Polisi yaafiki kuwa upekuzi wa nyumba za Mwanamfalme Andrew ulikuwa kinyume cha sheria, mahakama yaambiwa
Polisi katika kituo cha Valley Thames wamekubali kwamba vibali vya upekuzi vilivyotumika kupekua nyumba za Andrew Mountbatten-Windsor mapema mwaka huu vilikuwa kinyume cha sheria, Mahakama Kuu imesikia.
Imesema imekubali "uamuzi wa mahakama ya awali wa kutoa vibali chini ya sheria maalum iliyotumika haukuwa sahihi" walipopewa ruhusa ya kupekua mali za mwanamfalme huyo wa zamani mnamo tarehe 19 Februari.
Andrew alikamatwa na Polisi wa Thames Valley kwa tuhuma za utovu wa nidhamu katika ofisi ya umma. Anakana makosa yoyote.
Hati hizo zilitolewa kabla ya kukamatwa kwake na mawakili wake wanapinga uhalali wake.
Kukamatwa kwake mwezi Februari kuliibuka baada ya Idara ya Sheria ya Marekani kuchapisha nyaraka zilizodokeza kwamba alikuwa ametuma taarifa za siri kwa mhalifu wa kingono aliyehukumiwa wakati Mountbatten-Windsor alipokuwa mjumbe wa biashara wa Uingereza mwaka 2010.
Amekuwa akikanusha mara kwa mara makosa yoyote kuhusiana na Epstein.
Unaweza pia kusoma: