Shahidi wa kificho wa 17 wa Jamhuri anatoa ushahidi wake
Jaji: Tuendelee
Wakili wa Serikali: Bwana P unanisikia? nitakuongoza kutoa ushahidi wako wa msingi, ninaomba ujibu kadiri ntakavyokuwa na kuongoza
Wakili anaendelea
Wakili: Bwana P unajishughulisha na nini?
Shahidi P: Mimi ni mwandishi wa habari Jambo Televisheni
Wakili wa Serikali: Una muda gani sasa?
Shaid P: Niko tangu 2023 tangu sasa
Wakili wa Serikali: Majukumu yako ni yapi?
Shahidi P: Majukumu yangu ni kuchukua matukio ya video na picha
Wakili wa Serikali: Ujuzi wako kwenye kazi unayofanya ni upi yani ngazi ya elimu yako
Shahidi P: Nina Diploma ya uandishi wa habari
Wakili wa Serikali: Ulipata wapi hiyo elimu na mwaka gani
Shahidi P: Nilipata katika chuo cha DSJ mwaka 2023
Wakili wa Serikali: Unaweza kuiambia Mahakama unapigaje picha za matukio na video
Shahidi P: Nafanya haya yote kwa kutumia kifaa cha kamera aina ya Sony AX
Wakili wa Serikali: Umetuambia kuna matukio ya picha na video kamara Sony A x unaitumia kwenye matukio ya aina gani
Shahid P: Ax naitumia kwenye video
Wakili wa Serikali: Na matukio ya picha unatumia nini
Shahidi P: Natumia kifaa kinachoitwa Cannon kwa ajili ya picha
Wakili wa Serikali: Baada ya kutujuza kazi unazofanya nikurejeshe tarehe tatu April 2025, ulikuwa na jukumu gani
Shahidi P: Siku hiyo nilipangiwa kazi na Bosi wangu kwenda kufanya kazi kwenye tukio la CHADEMA ofisi za makao makuu nikiwa na mwenzangu shahidi P1
Wakili wa Serikali: Boss wenu ni nani?
Shahidi P: John Marwa
Lissu: "Hii sio kesi ya wizi wa mbuzi ni kesi ya uhaini"
Kesi imeanza;
Wakili wa serikali: Tunaomba radhi kwa kuchelewa kwa sababu zisizozuilika shahidi alipata changamoto za usafiri ila kwa uweza wa Mungu tayari amefika na tuko tayari kuendelea waheshimiwa
Jaji: Mshitakiwa uko tayari?
Lissu: Majaji naomba msirihusu huu mchezo wa kuchelewa, shahidi anapaswa afike kwa wakati kama Mahakama ilivyoelekeza hii sio kesi ya wizi wa mbuzi ni kesi ya uhaini. Hii kesi inamshitakiwa mmoja leo tuna mwaka na miezi minne kwa utaratibu huo hautafika tukisema tunaanza saa tatu tunaanza saa tatu msikubali waheshimiwa majaji
Wakili wa serikali: Waheshimiwa tunashahidi wetu mmoja ambaye ni shahidi wa kulindwa
Shahidi ameshaingia ingia kwenye kisanduku cha siri jaji anamuuliza maswali ya utambulisho ikiwemo umri dini
Shahidi P: Nina miaka 26, Dini Muislam
Shahidi anakula kiapo cha uaminifu kulingana na imani yake akiwa ameshika kitabu cha dini (msahafu)
Picha kutoka Mahakamani kesi ikianza punde
Maelezo ya picha, Lissu ameshaingia na kesi inaanza
Maelezo ya picha, Mwanasheria wa CHADEMA, Dkt. Rugemeleza Nshala (katikati) akiwa na Kaka wa Lissu, Wakili Alute Mughwai na mwanasheria Peter Madeleka (kushoto)
Maelezo ya picha, Mawakili, akiwemo Nassoro Katuga wa Serikali wakisaliamiana
Maelezo ya picha, Katibu wa CHADEMA kulia, John Mnyika
Shahidi wa 17 anatarajiwa kuanza kutoa ushahidi katika kesi ya Lissu
Shahidi wa 17 wa upande wa mashtaka anatarajiwa kuanza kutoa ushahidi wake katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, katika Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam.
Makarani wa Mahakama wameanza maandalizi na kuweka vipakatalishi vya majaji pamoja na vifaa vingine kwa ajili ya mwenendo wa kesi. Bado Mawakili wa Serikali hawajaingia.
Baada ya shahidi huyo wa 17 kusikilizwa, upande wa mashtaka utakuwa umesalia na mashahidi 14 wa kutoa ushahidi katika kesi hiyo.
Kesi hiyo inaendelea mbele ya jopo la majaji watatu katika Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam.
Mahakama yawataka mawakili kutozungumza na vyombo vya habari ndani ya viunga vya Mahakama
Mahakama Kuu ya Tanzania imewakumbusha mawakili kutofanya mahojiano na vyombo vya habari katika viunga vya Mahakama kuhusu mashauri yanayoendelea.
Taarifa iliyotolewa na Mahakama Kuu na kusainiwa na Msajili wa Mahakama Kuu, C.M. Tengwa, Agosti 12, 2026, imesema mawakili wanapaswa kuzingatia sheria, kanuni na maelekezo ya Mahakama katika mwenendo wao ndani na nje ya Mahakama.
Mahakama imesema hatua hiyo inafuatia taarifa kwamba Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kiliwataka wanachama wake kuzungumza na vyombo vya habari katika eneo la Mahakama baada ya mashauri kuahirishwa.
Hata hivyo, Mahakama Kuu imewakumbusha mawakili kutofanya mahojiano na vyombo vya habari katika viunga vya Mahakama wala kueleza mwenendo wa mashauri yanayoendelea kwa namna inayoweza kuathiri mwenendo wa mashauri hayo.
Mahakama imesema mwenendo wa mawakili, ndani na nje ya Mahakama, kuhusu mashauri yanayoendelea unapaswa kuzingatia Katiba, sheria, kanuni, taratibu na maelekezo ya Mahakama ya Tanzania.
Taarifa hiyo imetolewa wakati kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, ikiendelea katika Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam. Kesi hiyo ilianza tena kusikilizwa Agosti 10 na imepangwa kuendelea hadi Septemba 7, 2026.
