Hukumu ya kesi ya Lissu kutolewa tarehe sita Novemba
Kwa ushahidi huu ni wazi kuwa mshtakiwa amesambaza nia yake kwa umma ya kuitishia serikali waheshimiwa majaji tukianza na mashahidi ambao walikuwa washtakiwa kisha baadaye wakaja kuwa mashahidi kifungu cha 151 cha sheria ya ushahidi urekebu wa 2023 kinasema kama hawa mashahidi walikuwa wamechochewa na maneno ya mshtakiwa ni washtakiwa wenza, lakini walikuwa na interest to serve na kwa mujibu wa kifungu hiki hawa ni mashahidi na wako compitent kutoa ushahdii.
Lakini sio tu kuishia kuwa wana interest to serve, je waliona video hawakuona walichocheka hawakuchochewa uzito wake ni kutokana na kile wanachosema na ili kuwadiscredit lazima ku prove wapi walisema uongo.
Waheshimiwa majaji hoja ya mwisho kabisa ilikuwa ni lalamiko kuhusu malalamiko ya ushahidi wa polisi, statement na ushahidi uliotolewa mahakamani.
Hayo sio contradiction bali ni futher elaboration of the witness. Haya si maneno yangu waheshimiwa.
Mahakama katika kesi ya Abeli Orua alias Matiku dhidi ya Jamuhuri criminial appeal number 421 ilieleza PW4 alitoa ufafanuzi zaidi mahakamani kuelezea zaidi kile alichofikisha kama maelezo polisi na hakukuwa na mpishano wowote.
Waheshimiwa majaji kwa kusema hayo submission yetu ndio hiyo kwa ushahidi wa mashahidi 17 ikiungwa mkono na ushahidi wa mashahidi wa utetezi hivyo tumefanya kazi yetu kwa ukamilifu na ni ombi letu mshtakiwa ahukumiwe sawasawa na shtaka lake.
Nasi tuwashukuru sana kwa kipindi chote mlichotusikiliza,kuanzia mwezi Septemba mwaka jana hadi mwaka huu mwezi Septemba mwishoni.
Tunashukuru kwa uvumilivu wenu.
Pia tunaomba kumshukuru kaka yetu japo hataki kwa kipindi chote ambacho tumekuwa naye kwenye kesi hii, kwa niaba ya Jamhuri hatukua na nia tofauti zaidi ya kuthibisha shtaka kwa kifungu hiki ambacho ni kwa mara ya kwanza kinakuwa tested.
Jaji: Shtaka limekuwa refu na haya yote lazima tuyasome na tutafakari tunawashukuru pia na wanachi walikuwa wanakuja wakati wote.
Kwa leo tunaishia hapa ushahidi ni mrefu tutahitaji muda wa kutosha ili tuweze kutoa maamuzi sababu hili ni shauri la namna yake, tutatoa hukumu tarehe sita mwezi wa kumi na moja saa tatu asubuhi.
Katuga: Hati ya mashtaka inasema mshtakiwa aliuchochea umma
Waheshimiwa majaji mtaona kwa mujibu wa kifungu kidogo cha tisa ili mtu ashtakiwe kwa kosa la uhaini ni lazima awe na utii kwa jamuhuri ya muungano na awe ndani au nje ya nchi ya Tanzania.
Na kuwe na nia ya aina yoyote na hati ya mashtaka imechukua false intention to instigate.
Hati ya mashtaka inasema mshtakiwa aliuchochea umma wakati wa uchaguzi mkuu mwaka 2025.
Ukiachana na neno did ikachukua neno for the purpose of intimidating the executive na kuacha bunge na mahakama.
Ukiangalia kwenye hati yetu utaona kwamba ile njia aliyoitumia mshtakiwa kudhihirisha njia yake imeachana na maneno kadhaa na hati yetu mashtaka imechukua manifestation by his deed alidhihirisha nia kwa kitendo chake.
Waheshimiwa majaji sehemu zote ambazo nimewaambia tumechukua hili na kuacha hili neno lilotumika maana yake they are not similar, Ili maneno haya yawe sawa lazima kuwe na maneno yanayofanya hivyo mfano neno similar lenyewe au maneno mengine yanayoonesha similarities.
Kwahiyo haya maneno yanayotenganishwa na or hatuwezi kuyatumia yote kwa pamoja kwenye hati ya mashtaka na haya sio maneno yetu na tumetumia neno public ili kufanya hati ya mashtaka iweze kueleweka kulingana na ushahidi ambao upande wa jamuhuri ilitegemea kuutoa.
Maneno haya any person yametoka kwenye kifungu cha tano cha kanuni ya Adhabu, Jamuhuri inamtuhumu mshtakiwa kuchochea Umma kulingana na aina ya maneno yalivyokuwa na hakulenga kikundi fulani au kumlenga mtu fulani.
Ili Jamuhuri ikutaje kwa jina kwa hiyo inatafutwa tafsiri ambayo ita tupa tafsiri ya group of people na hakuna namba kamili ya group of people
kwa hiyo watu watakuwa ni group of people.
Hii sasa tunaipata kwenye tafsiri ya neno public na tafsiri yake tunaipata kwenye kifungu hiki manifestation inaweza kusababishwa kwa kusambaza maandishi au michoro lakini pili kuna ku manifest by overt act
Lakini tatu kuna ku manifest y deer ambapo hati ya mashitaka iliyoko mbele yetu ilionesha kwamba alitamka maneno na kuyasambaza.
Tunasema kwamba kutamka maneno ni kitendo katika tafsiri ya kisheria waheshimiwa majaji na tunalichukua hili kwa kuzingatia kwamba elements za makosa kifungu cha 89 kifungu kidogo cha kwanza.
Mahakama ione kutoa maneno ni kitendo maneno ya kichochezi au lugha chafu na publishing ni kufanya taarifa fulani ijulikane kwa umma
Na tunamtuhumu mtuhumiwa kwa kusema haya maneno akayasambaza na kuyaweka known to the public na mahakama yenu itajiuliza haya maneno ni sentensi iliyokamilika kuleta maana au zisizo na maana.
Waheshimiwa hayo maneno shall be liable sio ya kwangu yamezungumzwa na kesi nyingi.
Preliminary Hearing haitumiki tena na tunaichia sasa jamuhuri jukumu la kuthibisha mashtaka kwa mujibu wa hoja zilizokataliwa.
Na baada ya kuwa tumemaliza hoja kwanza mahakama yenu tukufu tunabaki na hoja mbili tu kama mshtakiwa aliform intention kwa nia ya kuitishia serikali waheshimiwa majaji neno serikali kwenye hati ya mashtaka imetumiwa kuonesha excecutive judiciary na legislature.
Waheshimiwa majaji kwenye kanuni ya adhabu hakuna tafsiri mahususi ya neno executive wala judiciary
Kifungu hiki hakijstoa tafsiri ya hayo maneno kwa kifungu cha 39 kilivyo executive ni executive na neno judiciary and legislature havija define kumaanisha neno tofauti.
Maneno kukinukisha kwa mujibu wa ushahidi wao zililenga kuzuia kupiga kura katika ukurasa wa 619 mshtakiwa akidodosea maswali anasema the executive is responsible kutunza amani na jukumu la kulinda amani ni la polisi chini ya serikali.
Waheshimiwa majaji ushahidi huu unajionesha kilichotishwa ni serikali katika ku maintain peace and order point muhimu ya kuizingatia kwa mujibu wa hati ya mashtaka.
Neno lilitumika aliposema kitanuka kama pilau lengo ni kuitisha serikali wala jamuhuri haipaswi kuthibitisha kama serikali ilitishika au haikutikisika
Katuga: Kauli ya Mshtakiwa ndiyo Iliyotumika kama msingi wa mashtaka ya uhaini
Wakili wa serikali Peter Katuga ameieleza mahakama kuwa mshtakiwa anakabiliwa na shtaka la uhaini kinyume cha kifungu cha 39(2)(d) cha Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16, Marejeo ya mwaka 2022.
Akiwasilisha hoja zake mbele ya majaji, Katuga amesema kuwa kwa mujibu wa hati ya mashtaka, mshtakiwa anadaiwa kuwa Aprili 3, 2025 katika eneo la Kinondoni, Dar es Salaam, akiwa chini ya utii wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, alikusudia kuchochea umma kuzuia kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 kwa lengo la kuitishia Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Katuga amesema upande wa Jamhuri unadai kuwa mshtakiwa alidhihirisha nia hiyo kupitia maneno aliyoyatoa na kuyasambaza, akisema: "Wanasema kitu kimoja sahihi hapa..."
"Maneno hayo ndiyo yaliyochukuliwa na Jamhuri kama kiini cha mashtaka yao," amesema Katuga.
Amefafanua kuwa kifungu cha 39(2)(d) kinaeleza masharti ya kosa la uhaini kwa mtu yeyote aliye chini ya utii wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, iwe ndani au nje ya nchi, pale anapotengeneza au kuendeleza nia ya kutenda vitendo vinavyotafsiriwa kuwa vya uhaini.
