Hukumu ya kesi ya Lissu kutolewa tarehe sita Novemba

Mahakama imesema itahitaji muda wa kutosha ili iweze kutoa maamuzi sababu hili ni shauri la namna yake.

Muhtasari

Moja kwa moja

Na Waandishi wa BBC Swahili

  1. Upande wa Mashtaka wamaliza kumdodosa Lissu

    F

    Jaji Ndunguru: Shahidi unakumbushwa kiapo chako kinaendelea

    Lissu: Sawa sawa

    Wakili Nzengeli (Upande wa serikali): Shahidi unakumbuka jana tulipoishia naomba nikuulize swali moja la mwisho tuachane na wewe

    Lissu: Asante mmening'ang'ania sana

    Wakili wa Serikali- Nzengeli: Ni kweli au si kweli nia ya kutenda kosa inathibitishwa na matendo husika

    Lissu: Sio kweli

    Wakili Nzengeli: Waheshimiwa tulikuwa na hilo tu kwa shahidi huyu tunaomba kusema tumemaliza kwa shahidi huyu

    Upande wa Jamhuri umemaliza kumuuliza maswali Shahidi wa Kwanza wa utetezi, ambaye pia ni mshitakiwa katika kesi hiyo.

    Baada ya kukamilika kwa dodoso hilo, Tundu Lissu anatarajiwa kupewa nafasi ya kufanya majumuisho ya utetezi wake.

    Baada ya majumuisho hayo, mahakama itaendelea na hatua inayofuata ya kusikiliza ushahidi wa shahidi mwingine.

  2. Katika Picha: Matukio ya kabla ya kuanza kwa kesi ya Tundu Lisuu

    d
    Maelezo ya picha, Baadhi ya wanachama wa ngazi ya juu wa Chadema wakisubiri kufuatilia kesi dhidi ya Lissu
    h
    Maelezo ya picha, Ibada ya maombi kabla kesi kuanza
    D
    Maelezo ya picha, Shahidi namba moja anasubiriwa
    h
    Maelezo ya picha, Wafuasi wa Chadema wamewasili mahakamani wanasubiri kesi kuanza
  3. Kilichojiri jana Mahakamani

    h

    Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu, iliendelea jana katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Dar es Salaam, huku upande wa serikali ukiendelea kumuhoji Lissu kuhusu ushahidi alioutoa katika utetezi wake.

    Mawakili wa serikali walimhoji Lissu kuhusu kampeni yake ya “No Reforms, No Election”, wakitaka kujua kama mkutano alioufanya ulihitaji taarifa kwa polisi na kama ulikuwa unahusiana na uchaguzi.

    Lissu alisisitiza kuwa huo ulikuwa mkutano wa ndani na kwamba mikutano ya aina hiyo haihitaji kibali.

    Sehemu nyingine ya maswali ilijikita katika kauli za Lissu kuhusu mahakama.

    Wakili wa serikali Job Mtemba alimuuliza kama kauli kwamba majaji ni CCM na kwamba “mahakamani hapaendeki” ilikuwa na lengo la kupandikiza chuki dhidi ya mfumo wa utoaji haki.

    Lissu alikataa kauli hiyo na akasema alikuwa akizungumzia masuala ya uchaguzi.

    Lissu pia alikiri mbele ya mahakama kwamba uanaharakati na uanasiasa vina mipaka ya kisheria, na kwamba hakuna kinga inayomruhusu mwanaharakati au mwanasiasa kuvunja sheria.

    Hata hivyo, alisisitiza kuwa wananchi wana haki ya kupinga uchaguzi ambao wanaona si huru wala wa haki.

    Maswali mengine yalihusu video inayodaiwa kuwa na maneno yaliyosababisha kufunguliwa kwa kesi hiyo.

    Lissu aliendelea kusisitiza kuwa video hiyo ilipaswa kuwasilishwa mahakamani, akisema mashahidi waliodai kuiona na kuisikia hawawezi kuthibitisha kikamilifu yaliyomo bila kuwepo kwa video yenyewe.

    Katika sehemu nyingine, Lissu alihoji uaminifu wa baadhi ya mashahidi wa polisi na akaeleza kuwa hakuridhishwa na namna alivyokamatwa.

    Alisema baadhi ya malalamiko yake kuhusu kukamatwa na madai ya kushambuliwa hayakushughulikiwa na polisi, huku upande wa serikali ukimhoji kwa nini hakuchukua hatua nyingine za kisheria.

    Maswali ya upande wa serikali yaliendelea hadi mahakama ilipoahirisha mwenendo wa kesi hiyo.

    Leo kesi inatarajiwa kuendelea, Lissu akiendelea kujibu maswali ya dodoso kutoka kwa upande wa Jamhuri.

  4. Karibu katika matangazo ya moja kwa moja ya kesi ya uhaini ya Tundu Lissu, tarehe 28/08/2026.

  5. Nzengeli ahoji uhalali wa kampeni ya ‘No Reforms, No Election’

    .

    Nzengeli: Ni kweli kwamba wakati unafanya huo mkutano wa kuzuia uchaguzi hukuwa na kibali?

    Lissu: Mikutano ya ndani haihitaji kibali, inahitaji taarifa tu.

    Nzengeli: Hapo hukupi PGO?

    Lissu: Ndiyo.

    Nzengeli: Soma kifungu cha 40(3).

    Lissu: 40(3), aya gani?

    Nzengeli: Wakati natafuta, soma Sheria ya Vyama vya Siasa.

    Lissu: Nisaidie kusoma ili tusipoteze muda.

    Nzengeli: Soma kifungu cha 40(2), aya ya sita.

    Lissu: (Anasoma.)

    Nzengeli: Wewe umekielewaje?

    Lissu: Nilichoelewa ni kwamba wakati wa mikutano ya kampeni, wanasiasa watatoa taarifa kwa polisi.

    Nzengeli: Ni kweli au si kweli mkutano huo ulikuwa unazungumzia mambo ya uchaguzi?

    Lissu: Haukuwa mkutano wa kampeni, na uchaguzi ulikuwa bado miezi sita mbele.

    Nzengeli: Waheshimiwa majaji, ninaomba nimpe Sheria ya Vyama vya Siasa, kifungu cha 23.

    Lissu: Nisomee.

    Nzengeli: (Anasoma.)

    Lissu: Ahsante, uliza swali.

    Nzengeli: Je, kwa kifungu hiki ulipaswa kupeleka taarifa polisi?

    Lissu: Hapana, si kweli, kwa sababu ulikuwa mkutano wa wazi na ulikuwa mkutano wa ndani.

    Nzengeli: Shahidi, elewa swali.

    Lissu: Mikutano ya ndani, dada yangu, haihitaji notification.

    Lissu: Next.

    Nzengeli: Ni kweli au si kweli huo mkutano unaouita wa ndani ulikuwa na waandishi wa habari?

    Lissu: Ni kweli.

    Nzengeli: Ambao ulikuwa mubashara na kila mtu aliuona?

    Lissu: Ndiyo, ni mkutano wa ndani.

    Nzengeli: Una kifungu chochote kinachokupa ruhusa ya kufanya mkutano wa ndani?

    Lissu: Kifungu hicho hicho, kwa sababu hakuna mkutano unaohitaji ruhusa bali taarifa tu. Next.

    Nzengeli: Wewe usinipangie.