Hata hivyo, taarifa ya Mahakama Kuu haijamtaja Lissu, kesi yake wala wakili yeyote kwa jina.
Mambo 7 muhimu kuhusu kesi ya uhaini ya Lissu
Chanzo cha picha, X
Tundu Lissu, Mwenyekiti wa CHADEMA, anakabiliwa na kesi ya uhaini Tanzania. Usikilizwaji wa kesi hiyo unaendelea Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, huku upande wa Jamhuri ukiendelea kuwasilisha mashahidi wake. Kufikia jana, mashahidi 16 walikuwa wamefika kutoa ushahidi katika kesi hiyo.
1. Kesi ya Lissu inahusu nini?
Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, anakabiliwa na shtaka la uhaini nchini Tanzania.
Kesi hiyo inasikilizwa katika Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, na imekuwa ikiendelea kwa awamu huku upande wa Jamhuri ukiwasilisha ushahidi wake.
2. Lissu alikamatwa lini?
Lissu alikamatwa 8 Aprili 2025, na siku moja baadaye akafikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, ambako alisomewa shtaka la uhaini kama Mahakama ya ukabidhi.
Hapo ndipo mchakato wa kesi ulipoanzia kabla shauri hilo kuendelea kusikilizwa katika Mahakama Kuu.
3. Kesi ilifikaje Mahakama Kuu?
Baada ya hatua za awali katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kesi ya uhaini iliendelea katika Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Dar es Salaam.
Huko, upande wa Jamhuri ulianza kuwasilisha ushahidi na mashahidi wake katika kuunga mkono mashtaka dhidi ya Lissu. Na Mpaka sasa Mashahidi 16 wametoa ushahidi wao mpaka Agosti 12, 2026.
4. Kwa nini kesi ilisimama kwa miezi mitano?
Hili ni moja ya mambo muhimu katika historia ya kesi hiyo.
Februari 2026, Jamhuri iliwasilisha notisi ya kutaka kuongeza ushahidi mpya katika kesi hiyo.
Lissu alipinga hatua hiyo, na Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Dar es Salaam ikatupilia mbali notisi ya Jamhuri ya kuwasilisha ushahidi huo mpya.
Jamhuri haikukubaliana na uamuzi huo. Ilipeleka suala hilo Mahakama ya Rufani, ikiomba mapitio ya uamuzi wa Mahakama Kuu.
Kutokana na shauri hilo, Mahakama Kuu ilisimamisha usikilizwaji wa kesi ya uhaini hadi Mahakama ya Rufani itakapotoa uamuzi.
Hivyo, kesi hiyo ilisimama kwa takribani miezi mitano kuanzia Februari 2026.
5. Nini kilitokea Mahakama ya Rufani?
Baada ya suala hilo kufikishwa Mahakama ya Rufani, mahakama hiyo ilitoa uamuzi kuhusu hoja iliyokuwa imewasilishwa na Jamhuri.
Lissu alishinda katika suala hilo, na hivyo kuondoa kikwazo cha kisheria kilichokuwa kimesababisha usikilizwaji wa kesi kusimama.
Baada ya uamuzi huo, kesi ilirejea Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Dar es Salaam kwa ajili ya kuendelea na usikilizwaji wake.
6. Kesi ilianza tena lini?
Baada ya kusimama kwa takribani miezi mitano, usikilizwaji wa kesi ulianza tena Agosti 10, 2026.
Tangu kurejea kwake Mahakama Kuu, upande wa Jamhuri umeendelea na uwasilishaji wa ushahidi.
Kufikia Agosti 12, shahidi wa 16 wa upande wa Jamhuri, ACP Amin Mahamba, alikuwa amemaliza kutoa ushahidi wake na kuhojiwa na Lissu. Akitumia siku 3 Mahakamani
7. Nini kimejitokeza katika ushahidi wa mashahidi?
Katika hatua ya sasa ya kesi, Lissu amekuwa akiwahoji mashahidi wa Jamhuri kuhusu ushahidi waliowasilisha na taarifa walizowahi kutoa katika hatua za uchunguzi.
Katika ushahidi wa Agosti 12, kwa mfano, Lissu alimuuliza shahidi kuhusu tofauti kati ya maelezo aliyowahi kutoa wa maandishi na majibu ya mdomo aliyoyatoa mahakamani. Shahidi alisema hakuwa ameeleza sababu ya tofauti hiyo kwa maandishi, lakini akiongozwa na wakili wa Serikali alisema , alikuwa akijibu maswali kwa namna alivyoulizwa na mshitakiwa.
Lissu pia aliuliza kuhusu video zilizotumika katika uchunguzi. Shahidi alisema polisi walitazama video iliyokuwa mtandaoni, lakini hawakuangalia video iliyokuwa kwenye memory card na flash disk zilizotajwa mahakamani.
Jana, Agosti 12, shahidi wa 16 wa Jamhuri alimaliza kutoa ushahidi. Baada ya hapo, upande wa Jamhuri uliomba kesi iahirishwe kwa kuwa haukuwa umejiandaa na shahidi mwingine, na Jaji Dunstan Ndunguru akaahirisha kesi hadi leo, Agosti 13.
Kwa hiyo, leo macho yanaelekezwa Mahakamani kujua hatua inayofuata katika ushahidi wa upande wa Jamhuri.
Kesi ya uhaini ya Lissu kuendelea leo: Nini kinatarajiwa Mahakamani?
Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, inatarajiwa kuendelea leo katika Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, baada ya kesi hiyo kuahirishwa jana. Upande wa Jamhuri ulisema haukuwa umejiandaa na shahidi mwingine.
Kesi hiyo iliahirishwa jana baada ya shahidi wa 16 wa upande wa Jamhuri, ACP Amin Mahamba, kumaliza kutoa ushahidi wake. Upande wa Jamhuri uliomba muda zaidi kwa sababu haukuwa umejiandaa na shahidi mwingine.
Jaji Dunstan Ndunguru aliahirisha kesi hiyo hadi leo saa tatu asubuhi.
Kwa hiyo, kinachofuatwa leo ni hatua itakayochukuliwa na upande wa Jamhuri baada ya shahidi huyo kumaliza ushahidi wake.