Katuga pia amenukuu kifungu cha 135 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, Sura ya 20, Marejeo ya mwaka 2025, akisema sheria hiyo inaitaka hati ya mashtaka kueleza wazi kosa analoshtakiwa nalo mshtakiwa pamoja na namna kosa hilo linavyodaiwa kutendeka.
"Sheria inataka maelezo ya shtaka yaonyeshe wazi jinsi kosa lilivyofanyika ili mshtakiwa afahamu tuhuma zinazomkabili," amesema.
Aidha, amesema kifungu cha 138(3)(a) cha sheria hiyo kinaelekeza kuwa lugha inayotumika katika hati ya mashtaka inapaswa kuwa ya kawaida, iliyo wazi na isiyoleta mkanganyiko.
Katuga amesisitiza kuwa moja ya masharti muhimu ya kifungu cha 39(2)(d) ni kwamba mtuhumiwa lazima awe mtu aliye chini ya utii wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, awe ndani au nje ya mipaka ya nchi.
"Walifungua shtaka la uhaini kwa sababu muhusika alikuwa mtii wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kama kifungu hicho kinavyotaka," amesema Katuga.
Lissu: Kama kuna kosa hukumuni sawasawa na ilivyo kwa mujibu wa sheria
Ushahdi wa kesi hii unasemaje?
Mara tu Chadema na mwenyekiti mshtakiwa na makamu wake walipoanza mkutano ya kuhamasisha no reforms no election msajili aliingilia kati ni ushahdi wa DW2 ni ushahidi wa John Mnyika
na alisema kauli ya no reforms no election ilikuwa kauli ya kisiasa na akatoa taarifa kwa Umma na hiyo kabla ya tarehe tatu April na hiyo inaonesha msajili alikuwa tayari kuingilia na baadaye pia aliandika barua kwangu nikiwa tayari niko nguvuni na kesi ya uhaini.
Nimefunguliwa na hilo suala la msajili kuingilia halimo kabisa na jeshi la mawakili wa serikali na kwa mujibu wa sheria maana huwezi kufungua shauri la jinai kwenye jambo linaloweza kutatuliwa kimadai.
Kesi imefunguliwa bila kufuata sheria sababu walikuwa na haraka ya kuniua na kwa muktadha huo ni rai yangu kwamba mahakama hii itupilie mbali.
Hii kesi imefinguliwa kinyume cha sheria.
Hoja nyingine inayoonesha mashaka makubwa kuhusiana na kesi hii inahusu matumizi ya taratibu za kijanai kuendesha vita ya kisiasa kwa upande wa serikali.
Freeman Haikaeli Mbowe na viongozi wenzake saba wamelipishwa faini ya milioni 350 na mheshimiwa, mashahidi wote wa utetezi walikuja hapa walieleza miaka nenda rudi tunavyotengenezewa kesi wote walieleza walivyowekwa mahabusu wakashtakiwa.
Kesi yangu ya kwanza Christmas’s eve 22 wanangu ilikuwa krisimasi yao ya kwanza na wananiambia baba krisimasi yetu ya kwanza ulikuwa gerezani nimepewa kesi na Kikwete, Magufuli sasa nimepewa kubwa yenyewe na Samia.
Tumeteswa na makesi haya ya kisiasa tunagombania kuhusu mfumo wa uchaguzi sasa matumizi ya mifumo hii ya mashtaka na sheria inaturuhu kuikosoa na kupinga na hatulzimishwi na sheria kuwapenda.
Sheria inaturuhusu kuwa wapinzani na ninaposema sheria namaanisha katiba yetu na penal code inaturuhusu kuipinga kwa kila hali kupinga sera zake mifumo yake bila shida yoyote.
Hata kwenye mambo ya idara ya usalama wa taifa ambayo sheria imesema ni matishio kwa jamuhuri ya muungano, sheria hiyo imeweka wazi tukifanya harakati za kuiondoa serikali kwa kufuata taratibu hilo sio tishio la usalama wa taifa.
Sasa hii mchezo ya kutumia njia za kijinai dhidi ya washindani wa CCM huko sio kutenda haki hiyo ni political percecution.
Sasa waheshimiwa hizi kesi zinatakiwa zipigwe vita na mahakama inasemaje nianze na Freeman Haikael Mbowe mahakama hii ilikabiliwa na shtaka ambalo sio lake alikuwa amesema maneno ya yafuatayo ……Kesho patachimbika akakamatwa akashindwa kesi na mimi nilishtakiwa mara kibao maneno kama serikali imeiba hizo ni tuhuma sasa haziwezi tatuliwa kukamata watu na kuwafunga
serikali ya kidemokrasia lazima ikubali na ivumilie ukosoaji wa kisiasa mimi nimepewa kesi ya uhaini kwa kusema maneno ambayo ni malalamiko ya kiuchaguzi wanataka hawa waendesha mashtaka na mapolisi wao wanataka iwe a police state
kwa msimamo huohuo
Mahakama hii isikubali kuingilia mgogoro wa kisiasa uliogeuzwa kuwa jambo la kijinai.
Hoja yangu ya mwisho kwa mujibu shahidi DW2 aliyesema maneno haya amenifahamu kwa miaka 23 na kwamba ni mashtaka ya uongo mwingine ambaye amenifahamu kwa miaka 20 alisema mimi sio mtu ninayeweza kutenda uhaini
na wote wanasema nimekuwa mhanga wa mabavu ya serikali ya Tanzania na sio rahisi kwa mzalendo kama mshtakiwa kuwa msaliti kwa nchi yake.
Hayo maneno sio ya machawa wangu hao sio machawa hao ni viongozi ambao nimefanya nao kazi nimepambana pamoja nao kupigania nao kupambania nchi yangu na kuthibitisha ushahidi ulioko mahakamani kwa rekodi yangu mbunge kwa kuchaguliwa rais wa TLS mshindi wa tuzo za kimataifa juu ya demokrasia na haki za binadamu.
Umoja wa Mataifa unasema niachiliwe na nilipwe fidia huyu ni mhaini wa aina gani anayepiganiwa na dunia nzima.
Nimepigania haki na demokrasia kwa shemu kubwa ya maisha yangu msimamo huo umenigharimu sana msimamo huo umeniletea madhila mengi sana msimamo huo kwa siku zilizobaki za maisha yangu nitaendelea kuupigania na kama ikibidi kufa ni msimamo ambao niko tayari kuufia.
Mwisho waheshimiwa majaji namalizia kosa la uhaini halina kosa dogo ambalo ukishindwa kuthibisha uhaini unaadhibu kosa dogo na adhabu yake kufa kunyongwa hadi kufa mzigo ambao uko mabegani mwenu ni kuamua kama kwa ushahidi huu mkiona kuna uhaini msigope kuadhibu sawa sawa na ilivyo.
Toeni hukumu inayostahili uhaini na kama hamjaona uhaini msiogope kusema hakuna uhaini hapa mshtakiwa hana hatia.
Kama kuna kosa hukumuni sawa sawa na ilivyo kwa mujibu wa sheria na kama ushahdi haufit basi futulieni mbali huo ni mzigo wa kwenu peke yenu. Mimi nimemaliza.
Tulipoanza niliijulisha mahakama kesi ya uhaini sio kesi rahisi na hata nyie mtakubali ukiachia mbali siasa zake na zinafanya uhaini kuwa kesi ngumu.
Pamoja na magumu yote ya kesi hii, mmetusikiliza mmetupa nafasi ya kujieleza mmenipa nafasi ya kujitetea mmetuvumilia mmefanya kazi nzuri na nilitaka niseme haya sababu sijui kama tutakutana tena kwenye mazingira haya na hawa mawakili wangu wa serikali wamepambana vyovyote mtakavyo amua nawapa pongezi nawatakieni kila la kheri kwenye tafakari yenu.
Ahsanteni sana hayo ndio nilitaka yaingie kwenye rekodi waheshimiwa majaji.
Lissu: Upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha ushahidi wa video
Jaji: Tuendelee
Lissu: Once it is understood haya maneno yanayolalamikiwa kuwa ni ya kihaini yanapoteza hiyo maana mbaya yaliyopewa na upande wa mashtaka.
Ukishaeleza tu mazingira maana ya kihaini yaliyopewa inapotea sababu context inakuwa imeelezea.
Hiyo kwenye context kwa ushahidi wa utetezi ni muhimu kiasi hicho
Na hiyo kinachobaki ni kwenye hayo maneno baada ya kupata ile context kinachobaki ni kile ambacho DW 2 alikisema, alisema hivi ukurasa 679 alisema Maneno …
Waheshimiwa majaji tuhuma inasema mshtakiwa alichapisha hayo maneno kwenye mtandao wa Jambo TV na hayo maneno sio ya kuchapisha ni video mashahidi wote 17 walizungumzia video mashahidi wote watano wa upande wa utetezi vilevile wamezungumzia video.