    Nzengeli: Je, maneno yaliyoko kwenye hati yako ya mashtaka unakiri uliyaongea?

    Lissu: Nimesema sijatangaza maneno ya uhaini mbele ya waandishi wa habari.

    Nzengeli: Uliyaongea au hukuyazungumza? Naomba uwaangalie majaji.

    Lissu: Nimeshitakiwa kwa kuchapisha maneno yanayodaiwa kuwa ya uhaini kwa zaidi ya saa tatu.

    Nzengeli: Uliyaongea au hukuyazungumza?

    Lissu: Nimeongea kwa zaidi ya saa tatu.

    Nzengeli: Je, ni kweli video ni kifaa tu kinachotumika kuchapisha?

    Lissu: Hiyo inahitaji wataalamu.

    Nzengeli: Kati yako na mahakama, nani anaweza kusema nani ni mhalifu?

    Lissu: Mahakama ndiyo inaweza kusema mtu huyu ni mhalifu.

    Nzengeli: Na ni kweli kwamba hujaleta namba za kesi za hao mashahidi wote ambao unasema ni wahalifu?

    Lissu: Mapolisi si walifuta?

    Nzengeli: Tuhuma ni shtaka au si shtaka?

    Lissu: Tuhuma si shtaka.

    Nzengeli: Shahidi, nimekusikia ukilalamika kuhusu mambo ya kukamatwa. Uliyapeleka hayo malalamiko mahakamani?

    Lissu: Niliyapeleka na hakimu wa mahakama niliyemkabidhi alikataa. Ulitaka nifanyaje wakati niko gerezani?

    Nzengeli: Unakubali kwamba sheria zote zilizotungwa na Bunge zinasimamiwa na Serikali?

    Lissu: Sheria ya uchaguzi inasimamiwa na Tume ya Uchaguzi, si Serikali.

    Nzengeli: Kwa hiyo sheria ya uchaguzi ni sheria kama sheria nyingine?

    Lissu: Ni sheria.

    Nzengeli: Ni kweli kwamba kuna tofauti kati ya kupinga uchaguzi na kuzuia uchaguzi?

    Lissu: Waheshimiwa majaji, sisi tulitaka kupinga uchaguzi mpaka mabadiliko yafanyike. Shughuli zote za uchaguzi, majimbo yasitangazwe, wagombea wasitangazwe, kwa ujumla kila kitu kisimame.

    Lissu: Utaratibu wetu wa saa kumi na moja umekuwa suspended.

    Jaji: Ngoja tuulize, tulikuwa tunajua anamalizia.

    Nzengeli: Kwa maelezo ya mshtakiwa, ni kweli amechoka na kibinadamu. Tunaomba tuahirishe.

    Lissu: Kesho nayo ni siku.

    Jaji: Tunaahirisha shauri mpaka kesho saa tatu asubuhi.

  6. Job ambana Lissu: “Je, ulipandikiza chuki dhidi ya mahakama?”

    .

    Job: Kwa mujibu wa ushahidi ulioutoa mbele ya mahakama hii, ulisema majaji ni wa CCM na kwamba mahakamani hapaendeki. Je, ni sahihi kwamba kupandikiza chuki kwa wananchi dhidi ya mfumo wa utoaji haki ni kosa kwa mujibu wa sheria zetu?

    Lissu: Kupandikiza chuki ni kufanya nini? Kupandikiza chuki ni kitu gani?

    Job: Hebu soma kifungu cha 52(1).

    Lissu: (Anasoma.)

    Job: Je, utakubaliana na mimi kwamba kwa maneno yako uliyoyatoa, ukisema majaji ni wa CCM na kwamba huko mahakamani hapaendeki, ulikuwa unapandikiza chuki?

    Lissu: Waheshimiwa majaji, sikubaliani na wakili.

    Job: Je, ni sahihi kwamba Mahakama Kuu ilishawahi kutoa amri ya ulinzi wa mashahidi?

    Lissu: Ndiyo.

    Job: Na swali lingine, je, ni sahihi kwamba shauri lililoamuru utolewaji wa ulinzi wa mashahidi ni tofauti na shauri hili?

    Lissu: Ni sahihi.

    Job: Na ni sahihi kwamba amri hiyo haijawahi kuondolewa na mahakama?

    Lissu: Ni sahihi.

    Job: Kama hukuridhishwa na amri hiyo, si ulikuwa na nafasi ya kuipinga, lakini hukuchukua hatua yoyote?

    Lissu: Hapana, sikuchukua hatua kwa sababu niko gerezani. Nitapigana vita ngapi?

    Job: Hao mashahidi unawakumbuka?

    Lissu: Niwakumbukeje wakati siwajui? Ninazikumbuka hizi herufi tu.

    Job: Ukiwa kama mwanasheria...

    Lissu: Mimi ni shahidi. Uliza swali kwa shahidi.

    Job: Utakubaliana na mimi kwamba uamuzi wa ulinzi wa mashahidi hauwezi kupingwa kupitia shauri hili?

    Lissu: Sikubaliani na wewe.

    Job: Ulieleza mahakama hii kwamba tarehe 12 Agosti 2024 ulipata pigo. Kuna kitu chochote uliwasilisha hapa mahakamani kama kielelezo?

    Lissu: Nilieleza kwa mdomo.

    Job: Ulieleza mahakama tarehe 23 Septemba 2024 kwamba ulivamiwa nyumbani kwako na Jeshi la Polisi. Je, ni sahihi kwamba hakuna ushahidi mwingine ulioutoa mahali pengine?

    Lissu: Nimeieleza mahakama hii hayo, na hakuna sehemu nyingine nilikotoa ushahidi huo.

    Job: Ulieleza mahakama hii kwamba PW1 George Bagemi alitoa maelezo kuhusu wewe kufunguliwa jalada.

    Lissu: Ndivyo yeye mwenyewe alivyosema.

    Job: Je, ni sahihi kwamba PW1 alitoa maelezo kuhusu kufunguliwa majalada mawili ya uchunguzi yenye namba zifuatazo... Utakubaliana na mimi kwamba wewe, ukiwa shahidi, hujui tofauti ya majalada hayo mawili?

    Lissu: Sijui sababu. Haiko kabisa kwenye notisi zangu. Nitajuaje wakati sikuiandika?

    Job: Katika kutokujua huko sasa, uliieleza mahakama hapa kwamba PW1, baada ya kuonyeshwa video na PW2, alipoamuru kufunguliwa kwa jalada la uchunguzi, hakukosea?

    Lissu: Sababu alipaswa amweleze DPP acoordinate uchunguzi wa masuala haya, na hakumwambia.

    Job: Kifungu gani?

    Lissu: Sina hapa, ila utaratibu uko hivyo. DPP ndiye msimamizi wa upelelezi wa masuala haya, na hayo majalada mengine unayoniambia siyafahamu kabisa.

    Job: Wakati wa kujitetea uliambia mahakama kufunguliwa kwa jalada hilo ilikuwa kinyume cha sheria, kwani kufunguliwa kwa jalada hilo kulikufanya uwe na hatia.

    Lissu: Walikuwa na majibu tayari, ndiyo maana walikuwa wanasema kosa la kwanza.

    Job: Hebu waambie majaji, ni chombo kipi chenye mamlaka ya kuamua nani ana hatia na nani hana hatia?

    Lissu: Ni mahakama.