Jana, Lissu aliomba mahakama izingatie agizo la kuwa upande wa Jamhuri uje na mashahidi wawili, akisema kuchelewa kwa kesi hiyo si kwa sababu yake na kwamba yeye anaendelea kukaa gerezani bila hatia.
BBC itaendelea kufuatilia kinachoendelea Mahakamani leo na kukuletea kila hatua kwenye ukurasa huu.
Kesi ya Lissu: Mambo muhimu yaliyojiri Mahakamani jana
Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, iliendelea jana katika Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, huku shahidi wa 16 wa upande wa Jamhuri, ACP Amin Mahamba, akimaliza kutoa ushahidi wake. Lissu alimuuliza shahidi maswali kuhusu ushahidi wake, matukio ya Oktoba 2025 na madai yanayohusishwa na uchaguzi na Katiba.
Miongoni mwa maswali yaliyoulizwa na Lissu ni kuhusu tofauti zilizopo kati ya maelezo ambayo shahidi aliwahi kutoa polisi na yale aliyoyasema mahakamani. Shahidi alikiri kuwa hakuwa ameeleza sababu za tofauti hizo.
Lissu pia alimuuliza shahidi kuhusu madai ya maandalizi ya vurugu wakati wa uchaguzi wa Oktoba 2025 na hatua zilizochukuliwa dhidi ya watu waliodaiwa kuhusika.
Katika sehemu nyingine ya dodoso, Lissu aliuliza kuhusu ushahidi wa video uliotumika katika uchunguzi. Shahidi alisema polisi walitazama video iliyokuwa mtandaoni, lakini hawakuangalia video iliyokuwa kwenye memory card na flash disk iliyotajwa Mahakamani.
Lissu pia alimuuliza shahidi kama ushahidi wake ulikuwa unathibitisha kwamba yeye ni mhaini. Shahidi alijibu: “Sijasema hivyo.”
Baada ya shahidi huyo kumaliza kutoa ushahidi, upande wa Jamhuri uliomba kesi iahirishwe kwa sababu haukuwa umejiandaa na shahidi mwingine.
Jaji Dunstan Ndunguru akaahirisha kesi hadi leo saa tatu asubuhi.
KARIBU KATIKA MUENDELEZO WA KESI YA LISSU LEO ALHAMIS 13.08.2026
Kesi yahahirishwa mpaka kesho Alhamisi Agosti 12, 2026
Upande wa Jamuhuri wameomba ahirisho la kesi kwa sababu hawakujiandaa na shahidi mwingine
Lissu: Ninaomba ile amri ya Mahakama ya kuwa wanapaswa kuja na mashahidi wawili, tumechelewa sana na sio kwa sababu zangu ni kwa sababu zao, mimi naendelea kukaa gerezani na sina hatia. Kuanzia kesho waje na mashahidi wa kutosha
Jaji: Shauri lina ahirishwa mpaka kesho saa tatu asubuhi...
Shahidi wa 16 wa Jamhuri amaliza kutoa ushahidi wake
Upande wa Serikali, Katuga, unamuuliza Shahidi, Mahamba
Katuga: Naomba ufafanuzi waambie majaji yale maneno yaliyoko kwenye hati ya mashitaka tutakinukisha, kuna neno serikali wafafanunulie majaji ulimaanisha nini
Shahidi: Nilipotamka neno serikali lipo nilimaanisha serikali ndio nyenye mamlaka ya kutekeleza na kusimamia sheria za nchi kwa hiyo kutamka maneno kama hayo kwamba utauzia uchaguzi au utavuruga uchaguzi ni kuitishia serikali kwani ndio ina wajibu wa kulinda amani ya nchi
Katuga: Tuendelee kujikita hapo hapo uliulizwa ni nani aliyechapisha mtandaoni ukamkomalia ukamwambia ni wewe na akaenda mbele akuuliza je akina P na P1 walifanya nini ukasema wao walisambaza na yeye ndio alichapisha ifafanulie Mahakama ulimaanisha nini?
Shahidi: Nilimaanisha kwamba mshitakiwa alikuwa akiongea mbele ya waandishi wa habari ambao walikuwa wakirusha yale matangazo tunaamuni kwamba hiyo ilikuwa ni nia yake na kama alikuwa hataki asingewaruhusu
Katuga: Ndio maana ukakomaa ni wewe ni wewe?
Shahdi: Ndio
Katuga: Uliulizwa haya maneno kunzia uchaguzi, kukinukisha je yamo kwenye kifungu cha 39/2 B
Shahdi: Yale maneno aliyotamka mshitakiwa tafsiri yangu ni kwamba kulikuwa na hiyo nia ya kuitishia serikali
Katuga: Umeulizwa sana hapa mambo ya Katiba na ukaulizwa kudai Katiba ifafanulie mahakama haya madai na kosa hili la uhaini au nini majibu yako kwenye hili la katiba na uhaini
Shahidi: Havihusiani
Katuga: Kuna maswali mengi uliulizwa juu ya mambo ya Oktoba 2025 mkaambiwa wewe na polisi mlifanya vurugu ulimaanisha nini
Shahidi: Sio kweli kwamba Polisi ilihusika kwenye vurugu ni wazi kwamba baada uchunguzi tuliofanya ulibaini kwamba kulikuwa na maandalizi ya awali
Lissu anaingilia:...Mimi sikuuliza hilo swali na kwakuwa shahidi anajibu kitu kipya nitaomba ni rudie kufanya dodoso
Katuga: Umeulizwa na mshitakiwa ushahidi uliosoma Mahakamani na ule uliandika polisi leo ukaulizwa je unataka ushahidi wako Mahakamani usiaminiwe ukasema ndio na uliandika Polisi ukasema ndio ukasema huajelezea sababu ya utofauti wa ushahidi wako wa kuandika na kuongea fafanua ulimaanisha nini uliposema sijaeleza
Shahidi: Kweli sijaeleza sababu ya hiyo tofauti ila majibu ya hapa mahakamani yalitokana na maswali niliyokuwa ninaulizwa na mawakili hapa mahakamani
Katuga: Waheshimiwa majaji ni hayo tu kwa shahidi huyu .
Jaji Nduguru: Shahidi umemaliza kutoa ushahidi wako unaweza kwenda...
