"Kwa karibu robo Karne naonewa" - Lissu
Lissu anaendelea, nikweli au si kweli ulichaguliwa kuwa mpelelezi wa matukio ya baada ya uchaguzi kama mpelelezi mkuu wa matukio hayo
Shahidi: Sikua mpelelezi wa matukio hayo nilikua kwenye team lakini sikua mpelelezi wa matukio hayo.
Lissu: Kutokana na upelelezi wa timu yako kuna watu walishitakiwa kwa uhaini kama mimi?
Shahidi: Sikumbuki.
Lissu: Kesi ya Paulina Palyango na wenzake 75 ya kula njama.
Shahidi: Sikumbuki
Lissu: Pia Niffer na wenzake shtaka la kwanza kula njama la pili uhaini
Shahidi: Sikumbuki
Lissu: Omar Pandu Salum na wenzake 33 na hili unalikumbuka?
Shahidi: Sikumbuki.
Lissu: Waeleze majaji hukumbuki kuna watu wengi sana walikamatwa na kushtakiwa kwa uhaini jumla ya watu 673 nchi nzima kwa upelelezi wako na wenzako.
Shahdii: Sikumbuki na mimi sio msemaji wa Jeshi.
Lissu: Waeleze majaji kwamba kesi zote hizi zilifutwa
Shahidi: Sikumbuki
Lissu: Nakurejesha kwenye mikutano ya hadhara, waeleze majaji kama sheria inazuia hii mikutano wakati wa uchaguzi tu.
Shahidi: Sina jibu.
Lissu: Pamoja na waandishi wa jambo unafahamu kulikuwa na waandishi wa Azam, ITV, Arusha one digital, Clouds media , walikuwepo waandishi wa Chanzo TV
Shahidi: Ndio ninafahamu
Lissu: Waeleze majaji kuwa hawa waandishi wengine walirusha mkutano kwenye vyombo vyao.
Shahidi: Walirusha kutokea kwa Jambo
Lissu: Waandishi wa habari wote hawa walifahamu hayo maneno na kuyarusha?
Shahidi: Kufahamu sijui ila waliyarusha.
Lissu: Mtu anayepata taarifa za uhaini anapaswa azitolee taarifa polisi ni iweli sio kweli?
Shahidi: Ndio
Lissu: Na huyu mtu asipotolea taarifa polisi anakuwa amefanya kosa la kuficha uhaini?
Shahidi: Sifahamu sina hakika nayo.
Lissu: Kuna hata mmoja kati ya waandishi hawa aliyetoa taarifa
Shahidi: Hakuna.
Lissu: Mtu ambaye amechapisha maneno hayo si anakua amefanya kusambaza?
Shahidi: Hawakufanya kosa
Lissu: Kwenye huo mkutano kulikua na watu zaidi ya 300 waeleze majaji kama hata mmoja alileta taarifa
Shahidi: Hakuna.
Lissu: Kuna hata mmoja kati yao ukiacha mimi alituhumiwa.
Shahidi: Hapana.
Lissu: Ulikuwa mkuu wa upelelezi waeleze majaji kama ndio ulitoa amri nikamatwe.
Shahidi: Hapana.
Lissu: Je ni kweli au sio kweli aliyetoa maelekezo nikamatwe ni Ramadhani Kingai
Shahidi: Ulikuwa umekamatwa kupitia boss wangu Ramadhani Nganzi
Lissu: Ni kweli si kweli DCI Kingai aliwapa maelekezo kuwa mtawasiliana naye kupitia Ramadhani nganzi
Shahidi: Ndio ni kweli.
Lissu: Je ni sahihi kusema kwamba DCI kingai alitoa taarifa kwa nganzi awape taarifa kwamba Lissu amekamatwa analetwa Dar es salaam.
Shahidi: Ndio
Lissu: Nani kati yako na msaidizi wako George Padem nani alitoa amri lifunguliwe jalada la uhaini?
Shahidi: Wakati nateuliwa nilikuta tayari wameshafungua file
Lissu: Waeleze majaji kama umesoma maelezo ya Geogre Padem amekuzungumzia wewe kwa sentensi mbili tu
Shahidi: Ni kweli
Lissu: Ulikuta kazi yote imefanyika na hukufanya la maana ndio maana umetajwa kwa mistari miwili tu
Shahidi: Sina hakika.
Lissu: Nataka nizungumzie la kwangu na mgogiro wangu wa muda mrefu wa Jeshi, waeleze majaji kama unafahamu kwamba kwa karibu robo karne jeshi la Polisi limenionea sana kwa kunikamata na kunifungulia kesi za uongo
Shahidi: Sifahamu
Lissu: Waeleze majaji kama unafahamu 2002 nilikamatwa na kufungiwa central
Shahidi: Sifahamu
Lissu: Waeleze majaji kama unafahamu ilipofika mwaka 2008 wakaifuta 2011 nilikamatwa na jeshi la polisi nikachaniwa nguo na kufungwa machakani na kesho yake nikafunguliwa shauri la ilegal trace passing
Shahidi: Sifahamu.
Lissu: Waeleze majaji kama unafahamu mwaka 2012 nilikamatwa kwa kusimama na wananchi wa Arusha ambao ndugu zao waliuawa na kesi ilifutwa.
Shahidi: Sifahamu.
Lissu: Waeleze majaji mwaka 2013 pia nilikamatwa kusimama na wananchi wa Arusha na kesi ikafutwa.
Shahidi: Sifahamu
Lissu: 2016 nilisema iwapo uchaguzi utarudiwa Zanzibar uliofutwa na Jecha kungetokea maaafa na Kingai na Hamduni walikuja kutoa ushahidi nikawakaanga kama wewe na aliyetoa amri nikamatwe ni Camilius Wambura leo ni IGP.
Shahidi: Sifahamu
Lissu: Hujajua kwamba hiyo kesi ilikuja kufutwa nikiwa Ubelgiji nikiwa napigania uhai wangu 2021.
Shahidi: Sifahamu.
Lissu: Waeleze majaji 2017 kama unafahamu nilikamatwa jimboni kwangu na kushtakiwa kwa kosa la uchochezi Waziri wa Mambo ya Ndani alikuwa Mwigulu Nchemba akawaambia huyo mbunge mnamsafirisha usiku akigongwa na malori.
Shahidi: Sifahamu.
Lissu: Nilikamatwa nikiwa bungeni 2017 nje baada ya kumwita Magufuli dikteta uchwara na kushtakiwa kwa uchochezi.
Shahidi: Sifahamu.
Lissu: Waeleze majaji kama unafahamu kati ya Juni 2016 na Julai 20217 nilikamatwa mara nane na kufunguliwa kesi mara sita na zote zilifutwa mwaka 2021
Shahidi: Sifahamu.
Lissu: Waeleze majaji kwamba sijawahi kutiwa hatiani hata mara moja sina criminal record.
Shahidi: Sifahamu.
Lissu: Waeleze majaji kama unafahamu kama baada ya majaribio hayo ya kuninyamazisha nililetewa watu wasiojulikana nikapigwa risasi
Shahidi: Nafahamu
Lissu: Hata watu kuniombea polisi waliwapiga marufuku, hata watu kunitolea damu walikatazwa, wakenya ndio walinitolea damu
Shahidi: Sifahamu
Lissu: Kwa karibu robo karne naonewa kama ilivyo kwenye kesi hii.
Kesi imeahirishwa mpaka kesho.