyekiti aliuambia umma, ni lini wazuie huo uchaguzi
Mnyika: Hakuwaambia
Katuga: Kwa kuwa hakuwaambia ni haki au sio haki watu kutoka kuzuia uchaguzi siku ya uchaguzi
Mnyika: Sio Haki
Katuga: Waambie Waheshimiwa majaji kama umesikia Mh. Jaji Chande akisema kwamba matukio ya Oktoba 29 yalilenga kuzuia uchaguzi
Mnyika: Nimemsikia lakini hatukukubaliana nae
Katuga: Waambie kama ulisikia Mheshimiwa Chande alisema matukio Yale yalitokana na kauli za wanasiasa
Mnyika: Tulimsikia lakini hatujakubaliana nae
Katuga: Ni kweli uliwahi kuwa mbunge
Mnyika: Kweli
Katuga: Mbunge wa kuteuliwa au kuchaguliwa
Mnyika: Kuchaguliwa
Katuga: Kupitia Experience (uzoeufu) ya ubunge utakua unauelewa kidogo wa masuala ya sheria
Mnyika: Kidogo
Katuga: Waambie Waheshimiwa majaji kama Unafahamu au hufahamu kwamba Tanzania kuwa huru ina Katiba yake
Mnyika: Ina Katiba yake
Katuga: Waambie Waheshimiwa majaji kama unafahamu Tanzania kuwa huru kwamba Mahakama ni chombo cha mwisho kuamua kwamba mtu huyu yupo huru au ana hatia
Mnyika: Mahakama za Tanzania na Mahakama za Kimataifa
Katuga: Waambie Waheshimiwa majaji kwamba ushahidi huu unamuweka mshatakiwa hatiani au haumtii hatiani
Mnyika: Sahihi
Katuga: Kwa uelewa wako (Mwendesha mashtaka) DPP akifuta kesi anaweza kuirudisha au hawezi
Mnyika: Anaweza
Katuga: Waambie kama unaijua mihimili ya dola
Mnyika: Naijua
Katuga: Iko mingapi
Mnyika: Mitatu
Katuga: Je unafahamu kwamba ni Bunge lenye kazi ya kutunga sheria
Mnyika: Ni kazi mojawapo
Katuga: Unajua kazi ya Mahakama ni kutafsiri sheria
Mnyika: Ni mojawapo
Katuga: Ni kweli kazi ya serikali ni kusimamia sheria
Mnyika: Ni jukumu moja wapo
Katuga: Mtu anapotishia kuvunja amani unakua umemtishia Rais na vyombo vyake
Mnyika: Sio kweli
Katuga: Waambie Waheshimiwa majaji siku ya uchaguzi wa tarehe 29, 2025 amani ilikuwepo au ilitoweka kwa muda
Mnyika: Kulikua na vurugu na kulikua na amani
Katuga: Kama Katibu Mkuu waambie kama kuchoma miundombinu, kuchoma vituo vya kura, waambie Majaji kama uvunjifu wa amani
Mnyika: Sifahamu
Katuga: Katika ushahidi wako ulisema mlipokamatwa kule Mbeya wewe, Sugu na Mwenyekiti wako ulisema Mwenyekiti wako alipelekwa kusikojulikana. Sasa usipopajua wewe au ndo huko kusikojulikana
Mnyika: Nisipopajua mimi
Katuga: Ni kweli au si kweli kwamba Mbowe alishtakiwa kwa ugaidi
Mnyika: Kweli
Katuga: Ni kweli kwamba kwenye kesi hiyo Mbowe alishtakiwa na wengine
Mnyika: Kweli na mashtka yao yakafutwa
Katuga: Ni kweli kwamba hao walioshtakiwa na Mbowe walikua ni Makomandoo wa Jeshi la Tanzania
Mnyika: Hilo nilisikia Mahakamni
Katuga: Kwa kuwa ulisema Mbowe ameshtakiwa kwa sababu ya madai ya Katiba Mpya. Sasa swali ni je kweli wale walioshtakiwa nao hawakuwa wanaharakati