Lissu amuuliza shahidi: “Ni ushahidi wako kwamba mimi ni mhaini?”Ajibu: “Sijasema hivyo”
Lissu hiyo taarifa ipo Mahakamani najua kuna taarifa ilikataliwa sababu haikuandaliwa na mtaalamu ilikataliwa
Shahidi: Tuendelee
Lissu Mpaka sasa wewe ni shahidi wa 16 nyie wote hakuna aliyewasilisha ushahidi wa video na hakuna kidhibiti hata kimoja zaidi ya stori
Shahidi: Ni sahihi
Lissu: Twende kwenye mkutano wangu uliyosababisha yote haya juu ya msimamo wangu na chama changu juu ya uchaguzi na katiba
Shahidi: Sina hakika kama ulizungumzia katiba
Lissu: Waeleze majaji kama unafahamu madai ya mfumo wa uchaguzi na katiba ni madai ya siku nyingi
Shahidi: Sifahamu
Lissu: Waeleze majaji kama una fahamu mwaka 1992, Tume ya Nyalali ilipendekeza itungwe katiba mpya itakapofikia Septemba 1993
Shahidi: Sijawahi kusikia
Lissu: Waeleze majaji kama unafahamu mapendekezo hayo ya Jaji Nyalali yalikataliwa na CCM chini ya serikali ya Rais Mwinyi
Shahidi: Sifahamu
Lissu: Rais Mkapa marehemu aliunda tume ya Jaji Robert Kisanga mwaka 1998, walipendekeza kuwe na Katiba mpya na Rais Mkapa akasema hakuwatuma waangalie hayo ya katiba
Shahidi: Sifahamu
Lissu: Rais Mkapa akaunda Tume nyingine ya Jaji Mark Bomani nayo ikapendekeza katiba mpya na Mkapa na CCM yake wakakataaa
Shahidi: Sifahamu
Lissu: Rais Kikwete akaunda tume ya Jaji Warioba na wakaanda rasimu ya Katiba mpya na mapendekezo ya mabadiliko kwenye mfumo wetu wa uchaguzi, Rais Kikwete naye akataaaa waeleze majaji
Shahidi: Sijawahi kusikia
Lissu: Waleze majaji kuwa tunafanya uchaguzi kila baada ya miaka mitano
Shahdi: Ni sahihi
Lissu: Tangu 1995 watazamaji wa uchaguzi huo kutoka nje kimataifa na kikanda kila kwenye uchaguzi mkuu wamependeza kwa serikali itungwe katiba mpya na mabadiliko kwenye mfumo wetu wa uchaguzi
Shahidi: Sifahamu
Lissu: Waeleze majaji mwaka 2015 ilani ya CCM ilikua na ahadi kuwa watakamilisha mchakato wa katiba mpya
Shahidi: Sifahamu
Lissu: Waeleze majaji hata mwaka 2020, CCM ya Magufuli iliahidi mchakato wa katiba mpya utakamilika
Shahidi: Sifahamu
Lissu: Hata alipokuja Samia naye alikataaa
Shahidi: Sifahamu
Lissu: Kila uchaguzi mkuu lazima kuwe na mauaji ya raia
Shahidi: Sifahamu
Lissu: Baada ya hotuba yangu ya tarehe tatu wewe na Jeshi mlichukua hatua ya kunitafuta na kuniuliza nilimaanisha nini
Shahidi: Sifahamu
Lissu: Kwa yote haya katika historia yetu ya miaka 35, No Reforms No Election ilikuwa sahihi kwenye mazingira haya
Shahidi: Hapana
Lissu: Jaji Chande anasema hivi ghasia za baada ya uchaguzi mkuu zilitokana na matatizo ambayo yamekueko kwa muda mrefu ikiwemo madai ya katiba mpya, mfumo wa uchaguzi. Maelfu ya watu wameuawa sababu ya kutotatuliwa kwa muda mrefu, je nakosea
Shahidi: Unakosea
Lissu: Kwa hiyo hata Jaji Chande na tume yake wamekosea?
Shahidi: Sifahamu
Lissu: Hayo unayosema ni makosa yangu waeleze majaji kama unafahamu kikosi kazi cha kamati ya haki za binadamu umoja wa mataifa kimetoa taarifa baada ya uchunguzi wa miezi tisa imesema kukamatwa kwangu ni kinyume cha sheria na nilipwe fidia
Shahidi: Sifahamu
Lissu: Waeleze majaji kama unafahamu tarehe 10 Juai, Kamati ya Mawaziri wanaowakilisha Jumuiya ya Madola imetoa taarifa inayoitaka serikali ya Tanzania kuniachilia huru ndani ya mwezi mmoja na wasipofanya hivyo kwenye kikao cha Septemba, watachuku hatua stahiki dhidi ya serikali ya Tanzania
Shahidi: Sifahamu
Lissu: Swali langu la mwisho bwana askari kama Umoja wa Mataifa, Jumuiya ya Madola wote wanasema niachiliwe na ni ushahidi wako kwamba mtu huyu anayepiganiwa na Taasisi zote hizi ni mtu mbaya mhaini na anayestahili kunyongwa
Shahidi: Sijasema hivyo
Lissu amemaliza kumuhoji shahidi wa 16, Mahamba
Lissu ahoji mahakamani kuhusu mauaji ya Oktoba 29
Lissu aendelea kumuhoji shahidi wa 16 wa upande wa Mashtaka, ACP Amin Mahamba.
Lissu: Waeleze Majaji kama ulidhamiria maelezo yako ya kizimbani ya juzi yaaminiwe na mahakama kama ushahidi wa kweli
Shahidi: Nilidhamiria yatumike
Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji kama maelezo yako uliyoandika polisi ulidhamiria yatumike mahakamani kama ushahidi wa kweli
Shahidi: Nilidhamiria yatumike
Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji kama kuna mahali popote umeelezea sababu ya hizo tofauti kati ya ulichoandika na ulichosema mahakamani
Shahidi: Hakuna mahali nilipoelezea
Lissu: Ushahdii wako kuhusiana na wale mashahidi waliofichwa mliowatoa mikoani unakumbuka ulisema kwamba hao mashahidi waliofichwa ni watu ambao walikamatwa na Polisi kweli si kweli
Shahidi: Kweli
Lissu: Na walikamatwa kwa kupanga njama za kufanya vurugu kwenye uchaguzi Mkuu
Shahidi: Walihamasisha
Lissu: Na walipokamatwa walikiri
Shahidi: Ndio
Lissu: Na waliandika maelezo yanayosema hivyo
Shahidi: Sahihi
Lissu: Hiyo mipango waliyokuwa wanaipanga ilikuwa makosa ya jinai
Shahidi: Kweli
Lissu: Wakakiri kwa maandishi, mkawaleta mahakamani wakakiri mahakamani au sio?
