Xi, Putin na Trump wakutana huku viongozi wa China na Urusi wakikosoa sera za Marekani
Rais wa China Xi Jinping hii leo ameahidi kupinga sera za “ulinzi wa biashara”, huku Rais wa Urusi Vladimir Putin, akikosoa vikwazo vya mataifa ya Magharibi muda mfupi kabla ya kukutana na Trump.
Muhtasari
- Wakenya na wasafiri kutoka DRC kukaa karantini siku 21 - Kenya
- Ethiopia na Eritrea zatuma wanajeshi wake mpakani, hofu ya vita ikiongezeka
- Rais Ruto atetea rekodi ya utendaji wa serikali yake
- Rais Xi na Putin wakosoa sera za Marekani huku wakikutana na Trump
- Mamia wanusurika MV Mwanza ikigonga miamba
- Rais wa Tanzania aanza ziara ya siku mbili Uganda
- Serikali ya Ghana yatetea hatua yake ya kununua ndege mpya ya Rais
- Iran yaishambulia Kuwait mzozo ukienea eneo la Ghuba
- THRDC yahoji hukumu aliyopewa Tundu Lissu
- Tazama kwa picha Trump alivyowasili China
- Xi ampokea Trump katika uwanja wa ndege wa Shenzhen kwa heshima ya kipekee
- Diplomasia ya mapokezi: Nani atampokea Trump atakapowasili China?
- Ndege 34 za Tanzania Zapigwa Marufuku Anga la Ulaya
- Xi na Putin wahitimisha mazungumzo yaliyodumu zaidi ya saa mbili
- Wayne Rooney afichua kuwa alifikiria kujiua wakati akiwa Manchester United
- Xi, Putin wafanya mazungumzo kabla ya ujio wa Trump
- Liverpool wamzidi Chelsea katika mbio za kumyakua Camara - Tetesi za Jumatano
- Nvidia yakataa kumrejesha Jensen Huang huku ikitangaza faida kubwa
- Rubio asema Marekani haikabiliwi na mashambulizi ya kimfumo
- Mapigano mashariki mwa DRC yalazimisha wagonjwa kuhamishwa kutoka hospitali ya Bunyakiri – MSF
- Iran yashambulia Kuwait na Bahrain
- Mtandao wa siri wa Shirika la Ujasusi la Marekani (NSA) wakumbwa na hitilafu ya muda
- Putin awasili China kabla ya mkutano wa kihistoria na Trump na Xi
Moja kwa moja
Na Faidha Ngaga & Beldeen Waliaula
Wakenya na wasafiri kutoka DRC kukaa karantini siku 21 - Kenya

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Waziri wa afya Kenya, Aden Duale Wakenya wanaoishi, kufanya kazi au kusafiri kupitia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na wanaopanga kurejea nchini Kenya kwa ajili ya sikukuu za mwisho wa mwaka watalazimika kukaa karantini na kufuatiliwa kiafya kwa muda wa siku 21.
Hatua hii ilitangazwa hapo jana na Waziri wa Afya Aden Duale, aliyesema Wakenya wote watakaowasili kutoka DRC, watatakiwa kuzingatia masharti hayo ya karantini.
Wasafiri kutoka DRC pia watalazimika kufanyiwa uchunguzi wa kina na tathmini ya afya katika vituo maalumu vya kuingilia nchini.
“Wakenya watakaorejea nchini kupitia uwanja wa ndege watalazimika kufanyiwa uchunguzi wa kina kupitia Lango la 16. Ili kulinda nchi yetu, wote wanaosafiri kutoka DRC watapaswa kukaa karantini kwa lazima kwa siku 21,” Duale aliliambia Kamati ya Seneti .
Waziri huyo alisema hatua hizo ni sehemu ya mpango mpana wa kudhibiti maambukizi ya Ebola ulioanzishwa na Wizara ya Afya kufuatia mlipuko wa aina ya Bundibugyo ya virusi vya Ebola.
Kenya awali iliripoti visa tisa vilivyothibitishwa vya Ebola na vifo viwili, vilivyotokana na kisa cha kwanza kilichoingizwa kutoka nje ya nchi.
Soma pia:
Ethiopia na Eritrea zatuma wanajeshi wake mpakani, hofu ya vita ikiongezeka

Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Rais wa Eritrea Isaias Afwerki Ethiopia na Eritrea zimetuma vikosi vyao vya kijeshi mpakani, hii ni kulingana na ripoti ya wachunguzi wa migogoro na watu wenye uhusiano na makundi ya waasi katika eneo la Tigray kaskazini mwa Ethiopia.
Hatua hiyo imezidisha hofu ya kuzuka kwa vita vya moja kwa moja kati ya mataifa hayo hasimu ya kihistoria.
Kutumwa kwa vikosi hivyo mpakani kumeziweka jeshi la Ethiopia na Eritrea katika umbali wa kushambuliana, kwa mujibu wa wachunguzi wa migogoro kutoka ACLED na International Crisis Group.
Shirika la ACLED liliripoti kuwa mashambulizi ya droni ambayo linaamini yalitekelezwa na jeshi la Ethiopia yalilenga wanajeshi wa Eritrea waliokuwa ndani ya ardhi ya Ethiopia. Hata hivyo, Ethiopia haijatoa maoni kuhusu mashambulizi hayo.
Eritrea nayo imekanusha madai ya kuingiza vikosi vyake nchini Ethiopia na kuishutumu serikali ya Addis Ababa kwa kutafuta sababu ya kuivamia nchi hiyo jirani .
Aidha serikali ya Ethiopia pia imeishutumu Sudan, ambayo yenyewe inakabiliwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe, pamoja na Misri, kwa kuwaunga mkono waasi eneo la Tigray.
Hata hivyo, Eritrea, Sudan na Misri zimekanusha madai hayo.
Soma pia:
Rais Ruto atetea rekodi ya utendaji wa serikali yake

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Picha ya Rais William Ruto Na Phylis Mwatee
Rais wa Kenya William Ruto ametetea rekodi ya serikali yake katika kuimarisha uchumi, akisema mageuzi yaliyotekelezwa tangu aingie madarakani mwaka 2022 yamechangia kurejesha uthabiti wa kiuchumi nchini humo.
Akihutubia bunge la Taifa la Kenya, Rais Ruto amegusia pia mustakabali wa maendeleo ya Kenya baada ya mwaka 2030, ushirikishwaji wa vijana katika uongozi na umuhimu wa kuzingatia uwezo na sifa katika uteuzi wa viongozi wa umma.
Hii ilikuwa ni hotuba yake ya nne ya Hali ya Taifa tangu alipoingia madarakani mwaka 2022.
Akilihutubia Bunge la Kenya katika kikao cha pamoja cha Baraza la Kitaifa na Seneti, Rais Ruto amesema thamani ya shilingi ya Kenya imeimarika kutoka takribani shilingi 162 kwa dola moja ya Marekani hadi shilingi 129.
Pia ametaja kupungua kwa riba za mikopo ya benki za biashara, kutoka asilimia 17.2 mwezi Novemba 2024 hadi asilimia 14.4 kufikia Septemba mwaka huu, pamoja na kuongezeka kwa akiba ya fedha za kigeni hadi kilele cha dola bilioni 15.3.
Katika hotuba yake ya nne ya Hali ya Taifa, Rais. Ruto pia alisisitiza azma yake ya kujenga Kenya yenye usawa, ambako kila mwananchi na kila jamii inanufaika na fursa za maendeleo bila kujali eneo au hali yake ya kiuchumi.
Hotuba hiyo imetolewa wakati ambapo serikali yake inaendelea kukabiliwa na shinikizo kuhusu gharama ya maisha, ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana, kodi na ongezeko la deni la taifa.
Aidha,hotuba hiyo inakuja chini ya miezi tisa kabla ya uchaguzi mkuu wa Agosti mwaka 2027.
Rais Xi na Putin wakosoa sera za Marekani huku wakikutana na Trump

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Picha ya pamoja ya Rais Donald Trump, Xi Jinping na Vladmir Putin Rais wa Marekani Donald Trump amekutana na Rais wa Urusi Vladimir Putin nchini China.
Viongozi hao watatu walikutana kabla ya kuanza kwa chakula cha jioni mjini Shenzhen.
Video iliyochapishwa na waandishi wa habari wa Kremlin inaonyesha Trump akiwa pamoja na mwenyeji wake, Rais wa China Xi Jinping na mkewe, wakati Putin alipowasili.
Huu ni mkutano wa kwanza wa ana kwa ana kati ya viongozi hao wawili tangu mkutano wa kilele wa Marekani na Urusi uliofanyika Alaska mwezi Agosti 2025.
Viongozi hao watatu wanatarajiwa kufanya mkutano rasmi wa pande tatu hapo kesho.
Awali katika mkutano wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi wa Asia na Pasific (APEC) mjini Shenzhen,Rais wa China Xi Jinping hii leo ameahidi kupinga sera za “ulinzi wa biashara”, huku Rais wa Urusi Vladimir Putin, akikosoa vikwazo vya mataifa ya Magharibi muda mfupi kabla ya kukutana na Trump.
Mamia wanusurika MV Mwanza ikigonga miamba