Waheshimiwa majaji upande wa mashtaka kwenye preliminary hearing waliahidi wataleta video kuja kuthibitisha shtaka lao kwenye list of documentary evidence ukurasa wa 135 kwenye orodha ya vielelezo vinane na tisa walisema wataleta video lakini hawajaleta wameshindwa kutimiza walichoahidi.
Watasema hivi lakini hawa watu wamekubali kuwa hayo maneno yalisemwa na mshtakiwa alikubali na mashahdi wake wakasema hivyo hakuna ubishi kuwa maneno yalisemwa.
Waheshimiwa majaji hiyo hoja wakija nayo sio hoja yoyote yenye maana sababu ya kwanza hakukua na makubaliano kuwa ushahdi uliopo kwenye video umekubalika na pande zote mbili hivyo hauhitaji kuthibitisha hivyo walipaswa walete hiyo video.
Wakati upande wa waleta mashtaka wanasema hayo maneno ni kisa upande wa utetezi umesema throughout hayo maneno sio kosa kwa mujibu wa sheria na msikubali kabisa ushahidi usiokuwa na video, ushahidi mkubwa zaidi ni kwamba mashahidi walijikanganya juu ya urefu wa hiyo video anasema ina saatatu na Dakika 38 na baadaye saa tatu na dakika 45 na huu ni ushahidi wa mtu mmoja.
PW16 anasema hiyo video ilikuwa ndefu na waliangalia kwa takribani kwa saa mbili na dakika kadhaa.
PW17 aliyerekodi na kuirusha anasema video yake ina karibu saa tatu sasa hapa ni ipi ya kwenda nayo hizi ni za upande wa mashtaka kuna version sita na hamjaona hata moja mtaenda na version ipi na kama hiyo haitoshi tuangalie za upande wa defence.
DW, mimi mwenyewe nilisema nilizungumza kwa kati ya saa tatu na tano na kama mazungumzo yangu yalirekodiwa then video yangu ina urefu huo na wengine pia kila mmoja amekuja na muda wake kuna wasaa moja na wengine saa mbili sasa ipi ni sahihi.
DW 5 aliongeza mkorogo zaidi aliona video hiyohiyo jambo tv yenye saa mbili akaona video hiyo chanzo tv yenye dakika 60 na akaona video hiyo The chanzo tv yenye dakika 45 waheshimiwa nani alikuwa na wajibu wa kuthibisha juu ya video? ni upande wa mashtaka hawajathibisha video yoyote just to show how hopeless the case is.
Hicho kipande kina urefu kiasi gani waheshimiwa majaji?.
Waheshimiwa majaji na video hii ilikataliwa na mahakama hii mwezi wa kumi mwaka jana na hawakufanya chochote kurekebisha msiikubali ikataeni.
Waheshimiwa majaji sasa jambo jingine hii kesi imefunguliwa kinyume cha sheria. Jambo likiwa na sura ya kimadai au kijinai lazima zile sura za kimadai zimalizwe kwanza ndipo kesi ya jinai ifunguliwe.
Waheshimiwa majaji ushahidi unasemaje kabla ya ushahidi ni kipi ambacho kina sura ya kiutawala au kimadai waheshimiwa majaji mmeambiwa mara kadhaa mshtakiwa ni mwenyekiti wa chadema chama kilichopo kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa.
Masuala ya vyama siasa na viongozi wao na matendo yao na makosa wakikosea yamekabidhiwa kwa ofisi ya msajili wa vyama vya siasa hatua ya kwanza inachukuliwa na ofisi ya msajili wa vyama vya siasa na yako kwenye kifungu cha saba cha sheria hiyo.
Lissu:Hakuna ushahdi wa kumfunga mshtakiwa
Jaji subiri kidogo
Jaji: uendelee
Lissu: Waheshimiwa majaji ushahdi unapaswa kuchambuliwa vyema kila mmoja kiundani, nimeuzungumzia ushahidi upande wa mashtaka kwa ujumla wake na vipande vipande vyake nimerejea kesi ya Nguza Viking na Oscar Lwela na ndivyo nilivyofanya waheshimiwa majaji.
"Swali muhimu la kujiuliza ni je, huu ushahidi unalinganishwaje?
Viongozi wa juu viongozi wanaojulikana, viongozi wa juu viongozi wenye sifa njema ndio walikuja kutoa ushahidi mbele yenu waheshimiwa majaji.
DW1, mwanaharakati anayejulilana kwa kupigania demokrasia na haki za binadamu.
Ushahdi wa DW1 na wasifu wake uko kurasa 559 hadi 566 hadi 577 hizo zote zinazungumzia wasifu wa shahdi namba moja wa utetezi.
Jaji: Ndio
Waheshimiwa majaji DW2 katibu mkuu wa Chadema mwanasiasa mbobevu na wasifu wake uko katika kurasa 658 hadi 687 hadi 725 za rekodi za mahakama utaona wasifu wake.
DW3, Amani Sama Golugwa, Naibu Katibu Mkuu Chadema 729 -730 ushahdi wake uko na 754 hadi 759 na 764 wa rekodi ya mahakama.
DW4, Brenda Rupia, Mkurugenzi wa mawasiliano Chadema miaka 13 ndani ya chama na wasifu wake uko 807-810 814/821 na 827 hadi 828.
Waheshimiwa majaji, D5, John Wegesa Heche na wasifu wake uko katika ukurasa wa 839 hadi 848 hadi 856 na 892 hadi 896.
Waheshimiwa majaji hao ndio walikuja kutoa ushahdi mbele yenu watu wa maana katika siasa na uongozi wa nchi hii, sio watu wa mafIchoni, watu wa maana kabisa.
Mashahidi wote wa upande wa utetezi walikuwa ni mashahidi wa kuona walikuwepo walioona na kusikia kila kilichotokea siku hiyo ulikinganisha na upande wa mashtaka isipokuwa shahidi mmoja ambaye ameungana mkono na mashahidi wa utetezi wote.
Mashahdi wote hawa sio tu walizungumza mambo yaliyotokea tarehe 03/04/ 2025 bali uzoefu wao, matatizo ya kimfumo ya demorasia walizungumza kutoka mioyoni mwao na waliwaambia kila mmoja wao ambavyo wamewahi kukamatwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za uongo na kufunguliwa mashtaka na jeshi la Polisi Tanzania, na walizungumza kutoka kwenye uzoefu wao binafsi.
Waheshimiwa majaji viongozi wote hawa waliambia mahakama hii kile ambacho hawakuambiwa na mashahidi wa upande wa mashtaka, context hayo maneno yalizungumzwa mazingira gani na kwanini
Jaji: Ndio
"Waheshimiwa majaji mashahdi wote wale walisema wana maslahi na kesi hii na hawakukana.
Mwenyekiti wao yuko ndani anashtakiwa kwa kisa uhaini.
Ni kiongozi gani ataona mwenyekiti wao yuko ndani na hawakuwa na maslahi na walikuja sababu wanataka haki na ukweli kwa hiyo maslahi yao waliyoyakubali ni maslahi ya kutendeka haki.
Mateso dhidi ya Mwenyekiti wao yakome katiba yao na wale wahalifu waliogeuzwa mashadi walikuja na nia njema ya kusema kweli.
Kwenye kesi, Goodluck Kyando, Mahakama ya rufani ilisema kila shahidi anastahili kukubaliwa ushahdi wake isipokuwa pale palipo na sababu za kutosha za kuukataa ushahidi wake.
Swali langu kati ya ushahdi wa viongozi hawa na wahalifu hawa na mapolisi hawa, mahakama inatakiwa iamini ushahdi upi? ushahidi wa mashahidi hawa walioletwa na mapolisi haustahili kuaminiwa wapo 17 na nataka kumuondoa PW17 kwa sababu ushahidi wake kwa kiasi kikubwa ni ukweli lakini hawa wengine wote hawastahili kuaminiwa hata kidogo na kwa upande mwingine ushahdi wote wa upande wa utetezi unapaswa kuaminiwa na kukubaliwa kwa sababu ambazo nimezieleza kwa kirefu na kwa kusema hayo naomba nisinukuliwe kwamba ushahidi wote wa utetezi haukuwa na mawaaa
Kwa Mungu huko ndio ushahidi unakuwa spotless lakini duniani hapa ni ushahidi wa binadamu hivyo dosari hazikosekani.
Nitoe mfano waheshimiwa majaji mashahidi wengi wa utetezi pamoja na mimi tuliburuzwa sana kwenye cross examination na waliweza sana kuonesha madhaifu ya utetezi wetu,kuna shahidi aliulizwa una magari mangapi akasema mawili akaoneshwa ana magari matano ninachotaka kusema kwenye ushahdi wa msingi walikuwa thabiti kasoro kwenye masuala ambayo hayahusiani na kesi hii na hayaamui kesi hii.
Kwa hiyo ninaposema ushahidi wao nina maana hiyo. Nguza Viking Babu Seya mahakama ilisema nini juu ya discrepancies
Jaji Natalia Kimaro Mahakama ilisema hivi hukumu haitatolewa kutokana na contradictions na kipimo ni ushahidi usio na udhaifu wa namna yoyote na hayo mengine yanaisaidia mahakama tu kuthibitisha ushahidi wao huo.