    Job: Kwa hiyo utakubaliana na mimi kwamba jalada hili ambalo PW1 alielekeza lifunguliwe kwa ajili ya uchunguzi, ilikuwa si makosa kwa maneno aliyoyasema?

    Lissu: Ndiyo, sababu tayari walishaniamua nina makosa.

    Job: Ni wakati gani mshtakiwa anakutwa na hatia?

    Lissu: Ni baada ya mahakama kufanya maamuzi.

    Job: Je, mahakama hii tayari imeshaamua?

    Lissu: Hapana.

    Job: Waheshimiwa majaji, ninaomba kuishia hapo.

  7. Lissu: Watu wafuate sheria, lakini si kila mgogoro hukimbiliwa mahakamani

    Job: Wakati unatoa utetezi wako, ulieleza mahakama hii kwamba huwezi kuwa Rais wa TLS kama wewe ni mtu wa hovyo hovyo. Na wakati unashitakiwa tarehe 25, ulikuwa Rais wa TLS?

    Lissu: Hapana.

    Job: Kwa hiyo, baada ya kutoka kuwa Rais wa TLS unaweza kuwa mtu wa hovyo?

    Lissu: Mimi si mtu wa hovyo, hata kidogo.

    Job: Baada ya kukutwa una kesi ya kujibu, umekaribia kuwa mtu wa hovyo?

    Lissu: Mimi si mtu wa hovyo, hata kidogo.

    Job: Umewahi kuandika maelezo polisi kuhusu kushambuliwa kwako?

    Lissu: Hapana. Wamekataa, licha ya kushambuliwa. Wamekataa tangu nilipokuwa Nairobi, na ulinzi nikaondolewa.

    Job: Wewe si ulijinasibu kuwa mwanasheria?

    Lissu: Una shaka na hilo?

    Job: Mimi nauliza maswali kwa mujibu wa sheria. Waheshimiwa majaji, naomba mshitakiwa atusomee kifungu cha 1 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai.

    Lissu: (Anasoma.).

    Job: Kwa mujibu wa hicho kifungu, wewe unakielewaje?

    Lissu: Kina maana kwamba taarifa ya makosa ya jinai inaweza kutolewa kwa afisa wa polisi, kwa maneno au kwa maandishi, kuhusu kosa au taarifa za kosa.

    Job: Utakubaliana na mimi kwamba jinai haifi?

    Lissu: Niliporudi, nilikwenda kwa RPC Dodoma nikamwambia nimekuja nichukueni maelezo. Walikataa. Nikawaambia wanipatie gari yangu.

    Job: Umeleta chochote kama ushahidi kuhusu wewe kushambuliwa?

    Lissu: Nimeieleza mahakama.

    Job: Umesema wewe ulikuwa mwanaharakati kwa muda. Je, utakubaliana na mimi kwamba unapopata taarifa za vitisho au uvunjifu wa sheria, unatakiwa kutoa taarifa kwa polisi?

    Lissu: Huwezi kutoa taarifa polisi kama vitisho vyenyewe vinatoka polisi. Ramadhani Kingai na hawa polisi wanaotoa ushahidi, hawa lao ni moja.

    Job: Utakubaliana na mimi kwamba, kwa mujibu wa Katiba, mahakama inaongozwa kwa kufuata misingi ya haki?

    Lissu: Ndivyo Katiba inavyosema.

    Job: Na utakubaliana na mimi kwamba wananchi wa Tanzania, na watu wanaoishi hapa, inapotokea mgogoro sehemu yao ya kukimbilia ni mahakamani?

    Lissu: Inategemeana na mgogoro. Kama ni wa kisheria, wanakimbilia mahakamani; kama ni wa kidini, wataenda makanisani au misikitini; kama ni wa kisiasa, wanamaliza kisiasa.

    Job: Utakubaliana na mimi kwamba si sahihi kusema mahakama haifanyi haki kwa mujibu wa Katiba?

    Lissu: Sikubaliani na wewe. Tume ya Warioba ilisema majaji hawatendi haki.

    Job: Hiyo taarifa ya Warioba umeileta hapa?

    Lissu: Ripoti ilieleza wazi kwamba baadhi ya majaji hawatendi haki na kwamba kuna rushwa mahakamani.

    Job: Wewe, kwa namna unavyoamini, watu wasifuate mfumo wa kimahakama?

    Lissu: Hapana. Watu wafuate sheria.

  8. Lissu: Uanaharakati na uanasiasa havitoi kinga ya kuvunja sheria

    .

    Job: Hebu waambie majaji, hakuna mahali sheria zetu zinaruhusu watu kujichukulia sheria mkononi, kuchoma mali za watu au kuharibu uchaguzi.

    Lissu: Hakuna sheria inayoruhusu watu au mtu kujichukulia sheria mkononi, ila uchaguzi usio huru wala wa haki ni haki ya wananchi kuuzuia.

    Job: Hivi ukiwa mwanaharakati una kinga ya kutofuata sheria?

    Lissu: Hakuna kinga ya namna hiyo.

    Job: Vivyo hivyo ukiwa mwanasiasa?

    Lissu: Hakuna kinga ya mtu kutofuata sheria.

    Job: Wakati unajitetea, ulieleza mahakama hii kwamba kesi hii ni ya kisiasa. Wewe umeshitakiwa kama Tundu Lissu au kama mwanasiasa?

    Lissu: Nimeshitakiwa kama Tundu Lissu. Nisingekuwa mwanasiasa, nisingekuwa hapa. Nisingekuwa Mwenyekiti wa Chadema, nisingekuwa hapa.

    Job: Kwa mujibu wa hati ya mashitaka, kuna sehemu umeshitakiwa kama mwanasiasa?

    Lissu: Hati haisemi hivyo, ila mashahidi wote wanasema mwenyekiti wa Chadema, mwenyekiti wa Chadema, mwanasiasa. Maelezo yote yanasema hivyo.

    Job: Utakubaliana na mimi kwamba katika ushahidi wako huu ulioutoa mbele ya mahakama hapa, hujaieleza mahakama ulishitakiwa kwa kesi gani na namba gani?

    Lissu: Hapana, sikubaliani na hilo. Nimesema kesi namba, ila ndiyo sijaitaja..

    Job: Ni kweli au si kweli ulitaja namba? Hukuitaja?

    Lissu: Ni kweli, namba sikuitaja. Ukitaka nikukumbushe, nitakukumbusha.

    Job: Utanikumbusha baadaye.

  9. Lissu akiri uanaharakati una mipaka ya kisheria mahakamani

    .

    Job: Je, ni kweli au si kweli kwamba wewe ni mwanaharakati, na ulianza lini harakati zako?

    Lissu: Nimekuwa mwanaharakati siku nyingi, tangu nilipokuwa shule ya sekondari, baadaye jeshini na kwingineko.

    Job: Hebu waeleze majaji, uanaharakati ni nini?

    Lissu: Ni mtu anayefanya mambo au jambo fulani kupigania kitu fulani.

    Job: Ulijitambulisha pia kuwa wewe ni mwanasheria. Huu uanaharakati uliokuwa ukifanya unatambulika kwa mujibu wa sheria za nchi yetu?

    Lissu: Ndiyo, unatambulika.

    Job: Hebu wasaidie majaji. Ni kifungu gani na sheria gani mahsusi inayoutambua?

    Lissu: Katiba yetu imetoa uwanda mpana kwa wananchi kupigania mambo ambayo tunaona yanastahili kupiganiwa.