Chanzo cha picha, PPRA
Taarifa za vyombo vya habari nchini Tanzania vinaripoti Meli ya MV Mwanza imepoteza mwelekeo na kugonga miamba ya Bismarck wakati nahodha akifanya jitihada za kuitia nanga katika Bandari ya Mwanza, Ziwa Victoria.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, muda mfupi baada ya meli hiyo kugonga miamba, moshi mwingi ulianza kutoka, hali iliyosababisha taharuki miongoni mwa watu waliokuwa eneo hilo.
Hata hivyo, hadi sasa hakuna taarifa zilizoripotiwa kuhusu watu kujeruhiwa kutokana na tukio hilo. Chanzo cha ajali hiyo na kiwango cha uharibifu wa meli bado havijafahamika.
MV Mwanza ni miongoni mwa miradi mikubwa ya serikali katika kuboresha usafiri wa majini nchini Tanzania. Meli hiyo ilizinduliwa Januari, 2026, na Waziri Mkuu Dk Mwigulu Nchemba katika Bandari ya Mwanza Kusini.
Meli hiyo yenye urefu wa mita 92.6, upana wa mita 17 na ghorofa nne, ilijengwa kwa gharama ya zaidi ya Shilingi bilioni 120, kwa ushirikiano kati ya kampuni za Korea Kusini na taasisi za Tanzania.
Ina uwezo wa kubeba abiria 1,200, tani 400 za mizigo, magari madogo 20 na malori matatu kwa safari moja. Pia ina vifaa vya kisasa vya usalama na mawasiliano vinavyowezesha kutoa taarifa kwa vituo vya utafutaji na uokoaji.
Taarifa zaidi kuhusu tukio hilo zinatarajiwa kutolewa na mamlaka husika.
Rais wa Tanzania aanza ziara ya siku mbili Uganda

Chanzo cha picha, Ikulu Tanzania
Maelezo ya picha, Rais Samia Suluhu na Rais Yoweri Museveni Rais wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan, ameanza ziara yake ya siku mbili nchini Uganda.
Rais Samia aliwasili mapema leo katika ikulu ya Entebbe na kukutana na mwenyeji wake, Rais Yoweri Kaguta Museveni.
Viongozi hao wanatarajiwa kujadiliana kuhusu nishati, biashara, kilimo,viwanda na jinsi ya kuendeleza ujenzi wa bomba la mafuta ghafi la Afrika Mashariki (EACOP).
Ziara hiyo ya Rais Samia, inafuatia safari ya Rais Museveni ya mwezi Agosti 2026, jijini Dar es Salaam, ambapo viongozi hao wawili walitia saini makubaliano ya kuanzisha kituo cha kikanda cha nishati mkoani Tanga.
Kituo hicho kinatarajiwa kuhifadhi mafuta, kusafisha mafuta ghafi na kuyasambaza.
Kituo hicho kinajengwa kupitia mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP), lenye urefu wa kilomita 1,443, litakalo safirisha mafuta ghafi ya Uganda kutoka Hoima hadi pwani ya Tanzania karibu na bandari ya Tanga.
Tazama kwa picha Rais Samia alivyowasili Entebbe:

Chanzo cha picha, Ikulu Tanzania
Maelezo ya picha, Rais Suluhu akipokelewa na Rais Museveni katika Ikulu ya Entebbe 
Chanzo cha picha, Ikulu Tanzania
Maelezo ya picha, Rais Suluhu akikagua gwaride katika Ikulu ya Entebbe 
Chanzo cha picha, Ikulu Tanzania
Maelezo ya picha, Rais Suluhu akitembea na Rais Museveni Serikali ya Ghana yatetea hatua yake ya kununua ndege mpya ya Rais

Chanzo cha picha, Ghana Airfoce
Serikali ya Ghana imetetea hatua yake ya kununua ndege mpya ya rais, licha ya kukosolewa kutokana na gharama yake, wakati wananchi wengi nchini humo wanakabiliwa na gharama ya juu ya maisha.
Ndege hiyo aina ya Falcon 6X iliyotengenezwa nchini Ufaransa, yenye thamani ya dola milioni 60, imezua mvutano wa kisiasa, huku wanasiasa wa upinzani wakiishutumu serikali ya Rais John Mahama, kwa kuwa na vipaumbele visivyo sahihi.
Hata hivyo, serikali ya Ghana imejitetea kwa kusema, ununuzi huo una sababu za msingi,na kuimarika kwa uchumi wa Ghana kumeiwezesha kumudu gharama ya ndege hiyo.
Ndege hiyo itachukua nafasi ya ndege ya zamani inayotumiwa na rais.
Serikali ya John Mahama, imekuwa ikipitia wakati mgumu kuthibitisha kuwa uchumi wa taifa hilo umeimarika, baada ya taiafa hilo kutafuta msaada kutoka kwa shirika la fedha duniani (IMF)
Bunge liliidhinisha ununuzi wa ndege hiyo mwezi Desemba mwaka uliopita kama sehemu ya mpango mpana wa kuboresha vifaa vya usafiri wa anga vya jeshi la Ghana. Mpango huo pia unajumuisha ununuzi wa helikopta nne kutoka kampuni ya Airbus.
Wakati akiwa upinzani, Rais Mahama mwenyewe alipinga ununuzi wa ndege mpya ya rais.
Hatua hiyo sasa imeibua maswali kuhusu sababu zilizoifanya serikali yake kuendeleza ununuzi huo.
Soma pia:
Iran yaishambulia Kuwait mzozo ukitanuka eneo la Ghuba

Chanzo cha picha, Reuters
Iran imesema imelenga maeneo yanayotumiwa na Marekani kuhifadhi ndege zisizo na rubani na makombora nchini Kuwait usiku kucha, baada ya Marekani kushambulia kisiwa cha Qeshm katika Mlango-Bahari wa Hormuz.
Hii ni mara ya kwanza kwa Iran kuishambulia nchi hiyo ya Ghuba yenye uhusiano wa karibu na Marekani tangu mwezi Septemba.
Mapema leo, Bahrain imesema ilifanikiwa kuzuia mashambulizi ya anga kutoka Iran, ikiwa mara ya tatu Iran inaishambulia taifa hilo.
Bahrain imeikashifu Iran kwa kuilenga nchi hiyo ambayo ni makao makuu cha kikosi cha tano cha Jeshi la wanamaji wa Marekani.
Mashambulizi haya ya hivi karibuni yanajiri wakati kumekuwa na juhudi za kutatua mzozo huo kwa njia ya diplomasia.
Soma pia:
THRDC yahoji hukumu aliyopewa Tundu Lissu

Chanzo cha picha, Online
Muungano wa kutetea haki za kibanadamu nchini Tanzania (THRDC) imetoa wito wa kurejelewa tena kwa hukumu ya miaka minne, aliyopewa Tundu Lissu, baada ya mahakama kumhukumu kwa kosa la uchochezi wala si uhaini aliloshtakiwa nalo.
Katika taarifa iliyotolewa mapema hii leo, shirika hilo lilihoji iwapo mahakama ilizingatia vipengele vyote vya kisheria kabla ya kumhukumu kwa uchochezi na kumpa kifungo cha miaka minne, ilhali Lissu tayari amekuwa akizuiliwa rumande kwa zaidi ya siku 577.
Lissu alikamatwa mwezi Aprili mwaka wa 2025, na kufunguliwa mashtaka ya uhaini, baada ya semi zake za “No Reforms No Elections" kwenye mkutano wa CHADEMA.
Mahakama kuu ilitoa hukumu yake tarehe 6 mwezi Novemba 2026, na kumuondolea mashtaka ya uhaini ila ikampata na hatia ya uchochezi.
THRDC inasema mahakama haikutoa ushahidi wa kutosha wa kuthibitisha Lissu alichochea watu kuandamana.
THRDC inasema kuwa mtu kutaka mageuzi yafanyike katika mfumo wa uchaguzi haiwezi kuchukuliwa kuwa uhaini.
Kwenye taarifa yao, THRDC inapendekeza;
Kufutwa kwa Shauri la Makosa ya Mtandao, na kutoa wito kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kuondoa Shauri la Jinai la mwaka 2025 lililopo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, ambalo limetokana na kauli alizozitoa Lissu tarehe 3 Aprili 2025 zilizokuwa msingi wa shauri la uhaini.
THRDC inasema kuendelea kwa shauri hilo kunaibua hoja za kisheria kuhusu uhalali wa kumshtaki mtu mara mbili kwa kauli zilezile, ambazo wamedai ni kujirudia katika mashtaka.
Soma pia:
Tazama kwa picha Trump alivyowasili China

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Picha ya Trump na Xi Jinping Rais wa Marekani Donald Trump, amewasili katika mji wa Shenzhen, nchini China.
Trump amelakiwa na mwenyeji wake Rais Xi Jinping.
Tazama kwa picha Trump alivyowasili China.

Chanzo cha picha, Getty Images

Chanzo cha picha, Getty Images

Chanzo cha picha, Getty Images

Chanzo cha picha, Getty Images
Xi ampokea Trump katika uwanja wa ndege wa Shenzhen kwa heshima ya kipekee

Chanzo cha picha, Getty Images
Hili si tukio la kawaida la Rais wa China, Xi Jinping, kumpokea Rais wa Marekani, Donald Trump, katika uwanja wa ndege.
Ni tukio la kidiplomasia lililopangwa kwa umakini mkubwa.
Xi anatambua uzito wa ishara hiyo, ambayo inaaminika kuwa ni mara ya kwanza kwake akiwa Rais wa China kumpokea kiongozi wa nchi nyingine katika uwanja wa ndege.
Kwanza, anarejesha heshima ambayo Trump alimpa.
Rais huyo wa Marekani alimfuata Xi kumpokea katika uwanja wa ndege mjini Washington mapema mwaka huu, na sasa kiongozi huyo wa China anamlipa heshima hiyo.
Hata hivyo, Xi pia anafahamu kuwa Trump anathamini sana kutambuliwa binafsi, sherehe za heshima na hadhi ya uongozi.
Kwa kutoikabidhi jukumu hilo kwa kiongozi mwingine, Rais Xi anampa Trump heshima ya pekee na kumfanya ajione kuwa mtu muhimu kwa kumchagua yeye mwenyewe kumpokea.
Huenda Xi anatumai kuwa ishara hiyo ya nia njema itarahisisha mazungumzo kuhusu biashara, Taiwan na teknolojia.
Pia, anaweza kuonyesha ukarimu huo bila kupoteza hadhi yake. Hii ni kwa sababu China tayari inadhibiti mazingira na mipangilio ya mkutano huo wa kilele usio wa kawaida unaowahusisha Trump, Xi na Putin.
Unaweza pia kusoma:
Sudan: Droni za RSF zaua raia 37, Amnesty yataka uchunguzi