Mnyika: Hawakua wanaharakati, walikua walinzi
Katuga: Waambie Waheshimiwa majaji ulisema wewe ulikua afisa masuhuli
Mnyika: Ndio
Katuga: Waambie Waheshimiwa majaji kama ulikua unahusika kuwalipa hawa walinzi wa Mbowe
Mnyika: Sikuwa nahusika
Katuga: Waeleze kama ulikua unatembea nao, unalala nao kuweza kujua yote
Mnyika: Sikua natembea nao kujua yote
Katuga: Kwa kuwa hukua unatembea nao hujui wanachoongea nitakua sahihi nikisema hujui walichokuwa wanatuhumiwa nacho
Mnyika: Najua kilichozungumzwa Mahakamani
Katuga: Nimekusikia hapa ukisema kwamba kwa ufahamu wako hii kesi ni mwendelezo ukandamizaji wa Serikali na vyombo vyake kubambikiza Viongozi wa Chadema
Mnyika: Sahihi
Katuga: Ukisema na vyombo vyake unamaanisha
Mnyika: Jeshi la Polisi
Katuga: Ni kosa gani la Jeshi la Polisi kumkamata mtu anayepanga kuvunja usalama wa raia na mali zake
Mnyika: Sio kosa
Katuga: Sasa ni sheria gani inayompa Mwenyekiti wa Chadema kinga ya kutoshtakiwa na Jeshi la Polisi kama atakua na makosa
Mnyika: Hakuna
Katuga: Ebu Waambie Waheshimiwa majaji kwamba ulisema baada ya ile kauli ya Mwenyekiti ya tarehe 3 Aprili 2025, msajili aliwaandikia barua alitaka mjieleze huo ndio ulikua ushahidi wako?
Mnyika: Sahihi
Katuga: Aliwataka mjieleze nini
Mnyika: Alimtuhumu Mwenyekiti kwa kauli za kisiasa
Katuga: Waambie Waheshimiwa majaji kama huyu Msajili wa Vyama vya siasa ana mahusiano na Jeshi la Polisi
Mnyika: Sio Sehemu ya Jeshi la Polisi
Katuga: Pia nimekusikia ukisema Chadema ilizuiwa kushiriki uchaguzi kwa sababu Katibu Mkuu hakusaini fomu za maadili ya uchaguzi
Mnyika: Sahihi
Katuga: Ulisaini au hukusaini
Mnyika: Sikusaini
Katuga: Je sheria inakutaka usaini au usisaini
Mnyika: Sheria kabla ya uchaguzi ilikua hailazimishi
Katuga: Unajua haki ya kushiriki uchaguzi ni haki ya kikatiba
Mnyika: Najua
Katuga: Kama mtendaji unajua kwamba kuvunjwa kwa hiyo ya kikatiba sheria inaruhusu kuidai hiyo haki ya kikatiba Mahakamani
Mnyika: Sio haki zote ni lazima uende ukazidai Mahakamani
Katuga: Waambie Waheshimiwa majaji kama Chama chako kilizuiwa kushiriki uchaguzi Mkuu na kama kilifungua kesi kuhusu Chadema kuzuiwa kushiri uchaguzi
Mnyika: Kama chama hakijafungua ila nafahamu kuwa kuna watu nje ya Chama walifungua
Katuga: Kwa ushahidi wako kuhusiana na masuala ya uchaguzi uliiambia mahakama kwamba
Mnyika: Sio huru, sio halali sio wa haki
Katuga: Hayo yalikua maoni yako au Mwenyekiti wako au wanachama wako
Mnyika: Ni msimamo wa Chama kupitia maazimio ya Kamati Kuu
Katuga: Iambie Mahakama hii nitakua sahihi nikisema kwamba msimamo wa Mwenyekiti na wewe na wa kamati kuu kwamba Tanzania haina uchaguzi huru, sasa njia ya kutumia ni njia isiyo ya Kidemokrasia kupata uchaguzi huru
Mnyika: Sio sahihi