    Job: Tunaomba shahidi atuonyeshe na atusomee ibara hiyo.

    Lissu: Nimesema...

    Job: Nimesema tusomee kifungu hicho kinachoruhusu kufanya harakati.

    Lissu: Katiba haiko hivyo, ila inatupa uhuru wa kufanya harakati.

    Job: Harakati unazozifanya zina mipaka ya kisheria?

    Lissu: Ndiyo, zina mipaka ya kisheria.

    Job: Je, unakubali kwamba unapotafuta haki za upande mmoja, hutakiwi kubughudhi haki za upande mwingine?

    Lissu: Sahihi, hilo ninafahamu.

    Job: Sasa hebu waambie waheshimiwa. Kama nimekusikia vizuri, wakati unaongozwa ulikubali kwamba yale maneno yaliyomo kwenye hati ni sahihi?

    Lissu: Ni sahihi.

    Job: Sasa utakubaliana na mimi kwamba waliyosikia yale maneno waliyatafsiri kadiri yalivyo?

    Lissu: Sina hakika.

    Soma Zaidi:

  10. Katuga ahoji msimamo wa Lissu kuhusu ushahidi wa polisi

    Lissu Mahakamani

    Katuga: Waheshimiwa majaji, tunaendelea na ushahidi wa PW16, ushahidi wa Amini Mahamba. Sasa shahidi, hebu iambie mahakama kama ni ushahidi wako kwamba wapelelezi hawajakupa nafasi au hawajakupa maana ya maneno yaliyoandikwa kwenye hati ya mashtaka.

    Lissu: Huo ndio ushahidi wangu.

    Katuga: Kama unakumbuka, wakati shahidi PW1 alisema ulipofikishwa kwake, anasema alikupa nafasi ya kukuhoji ili umwelezee kuhusu maneno yako.

    Lissu: Wala hakuniuliza maana ya hayo maneno. Si kweli. Aliniambia anataka kuchukua maelezo yangu tu.

    Katuga: Na wewe ulijibu nini?

    Lissu: Nilimjibu kwamba kwa kuwa mmeshanikamata na mmeshanishtaki, tutakutana mahakamani.

    Katuga: Waambie hawa majaji, hawa wapelelezi walikupa nafasi ya kukuhoji au la.

    Lissu: Hawakunipa nafasi kwa sababu tayari nilikuwa nimeshashtakiwa.

    Katuga: Kwa hiyo ni uelewa wako wa kisheria kwamba mtuhumiwa hakamatwi?

    Lissu: Mimi nilikamatwa, nikawaambia tutakutana mahakamani.

    Katuga: Ulizuiwa na nini kutoa maana ya maelezo yako?

    Lissu: Walitaka maelezo yangu ya nini wakati walikuwa wameshanikamata?

    Katuga: Je, pale ulipokuwa, ulishindwa na nini kumpa tafsiri ya maneno hayo na Bwana Bagemi alikupa nafasi ya kutoa maelezo?

    Lissu: Ningesema nini wakati nilikuwa nimeshashtakiwa? Nimeshtakiwa kwa kosa la kifo na watu walionitesa kwa miaka 24. Ulitaka nijieleze tu?

    Katuga: Ulisema maelezo D1 hadi D16 ni vielelezo vya utetezi wako, na nakumbuka katika utetezi wako ulirejea Kielelezo D15. Waambie majaji, ni kielelezo ambacho ulikiamini na kukirejea katika utetezi wako?

    Lissu: Maneno yapi? Sikumbuki.

    Katuga: Baada ya kuunda timu, mimi na timu nzima tulitazama na kusikiliza video hiyo ambayo bado ilikuwa mtandaoni, na kama nilivyotafsiriwa nikabaini kosa la kwanza ni uhaini na kuchapisha mtandaoni. Ukaambia mahakama kuwa PW16 tayari alikuwa amekuhukumu kwa uhaini.

    Lissu: Niliyarejea nikiunganisha na ushahidi wa PW1 na PW17.

    Katuga: Kwa hiyo, kwa mujibu wa maneno ya shahidi huyu, aliona uhaini kwenye kielelezo chake au hakuona uhaini?

    Lissu: Sikusema ninawaamini. Mimi siwaamini polisi hawa.

    Katuga: Umechukua maelezo ya mashahidi wawili tofauti kwa sababu uliwaamini na ukawaambia majaji kwamba maelezo yao yanatofautiana?

    Lissu: Mimi niwaamini polisi? Hapana. Mimi niliyatoa kwa sababu yana tofauti; mmoja ameona uhaini, mwingine hajaona.

    Katuga: Unajua nimekuuliza swali la kwanza. Je, hiki ni kielelezo chako cha utetezi kwa sababu unakiamini?

    Lissu: Niliomba kiwe kielelezo changu kwa sababu kinatofautiana na maelezo mengine kwa kuwa kinaonyesha mgongano wa maelezo (contradiction).

    Katuga: Kwa maelezo yako mwenyewe sasa, shahidi, uko timamu?

    Lissu: Wewe unanionaje?

    Katuga: Wewe iambie mahakama.

    Lissu: Move on.

    Katuga: Maelezo haya unayaamini au huyaamini?

    Lissu: Niyaamini kwa jambo gani?

    Katuga: Waambie majaji kama uliwaomba kwamba maelezo yaliyomo kwenye vielelezo hivi vyote yaweze kutumika.

    Lissu: Nimejibu hilo swali. Move on.

    Katuga: Waambie majaji vielelezo D1 mpaka D15 vitumike kuonyesha nini?

    Lissu: Vitumike kuonyesha omissions na contradictions.

    Katuga: Kwa kuwa umeiambia mahakama vielelezo hivi vitumike, je, kuna sehemu umesema vielelezo vitumike hapa na visitumike pale?

    Lissu: Waheshimiwa majaji, hilo nitalifanya wakati wa kuwasilisha hoja zangu za mwisho.

    Katuga: Swali ni, uliwaambia au hukuwaambia majaji?

    Lissu: Nitawaambia wakati wa kuwasilisha hoja zangu za mwisho.

    Katuga: Waheshimiwa majaji, naomba swali hilo lirudiwe na lijibiwe.

    Lissu: Sikuwaambia.

    Katuga: Je, ni haki ya mahakama kutumia vielelezo vyako?

    Lissu: Sasa hilo ni uamuzi wa mahakama kuona namna itakavyotumia vielelezo hivyo.

    Katuga: Waheshimiwa majaji, ikiwapendeza, naomba niishie hapa na nimkaribishe wakili mwenzangu wa serikali.

    Soma Zaidi:

  11. Lissu ang’ang’ania video iletwe mahakamani, Katuga apinga hoja

    .

    Katuga: Kwenye ile video unachokiona ni nini, maneno au video?

    Lissu: Sijaiona, si hamjaileta?

    Katuga: Katika sheria ya ushahidi, mtu akikutolea ushahidi wa maneno, anatoa ushahidi wa kusikia?

    Lissu: Ndiyo, wa kusikia kama ni wa maneno tu, ila kama ni video ni wa kuona na kusikia.

    Katuga: Unatuhumiwa kufanya nini?

    Lissu: Kutoa maneno na kuyachapisha.

    Katuga: Umewaambia majaji kwamba upande wa Jamhuri haujathibitisha shtaka hilo kwa sababu video hawajaileta. Waambie mashahidi wa Jamhuri walisemaje.