Chanzo cha picha, Getty Images
Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limetaka kufanyika kwa uchunguzi kuhusu mashambulizi ya droni yanayodaiwa kutekelezwa na kundi la wanamgambo la Rapid Support Forces (RSF) nchini Sudan.
Katika ripoti iliyotolewa Jumatano, shirika hilo limesema limechunguza mashambulizi tisa yaliyotekelezwa na RSF katika mji wa El Obeid, jimbo la Kordofan Kaskazini, yaliyosababisha vifo vya raia 37 kati ya Juni na Agosti 2026.
Mashambulizi hayo yalilenga makazi ya watu, miundombinu ya umeme, vituo vya mafuta, masoko na magari yaliyokuwa yakisafiri. Amnesty imesema haikubaini uwepo wa maeneo yoyote ya kijeshi karibu na maeneo yaliyoshambuliwa.
Mashambulizi matatu yalilenga maeneo ya makazi na kusababisha vifo vya raia wakiwa majumbani mwao na katika vitongoji walimoishi. Mashambulizi mengine manne yalilenga miundombinu ya kiraia, ikiwemo vituo vya umeme, vituo vya mafuta na soko kuu, huku mawili yakilenga magari yaliyokuwa yakisafiri.
Miongoni mwa matukio yaliyorekodiwa ni shambulizi la droni la Juni 10 lililomuua kijana mmoja. Shambulizi jingine dhidi ya watu waliokuwa wakisafirisha mwili wake kwenda kuuzika liliripotiwa kuua watu wasiopungua watano.
Siku iliyofuata, shambulizi jingine lililenga nyumba katika kitongoji cha Al-Matar na kuua raia wasiopungua tisa. Tarehe 6 Julai, shambulizi la droni dhidi ya gari lililokuwa limewabeba watu waliohudhuria harusi liliua watu 13.
Amnesty pia imeripoti kuwa mashambulizi dhidi ya vituo vya mafuta yaliua raia, kuharibu magari na kuzidisha uhaba wa mafuta, hali iliyochangia kupanda kwa bei ya mafuta.
RSF imekanusha kuhusika na mashambulizi hayo na badala yake kuilaumu jeshi la Sudan (SAF). Kundi hilo limesema linazingatia uwezekano wa kuunda kamati ya uchunguzi.
Amnesty imezitaka Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika kuimarisha ulinzi wa raia, kushinikiza pande zinazopigana kufikia makubaliano ya kusitisha mapigano na kupanua vikwazo vya sasa vya silaha ili vijumuishe maeneo yote ya Sudan, pamoja na usambazaji wa droni.
Matumizi ya droni katika vita nchini Sudan yameongezeka, hasa tangu mwaka 2025, huku pande zote mbili zinazopigana zikizidi kutumia mifumo ya ndege zisizo na rubani, ambayo inaripotiwa kusambazwa na mataifa ya kigeni.
Kwa mujibu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu, zaidi ya raia 1,630 waliuawa katika mashambulizi ya droni kati ya Januari na Oktoba 2026.
Unaweza pia kusoma:
Diplomasia ya mapokezi: Nani atampokea Trump atakapowasili China?

Chanzo cha picha, Getty Images
Moja ya mambo yatakayofuatiliwa kwa karibu ni nani atakayempokea Rais wa Marekani, Donald Trump, katika uwanja wa ndege atakapowasili China.
Uamuzi wa Beijing kuhusu kiongozi wa China atakayemkaribisha rais huyo wa Marekani utatoa ishara ya namna wanavyothamini ziara yake.
Wakati wa ziara ya kitaifa ya Trump nchini China mwezi Mei, uongozi wa China ulimtuma Makamu wa Rais Han Zheng kumpokea rais huyo katika uwanja wa ndege.
Aidha, wakati wa ziara ya kitaifa ya Rais Xi Jinping nchini Marekani mwezi Septemba, Trump alichukua hatua isiyo ya kawaida ya kumlaki mwenyewe Xi katika uwanja wa ndege.
China bila shaka ingependa kulipa ishara hiyo ya heshima kwa kumtuma kiongozi wa ngazi ya juu kutoka Kamati ya Siasa ya Chama cha Kikomunisti (Politburo) kumpokea Trump.
Hata hivyo, kuna uwezekano mdogo wa Xi mwenyewe kwenda kumpokea uwanja wa ndege kutokana na ratiba yake kuwa na shughuli nyingi.
Cai Qi, ambaye kwa vitendo ni mkuu wa utumishi wa Rais Xi, angekuwa mbadala anayefaa kwa jukumu hilo.
Cai pia ndiye aliyempokea Rais wa Russia, Vladimir Putin, leo asubuhi. Hatua hiyo ingeipa Beijing fursa ya kuonesha kuwa inathamini ziara za viongozi wa Marekani na Russia kwa kiwango sawa.
Unaweza pia kusoma:
EU yapiga marufuku mashirika 34 ya ndege ya Tanzania kutumia anga yake

