Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za Soka Ulaya Jumanne: Man City na Tottenham zaingia kwenye kinyang'anyiro cha kumnasa Gakpo
Manchester City wameingia kwenye kinyang'anyiro cha kumsajili mshambuliaji wa Liverpool na Uholanzi Cody Gakpo, 27, huku Tottenham pia ikitaka kumsajili. (Soccer News NL)
Newcastle wamefikia makubaliano ya mdomo na Manchester City kumsajili kiungo wa kati wa Uhispania, Nico Gonzalez, 24, kwa pauni milioni 47 pamoja na nyongeza ya pauni milioni 3. (Fabrizio Romano)
Manchester United wanataka kuishawishi Arsenal kumuuza Myles Lewis-Skelly, 19, wa Uingereza, ingawa bei inayotarajiwa ya zaidi ya pauni milioni 50 inasalia kuwa kikwazo katika mpango huo kwa mchezaji huyo ambaye anaweza kucheza beki wa kushoto na kiungo wa kati. (Sun)
Newcastle wamewasilisha ofa yenye thamani ya euro milioni 40 (£34.2m) bila kujumuisha bonasi kwa mshambuliaji wa Lille na Ubelgiji, Matias Fernandez-Pardo, 21. (L'Equipe)
Ofa tatu za Chelsea zimekataliwa msimu huu wa joto kwa kiungo wa Bournemouth na Uingereza, Alex Scott, 23. (The i)
Hull wamewasilisha ofa ya euro milioni 21 (£17.9m) kwa mshambuliaji wa Union Berlin na Ujerumani chini ya umri wa miaka 21 Ilyas Ansah, huku mazungumzo kuhusu mkataba wa muda mrefu yakiwa katika hatua nzuri. (Sky Deutschland)
AC Milan wanafikiria katika mwishoni mwa dirisha la uhamisho kumsajili beki wa Manchester United na Morocco Noussair Mazraoui, 28. (CaughtOffside)
Coventry wamekubali mkataba wa pauni milioni 6 kumsajili beki wa Brentford na Jamaica, Ethan Pinnock, 33. (Athletic)
Monza itampa mkataba wa mwaka mmoja kiungo wa zamani wa Tottenham na England, Dele Alli, 30. Amekuwa bila klabu tangu aondoke Como mnamo Septemba 2025. (Fichajes)