    Lissu: Walisema wameona video na kusikia maneno.

    Katuga: Kwa hiyo waliona na kusikia?

    Lissu: Huwezi kutenganisha video na sauti, kwa hiyo lazima iwe kuona na kusikia.

    Katuga: Unajua kwamba kila shahidi ana haki ya kuaminiwa?

    Lissu: Ndiyo, ninajua, na anastahili kuaminiwa kama kuna misingi ya kumuamini.

    Katuga: Sasa iambie mahakama hii, katika mashahidi wa Jamhuri wale waliosema wameona video, ni kifungu kipi kinaelekeza kwamba lazima walete video hiyo mahakamani licha ya kwamba wameiona?

    Lissu: Lazima wailete mahakamani ili waaminike.

    Katuga: Iambie mahakama, ni kweli kwamba mtu anayepandisha video mtandaoni anaweza kuja kuifuta?

    Lissu: Ndiyo.

    Katuga: Unaelewa kwamba kitu fulani kinaweza kupotea ghafla. Kama mtu atakuwa amefanya kosa kwa kupandisha video yenye tatizo kisha akaifuta, iambie mahakama kwamba mtu huyo hawezi kuja mahakamani kutoa ushahidi? Kwa hiyo kilicholetwa hapa ni nini?

    Lissu: Maneno na video havitengani. Video yenyewe haijaletwa.

    Katuga: Tuiombe mahakama ikuchukulie wewe ni muongo?

    Lissu: Jaji alisema hakumbuki, tuendelee.

    Katuga: Unataka shahidi PW17, ambaye alisema alikusikia ukisema hayo maneno ya kukinukisha, ayalete hapa mahakamani?

    Lissu: Ndiyo, ayalete hapa.

    Katuga: Ni ushahidi wako kwamba mashahidi kutoka polisi waliandika maelezo yao wenyewe na kwa hiyo si wa kuaminika? Sasa mashahidi hawa wasiaminiwe kwa sababu wameandika maelezo wenyewe. Ni kifungu gani kinaipa mahakama mamlaka hayo?

    Lissu: Kifungu cha 11 kinaelekeza kwamba polisi ambao hawakufuata utaratibu hawaaminiki.

    Katuga: Wasomee majaji.

    Lissu: (Anasoma.)

    Katuga: Waambie majaji, kwa mujibu wa kifungu hicho, kimeeleza nini kuhusu polisi anayefanya upelelezi; anapaswa kuandika maelezo?

    Lissu: Kama afisa huyo ni shahidi, basi haandikiwi maelezo.

    Katuga: Afisa mdogo wa polisi anaweza kumwandikia afisa wa juu maelezo?

    Lissu: Ndiyo, anaweza.

    Katuga: Unajua kwamba maelezo ya shahidi yanaandikwa kwa mujibu wa sheria?

    Lissu: Sikumbuki.

    Katuga: Unajua kwamba tamko ni tamko la kiushahidi, na unajua kwamba shahidi lazima aonywe?

    Soma Zaidi Hapa:

  12. Lissu ajibu maswali kuhusu ushahidi wa video

    Lissu

    Katuga: Kama uliwaambia majaji hawa waendesha mashtaka hawajaleta video na kwamba, kwa kuwa mahakama haina video hiyo, wameshindwa kuthibitisha mashtaka yao, waambie majaji kama wakati unasema hayo ulikuwa unajua au umesoma mashtaka yanayokukabili.

    Lissu: Nilikuwa nimesoma mashtaka yanayonikabili na niliyaelewa kwa undani.

    Katuga: Kwa mujibu wa mashtaka, kuna sehemu unashtakiwa kwa kuchapisha video?

    Lissu: Nashtakiwa kwa kuchapisha maneno kwenye mtandao wa Jambo TV.

    Katuga: Je, nitakuwa sahihi nikisema video unasikia na kuona kama video hiyo ina maneno?

    Lissu: Video ni kuona na kusikia. Kwa mujibu wa sheria ya ushahidi, mtu akitoa ushahidi kuhusiana na maneno anakuwa ametoa ushahidi wa kusikia.

    Katuga: Kwa mujibu wa mashtaka, unatuhumiwa kuyachapisha na kutoa maneno kwenye mtandao wa YouTube wa Jambo TV. Uliiambia mahakama kuwa upande wa Jamhuri haujathibitisha mashtaka kwa sababu video hiyo hawajaileta?

    Lissu: Mashahidi wote wa Jamhuri walisema kuwa wameona na kusikia maneno.

    Katuga: Unafahamu kwamba kila shahidi ana haki ya kuaminiwa isipokuwa kama mahakama ina sababu za kutomuamini, na sababu hizo lazima zionyeshwe? Iambie mahakama hii, wale mashahidi waliosema wameona video, ni kifungu gani cha sheria kinachosema kuwa ili waaminiwe lazima walete video?

    Lissu: Si lazima sheria iseme hivyo, bali hiyo ni common sense.

    Katuga: Ni kweli kwamba mtu anayeipandisha video mtandaoni ana uwezo wa kuifuta?

    Lissu: Ana uwezo huo.

    Katuga: Je, mtu akiwa amefanya kosa kwa kuchapisha video mtandaoni halafu akaifuta, na mtu mwingine akaiona video hiyo kabla haijafutwa, ni ushahidi wako kwamba hawezi kuthibitisha alichoona?

    Lissu: Hawezi kuthibitisha.

    Katuga: Video na maneno, kilicholetwa hapa mahakamani ni nini?

    Lissu: Wameleta maneno tu, na hayo si maneno ya kwenye video, kwa sababu maneno ya video huwezi kuyatenganisha na video yenyewe.

    Katuga: Unakumbuka PW17 ndiye shahidi pekee aliyekuwa live eneo la tukio?

    Lissu: Ndiyo.

    Katuga: Unakumbuka shahidi PW17 alisema Lissu alisema atauzuia uchaguzi?

    Lissu: Sikumbuki.

    Katuga: Kwa kuwa shahidi alikuwa eneo hilo, alihitajika kuileta video hiyo?

    Lissu: Alipaswa kuileta video hiyo.

    Katuga: Anasema alikusikia ukisema unaenda kuzuia uchaguzi na kwamba utaenda kukinukisha. Je, unataka shahidi huyo alete video hapa mahakamani?

    Lissu: Ndiyo, lazima.

    Katuga: Ni ushahidi wako kwamba mashahidi kutoka Jeshi la Polisi hawaaminiki kwa sababu waliandika maelezo bila kufuata utaratibu?

    Lissu: Ni kweli hawaaminiki kwa sababu hawakufuata utaratibu.

    Katuga: Ni kweli kwamba mashahidi wote uliowataja walikuja hapa mahakamani kutoa ushahidi, na kwa kufanya hivyo mahakama imepata fursa ya kutathmini uaminifu (credibility) wao?

    Lissu: Hayo ni ya majaji.

    Katuga: Ni kifungu gani cha sheria kinachoipa mahakama mamlaka ya kutowaamini polisi waliokuja kutoa ushahidi?

    Lissu: Utaratibu wa kuandika maelezo upo chini ya Kifungu cha 11(4) cha CPA. Kifungu hicho hakijaeleza chochote kuhusu hilo.

    Katuga: Umesema maelezo haya yalitakiwa yaandikwe mbele ya afisa wa polisi na si mpelelezi.