Chanzo cha picha, Getty Images
Umoja wa Ulaya (EU) umeendeleza vikwazo vya usafiri wa anga dhidi ya mashirika ya ndege kutoka nchi 12 za Afrika, huku mashirika 87 ya ndege yakiwekwa kwenye orodha yake ya usalama wa anga kutokana na wasiwasi kuhusu usimamizi wa viwango vya usalama.
Katika orodha hiyo ya hivi karibuni, Tanzania ndiyo nchi yenye idadi kubwa zaidi ya mashirika ya ndege yaliyotajwa, ikiwa na mashirika 34, yakifuatiwa na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (13), Sudan (12) na Libya (10).
Nchi nyingine zilizoathiriwa na marufuku hiyo ni Angola, Congo-Brazzaville, Djibouti, Guinea ya Ikweta, Eritrea, Liberia, São Tomé na Príncipe, Sierra Leone na Sudan.
Kwa mujibu wa Tume ya Ulaya, mashirika ya ndege yaliyoidhinishwa na mamlaka za anga za nchi hizo hayaruhusiwi kufanya safari ndani ya anga ya Umoja wa Ulaya kutokana na kile ilichosema kuwa ni udhaifu wa mifumo ya usimamizi wa usalama wa ndege katika nchi husika.
Hata hivyo, Angola imepewa msamaha kwa mashirika mawili, TAAG Angola Airlines na Heli Malongo, ambayo yanaendelea kuruhusiwa kuruka katika anga ya Ulaya.
EU imeeleza kuwa kuwekwa kwa nchi kwenye orodha hiyo hakumaanishi kuwa kila shirika la ndege limekiuka viwango vya usalama, bali mara nyingi huakisi wasiwasi kuhusu uwezo wa mamlaka za usafiri wa anga za nchi husika kusimamia na kuthibitisha usalama wa mashirika yaliyo chini yao.
Mashirika yaliyowekewa vikwazo yanaweza kuondolewa kwenye orodha hiyo iwapo yataonyesha kutimiza viwango vya kimataifa vya usalama wa anga.
Unaweza pia kusoma:
Xi na Putin wahitimisha mazungumzo yaliyodumu zaidi ya saa mbili

Chanzo cha picha, Getty Images
Mazungumzo kati ya Xi Jinping na Vladimir Putin yamehitimishwa baada ya kudumu kwa zaidi ya saa mbili, huku Putin akiondoka katika makazi ya serikali ambako mkutano huo ulifanyika, kwa mujibu wa shirika la habari la serikali ya Urusi, TASS.
TASS imesema kuwa miongoni mwa ajenda zilizojadiliwa na ujumbe wa viongozi hao wawili ni "matarajio ya kuimarisha zaidi ushirikiano wa kiuchumi kati ya Urusi na China."
Katika nukuu ya hotuba za ufunguzi za Xi na Putin, iliyochapishwa na Kremlin, viongozi hao wawili walisifu uhusiano wa nchi zao na kubainisha kuwa huu ulikuwa mkutano wao wa tatu wa ana kwa ana mwaka huu.
Xi alizihimiza nchi hizo mbili "kuendelea kusonga mbele kwa uthabiti na ujasiri, huku zikifungua daima uwezo mkubwa uliopo katika mahusiano ya pande mbili."
Kwa upande wake, Putin alieleza ukuaji wa biashara kati ya nchi hizo mbili na kusisitiza kile alichokiita "mazungumzo yenye tija katika utafiti wa kisayansi na ubunifu."
Unaweza pia kusoma:
Wayne Rooney afichua kuwa alifikiria kujiua wakati akiwa Manchester United

