Syria yatathmini uwezekano wa kuisaidia Saudi Arabia kijeshi dhidi ya Wahouthi

Chanzo cha picha, Getty Images
Syria kwa sasa inachunguza kwa makini uwezekano wa kutoa msaada wa kijeshi kwa mshirika wake mkuu, Saudi Arabia, huku vita dhidi ya Wahouthi wanaoungwa mkono na Iran nchini Yemen vikiendelea kushamiri.
Kwa mujibu wa taarifa zilizochapishwa na shirika la habari la Reuters, likinukuu afisa wa Marekani pamoja na afisa wa jeshi la Syria mwenye ufahamu wa suala hilo, chaguzi za kutuma wanajeshi Syria nchini Yemen bado zinajadiliwa.
Vyanzo hivyo vimesema kuwa miongoni mwa chaguzi zinazozingatiwa ni kutoa msaada wa kujihami ili kuisaidia Saudi Arabia kujilinda dhidi ya mashambulizi.
Pia kutuma vikosi vyenye uwezo wa kushiriki katika operesheni za mashambulizi ili kusaidia vikosi vya Yemen vinavyoungwa mkono na Saudi Arabia katika mapambano dhidi ya Wahouthi.
Ripoti hiyo inaashiria uwezekano wa kuongezeka kwa ushiriki wa Syria katika mzozo wa Yemen iwapo uamuzi wa mwisho wa kutuma vikosi utapitishwa.
Taarifa kama hizo pia ziliripotiwa na tovuti ya habari ya Marekani Axios, ambayo ilisema kuwa mipango hiyo bado iko katika hatua ya tathini na haijathibitishwa rasmi na mamlaka za Syria au Saudi Arabia.
Ikiwa hatua hiyo itatekelezwa, inaweza kuashiria mabadiliko muhimu katika ushirikiano wa kijeshi wa kikanda na kuongeza shinikizo dhidi ya kundi la Wahouthi katika vita vinavyoendelea nchini Yemen.
Unaweza kusoma;


