Msimamo wa kesi ya Babu Sea pia uko kwenye kesi ya Mohamed Haruna Supra kesi ya Vitalis Joseph Supra
waheshimiwa majaji nimemaliza kuusemea ushahidi na kwa ushahidi huu hakuna ushahdi wa kumfunga mshtakiwa badala yake kuna ushahdi wa kutosheleza kumuachia mshtakiwa.
Pia naomba niongeleee eneo jingine linaloleta mashaka katika kesi hii waheshimiwa.
Mashaka makubwa na ya msingi, mashaka ni jinsi upande wa mashtaka umejaribu kuficha mambo muhimu kwenye hiyo hotuba ya tarehe 3/4/2026 na kesi imetengenezwa kwa kunyofoa maeneo mengi ambayo kama yangekuwepo yangeonesha hakuna kesi wamefanya cherry picking maneno waliyotaka na wasiyotaka yaingine kwenye hati ya mashtaka ionekane kuna mambo makuuuuubwa yalifanyaka hiyo siku ya mkutano.
Sababu ya kuokota okota tu maneno naomba kwa ridhaa yenu ni warudishe katika hati ya mashtaka kwenye hayo maneno wanayolalamikia ukiangalia hayo maneno kwa makini unabaini kwamba kuna mambo wameyaondoa wanasema msimamo huu una ashiria uasi ni kweli sababu ………. sababu tunaenda kukinukisha sana sana.
Hayo ndio maneno mtu asiye makini ataona shida inaanza kabla ya neno la kwanza kuna zile doti tatu zina maana kwamba kulikuwa na maneno kabla wanasema kitu kimoja sahihi hapa hayo maneno ya kabla yameondolewa na uthibitisho ni hizo alama.
Baada ya neno mabadiliko kuna alama hizohizo tena, kuna maneno yameondolewa hayo yaliyokuwepo
kabla ya wanasema ni maneno gani yalikuwa na maaana gani na kwanini yameondolewa.
Hivyohivyo kwenye maneno mengine kuna maneno yalikuwepo pia kati ya kukinukisha na sasa yameondolewa kwani yameondolewa huu uchaguzi tutauvuruga kuna maneno yaliyofuata yameondolewa ni maneno gani na kwanini yaondolewe.
Kwa kuangalia hati ya mashtaka hakuna mtu anaweza kupata majibu yake na waleta mashtaka hawajaleta majibu yoyote juu ya meneno hayo.
Waheshimiwa majaji facts are stubborn ukweli una tabia ya ubishi na huwa unakataa kufichwa.
Ukweli ni mgumu kama jiwe hicho ambacho kimefichwa kimeletwa kwenye ushahidi, kile ambacho hati ya mashtaka haikutaka mjue.. kwanza, hii kesi ni kunusu mgogoro wa kisiasa kwa zaidi ya mika 30, ni mgogoro wa kikatiba kubusu chaguzi za nchi hii, mgogoro kati ya Chadema na CCM na serikali.
Kielelezo D16 kinaonesha ni
mgogoro wa kiuchaguzi. Ushahidi ulitolewa na mashahdi wote mashahdi 17 na mashahdi wa utetezi ni ushahidi unaonesha ni mgogoro wa kisiasa kuhusu uchaguzi huo ni muktadha muhimu katika kuelewa hii kesi
Mgogoro huu umekuwa unapiganiwa kwenye majukwaa ya kisiasa na vyombo vya habari sasa huu mgogoro, serikali na mapolisi wameuvalisha vazi sasa kuwa ni mgogoro wa kijinai.
Katika ushahdi wa pande zote mbili ushahidi wa upande wa utetezi ndio umetoa muktadha sahihi wa kesi hii.
DW4 alituambia wanasema hai hii inashiria uasi, je ni akina nani?
Ni shahidi huyu ndio alitupa lawama wanaosema ni G55 hawakutuoa maana ya kukinukisha bali tumeipata kwenye ushahidi wa utetezi kwa jinsi walivyoandaa hati ya mashtaka na kunyofoa.
Wanajaribu kuonesha kuna kosa kubwa sana limefanyika hapa na context yote tumeipata kwenye ushahidi wa utetezi.
Ushahidi wa utetezi umetupatia missing context hicho ambacho upande wa mashtaka haukutaka kijulikane kwa kunyofoa nyofoa maneno na kimejulikana kwasababu ya ushahidi wa utetezi
Waheshimiwa majaji.
Tutafakari yaliyo katika ushahidi wa PW1
Jaji kwani tusiende break afu ndio unamalizia
Lissu.
Lissu: Majaji wafuate kauli ipi, kupindua au kuitishia serikali?
Tundu Lissu, anaendelea kuhoji uaminifu wa ushahidi uliowasilishwa na upande wa mashtaka, akidai kuwa mashahidi wa siri waliotumika katika kesi hiyo walikuwa na maslahi binafsi na hivyo ushahidi wao haupaswi kupewa uzito bila kuungwa mkono na ushahidi mwingine huru.
Akiwasilisha hoja zake kwa majaji, Lissu amesema ushahidi uliotolewa na maofisa wa polisi walioongoza uchunguzi wa kesi hiyo una mkanganyiko mkubwa kiasi cha kuzua shaka iwapo walikuwa wakizungumzia kesi moja.
“Kwa kulinganisha ushahidi wao, mtu hawezi kukubali kwamba maofisa hawa wawili wa polisi wanazungumzia kesi moja. Kwa kutumia akili ya kawaida tu, mtu hawezi kusema ni kesi moja,” amesema Lissu.
Amedai kuwa shahidi wa 16 (PW16) alitoa maelezo yanayokinzana na hoja za upande wa mashtaka kwa kudai kuwa mshtakiwa alikuwa na lengo la kuipindua Serikali, wakati hati ya mashtaka inadai lengo lilikuwa kuitishia Serikali.
“PW16 anasema mshtakiwa alikuwa na lengo la kuipindua Serikali, huku mashitaka yakisema ilikuwa ni lengo la kuitishia Serikali. Kupindua Serikali ni kesi tofauti kabisa na kuitishia Serikali. Sasa mtaenda na kauli ipi waheshimiwa majaji?” amehoji.
Lissu pia amepinga madai ya kuwapo kwa mwanasheria aliyeshirikishwa katika uchunguzi huo, akisema hakuna ushahidi unaothibitisha ushiriki wake.
“PW16 alisema kulikuwa na mwanasheria, lakini hakutaja jina lake. Kwenye vielelezo hakuna maelezo yoyote ya mwanasheria huyo, na hakuna mwanasheria aliyekuja hapa kutoa ushahidi. Hayo ni maelezo ya polisi ambayo hayajathibitishwa,” amesema.
Aidha, amedai kuwa PW16 alitoa maelezo yanayokinzana kuhusu ushirikishwaji wa Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), akiwataja baadhi ya watu waliodaiwa kuhusika katika uchunguzi bila kuitwa mahakamani kuthibitisha madai hayo.
“Akasema aliwasiliana na Ofisi ya DPP kupitia mtu anayeitwa Mayenda, lakini huyo Mayenda hakuitwa mahakamani kutoa ushahidi. Hayo yanabaki kuwa maneno ya shahidi pekee,” amesema.
Akizungumzia mashahidi wa siri, Lissu amesema wengi wao walikamatwa kwa tuhuma za kupanga vitendo vya uhalifu kabla ya baadaye kugeuzwa mashahidi wa upande wa mashtaka.
“Walikamatwa, wakaandikishwa maelezo kama mashahidi na baadaye wakaletwa mahakamani kwa kificho. Hawa si mashahidi huru, ni watu waliokuwa wanakabiliwa na tuhuma na baadaye wakawa mashahidi wa upande wa mashtaka,” amesema.
Kwa mujibu wa Lissu, mashahidi hao walikuwa na maslahi binafsi katika kesi hiyo na hivyo ushahidi wao ulipaswa kuungwa mkono na ushahidi mwingine wa kujitegemea.
“Ushahidi wa mtu mwenye maslahi binafsi unapaswa kuchukuliwa kwa tahadhari kubwa na hautakiwi kutumiwa isipokuwa kama umeungwa mkono na ushahidi mwingine huru,” amesema, akirejea maamuzi mbalimbali ya Mahakama ya Rufani.
Amedai pia kuwa hakuna hata mmoja wa mashahidi hao aliyedai kutishiwa maisha yake au ya familia yake, jambo ambalo kwa maoni yake linaibua maswali kuhusu matumizi ya utaratibu wa ushahidi wa siri.
“Niliwauliza kama walitishiwa maisha yao au ndugu zao wakatishiwa, wote wakasema hapana. Sasa msingi wa kuwaficha ulikuwa upi?” amehoji.