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Rooney ameichezea timu ya taifa ya England mechi 120 na kufunga mabao 53. TAHADHARI : Makala haya yanamaudhui yanayohusu mawazo ya kujiua.
Wayne Rooney amefichua kuwa aliwahi kufikiria kujiua alipokuwa akiichezea Manchester United, na hata alitafuta msaada wa mtaalamu wa afya ya akili ili kutambua na kutibu matatizo yaliyokuwa yakimsumbua.
Nahodha huyo wa zamani wa England alijiunga na Manchester United akitokea Everton mwaka 2004 na kufunga mabao 253 katika mechi 559 alizoichezea klabu hiyo.
Hata hivyo, katika mahojiano na mwanahabari Gabby Logan kwenye podikasti ya Life at the Midpoint, Rooney alizungumzia mapambano makubwa aliyokuwa akipitia nje ya uwanja wakati mwanawe mkubwa, Kai, akiwa mtoto mchanga. Kwa sasa Kai ana umri wa miaka 17.
"Kulikuwa na kipindi nilijifungia ndani kwa siku mbili na nilikunywa pombe bila kukoma, na huo ulikuwa wakati ambao nilikuwa katika kilele cha mafanikio yangu ya soka," alisema Rooney.
Rooney, mwenye umri wa miaka 41, alisema alikuwa akipambana na hisia zake za ndani, na baada ya kushirikisha tatizo lake kwa mkewe, Colleen, pamoja na mama yake, alitambua kuwa alihitaji msaada ili kuweza kulishinda.
"Leo ninapotazama nyuma, ninaona nilikuwa mbinafsi na mwenye tamaa, lakini nilikuwa na ugumu wa kutambua tatizo langu. Nilifikia hatua ya kuelewa kwamba nisingeweza kulikabili peke yangu, na nilijificha kwa sababu sikutaka Kai anione katika hali hiyo," alisema.
"Nilifikia hatua ambayo nilikuwa nikifikiria kujiua. Sikupenda kuchangamana na watu na nilitaka kuwa peke yangu. Nilijisikia vizuri nikiwa uwanjani, lakini nje ya uwanja nilikuwa napitia kipindi kigumu sana," aliongeza Rooney.
Unaweza pia kusoma:
Xi, Putin wafanya mazungumzo kabla ya ujio wa Trump

Chanzo cha picha, Getty Images
Rais wa China, Xi Jinping, amemuita Rais wa Russia, Vladimir Putin, kuwa ni "rafiki wa muda mrefu" walipokutana mjini Shenzhen, kabla ya mkutano wa viongozi wa nchi za Asia-Pacific (APEC) unaoandaliwa na China.
Putin na Xi wanakutana Shenzhen kwa mara ya 50 leo, huku wakisifu uhusiano wao wa karibu na thabiti katika kile walichokiita "dunia yenye misukosuko na mabadiliko mengi".
Katika mazungumzo yao ya chakula cha mchana, viongozi hao huenda walijadili masuala muhimu ya kimataifa ikiwemo vita vya Russia nchini Ukraine, usambazaji wa nishati, pamoja na nafasi ya Rais wa Marekani, Donald Trump, katika siasa za dunia.
Wakati huo huo, mjini Manila, Trump alipokelewa katika mkutano wa ASEAN kwa ukarimu mkubwa, akiwemo kutunukiwa chakula maarufu cha Jollibee, na kusifiwa na viongozi wa eneo hilo. Hata hivyo, mkutano huo umezaa ahadi chache zenye masharti au maelezo ya kina.
Trump tayari amesaini makubaliano ya biashara na Thailand pamoja na Ufilipino, lakini makubaliano hayo bado yanakosolewa kwa kukosa maelezo ya kutosha kuhusu utekelezaji na faida zake mahsusi.
Sasa macho yote yanaelekezwa katika mkutano wa kihistoria unaotarajiwa kufanyika kesho kati ya Trump, Xi na Putin, kandokando ya mkutano wa APEC mjini Shenzhen. Mkutano huo unatarajiwa kujadili masuala muhimu ya biashara, usalama wa dunia na mwelekeo wa uhusiano kati ya mataifa hayo matatu yenye ushawishi mkubwa duniani.
Unaweza pia kusoma:
Liverpool wamzidi Chelsea katika mbio za kumyakua Camara - Tetesi za Jumatano