Shahidi: Ndio
Lissu: Waeleze Majaji hizo tuhuma za kijinai mlizowakamata nazo ziliishia wapi?
Shahidi: Nikirejea maelezo yangu baada ya kuwakamata baada ya kupata taarifa kutoka kwa RCO tuliitisha jalada tukalisoma tukalipitia tulibaini wote walikua wamechochewa na wewe
Lissu: Ni kweli au si kweli mliwafutia kesi wote
Shahidi:.....
Lissu: Katika hao mashahidi walikuwepo waliotokea Dar es Salaam. Waeleze Majaji kama ni kweli au si kweli Dar es Salaam kulitokea vurugu zilizoua watu 182
Shahidi: Mimi sio Msemaji wa Jeshi la Polisi
Lissu: Kwa mujibu wa Tume ya Jaji Chande watu 182 waliiawa Dar es Salaam kweli si kweli
Shahidi: Si kweli
Lissu: Mliwashtaki kwa makosa mliyowakamata
Shahidi: ....
Lissu: Siku ya uchaguzi tarehe 29 kwa mujibu wa Jaji Chande waliuawa watu 23 na watu ambao mlikuwa mnajua wameandika walikuja mahakamani wakasema tutaleta fujo mmewaachia
Shahidi:Si kweli
Lissu: Umesema ulikuwa mpelelezi wa matukio ya Okt 29 Shahidi: Ndio
Lissu: Kuna watu mliwakanata Mbeya mkawaandika maelezo mkawaleta mahakamani halafu mkawaachia
Shahidi: Kweli
Lissu: Kwenye Mji wa Mbeya kwa mujibu wa ripoti ya Jaji Chande waliuawa watu 80
Shahidi:...
Lissu: Waeleze waheshimiwa majaji kama hiyo mikoa mitatu Dar es Salaam Arusha Mbeya, jumla ya watu walioawa ni watu 315 kama kuna RPC, ZPC, RCO, OCD, OCCID au Mkuu wa Mkoa au Mkuu wa Wilaya aliyechukiliwa hatua kwa uzembe
Shahidi: Sina uhakika
Lissu: Waeleze majaji kama wale waliosema wataenda kufanya vurugu na wakafanya kama kuna hata mmoja aliyechukuliwa hatua mpaka sasa
Shahidi: Ni matukio mawili tofauti
Lissu: Kuma mikoa mingine nane Mkoa wa Mwanza hawakukuletea taarifa kwamba kuna shida inapangwa kwenye uchaguzi
Shahidi: Sikupata
Lissu: Mwanza Okt 29 kwa mujibu ws Ripoti ya Jaji Chande waliuawa watu 90 waeleze majaji Mwanza mna RPC
Shahidi: Ndio
Lissu: Kuna RCO, Mtu wa usalama wa taifa au mapolisi wote kama kuna aliyechukuliwa hatua kwa kutoona janga kubwa lililoukuta mkoa wa Mwanza
Shahidi: Sina uhakika
Lissu: Kwa Mikoa minne wameuawa watu 405 kwa mujibu wa Ripoti ya chande Songwe, Geita Mara, Shinyanga, Geita, Ruvuma katika mikoa hiyo ni Ruvuma pekee mlipewa taarifa kwamba watu wanapanga kufanya vurugu mkawakamata wakaandika maelezo ya mashtaka mkawaleta mahakamani mkawaachi ni kwel isi kweli?
Shahidi: Si kweli
Lissu: Kwa hiyo wa Songea mliwaleta mahakamani mkawashtaki
Shahidi: Waliachiwa kwa mujibu wa sheria
Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji kama wote hawa vyombo vya ulinzi na usalama wamechukuliwa hatua yoyote
Shahidi: Sina uhakika
Lissu: Niambie kama nipo sahihi au nakosea kwamba katika hsitoria yetu yote kama nchi ilianza wakati wa Wajerumani mara ya mwisho katika nchi hii watu waliuawa kwa kiasi kikubwa hivyo ilikuwa 1907 wakati Wajerumani wanazima vita vya maji maji kuanzia hapo Wajerumani hawakuua watu kama ilivyokuwa mwaka jana Waingereza walikaa kwa miaka 40 hawakuua, Nyerere miaka 21, miaka 10 ya Mwinyi hayakuwepo, miaka 10 ya Mkapa hayakuwepo, miaka 10 ya Kikwete hayakuwepo, miaka sita ya Magufuli yalikuwepo kidogo sana lakini ndani ya wiki moja ya utawala wa Samia wameuawa watu 500 kuliko miaka yote
Shahidi: Sio sahihi
Lissu: Je, video mliyoangalia ikiwa mtandaoni au iliyokuwa kwenye Memory card iliyopokelewa Dodoma au kwenye flash Disc iliyoandikwa Aldepo
Shahidi: Iliyokuwa mtandaoni
Lissu: Kwa hiyo kwa jibu hilo ntakua sahihi hamkuangalia video ikiyokuwa kwenye Memory card na iliyokuwa kwenye Flash Disc
Shahidi: Hatukuangalia
Lissu: Nitakuwa sahihi au nitakosea nikisema kwamba pengine kwenye hiyo flash disc Aldeepo hakuna video yoyote
Shahidi: Sio sahihi
Lissu: Unajuaje wakati hukuangalia
Shahidi: Si kuna taarifa
Lissu: Unafahamu kama hata mahakamani hazikuletwa?
Kesi ya uhaini ya Tundu Lissu inaendelea, Mahakama inasikiliza ushahidi
Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, inaendela sasa katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Dar es Salaam.
Lissu ameendelea na maswali ya dodoso ya shahidi wa Jamhuri, ACP Amin Mahamba.
Katika maswali ya leo, Lissu amemuuliza Mahamba kuhusu watu waliokamatwa kabla ya uchaguzi kwa tuhuma za kupanga vurugu na baadaye kuachiwa baada ya majalada yao kupitia upya.
Mahamba amethibitisha kuwa baadhi ya watu hao walikamatwa wakiwa wanatuhumiwa kupanga njama na vurugu, na kwamba baadaye mashtaka yao yalifutwa.
Lissu pia amemuuliza kuhusu matukio ya vifo Dar es Salaam, Arusha na Mbeya, akirejea takwimu za Tume ya Jaji Chande zinazodai watu 315 waliuawa katika maeneo hayo.
Alipoulizwa kama kuna makamanda wa polisi au viongozi wa serikali waliochukuliwa hatua kutokana na vifo hivyo, ACP Mahamba amesema hana hakika kama kuna aliyechukuliwa hatua.
Lissu amesema hana maswali mengi leo na anataka kumaliza “loose ends” katika ushahidi wa shahidi huyo.
Yaliyojiri jana Lissu akiendelea kumuhoji shahidi wa 16 katika kesi ya uhaini
Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, anaendelea kumuhoji Kamishna Msaidizi wa Polisi Amini Mahamba, shahidi wa 16 wa upande wa mashtaka katika kesi ya uhaini inayomkabili katika Mahakama Kuu, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam.
Lissu alianza kumuhoji shahidi huyo jana, baada ya Mahamba kumaliza kutoa ushahidi wake wa msingi. Katika hatua ya maswali ya dodoso, Lissu ameuliza karibu maswali 300 akichunguza upelelezi wa kesi hiyo na tofauti kati ya ushahidi wa shahidi mahakamani na maelezo yake ya awali.
Kesi ya Lissu ilifikia wapi?
Julai 30, 2026, Mahakama ya Rufani ilitupilia mbali ombi la Jamhuri la kutaka kuwasilisha ushahidi wa nyongeza katika kesi hiyo.
Mahakama hiyo ilikubaliana na hoja za Lissu kwamba kifungu cha sheria kilichotumiwa na upande wa mashtaka hakikuruhusu ushahidi huo kuwasilishwa katika hatua hiyo ya kesi.
Kesi hiyo imeanza tena baada ya kusimama tangu Februari 24, 2026, na imepangwa kusikilizwa kwa mfululizo hadi Septemba 7, 2026.
Lissu anakabiliwa na shtaka la uhaini chini ya Kifungu cha 39(2)(d) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu. Upande wa mashtaka unahusisha shtaka hilo na kauli alizotoa kuhusu kusudio la kuzuia kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.
Kilichojiri mahakamani jana
Katika maswali yake, Lissu amekuwa akimuuliza shahidi kuhusu namna upelelezi wa kesi hiyo ulivyofanywa, akilenga pia tofauti kati ya maelezo yake ya awali na ushahidi alioutoa mahakamani.
Katika sehemu kadhaa, shahidi amekiri kwamba mambo aliyoyataja jana katika ushahidi wake hayakuwepo kwenye maelezo yake yaliyoandikwa. Hayo ni pamoja na baadhi ya maelezo kuhusu uchunguzi wa video ya hotuba ya Lissu, hatua za upelelezi na mawasiliano na baadhi ya taasisi.
Lissu pia amemuuliza shahidi kuhusu video ya hotuba yake iliyochapishwa na Jambo TV. Alitaka kujua kama polisi walikuwa na ushahidi kwamba yeye ndiye aliyechapisha video hiyo. Shahidi amesema Lissu ndiye aliyechapisha, lakini alipoulizwa kama anajua iwapo Lissu alikuwa mfanyakazi au mpiga picha wa Jambo TV, au alikuwa na nywila za akaunti hiyo, amesema “sina hakika.”
Lissu amemuuliza pia shahidi kuhusu madai ya vitisho dhidi ya mashahidi wa upande wa mashtaka. Amehoji iwapo majina ya watu waliodaiwa kutishiwa, aina ya vitisho, tarehe na maeneo yalitajwa katika hati ya kiapo ya shahidi.
Katika sehemu nyingine ya maswali, Lissu amemuuliza shahidi kuhusu watu waliokamatwa au kushtakiwa kwa makosa yanayohusishwa na matukio ya baada ya uchaguzi. Shahidi amesema “sikumbuki” alipoulizwa kuhusu baadhi ya kesi hizo.
Lissu pia amezungumzia historia yake ya kukamatwa na kufunguliwa kesi mbalimbali na polisi, akisema: “Kwa karibu robo karne naonewa.” Shahidi amesema hafahamu kuhusu matukio kadhaa aliyoyataja, huku akikiri kufahamu tukio la mwaka 2017 ambapo Lissu alipigwa risasi.
Aidha, Lissu amemuuliza shahidi kama katika upelelezi wake alizingatia haki za kikatiba za kutoa maoni na kukutana, pamoja na iwapo alishirikisha taasisi nyingine za usalama katika upelelezi huo.
Kesi inaendelea leo, Agosti 12, 2026, Lissu akitarajiwa kuendelea kumuhoji shahidi huyo wa 16 wa upande wa mashtaka.
Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, anaendelea leo kumuhoji Kamishna Msaidizi wa Polisi Amini Mahamba, shahidi wa 16 wa upande wa mashtaka katika kesi ya uhaini inayomkabili.
Lissu amekuwa akimuhoji shahidi huyo tangu Jumatatu, Agosti 10, huku jana akiendelea na maswali ya dodoso (cross-examination) kwa mfululizo wa maswali kuhusu upelelezi wa kesi hiyo, ushahidi wake mahakamani na tofauti kati ya ushahidi huo na maelezo yake ya awali.
Kwa siku mbili za mahojiano, Lissu amemuuliza shahidi huyo karibu maswali 300, huku sehemu kubwa ya maswali ikijikita katika upelelezi wa polisi na ushahidi unaohusishwa na video ya hotuba yake iliyochapishwa na Jambo TV.
Kesi hiyo inaendelea leo katika Mahakama Kuu, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam. BBC inaendelea kufuatilia kinachojiri mahakamani.