Lissu ameendelea kuhoji uaminifu wa baadhi ya mashahidi wa upande wa mashtaka, akidai walitoa maelezo yanayokinzana kuhusu taarifa zao binafsi, ikiwemo dini, kazi na uanachama wao wa kisiasa.
“PW5 alitoa maelezo yanayokinzana hata kuhusu dini yake. Mtu anayetoa maelezo tofauti kuhusu jambo la msingi namna hiyo, mahakama inapaswa kuupima ushahidi wake kwa umakini mkubwa,” amesema.
Kwa mujibu wa Lissu, kati ya mashahidi wa siri walioitwa na upande wa mashtaka, wengi wao walikuwa mashahidi wenye maslahi binafsi na hakuna ushahidi huru uliowasilishwa kuthibitisha madai yao.
“Katika mashahidi wa siri walioitwa, wengi wao ni mashahidi wenye maslahi. Ushahidi wao haujathibitishwa na ushahidi mwingine huru. Huo ndio ushahidi ambao upande wa mashtaka unatarajia mahakama iutegemee,” amesema.
Lissu amehitimisha kwa kueleza kuwa ushahidi wa shahidi wa 17 (PW17), kwa mtazamo wake, uliunga mkono hoja za utetezi badala ya kuimarisha kesi ya upande wa mashtaka.
Lissu: Ushahidi wa mashtaka unaibua mashaka makubwa katika kesi
Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, akiwasilisha hoja zake mbele ya majaji, amedai kuwa mbali na upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha hoja saba za msingi katika kesi hiyo, ushahidi uliowasilishwa umeacha mashaka makubwa kuhusu uhalali wa uchunguzi uliofanyika na msingi wa mashtaka yenyewe.
Lissu amesema chanzo kikuu cha mashaka hayo ni kile alichodai kuwa kesi hiyo iliasisiwa na mtu mmoja au wawili, akimtaja shahidi wa kwanza wa upande wa mashtaka, George Bagyemu, kuwa mhusika mkuu katika hatua za awali za uchunguzi.
Kwa mujibu wa Lissu, Bagyemu ndiye aliyeamua peke yake kuwa maneno yanayolalamikiwa yalikuwa yanaunda kosa la uhaini.
“Kesi hii yote imetengenezwa na mtu mmoja, au pengine wawili. George Bagyemu ndiye aliyeamua yeye peke yake kwamba maneno haya yanatengeneza kosa la uhaini,” amesema Lissu.
Amesema rekodi za mahakama zinaonyesha kuwa shahidi huyo aliamua kufungua faili la uhaini siku chache baada ya kuonyeshwa video iliyokuwa sehemu ya ushahidi wa kesi hiyo.
“Baada ya kuoneshwa video, akaamua kufungua faili la uhaini kabla hata hajawashirikisha wakuu wake wa kazi. Aliwafahamisha baadaye, baada ya uamuzi kuwa tayari umefanyika,” amesema.
Lissu amedai kuwa Bagyemu alifungua faili hilo kabla ya kuwashirikisha viongozi wake wa kazi, wakiwemo ZPC na DCI, na kwamba aliwajulisha baada ya hatua hiyo kuwa tayari imechukuliwa.
Aidha, amesema shahidi huyo hakuomba wala kupata ushauri wa kisheria kabla ya kufungua faili la uhaini, na kwamba hata baada ya kulifungua hakumuarifu Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).
“PW1 hakupata ushauri wowote wa kisheria kabla ya kufungua faili hili. Hata DPP hakujulishwa, na hakuna hata mmoja wa watu walioambiwa kuhusu kesi hii aliyekuja mahakamani kutoa ushahidi,” amesema.
Katika hoja nyingine, Lissu amesema Bagyemu hakushirikisha mamlaka nyingine za uchunguzi au taasisi za serikali katika hatua za awali za uchunguzi.
“Unafanya uchunguzi wa kesi ya uhaini lakini hushirikishi mamlaka nyingine za uchunguzi wala taasisi husika za serikali. Hilo pekee linaibua mashaka makubwa,” amesema.
Pia amedai kuwa ushahidi wa shahidi huyo ulitofautiana na maelezo ya baadhi ya mashahidi wengine wa upande wa mashtaka.
Akimtaja shahidi wa 16 (PW16), Lissu amesema ushahidi wake ulionyesha kuwa vyombo husika havikushirikishwa katika uchunguzi huo, jambo ambalo, kwa mujibu wake, linaongeza mashaka kuhusu mwenendo wa kesi na msingi wa mashtaka yaliyofunguliwa dhidi ya mshtakiwa.
“PW16 alithibitisha kwamba hawakushirikisha vyombo husika. Haya ni mambo yanayoonyesha uwepo wa mashaka makubwa na ya msingi juu ya kesi nzima ya upande wa mashtaka,” amesema Lissu.
Lissu: Upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha tuhuma zote dhidi ya mshtakiwa
Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, ameiambia mahakama kuwa upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha mashtaka yake dhidi ya mshtakiwa kwa kiwango cha kisheria cha uthibitisho bila kuacha shaka yoyote ya msingi.
Akitoa hoja zake, Lissu amesema upande wa mashtaka ulipaswa kuthibitisha tuhuma zote zinazomkabili mshtakiwa, lakini umeshindwa kufanya hivyo katika maswali saba aliyopendekeza majaji wayatafakari wakati wa kufanya uamuzi wao.
Kwa mujibu wa Lissu, upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha kuwa mshtakiwa ndiye aliyeitisha au kuandaa mkutano wa Aprili 3, 2025, ambapo maneno yanayolalamikiwa yanadaiwa kutolewa. Pia amesema ushahidi uliowasilishwa hauonyeshi kuwa mshtakiwa ndiye aliyewaalika waandishi wa habari kuhudhuria mkutano huo.
Ameongeza kuwa upande wa mashtaka haukuthibitisha kuwa mshtakiwa alikuwa na nia ya kuchochea watu kuzuia uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 kwa lengo la kuitishia Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Lissu pia amedai kuwa mashtaka yameshindwa kuonyesha kuwa maneno yanayodaiwa kutamkwa na mshtakiwa yanaunda kosa lolote linalotambuliwa na sheria za Tanzania, wala kuthibitisha kuwa maneno hayo yanaweza kuchukuliwa kama matendo kwa mujibu wa sheria.
Vilevile, amesema hakuna ushahidi unaothibitisha kuwa mshtakiwa ndiye aliyechapisha video yenye maneno hayo katika mtandao wa YouTube wa Jambo TV.
Kuhusu hoja ya mwisho, Lissu amesema upande wa mashtaka haukutoa ushahidi unaoonyesha kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano ilitishika kutokana na maneno yanayodaiwa kuwa ya kihaini.
Kwa ujumla, Lissu amesisitiza kuwa katika maswali yote saba, upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha tuhuma zake, na kwamba ushahidi uliopo mahakamani haukidhi kiwango cha kisheria kinachohitajika ili kumpata mshtakiwa na hatia.
Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu inaendelea leo ikiwa katika hatua ya majumuisho.
Katika majumuisho yake ya mwisho jana, Tundu Lissu alijikita katika hoja yake; Je, maneno aliyotamka kwenye mkutano wa CHADEMA tarehe 3 Aprili 2025 yanatengeneza kosa la jinai kwa mujibu wa sheria za Tanzania?
Lissu alidai kuwa maneno yanayolalamikiwa ikiwemo “tutazuia uchaguzi”, “tutahamasiha uasi” na “tutakinukisha sana” hayajaainishwa kama kosa katika sheria ya uchaguzi wala hayafikii tafsiri ya kosa la uhaini chini ya Kanuni ya Adhabu. Alisema Sheria ya Uchaguzi ya mwaka 2024 imeorodhesha makosa na adhabu zake, lakini haijaweka kuzuia uchaguzi au kuhamasisha kususia uchaguzi miongoni mwa makosa hayo.
Aliendelea kupinga hoja ya upande wa mashtaka kwamba maneno hayo yalikuwa tishio kwa Serikali kwa sababu uchaguzi unasimamiwa kwa mujibu wa sheria na Katiba. Lissu alisema hata shahidi muhimu wa upande wa mashtaka, PW17, aliyekuwepo kwenye mkutano huo, hakuyataja baadhi ya maneno yanayolalamikiwa katika maelezo yake ya awali na hakusema aliona kosa la uhaini katika mkutano huo.
Kwa upande mwingine, Lissu alisema mashahidi wa upande wa mashtaka walijenga hoja kwamba maneno hayo yalilenga kuitishia Serikali kwa sababu Serikali ndiyo inayosimamia uchaguzi. Alipinga tafsiri hiyo, akisema hakuna mahali katika maneno aliyotamka ambapo alitaja Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Rais, Makamu wa Rais au viongozi wengine wa Serikali.
Lissu pia alihamisha hoja kwenye maana ya kisheria ya “nia”, “kitendo” na “uchapishaji”, akisema upande wa mashtaka umejaribu kuyafanya maneno yake yaonekane kama “matendo” ili kujenga kosa la uhaini. Hoja yake ilikuwa kwamba maneno hayawezi kubadilishwa kuwa matendo kwa tafsiri ya upande wa mashtaka bila msingi wa sheria.