    Lissu: Ndiyo.

    Unaweza kusoma;

  13. Lissu akiri kuridhia yaliyomo kwenye vielelezo vyake mahakamani

    .

    Katuga: Unakumbuka kwamba uliambia mahakama kuwa umetoa vielelezo D1 hadi D15. Je, ni vielelezo vyako au si vyako?

    Lissu: Ni vyangu kwa sababu mimi ndiye niliyeomba viingizwe mahakamani.

    Katuga: Je, nikisema kwamba uliomba vipokelewe mahakamani kama vielelezo vyako, umeridhika na yaliyomo ndani ya vielelezo hivyo?

    Lissu: Ndiyo, nimeridhika.

    Katuga: Umeridhika vitumike kama vielelezo vyako, na unaridhika na vielelezo ulivyovitoa?

    Lissu: Nimeridhika vitumike katika utetezi wangu.

    Katuga: Waheshimiwa Majaji, tunaomba vielelezo D1 hadi D15 ...

    Soma Zaidi Hapa:

  14. Uko timamu mzee wangu? Lissu aulizwa na upande wa serikali

    ;;

    Katuga: Naona tutakaa hapa siku mbili

    Lissu: Unanitisha na siku mbili nimekaa ndani mwaka na miezi mitano

    Katuga: Iambie mahakama ulinzi wa mashahidi maana yake nini

    Lissu: Ni mashahidi wa kificho/ ni mashahidi wanaolindwa

    Katuga: Iambie mahakama, Je, ulisema baadhi ya watu huenda tulikuwa nao humu ndani. Je, huu ni ushahidi au hisia tupu?

    Lissu: Ndio ni shahidi wangu sababu hawajulikani hakuna anayewajua isipokua nyie

    Katuga: Je ushahidi wa kwamba hawa ni mapolisi. Je, ni ushahidi au fununu tu?

    Lissu: Ni ushahidi sababu hawajulikani na yeyote

    Katuga: Sasa shahidi tunataka majibu sahihi ni kweli au sio kweli. Ushahidi wa kwamba baadhi ya mashahdi huenda tulikuwa nao humu ndani. JE, ni kweli, sio kweli, sio wa kuona wala kusikia?

    Lissu: Sio Kweli

    Katuga: Iambie mahakama kama ni kweli au sio kweli unatuhuma nyingie za kuchapisha uongo mtandaoni

    Lissu: Ni kweli

    Katuga: Iambie mahakama unakumbuka ulisomewa hoja za awali na ikaanza kusikilizwa

    Lissu: Ndio nianakumbuka

    Katuga: Unakumbuka uliposomewa hoja za wali ulisema majaji ni ma-CCM

    Lissu: Sikumbuki

    Katuga: Iambie mahakama hii katika hotuba yako pia ulitangaza kutogumbea kwa chama chako

    Lissu: Sikumbuki, nakumbuka nilisema tutahamasisha ….

    Katuga: Hapana, hukumbuki nimsekia ukijiita mwenyekiti wa Chadema. Iambie mahakama kama chama chako kilishiriki uchaguzi mwaka jana

    Lissu: Hapana hakikushiriki

    Katuga: Je, ni kweli kwamba uliposema mahakamani hakuendeki huna imani na mahakama

    Lissu: Kwenye maswala haya ya uchaguzi sina imani na mahakama

    Katuga: Kwenye zile njia ulizotuambia jana. Je, nitakuwa sahihi kwamba hukupanga kabisa kuiomba mahakama kutumia sheria

    Lissu: Sikupanga kabisa

    Katuga: Kwa hiyo ni sahihi kwamba swala la kupinga sheria kwa njia ya mahakama sio njia mbadala wala ya kidemokrasia

    Lissu: Hapana

    Katuga: Kwa hiyo kukinukisha ni njia ya kidemokrasia?

    Lissu: Ndio ni njia ya kidemokrasia

    Katuga: Kuhamasisha uasi ni njia ya kidemokrasia?

    Lissu: Ndio ni njia ya kidemokrasia

    Katuga: Uko Timamu mzee wangu

    Lissu: Kimya

    Katuga: Kama nilikusia ulitamka vifungu vya 55, 63, 52 kifungu cha 52 cha sheria ya habari. Ni kweli kwamba sheria ya habari iliundwa kwa ajili ya kuendesha tasnia ya habari?

    Lissu: Ndio

    Katuga: Kama nilikusikia vyema ulisema kuikosoa serikali sio kosa

    Lissu: Nilisema kuipinga serikali sio kosa

    Katuga: Kama una kanuni yako ya adhabu hapo kwa ridhaa ya mahakama hiki kifungu cha 55, yale maneno uliyotumbua, 'ya kuzuia uchaguzi' waambie majaji kuzuia uchaguzi ni kuipinga serikali au kuzuia uchaguzi?

    Lissu: NI kuzuia uchaguzi

    Katuga: Kuhamasisha uasi, kukinukisha nikupinga serikali au kupanga kuipindua serikali?

    Lissu: Ni kuipinga serikali, sikuwa nazungumza habari ya serikali tulikuwa tunapanga kuzuia uchaguzi

    Katuga: Unakumbuka umesema kwenye hotuba yako ulikuwa huzungumzii serikali

    Lissu: Ndio sikuwa napinga serikali nilikua nazungumza habari za uchaguzi

    Katuga: Kama nikikusikia vyema uliwaambia waheshimiwa hawa mashahidi wanaotoka jeshi la polisi, kasoro mmoja, wote wamejiandikia maelezo kitu ambacho ni kinyume cha sheria. Waambie majaji kama uliwatajia kifungu cha sheria na sheria yenyewe

    Lissu: Sikuwaambia kifungu lakini kipo

    Katuga: Unajua kwamba askari aliyemuandika shahidi maelezo na yeye ni shahidi kama huyo shahdi hata fika mahakani

    Lissu: Sikumbuki

    Soma Zaidi Hapa:

  15. Lissu aendelea kujibu maswali ya upande wa serikali

    ;

    Katuga: Kama nilikusikia vyema uliiambia mahakama hii kwamba shahidi PW1 hakusema kama alivyogundua ni kosa la uhaini hakuwasiliana na ngazi za juu akiwemo DCI, kwamba ilipelelezwa vibaya

    Lissu: nilisema ilipelelezwa vibaya

    Katuga: Iambie mahakama kama sheria inaelekeza ukigundua kosa la uhaini lazima uwasiliane na hizo mamlaka zote, imabie mahakama kama ulitaja kifungu

    Lissu: Hapana sikutaja kifungu

    Katuga: Je unakumbuka ulisema kuna kutoelewana kati yako na Kingai (Kamishna wa Polisi Ramadhani Kingai ni Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) nchini Tanzania) pamoja na IGP Wambura (Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Camillius Wambura)

    Lissu: Ni kweli nimekamatwa mara kadhaa bila kuzingatia taratibu

    Katuga: Umekuwa mwanasheria muda mrefu na mwana siasa miaka 24. Je, ushawafunguliwa wawili hawa mashitaka?

    Hapana: Sijawafungulia

    Katuga: Kama nimekusikia vizuri uliambia mahakama hii kwamba wale mashahdi walioletwa ni mashahidi ambao walikuwa ni washitakiwa

    Lissu: Nilisema walikiri kupanga uhalifu

    Katuga: Je, kuna sheria inayozuia mtu aliyefanya uhalifu kuja kutoa ushahidi?

    Lissu: Hapana

    Katuga: Katika ushahidi wa mashahidi toka Jeshi la polisi walieleza walikamata wote

    Lissu: Waliokamata waliweza kuwatambua

    Katuga: Kwa ushahidi huo ina maana inawezekana kukawa na wengine

    Lissu: Hawakutambuliwa au hawakukamatwa

    Katuga: Nakukumbusha ile kauli yako si ndio uliambia mahakama mtu yeyote anaweza kutafsiri vyovyote vile na wale walisema wamehamasika kutokana na nini

    Lissu: Maneno yangu

    Katuga: Kwa hiyo nitakuwa sahihi nikisema walielewa hotuba yako na kufanyia kazi maneno yako kwa jinsi walivyoelewa

    Lissu: Hapana siwezi sema sababu siwajui na siwezi kuwasemea

    Katuga: Je, uliiambia mahakama hawa mashahidi ni waongo na hawastahili kuaminiwa na mahakama?

    Lissu: Ndio, niliambia mahakama hawapaswi kuaminiwa wao na ushahidi wao

    Soma Zaidi Hapa:

  16. Upande wa serikali unaendelea na maswali ya dodoso kwa Tundu Lissu

    l

    Wakili wa serikali (Nassoro Katuga): Umesema umepata tuzo kadhaa kwa kupigania haki. Je, ulitaja nchi za Afrika ulizopigania haki?

    Lissu: Hapana

    Katuga: Je uliiambia mahakama pamoja na kukaa kwako gerezani unasema heshima yako imeongezeka. Waambie majaji ni lini ulifanya huo utafiti ukajua heshima yako imeongezeka?

    Lissu; Heshima haitokani na sensa

    Katuga: Sasa wewe umejuaje heshima yako imeongezeka?

    Lissu: Heshima inaongezeka kwa watu kukuheshimu

    Katuga: Oooh pamoja na wazungu?

    Lissu: Hapana, sio wao tu, watu wote zikiwemo taasisi za kimataifa

    Katuga: Shahidi kama nilikuelewa vyema ukiwa unazungumzia mapungufu ya sheria za uchaguzi ulimuelezea mgombea wako wa jimbo la Mlimba kwamba alirudisha fomu akamkuta mtu hayupo. Ulikuwepo au uliambiwa?

    Lissu: Niliambiwa na nilisoma kweye taarifa rasmi

    Katuga: Waambie majaji kuwa mashahidi wa Jeshi la Polisi, hao mashahidi wa kificho hawajulikani na mtu mwingine

    Lissu: Ndio

    Katuga: Waambie waheshimiwa majaji kama uliwahi leta pingamizi juu ya kizimba cha mashahidi wa siri

    Lissu: Ndio

    Katuga: Iambie mahakama maamuzi ya mahakama ni nini

    Lissu" Waliamua wawaone wao

    Katuga" iambie mahakama hawa ulikua unawaIta P ni akina nani

    Lissu: Hayo ni majina, hizo ni alama, hayo ni mambo ya kuwaficha

    Katuga: Je unajua maamuzi ya mahakama hii juu ya kuficha utambulisho wa mashahidi

    Lissu: Iliamua wafichwe

    Katuga: Imabie mahakama ni sheria gani inayotaka ujue jina la shahidi ndio shahidi atoe ushahidi

    Lissu: CPA na Sheria ya Ushahidi inaelekeza mpaka ajulikane

    Katuga: Iambie mahakama

    Lissu: Kwa CPA na sheria ya mwenendo wa ushahidi, lazima afahamike na majaji na mahakama na watuhumiwa na sio upande wa utetezi peke yake

    Katuga: Waambie majaji ni kifungu gani cha CPA

    Lissu: Naomba nisome waheshimiwa majaji ni kifungu cha 112 kinachosema mashahidi watatoa ushahidi mbele ya hadhara ya mahakama na utambulisho wao utawekwa wazi, majina, dini zao na makazi yao

    Katuga: Je, kifungu kinasema hawatatoa ushahidi mpaka majina yao ya kweli yafhamike

    Lissu: Ndio hivyo kifungu kinasema

    Katuga: Waambie majaji wapi pameandikwa majina ya kweli yatajwe

    Lissu: Hakuna ila ni lazima mahakamma itambue utambulisho wao

    Katuga: Hivi unakumbuka wakati PW17 aliiambia mahakama baada ya kutoa hotuba, mliwatoa nje waandishi ili mkae kikao cha ndani

    Lissu: Ndio

    Katuga: Waambie majaji kama uliwahi kukanusha kama mliwatoa waandishi nje

    Lissu: Ndio hayakuwa yanawahusu tuliwaita kwa ajili ya mkutano na watia nia na sio zaidi ya hapo na baada ya kuwatoa waliondoka sio kwamba tuliwatoa na kuwarudisha

    Katuga: Unajua majibu yako yanavutia sana

    Lissu: Inabidi ufurahi kama yanavutia

    Katuga: Kwa hiyo nicheke cheke

    Lissu: Ndio cheka cheka si yanavutia sasa

    Katuga: Tafsiri sahihi inamaana wewe na wenzako mliwatoa waandishi wa habari

    Lissu: Ndio tuliwatoa

    Katuga: Mnasema mliwatoa sababu hayakua sehemu ya yale mliyowaitia

    Lissu: Ndio

    Katuga: Kwa hiyo yale ambayo hamkutaka yachapishwe mliwatoa nje

    Lissu: Ndio

    Katuga: Kwahiyo unawaambia majaji yale yaliyochapishwa ni yale uliyotaka yachapishwe

    Lissu: Ndio yote tuliyotaka wawepo walikuepo waandishi wa habari na si vinginevyo, ila sikuwa lazimisha wachapishe

    Soma Zaidi Hapa:

  17. Habari picha: Matukio ya kabla ya kuanza kwa kesi ya Tundu Lissu

    OL
    k
    Maelezo ya picha, Ibada ya maombi kabla kesi kuanza
    l
    l
    Maelezo ya picha, Wafuasi wa Chadema wakiwa tayari kufuatilia kesi
    ;
    Maelezo ya picha, Baadhi ya wanachama wa ngazi ya juu wa Chadema
  18. Kesi ya uhaini ya Tundu Lissu kuendelea leo

    ;

    Kesi ya uhaini inayomkabili mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), inaendelea tena leo katika mahakama jijini Dar es Salaam, baada ya kuahirishwa hapo jana.

    Mwenendo wa kesi hapo jana ulifikia katika hatua ya upande wa serikali kumuuliza mshtakiwa maswali ya dodoso baada ya Lissu kuwasilisha ushahidi wa kujitetea.

    Soma Zaidi Hapa:

  19. Karibu katika matangazo ya moja kwa moja ya kesi ya uhaini ya Tundu Lissu, tarehe 27/08/2026

  20. Maswali ya dodoso kwa Lissu yakiendelea

    Katuga: Kama nimekusikia vyema umesema ulitoa hotuba kwa watia nia wa Chadema na pia ulitoa hotuba hii mbele ya waandishi wa habari waambie majaji kama katika ushahdi wako umewaambia waandishi wa habaari wasipeleke rekodi zile na yale mliyozungumza.

    Lissu: Hapana sikuwaambia.