KARIBU TENA SIKU YA 3 YA USIKILIZWAJI WA KESI YA UHAINI YA LISSU BAADA YA KUANZA TENA
Yaliyojiri leo katika kesi ya uhaini ya Lissu, ikihairishwa hadi kesho, Kwa ufupi kilichojiri leo
Chanzo cha picha, Getty Images
Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, ameendelea leo kumuhoji Kamishna Msaidizi wa Polisi Amini Mahamba, shahidi wa 16 wa upande wa mashtaka katika kesi ya uhaini inayomkabili katika Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam.
Katika maswali ya dodoso (cross-examination), Lissu amekuwa akimhoji shahidi kuhusu upelelezi wa kesi hiyo, akilenga hasa tofauti kati ya ushahidi alioutoa mahakamani na maelezo yake ya awali. Shahidi amekuwa akijibu mara kwa mara kuwa baadhi ya mambo aliyoyataja kwenye ushahidi wake wa jana Mahakamani hayapo katika maelezo yake yaliyoandikwa.
Lissu pia amemuuliza shahidi kuhusu namna video ya hotuba yake iliyochapishwa na Jambo TV ilivyopatikana na kuchunguzwa, ulinzi wa mashahidi, mawasiliano na Ofisi ya DPP pamoja na maafisa wengine wa usalama. Amehoji pia madai ya polisi kuhusu vitisho kwa mashahidi na kama ushahidi huo uliainishwa katika maelezo ya shahidi.
Katika sehemu nyingine ya maswali, Lissu ameuliza kuhusu historia yake ya kukamatwa na kufunguliwa kesi mbalimbali na polisi, akisema amekuwa akionea na jeshi hilo kwa karibu robo karne. Shahidi amesema “sifahamu” alipoulizwa kuhusu matukio mengi ya nyuma, huku akikiri kufahamu kuwa Lissu alipigwa risasi mwaka 2017.
Lissu pia amehoji kama polisi walikuwa na ushahidi kwamba yeye ndiye aliyechapisha video hiyo kwenye YouTube ya Jambo TV. Shahidi amesema “ndio”, lakini alipoulizwa kama anafahamu kama Lissu alikuwa mfanyakazi, mpiga picha au alikuwa na nywila za Jambo TV, amejibu mara kadhaa “sina hakika.”
Kesi imeahirishwa hadi kesho, Agosti 12, 2026, ambapo Lissu anatarajiwa kuendelea na maswali ya dodoso ya shahidi huyo.
Lissu anaendelea, nikweli au si kweli ulichaguliwa kuwa mpelelezi wa matukio ya baada ya uchaguzi
kama mpelelezi mkuu wa matukio hayo
Shahidi: Sikua mpelelezi wa matukio hayo nilikua kwenye team lakini sikua mpelelezi wa matukio hayo.
Lissu: Kutokana na upelelezi wa timu yako kuna watu walishitakiwa kwa uhaini kama mimi?
Shahidi: Sikumbuki.
Lissu: Kesi ya Paulina Palyango na wenzake 75 ya kula njama.
Shahidi: Sikumbuki
Lissu: Pia Niffer na wenzake shtaka la kwanza kula njama la pili uhaini
Shahidi: Sikumbuki
Lissu: Omar Pandu Salum na wenzake 33 na hili unalikumbuka?
Shahidi: Sikumbuki.
Lissu: Waeleze majaji hukumbuki kuna watu wengi sana walikamatwa na kushtakiwa kwa uhaini jumla ya watu 673 nchi nzima kwa upelelezi wako na wenzako.
Shahdii: Sikumbuki na mimi sio msemaji wa Jeshi.
Lissu: Waeleze majaji kwamba kesi zote hizi zilifutwa
Shahidi: Sikumbuki
Lissu: Nakurejesha kwenye mikutano ya hadhara, waeleze majaji kama sheria inazuia hii mikutano wakati wa uchaguzi tu.
Shahidi: Sina jibu.
Lissu: Pamoja na waandishi wa jambo unafahamu kulikuwa na waandishi wa Azam, ITV, Arusha one digital, Clouds media , walikuwepo waandishi wa Chanzo TV
Shahidi: Ndio ninafahamu
Lissu: Waeleze majaji kuwa hawa waandishi wengine walirusha mkutano kwenye vyombo vyao.
Shahidi: Walirusha kutokea kwa Jambo
Lissu: Waandishi wa habari wote hawa walifahamu hayo maneno na kuyarusha?
Shahidi: Kufahamu sijui ila waliyarusha.
Lissu: Mtu anayepata taarifa za uhaini anapaswa azitolee taarifa polisi ni iweli sio kweli?
Shahidi: Ndio
Lissu: Na huyu mtu asipotolea taarifa polisi anakuwa amefanya kosa la kuficha uhaini?
Shahidi: Sifahamu sina hakika nayo.
Lissu: Kuna hata mmoja kati ya waandishi hawa aliyetoa taarifa
Shahidi: Hakuna.
Lissu: Mtu ambaye amechapisha maneno hayo si anakua amefanya kusambaza?
Shahidi: Hawakufanya kosa
Lissu: Kwenye huo mkutano kulikua na watu zaidi ya 300 waeleze majaji kama hata mmoja alileta taarifa
Shahidi: Hakuna.
Lissu: Kuna hata mmoja kati yao ukiacha mimi alituhumiwa.
Shahidi: Hapana.
Lissu: Ulikuwa mkuu wa upelelezi waeleze majaji kama ndio ulitoa amri nikamatwe.
Shahidi: Hapana.
Lissu: Je ni kweli au sio kweli aliyetoa maelekezo nikamatwe ni Ramadhani Kingai
Shahidi: Ulikuwa umekamatwa kupitia boss wangu Ramadhani Nganzi
Lissu: Ni kweli si kweli DCI Kingai aliwapa maelekezo kuwa mtawasiliana naye kupitia Ramadhani nganzi
Shahidi: Ndio ni kweli.
Lissu: Je ni sahihi kusema kwamba DCI kingai alitoa taarifa kwa nganzi awape taarifa kwamba Lissu amekamatwa analetwa Dar es salaam.
Shahidi: Ndio
Lissu: Nani kati yako na msaidizi wako George Padem nani alitoa amri lifunguliwe jalada la uhaini?