Akitumia pia uamuzi wa Mahakama katika kesi ya Freeman Mbowe, Lissu alisema sheria za jinai zinapaswa kuwa wazi ili kumlinda raia dhidi ya matumizi holela ya mamlaka na kulinda haki ya kutoa maoni.
Leo, Lissu anaendelea na majumuisho yake ya mwisho, akitarajiwa kuingia zaidi katika ushahidi uliotolewa na mashahidi wa upande wa mashtaka na utetezi kuhusu nia yake, mkutano wa 3 Aprili 2025 na maana ya maneno yaliyotumika. Upande wa Mashataka nao utapata nafasi ya kufanya majumuisho.
KESI YA LISSU INAENDELEA LEO SEPT 25, 2026
Tundu Lissu: Je, haya maneno yanayolalamikiwa ni makosa kwa mujibu wa sheria?
Lissu: Sasa
nataka kufunga hoja yangu kwenye suala hilo na je, haya maneno yanayolalamikiwa
ni makosa kwa mujibu wa sheria?
Ni makosa
yanayotambuliwa na sheria majibu ni hilo ambalo nimelionesha hayo maneno
yanayolalamikiwa sio makosa ya uhaini wala sio makosa ya jinai nyingine
yanayotambuliwa na nchi hii kwa sababu hilo jibu la suala namba 4 ni hapana,
maneno yanayolalamikiwa sio makosa kwa mujibu wa sheria za Tanzania achilia
mbali uhaini
Waheshimiwa
majaji naomba kwa ruhusa yenu niende kwenye suala namba 5 ambalo linahusu
uchapishaji
Uchapishaji
waheshimiwa majaji ni kitendo
Suala
linasema hivi kutamka yale maneno ni kitendo kwa mujibu wa kifungu cha 39 (2)D cha
kanuni ya adhabu?
Suala hili
kwa lugha rahisi upande wa mashtaka unasema kusema ni kitendo ukitoa maneno ni
kitendo kwa hiyo suala ni je maneno ni matendo?
Kwanza
naomba nianze kufafanua, huu mkanganyiko umetokea wapi, mkanganyiko huu ni wa kutengeneza
makusudi na upande wa mashtaka ili kuhalalisha hoja fulani kifungu cha 39 (2) D
kinasema “mtu yeyote ambaye ana nia ya kumchochea mtu au kikundi cha watu
kususia shughuli za serikali kwa kuchapisha, kutenda kwa namna yoyote
atakabiliwa na uhaini” masharti ya kifunguhicho lazima uthibitishe nia ya kutenda uhaini kwa kuchapisha, au
kufanya kitendo cha wazi, sasa kosa langu ni kusema na maneno matupu kwenye
uhaini hayatengenezi kosa kwa hiyo ili kunitengeneza kosa ilibidi mawakili
waseme maneno yangu ni matendo wangepambana na Katiba hadi ndiyo maana
wameitengeneza kwa kusema “mshtakiwa Kwa kitendo chake cha kutamka” kwa hiyo
wametafuta namna ya kuhalalisha maneno haya ni kosa wamebadilisha kuwa matendo
wanataka kuepeuka masharti ya sheria kwamba maneno sio uhaini wanataka kuepuka
kwa kusema maneno ni matendo ndiyo mkanganyiko ulipo
Na wamefanya
kitu kingine wametenengeza maneno mawili tofati
Nianze na
Haya kitendo ni nini na nia nini ?
Hoja yangu
ya kwanza ni kwamba kitendo na nia kwa maana yake ya kawaida yana maanisha kitu
kimoja
Kwenye kiingereza kwa maana nia maana yake ni nini kwa mujibu wa kamusi ya Oxford, KITENDO kimetafsiri kuwa kitu fulani ambacho mtu anakifanya na hiyo kamusi inasema ni sawa na kusema kutenda
Nia ni nini kwa mujibu wa kamusi ya oxford, NIA ni kitu ambacho mtu anakifanya hivyo NIA ni sawa na kitendo ni kitu kile kile kwa hiyo kifungu cha 39 (2) D kinaposema nia ya kufanya uhaini ni kitendo ambacho mtu anatakikiwa kukifanya sasa hayo maneno mawili kuthibitisha kwamba yanamaanisha kitu kimoja twende kwenye kamusi ya sheria inasema nini kuhusu kitendo, ni kitu kilichofanywa au kinachotekelezwa.
Matumizi ya kawaida ni kitu fulani kinachofanywa. Kamusi ya kisheria inasema pia ni nia, ikiwa kitendo pia ni nia ni matendo.
Kama kitendo ni sawa na nia kuwa ni kitu ambacho kinafanywa haiwezi kuwa kitu kilichosemwa maneno hayawezi yakawa vitendo kwa hiyo hii kesi inayonikabili inaposema nilithibitisha nia ya kutenda uhaini kwa matendo yangu ya maneno ni kitu kisichowezekana.
Maneno hayawezi kuwa matendo..hii hati ya mashtaka ni mbovu sababu imetaja kitu ambacho hakipo kwenye sheria
Sasa nimetumia kamusi ya Oxford na kamusi ya wanasheria kwa sababu sheria yetu haijafafanua hayo maneno
Jana wakati naaga nilisema kesi hii vyovyote mtakavyoamua mtetengeneza msingi kwa miaka ijayo na kutoa msimamo juu ya maneno hayo mawili. Hii ni sehemu moja ambapo busara zenu zinahitajika
Ukitaka kujua hiyo taarifa walioleta hapa hawajui lolote kuna neno altering.
Altering maana yake kisheria ni nini sheria inasema ni matendo yanayohusiana na kughushi, kufoji
Ndiyo maana moja wamashahidi nilimuiliza hilo neno altering limetafasiriwa wapi?
Hilo neno ambalo wamelileta walilitoa kwenye kifungu cha 53 (1) cha sheria ya huduma za Habari.
Ukitumia altering kwenye sheria ya kanuni ni kufoji ukitaka ya maneno ipo kwenye kifungu 53 ya sheria ya vyombo vya habari
Swali langu ni unatumiaje neno moja kutoka kwenye sheria moja kwenda kwenye nyingine inawezekanaje sasa Kwakua nimeshtakiwa kwa sheria ya kanuni ya adhabu ni kufoji……
Tundu Lissu: 'Makosa ninayoshtakiwa nayo sio makosa ya uhaini'
Tundu Lissu:
Maneno yanayolalamikiwa ni maneno ya kuzuia uchgauzi, kuvuruga uchaguzi,
kuhamasisha watu kuvuruga uchaguzi na mashahidi wote wamezungumzia uchaguzi. Je,
hayo maneno ni makosa kwa mujibu wa sheria za uchgauzi Tanzania?
Jibu la
swali hilo linapatikana katika sheria ya uchgauzi wa rais, wabunge na madiwani
ya mwaka 2024 sheria namba moja, sheria hii ndiyo iliyotumika kwa mara ya
kwanza katika maafa yaliyofanyika Oktoba 29, ilitungwa itumike katika uchaguzi.
Sheria hii ilitungwa kwa ajili hiyo - swali ni je yapo mahali popote kwenye
sheria hii makosa ninayoshtakiwa nayo ?
Jibu lake lipo katika sura ya 7 katika sheria
ya uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, Sura ya saba kichwa chake cha habari
ni makosa na adhabu zake.
Sheria hii
katika sura ya saba imeorodhesha jumla ya makosa 23 na adhabu zake, kuanzia
kifungu cha 114 hadi 136 ni orodha ya makosa na adhabu zake.
Makosa
ambayo ukiyatenda unaweza ukashtakiwa ukafungwa au ukapewa adhabu ya kijinai
makosa 23.
Maneno
ambayo tunataka tujue kama ni makosa yake ni maneno” tutazui uchaguzi, tutavuruga
uchaguzi, tutahamasisha uhasi, yote yale yaliyoimbwa tunataka kujua ni uhaini
au ni makosa ya uchgauzi.
Uzuri wa
sheria hii ya uchgauzi imeandikwa kiswahili kila anayejua kusoma kiswahili
anaweza kuisoma.
Kosa la
kwanza lipo kwenye kifungu cha 114 inahusu makosa ya uandikishaji wa wapiga kura
lipo kwenye kuzuia uchgauzi ? Halipo
Kosa la pili
kifungu cha 115 linaitwa kutumia wadhifa kushawishi watu wengine wasiombe kuwa
wagombea lina uhusiano wowote na ninayoshtakiwa nayo?