    Katuga: kwa hiyo ulitaka habari yako iende kwa walaji?

    Lissu: Ndio nilitaka iwafikie wananchi.

    Katuga: Katika ushahidi wako ulisema kama ulitoa mipaka kwa watu wanaopaswa kusikia ile hotuba.

    Lissu: Hapana sikutoa mipaka

    Katuga: Wale watia nia ulikua nao pale ambao ndio ulikuwa umewakusudia?

    Lissu: Ndio walikuwepo

    Katuga: Waambie majaji kama unakumbuka mkutano ulikuwa mubashara.

    Lissu: Ndio ni kweli

    Katuga: Waambie majaji kama uliwapa waandishi wa habari hotuba yako kabla kuzungumza.

    Lissu: Hapana sikuwapa.

    Katuga: Hivyo walikuwa hawajui unakwenda kuzungumza nini?

    Lissu: Ni sahihi

    Katuga: Kwa kuwa walikuwa hawajui nitakuwa sahihi nikisema haya maneno PW17 na wenzake walikuwa hawajui kabla ya wewe kuyatamka.

    Lissu: Ndio walikuwa hawajui.

    Katuga: Unakumbuka mashahidi walisema ulikuwa umevaa kombat na tishrt nyeusi?

    Lissu: Ndio nakumbuka.

    Katuga:Kuna sehemu umekanusha vazi ulilokuwa umevaa.

    Lissu: Ningekanushaje vazi langu rasmi la chama?

    Katuga: Kwa kuwa unasema ilikuwa hivyo nitasema mashahidi wa jamuhuri walikutambua kwa usahihi baada ya kutazama ile video.

    Lissu: Ninasema mashahdi wa jamhuri wananitambua siku nyingi ni sahihi nilikua nimevaa hivyo.

    Katuga: Unajua Principle ya constructive possession na constrtuction

    Lissu: Hapana siijui.

    Katuga: Umeiambia mahakama unakumbuka PW 17 alisema alichapisha kupitia wewe?

    Lissu: Hapana alisema walichapisha wao kupitia Mimi. Waheshimiwa majaji naomba nikae hii mvua ya maswali inanielemea.

    Jaji: Kaa.

    Katuga: Unapotoa hotuba kila mtu si ana haki ya kuelewa na kutelekeza vile alivyoelewa?

    Lissu: Ndio ni kweli

    Katuga: Maneno ya kwamba tutazuia uchaguzi si kila mtu ana haki ya kuelewa alivyolewa?

    Lissu: Ndio Maneno kama Tutazuia uchaguzi si kila mtu ana haki ya kuzuia uchaguzi kwa kutumia njia yake mwenyewe

    Katuga: Unakumbuka PW3 alipotoa ushahidi na kusema walipanga kuzuia uchaguzi kwa kurusha mawe kuchoma moto baada ya kauli zako walipanga kurushia watu mawe wasiende kupiga kura iambie mahakama hii kwamba uchaguzi upo kwa mujibu wa sheria.

    Lissu: Ndio

    Katuga: Mojawapo ya kazi za serikali ni kusimamia sheria

    Lissu: Ndio

    Katuga: Je, kuzuia watu kwenda kupiga kura kwa kuwarushia mawe ni uvunjifu wa amani sio ubunjifu wa amani?

    Lissu: Ndio ni uvunjifu wa amani

    Katuga: Na Jeshi la polisi liko chini ya nani?

    Lissu: Jeshi la Polisi liko chini ya serikali

    Katuga Unapotishia kuvunja amani umemlenga nani?

    Lissu: Hapana unapovunja amani hujalenga polisi.

    Katuga: Utanijibu tu ujanja hauna.

    Lissu: Twende

    Katuga: Anapotishia kuvunja amani anakuwa amefanyaje?

    Lissu: Anakuwa analipa Jeshi la polisi kazi ya kumzuia asivunje amani.

    Katuga: Kama niko sahihi ulisema unataka kuhamasisha maandamano ya kidemokrasia, je, kwenye haya maneno kuna maneno utahamasisha uasi wa kidemokrasia?

    Lissu: Hapana

    Katuga : Je, video ililetwa mahakamani au haikuletwa wewe si mkweli?

    Lissu: Ililetwa ikakataliwa na mahakama.

    Katuga: Je, wewe ungependa kuiona na kuiomba mahakama hii tukufu iilete mahakamani?

    Lissu: Hapana hamuwezi mkaleta takataka nije niwasaidie mimi.

    Katuga: Demokrasia inatoa haki kwa wote waounga mkono na wasio unga mkono yule anapenda kupiga kura. Je, yale maneno kuzuia uchaguzi yanatokana na demokrasia gani?

    Lissu: Kama kuna jambo mnaona halipendezi mna haki ya kukipinga na kuliondoa kwa mujibu wa sheria.

    Katuga: Je, unajua kuzuia uchaguzi ni kosa?

    Lissu: Hapana sheria haijasema.

    Katuga: Je, bado unasisitiza katiba inasema ni haki ya kikatiba kumzuia mtu kupiga kupiga kura kwa kufanya fujo?

    Lissu: Katiba sio ibara moja.

    Katuga: Tafsiri ya adhabu inaposema shall be liable pale ambapo kifungu cha sheria kinatoa maneno shall be liable je, kuna descretion ya mahakama?

    Lissu: Hapana.

    Katuga: Uko aware na kesi ya Shengi Muhagama?

    Lissu: Niko Gerezani nitajuaje?

    Katuga: Si ulikua unatoa kesi hapa?

    Lissu: Wewe unaangalia mtandaoni hapo mimi naanngalia wapi?

    Katuga: Si una watafiti we mzee?

    Lissu: Waambie mmenishtaki kunyongwa kosa la bure.

    Katuga: Unaweza kuisaidia mahakama tofauti ya mkanganyo na hapa halipo.

    Lissu: Mkanganyiko ni kama jambo linalokuwa na maelezo mawili yanayotofautiana lakini omission ni jambo ambalo halipo lakini limechomekewa.

    Katuga: umewahi kufungua shauri kwa jina lako kupinga sheria ya uchaguzi?

    Lissu: Hapana, kwa chama changu Yes

    Katuga: Kama nilikusikia vyema umeleta mambo ya jaji chande sana ya 29/10

    Lissu: Ndio

    Katuga: Je ni kweli kwamba ripoti yake ilisema pia matukio haya yalipangwa kabla kutokana na malalamiko ya muda mrefu ya mifumo ya uchaguzi, katiba ajira ……

    Lissu: Nisomeee unikumbushe.

    Katuga: Kwenye hotuba yako tuambie kama ulisema tukikinukisha watatufanya nini?

    Lissu: Hapana.

    Katuga: Sasa ulisema watanikamata watanifungulia kesi ya uhaini?

    Lissu: Hapana.

    Katuga: Unakumbuka kuwaambia majaji ni ma CCM?

    Lissu :Ndio.

    Katuga: Waheshimiwa majaji bado tuko nusu ila nikiangalia muda naona ni saa 11

    Jaji: Mshtakiwa unasemaje?

    Lissu: Waheshimiwa majaji kama ni saa 11 inatosha nimesimama ya kutosha kwa leo.

    Jaji: Kimsingi tunatamani kuanza saa tatu kamili ili tuwe tumetumia muda vyema. Tutakapowahi tutaanza.

    Tunahirisha mpaka kesho saa tatu asubuhi.