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Lamine Camara Liverpool wanaongoza mbio za kumsajili kiungo wa kimataifa wa Senegal, Lamine Camara, kutoka Monaco, huku Chelsea wakisubiri na hawajaondoa uwezekano wa kurejea tena kwenye kinyang'anyiro cha kumsaka nyota huyo mwenye umri wa miaka 22.
Kocha wa Barcelona, Hansi Flick, amepuuza uwezekano wa kuwasajili beki wa kati wa Liverpool, Virgil van Dijk (35), na kiungo wa Manchester United, Bruno Fernandes (32), akiamini umri wao ni mkubwa kwa mipango ya klabu hiyo.
Chelsea wanaendelea kumfuatilia beki wa kulia wa Ufaransa, Jules Kounde, ambaye sasa anaonekana kuwa tayari kuondoka Barcelona mwezi Januari baada ya kuanza mechi tatu pekee za La Liga msimu huu.
Kiungo wa England, Declan Rice (27), amekubaliana kwa mazungumzo ya awali kusaini mkataba mpya wa muda mrefu na Arsenal.
Rice anatarajiwa kuwa mmoja wa wachezaji wanaolipwa mishahara mikubwa zaidi katika kikosi cha Arsenal, huku mkataba wake mpya ukimfikisha kwenye mshahara wa takribani pauni 300,000 kwa wiki.
Manchester United na Barcelona wanaongoza mbio za kumsajili chipukizi wa Valerenga, winga wa Norway mwenye umri wa miaka 15, Gabriel Rajkovic.
Winga wa zamani wa Crystal Palace, Wilfried Zaha (34), amekuwa akifanya mazoezi na klabu hiyo tangu mkataba wake na Galatasaray umalizike majira ya kiangazi, hali inayofungua uwezekano wa kurejea kwa Muivory Coast huyo katika kikosi cha Eagles.
Sunderland wanataka kumsajili beki wa zamani wa Bournemouth na Newcastle United, Lloyd Kelly (28), ambaye ameshindwa kupata nafasi ya kudumu katika kikosi cha Juventus.
Kocha wa Argentina, Lionel Scaloni, amesema kuwa nyota wa zamani wa Inter Miami, Lionel Messi (39), anaweza kurejea katika timu ya taifa kama sehemu ya benchi la ufundi baada ya kustaafu soka la kimataifa.
Mustakabali wa beki wa England, Michael Keane (33), ndani ya Everton uko shakani huku mkataba wake ukitarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu na akiwa ameanza mechi moja tu ya Premier League msimu huu.
Newcastle United na Sunderland huenda zikapata ugumu kumsajili kiungo wa Sheffield United, Sydie Peck (21), mwezi Januari kwa kuwa klabu yake haitaki kumuuza katikati ya msimu.
Kocha wa Ujerumani, Jurgen Klopp, amefichua kuwa aliwahi kujaribu kumsajili kipa Marc-Andre ter Stegen (34) alipokuwa kocha wa Liverpool, lakini kipa huyo aliamua kubaki Barcelona badala ya kuhamia Anfield.
Sunderland pia wanamtaka kiungo wa zamani wa Cameroon, Franck Zambo Anguissa (31), kutoka Napoli mwezi Januari. Anguissa aliwahi kucheza Premier League akiwa na Fulham.
Winga wa QPR, Leon Scarlett (17), anafuatiliwa kwa karibu na Eintracht Frankfurt na AC Milan baada ya kupandishwa kikosi cha kwanza msimu huu.
PSV Eindhoven wamewasilisha ofa ya awali ya pauni milioni 1.5 kwa ajili ya kumsajili kiungo wa zamani wa Manchester City, Kevin De Bruyne (35), kutoka Napoli.
Unaweza pia kusoma:
Nvidia yakataa kumrejesha Jensen Huang huku ikitangaza faida kubwa

Chanzo cha picha, Getty/Nvidia via Reuters
Mauzo ya kampuni ya teknolojia ya Nvidia yameongezeka mara mbili na kuvuka dola bilioni 100 kwa mara ya kwanza, huku kampuni hiyo ikisisitiza kuwa haina mpango wa kumrejesha mwanzilishi mwenza wake aliyeondoka, Jensen Huang.
Katika matokeo yake ya kwanza ya kifedha tangu kuondoka kwa Huang, kaimu mtendaji mkuu wa kampuni hiyo, Colette Kress, amesema shughuli za kampuni zinaendelea kama kawaida na kuwaambia wawekezaji: "Tunaweza kulimudu hili."
Mauzo ya kampuni hiyo kwa robo ya mwaka yameongezeka mara mbili ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka uliopita, na kufikia dola bilioni 115.8 (pauni bilioni 86.9). Hali hiyo imesababisha hisa za kampuni hiyo kupanda kwa asilimia 4.8 katika biashara baada ya soko kufungwa.
Mapema siku ya Jumanne, Huang alisema angeheshimiwa kurejea na kuiongoza Nvidia, baada ya kuondoka kufuatia madai ya kuwa na mahusiano ya kimapenzi nje ya ndoa, yakiwemo uhusiano na mtu anayeshukiwa kuwa jasusi wa China.
Hata hivyo, mwenyekiti wa bodi ya Nvidia, Harvey Jones, amesema katika mazungumzo na wachambuzi wa masuala ya fedha siku ya Jumanne kuwa: "Bodi haina nia ya kumrejesha katika nafasi hiyo."
Faida ya kampuni hiyo pia imeongezeka mara mbili ikilinganishwa na mwaka uliopita. Katika robo ya mwaka iliyoishia Oktoba 25, faida ilifikia dola bilioni 65.
Mapato ya Nvidia kutoka katika biashara ya vituo vya kuhifadhi na kuchakata data (data centres), ambayo ni sehemu muhimu ya shughuli zake, pia yaliongezeka mara mbili na kufikia dola bilioni 107 katika kipindi hicho.
Kampuni hiyo imesema ukuaji wake wa haraka unatarajiwa kuendelea, huku mapato yakitarajiwa kuongezeka kwa asilimia 13 katika robo inayofuata.
Unaweza pia kusoma:



