Kosa la tatu
mwenendo usiofaa kwa mtendaji wa uchaguzi mimi sikuwa mtendaji wa uchaguzi
halinihusu
Kosa la nne
kifungu cha 119 kinahusu daftari la wapiga kura na kadi za wapiga kura ni kesi
ukiharibu daftari lenyewe linahusika hapa kwenye haya mashtaka? Halihusiki
Kosa la tano
linaitwa mwenendo usiofaa wa maafisa waandikishaji halihusiki sikuwa afisa muandikishaji
kifungu cha 120
Kosa la sita
lipo kifungu cha 121 ni makosa yanahusu fomu za uteuzi na karatasi za kura,
sijashtakiwa nalo hilo pia halihusiki
Kosa la 7
lipo kifungu cha 122 matangazo ya uongo ya kujitoa, mtu anatangaza kwamba
mgombea amejitoa kwenye kinyanganyiro sijashtakiwa na hilo sihusiki
Kosa la 8
lipo kwenye kifungu cha 123 ushawishi wa rushwa hilo vile vile sihusiki nalo
Kwenye
kifungu cha 124 kinasema kutoa ushahidi wa uongo au maelezo ya uongo wakati wa
uchaguzi, sijashtakiwa kwa kutoa matamko ya uongo kwa hiyo hilo vile vile
halinihusu
Kosa 9
linahusu utunzaji wa siri ukivuruga hizo siri ni kosa kila kitu ni giza ndiyo
maana tunataka kuleta mwanga…sijatuhumiwa kuvujisha siri
Kosa la 10
ni kosa la hongo, takrima au kuhujumu sitatuhumiwa kwa kutoa takrima au hongo
kwa hiyo sihusiki
Kosa la 11
ni kujifanya mtu mwingine unachukua kadi ya mpiga kura ya mwenzako unajifanya
wewe ndiyo yeye halinihusu
Kosa la 12
linaitwa kupoteza sifa kwa kuhumumiwa kwa kosa la rushwa sijashtakiwa kwa
kufanya matendo ya rushwa.
Kosa la 14
watu wanaodaiwa kuwa na hatia ya ushawishi mbaya sijashtakiwa kwa kuwa na
ushawishi mbaya
Kosa la 15
lipo kifungu cha 130 hongo, rushwa na ushawishi mbaya kwa maafisa wa tume,
sijashtakiwa kwa kuhonga maofisa wa tume halinihusu
Kosa la 16 ni hatia ya kujifanya mtu mwingine, mimi
ni Tundu Lissu wa miaka yote halinihusu
Kosa la 17 ni
adhabu ya vitendo vya rushwa na vitendo haramu vile vile halinihusu
Kosa la 18
kuingilia mikutano halali ya hadhara, makosa ninayokabiliwa nayo hayahusu haya
Kosa 19 ni
makosa yanayohusu siku ya uchaguzi, kuvaa nguo za chama siku ya uchaguzi ni kosa,
kufanya kampeni siku ya uchaguzi kosa pia, sijashtakiwa kwa kufanya hivyo
Kosa la 20
linaitwa unyanyasaji wa kijinsia, hilo nalo halinihusu
Kosa la
mwisho la 21 linaitwa kuchafua matangazo ya uchaguzi, wagombea wameweka picha
unararua
Hayo ndiyo
makosa kwa mujibu wa sheria ya uchgauzi ukiyafanya hayo ya adhabu zake hakuna
kuzuia uchaguzi, hakuna kukinukisha sio kosa, hakuna kufanya uhasi dhidi ya
uchaguzi sio makosa na sio makosa kwa sababu kifungu cha 5 cha kanuni ya adhabu
kimefafanua makosa ni kitu gani?
Ni kitendo,
jaribio au kutenda kitu ambacho sheria umekiwekea adhabu hayo ndiyo makosa kama
hakijawekewa adhabu sio makosa, kama sheria haijakitamka sio kosa, sasa hayo
maneno yanayodaiwa ya kihaini sio makosa ya uhaini kwa mujibu wa kifungu cha 39
chote sio na vile vile sio makosa kwa mujibu wa makosa yakiorodheshwa kwenye
sura ya 7 kwenye sheria ya uchgauzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya 2024 sio
makosa ya jinai popote…huwezi ukachochea mtu kufanya jambo halali unachochea
mtu kufanya jambo ambalo ni kosa ukichochea mtu afanye ambacho kile sheria
imekataza ni kosa
Lissu: 'Kosa ninaloshtakiwa nalo sio kosa la uhaini'
Waheshimiwa majaji tulipoenda kwenye mapumziko nilipendekeza tuingie kwenye
hoja ya sheria ya uchaguzi…kama ambavyo nimesema kosa la uhaini kama
ilivyofafanuliwa kwenye katiba, kosa ninaloshtakiwa nalo sio kosa la uhaini
kama uhaini ulivyofafanuliwa kwenye sheria ya kanuni ya adhabu, na sheria hii
ndiyo sheria pekee nchini ambayo imefafanua kosa la uhaini ni sheria pekee,
Kwa
hiyo kama haya matendo ambayo nimeshtakiwa nayo hayafiti katika sehemu yoyote
katika moja wapo ya matendo 10 ambayo kifungu cha 39 kimeyataja ukifanya haya
unakuwa umefanya kosa la uhaini kama matendo haya hayaingii popote na
yakiyokatazwa maana yake ni kwamba mimi sijafanya kosa lolote la uhaini, kama
sijafanya kosa lolote la uhaini Je, nimefanya kosa lingine lolote kwa mujibu wa
sheria za Tanzania? Ndicho ninachotaka nikijadili
Tundu Lissu: 'Majaji nimefungwa bure, nimeonewa mwaka mmoja na nusu gerezani'
Maelezo ya picha, Tundu Lissu
Lissu:
Majaji nimefungwa bure...nimeonewa mwaka mmoja unusu gerezani mimi ni baba.
Kuna watu hapa wanachama wanatoka kila sehemu ya Tanzania bara
mwenyekiti wao amefungwa gerezani .
Sasa Majaji kama hayo ninayodaiwa kufanya kwenye kanuni za adhabu ni ugomvi .
Sasa haya maneno ni makosa kwa
mujibu wa sheria ya Uchaguzi, kwenye kanuni ya adhabu hayo.
Je sheria ya
Uchaguzi tuliopanga kuuzuia ni makosa...?
Lissu: Upande wa mashtaka unapaswa kufafanua ni makosa gani niliyofanya
Lissu : Suala
la nne linasema je, hayo maneno yaliyotamkwa na mshtakiwa yanatengeneza kosa
lolote linalotambuliwa na sheria za nchi hii na maneno hayo yanaonesha kosa?
Sababu maneno sio kosa hakuwezi kuwa na kosa hilo ndilo suala nataka nilijibu
kwenye hoja hiyo…suala hili lilijitokeza kutokana na tuhuma iliyotolewa na
upande wa mashtaka kwamba “Maneno hayo yaliyosemwa yalikuwa ni kosa la jinai”
hayo maneno ni makosa?
Maneno yenyewe yakoje “kwenye mkutano wa 3-4-25
mtuhumiwa alidhirisha nia yake ya kihaini kwa kusema na kuchapisha maneno yafutayo…wanasema
hivi msimamo huu unaashiria uwasi ni kweli sababu tunasema tutasimisha
iuchaguzi…
tunakwenda kukinukisha vibaya sana” haya ndiyo maneno yaliyotuleta
hapa ndiyo yanadhiirisha nia yake uhaini haya ndiyo maneno yanayodaiwa kuwa ni
kosa la jinai….sasa kitu cha kwanza kabisa kuhusu maneno hayo ni kwamba hakuna
mahali popote ambapo upande wa mashtaka umeyafafanua hayo maneno hawajasema
kuvuruga uchaguzi ni nini na kama ni kosa..
hawajasema kuhamasiha uhasi ni nini
na kwa nini ni kosa…hawajasema kuzuia uchgauzi ni nini na kwa nini ni
kosa…hawajafafanua kukinukisha ni nini na kwa nini ni kosa..sio wajibu wangu
mshtakiwa mahali popote kuyatolea hayo maneno ufafanuzi na kuonesha kwamba si
makosa sio wajibu wangu ni wajibu wa upande wa mashataka kusema hayo maneno
yana maana yao na kwa nini wandhani ni makosa sio wajibu wangu kusema hayo
maneno sio kosa…
.sababu hajafafanua wameleta hisia zao juu ya hayo
maneno….ushahidi upande wa Mashataka juu ya haya maneno upo kwenye ukurasa 183
hadi 184 kwa PW2
Lissu: Ushahidi wa mashtaka una ndimi mbili kama nyoka
Lissu: Muhimu zaidi kuhusu shahidi huyu ni kwamba ushahidi wake unaunga mkono ushahidi wa utetezi kwenye masuala yote muhimu kwenye kesi hii, kwenye hilo suala muhimu Pw1, pw16 ushahidi wao umetofautiana kwenye jambo moja kwamba hayo maneno maana yake ushahidi wote wa mashtaka hauaminiki kabisa ndimi mbili kama nyoka.
Ulimi mmoja unasema uhaini mmoja unasema si makosa, kama ushahidi wa mashtaka hauaminiki kwenye jambo la je kulikuwa nia ya kutenda kosa la uhaini kama ushahidi hauamini kesi inakufa.