Shahidi: Wakati nateuliwa nilikuta tayari wameshafungua file
Lissu: Waeleze majaji kama umesoma maelezo ya Geogre Padem amekuzungumzia wewe kwa sentensi mbili tu
Shahidi: Ni kweli
Lissu: Ulikuta kazi yote imefanyika na hukufanya la maana ndio maana umetajwa kwa mistari miwili tu
Shahidi: Sina hakika.
Lissu: Nataka nizungumzie la kwangu na mgogiro wangu wa muda mrefu wa Jeshi, waeleze majaji kama unafahamu kwamba kwa karibu robo karne jeshi la Polisi limenionea sana kwa kunikamata na kunifungulia kesi za uongo
Shahidi: Sifahamu
Lissu: Waeleze majaji kama unafahamu 2002 nilikamatwa na kufungiwa central
Shahidi: Sifahamu
Lissu: Waeleze majaji kama unafahamu ilipofika mwaka 2008 wakaifuta
2011 nilikamatwa na jeshi la polisi nikachaniwa nguo na kufungwa machakani na kesho yake nikafunguliwa shauri la ilegal trace passing
Shahidi: Sifahamu.
Lissu: Waeleze majaji kama unafahamu mwaka 2012 nilikamatwa kwa kusimama na wananchi wa Arusha ambao ndugu zao waliuawa na kesi ilifutwa.
Shahidi: Sifahamu.
Lissu: Waeleze majaji mwaka 2013 pia nilikamatwa kusimama na wananchi wa Arusha na kesi ikafutwa.
Shahidi: Sifahamu
Lissu: 2016 nilisema iwapo uchaguzi utarudiwa Zanzibar uliofutwa na Jecha kungetokea maaafa na Kingai na Hamduni walikuja kutoa ushahidi nikawakaanga kama wewe na aliyetoa amri nikamatwe ni Camilius Wambura leo ni IGP.
Shahidi: Sifahamu
Lissu: Hujajua kwamba hiyo kesi ilikuja kufutwa nikiwa Ubelgiji nikiwa napigania uhai wangu 2021.
Shahidi: Sifahamu.
Lissu: Waeleze majaji 2017 kama unafahamu nilikamatwa jimboni kwangu na kushtakiwa kwa kosa la uchochezi Waziri wa Mambo ya Ndani alikuwa Mwigulu Nchemba akawaambia huyo mbunge mnamsafirisha usiku akigongwa na malori.
Shahidi: Sifahamu.
Lissu: Nilikamatwa nikiwa bungeni 2017 nje baada ya kumwita Magufuli dikteta uchwara na kushtakiwa kwa uchochezi.
Shahidi: Sifahamu.
Lissu: Waeleze majaji kama unafahamu kati ya Juni 2016 na Julai 20217 nilikamatwa mara nane na kufunguliwa kesi mara sita na zote zilifutwa mwaka 2021
Shahidi: Sifahamu.
Lissu: Waeleze majaji kwamba sijawahi kutiwa hatiani hata mara moja sina criminal record.
Shahidi: Sifahamu.
Lissu: Waeleze majaji kama unafahamu kama baada ya majaribio hayo ya kuninyamazisha nililetewa watu wasiojulikana nikapigwa risasi
Shahidi: Nafahamu
Lissu: Hata watu kuniombea polisi waliwapiga marufuku, hata watu kunitolea damu walikatazwa, wakenya ndio walinitolea damu
Shahidi: Sifahamu
Lissu: Kwa karibu robo karne naonewa kama ilivyo kwenye kesi hii.
Kesi imeahirishwa mpaka kesho.
"Mnanitesea nini kama mna ushahidi dhidi ya mnaosema wana makosa"
Chanzo cha picha, AFP
Lissu: Shahidi ni kweli au si kweli mmoja wa maafisa wa polisi walioshughulika na upelelezi wa kesi hii ni 'Assistant Andrew Chulu ndiye aliyechukua ile memory card kwa mashahidi P na P1 akavileta Dar es Salaaam.
Shahidi: Ndio
Lissu: Waeleze majaji kama ulisoma maelezo ya inspekta Andrew Chulu
Shahidi: Nimesoma
Lissu: Na umesema ulisoma maelezo ya P
Shahidi: Sijayasoma
Lissu: Waeleze majaji mnanitesea mimi nini kama mna ushahdi wa hao mnaosema wamefanya makosa
Shahidi: Huteswi
Lissu: Ninakurudisha kwenye PGO 1/25 crimes are acts defined by the law upelelezi wa polisi lazima ufuate masharti ya sheria kwa mujibu wa PGO tendo la kuvuruga uchaguzi ni uhaini.
Lissu: Kila askari polisi ana wajibu wa kuheshimu haki na uhuru wa raia na kufanya tofauti haikubaliki.
Shahidi: Ni kweli
Lissu: Waeleze majaji kwenye maelezo yako polisi mwaka jana wameonesha kuzingatia uhuru wangu
Lissu:Kwenye maelezo yako kuna eneo ulilozingatia uhuru wangu kwa mujibu wa katiba?
Shahidi: Kimya
Lissu: Kimya maana yake hakuna, ibara ya 19/1 kwenye katiba kila mtu anao uhuru wa kutoa maoni na kueleza fikra
20/1 kila mtu anao uhuru wa kukutana wengine na kuchangamana na kwa ajili hiyo kutoa mawazo yake hadharani.
Lissu: Chama changu kiliitisha uchaguzi wakaalika waandishi wa habari mwenyekiti wa chama akatoa maoni yake hadharani ulizingatia uhuru wangu?
Shahidi: Maneno yalikua ya vitisho
Lissu: Nilimtisha nani, Serikali?
Lissu: Nina haki ya kufaidi haki zote kwenye katiba waeleze majaji kama umezingatia haki zangu na umeandika kwenye maelezo yako
Shahidi: Hakuna
Lissu: Ni kweli au si kweli kwamba kwenye mkutano huo nilishambulia sana mfumo wa uchaguzi na nilisema mfumo umekua ukiipemdelea CCM na watumishi wote wa serikali wamekua wakiipendelea CCM na nilisema Tume ya uchaguzi wamekuwa na Tabia ya kuengua wagombea wa upinzani, mfano uchaguzi wa serikali za mitaa na vijiji ni kweli sio kweli?