Hoja hii inatosha kumaliza kesi lakini sio hii pekee yake, lakini hiyo dhana ni hoja ya maana kiasi gani.?...ninachotaka kusema ni kwamba kesi ya mashtakiwa kwenye suala hilo imejengwa kwenye hisia kwamba huyu mtu anapanga kuzuia uchaguzi ataitishia serikali hii imejengwa kwenye imani yao kwamba maneno ya mshtakiwa yalipanga kutishia serikali.
Ni imani, ni msingi hewa kesi imejengwa kwenye msingi wa hewa kwa nini nasema hayo?.. hawa mashahidi na mawakili wao wamerudia sana swali ninalitaka mtafakari jambo moja kwamba ni kweli kwamba serikali ni chombo pekee kinachosimamia sheria kwenye nchi hii?
Tuzungumze mambo ya wazi kwenye nchi hii kuna sheria ya usimamizi wa mahakama inasimamiwa na nani?
Inasimamiwa na mahakama haisimamiwi na serikali nchi hii kuna sheria inaitwa ya tume ya utumishi wa mahakama inasimamiwa na mahakama, nchi hii kuna sheria ya chuo cha mahakama Lushoto inasimamiwa na Mahakama.
Lissu: Uhaini ni kosa pekee ambalo limetajwa katika katiba ya nchi yetu na imesema yafutayo “Uhaini kama unafafanunuliwa na sheria utakuwa kosa la juu kabisa katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.”
WalionishtakI wanataka unihukumu kifo kwa sababu ya hisia zao kwa sababu wanahisi nililenga kuitishia serikali.
Mahakama hii kwa misingi hii ya kisheria haiwezi ikawakubalia na usiitikie wIto wao ni wito wa hisia msikubali wito wanaowapa wa kunitia hatiani kwa sababu tu wanahisi nililenga kuitishia serikali.
Nimezungumzia sana ushahidi wao ushahidi wa utetezi unasema? Mashahidi wangu na ushahidi wangu unasemaje juu ya hii hoja, ushahidi wa utetezi kwenye hii hoja ulikuwa mwepesi na wa moja kwa moja, ushahidi wangu upo kwenye ukurasa wa 589 hadi 590 mtaona kwenye hiyo sehemu DW1.
Aliimbia mahakama kuwa kikao cha tarehe3 Aprili, 2025 ulipanga kuwaleta pamoja watia nia wote wa chama kutoka kote nchini na ukiitwa kujadili sera ya chama ya ‘No reform No Election’ iliyowekwa na sekretarieti ya chama 21-1-2025 hiyo ndiyo ilikuwa nia….
Lissu: Lengo langu lilikiwa ni kuelezea changamoto iliyopo kwenye mfumo wetu wa uchgauzi ili waelewe na kuunga mkono sera ya No Reform No Election.
Hakukuwa na nia yoyote yakutishia, sababu kutishia serikali haikuwa sehemu ya ajenda yangu, sikuwataka watu wafanye vurugu, nilihamasisha kususia uchaguzi mpaka baadhi ya mabadiliko yafanyike.
Majaji kwenye maswali ya dodoso nilishughulikiwa kwelikweli lakini naomba muangalie kwenye rekodi kama huo ushahidi wangu juu ya nia yangu ya kusema maneno yale umehojiwa popote.
Wameniuliza mambo mengi lakini juu ya nia yangu kwenye mkutano ule na maneno yangu…Mtaona pia DW2 alihojiwa sana na upande wa mashtaka lakini hakubalisha msimamo wake mtaona kwenye ukurasa wa 691…ushahidi huo huo uliungwa mkono na DW3, ushahidi wa DW3 ulishughulikiwa kweli kweli kwenye suala la nia hakubadilika…ushahidi wote huo wa upande wa utetezi ulihojiwa sana na mawakili wa serikali lakini suala la nia halikuulizwa hata kidogo.
Lissu:Ushahidi wa shahidi PW17 unaunga mkono utetezi
Lissu: PW17 alisema yafuatayo kuhusu mkutano wa tarehe 3 Aprili, 2025 kikao hicho kilipanga kuwaleta pamoja watia nia wa CHADEMA kujadili mambo yanayohusu uchaguzi na sera ya chama ya ‘No reforms no elections’ mengi yakijadiliwa kwenye kikao hicho lakini kitu kikuu kilikuwa kinahusu sera ya ‘No reform no election’ na jinsi CHADEMA ilivyojipanga kwenye uchaguzi mkuu ujao.
Nakumbuka walisema bila mabadiliko ya sheria hawatoshiriki kwenye uchaguzi na kwa ziada mwenyekiti wao Tundu Lissu alisema namna walivyopanga kuzuia uchaguzi na maneno ninayoyakumbuka alisema ‘tutazuia uchaguzi tutakinukisha vibaya’ hayo ndiyo maneno ya shahidi aliyesikia hakuna uhaini wala kosa aliloliona.
Lissu: PW17 pia alihojiwa maswali ya dodoso. Alipiulizwa wewe ulikuwepo? uliona chochote cha kiuhaini na ulikiandika?
Alisema “Ni kweli kwenye maelezo yangu ya maandishi sikusema maneno yaliyozungumzwa na Lissu.
Lissu: Maelezo ya PW17 kielelezo D16 hayo maneno tutakinukisha, tuta nini hayapo kabisa kwenye maelezo ya shahidi huyu wa upande wa mashtaka, nilimuiliza kwa nini yeye hakuyasikia haya maneno majibu yake yanasema hivi:
"Maneno hayo haypo kwenye kielelezo D16, ni kweli kwamba nilikuwa kwenye kikao niliona na kusikia kila kinachoendelea mimi mwenyewe kwenye kielelezo D16 nakumbuka kuelezea kuhusu ‘No reforms no election’ nilipomuuliza kama maneno hayo ni makosa alisema “Viongozi hawakukosea kujadili changamoto zao zinazo wakabili.”
Angekuwa shahidi wangu tungetegemea kusema hivyo ila huyo ni shahidi wao.
Kifungu cha 67(1) cha sheria ya ushahidi kinazungumzia ushahidi wa moja kwa moja hicho kifungu kinaitwa “the best evidence rule” kama ni wakuona ni ushahidi wangu aliyeona kama ni wakunusa ni wa shahidi aliyenusa.
PW17 ni shahid bora ni shahidi aliyeona aliyesikia kila kinachoendelea na alisambaza……yeye ni shahidi bora zaidi nimekaa gerezani mwaka na nusu wakati wakiwa na maelezo ya PW17 nisipozungumza haya kwa ukali mawe yatazungumza.
PW17 alikuwa shahidi wa mafichoni na mimi ninashida sana na hilo sababu naamini kwenye ukweli ulio wazi, nina shida na hilo kwamba shahidi huyu alitoa ushahidi wake mafichoni lakini sio yeye aliyejipeleka mafichoni.
Aliwaambia majaji hakuna mtu hata mmoja ambaye alimtishia..huyu shahidi bora aliyetoa ushahidi wake mafichoni hakuwahi kukamatwa kwa kupanga njama.
Mashahidi wengine ni wahalifu waliopanga kufanya uhalifu PW17 hakukamatwa alikuja kama shahidi huru ushahidi wake unauzito mkubwa sana.
Lissu: Muhimu zaidi kuhusu shahidi huyu ni kwamba ushahidi wake unaunga mkono ushahidi wa utetezi kwenye maswala yote muhimu kwenye kesi hii, kwenye hilo swala muhimu Pw1, pw16 ushahidi wao umetofauti kwenye jambo moja kwamba hayo maneno maana yake ushahidi wote wa mashtaka hauaminiki kabisa ndimi mbili kama nyoka ulimi mmoja unasema uhaini mmoja unasema si makosa, kama ushahidi wa mashtaka hauaminiki kwenye jambo la je kulikuwa nia ya kutenda kosa la uhaini kama ushahidi hauamini kesi inakufa, Hoja hii inatosha kunaliza kesi lakini sio hii pekee yake, lakini hiyo dhana ni hoja ya maana kiasi gani..ninachotaka kusema ni kwamba kesi ya mashtak kwenye swala hilo imejengwa kwenye hisia kwamba huyu mtu anapanga kuzuia uchaguzi ataitishia serikali hii imejengwa kwenye imani yao kwamba maneno ya mshtakiwa yalipanga kutishia serikali ni imani ni msingi wa hewa kesi imejengwa kwenye msingi wa hewa kwa nini nasema hayo hawa mashahidi Nan mawakili wao wamerudia sanaa swali ninalitaka mtafakali jambo moja kwamba ni kweli kwamba serikali ni chombo pekee kinachosimamia sheria kwenye nchi hii? Tuzungumze mambo ya wazi kwenye nchi hii kuna sheria ya usimamizi wa mahakama inasimamiwa na nani? Inasimamiwa na mahakama haisimamiwi na serikali nchi hii kuna sheria inaitwa ya tume ya utumishi wa mahakama inasimamiwa na mahakama, nchi hii kina sheria ya chuo cha mahakama Lushoto inasimamiwa na Mahakama