Kwa Picha: Kuapishwa kwa rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa

Iliyochapishwa

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa amekula kiapo cha kuchukua uongozi katika uwanja uliojaa umati mkubwa wa watu katika mji mkuu wa Harare

Tunatazama picha za sherehe hiyo na umati mkubwa uliokongamana katika uwanja huo wa kitaifa wa michezo.

Uwanja wa michezo unaobeba watu 60,000 ulijaa huku raia wa Zimbabwe wakitaka kushuhudia kuapishwa kwa rais mpya.
Maelezo ya picha, Uwanja wa michezo unaobeba watu 60,000 ulijaa huku raia wa Zimbabwe wakitaka kushuhudia kuapishwa kwa rais mpya.
Kuapishwa kwa bwana Mnangagwa kunafuatia kuondoka madarakani kwa Robert Mugabe baada ya kuwa mamlakani kwa takriban miaka 37
Maelezo ya picha, Kuapishwa kwa bwana Mnangagwa kunafuatia kuondoka madarakani kwa Robert Mugabe baada ya kuwa mamlakani kwa takriban miaka 37
Bwana Mnangagwa alikuwa makamu wa rais wa Kwnaza ambaye alifutwa kazi mapema mwezi huu hatua iliosababisha jeshi kuingilia kati na kumshinikiza Mugabe kujiuzulu
Maelezo ya picha, Bwana Mnangagwa alikuwa makamu wa rais wa Kwnaza ambaye alifutwa kazi mapema mwezi huu hatua iliosababisha jeshi kuingilia kati na kumshinikiza Mugabe kujiuzulu
bwana Mnangagwa, ambaye alilitoroka taifa hilo alirudi kutoka mafichoni siku ya Jumatano tarehe 21 Novemba
Maelezo ya picha, bwana Mnangagwa, ambaye alilitoroka taifa hilo alirudi kutoka mafichoni siku ya Jumatano tarehe 21 Novemba
Rais mpya na mkewe Axilia
Maelezo ya picha, Rais mpya na mkewe Axilia
Bwana Mnangagwa amekuwa katikatiu ya urtawala wa Mugabe kwa takriban miaka 37
Maelezo ya picha, Bwana Mnangagwa amekuwa katikatiu ya urtawala wa Mugabe kwa takriban miaka 37
Mkuu wa jeshi jenerali Constantino Chiwenga, mtu aliyeongoza mapinduzi ya Robert Mugabe akitazama kuapishwa kwa Mnangagwa
Maelezo ya picha, Mkuu wa jeshi jenerali Constantino Chiwenga, mtu aliyeongoza mapinduzi ya Robert Mugabe akitazama kuapishwa kwa Mnangagwa
Bwana Mnangagwa anashirikishwa na wengi na mabaya yaliofanyika chini ya utawala wa Zanu-Pf
Maelezo ya picha, Bwana Mnangagwa anashirikishwa na wengi na mabaya yaliofanyika chini ya utawala wa Zanu-Pf
Katika hotuba yake alimsifu mtangulizi wake Robert Mugabe
Maelezo ya picha, Katika hotuba yake alimsifu mtangulizi wake Robert Mugabe
Pia aliahidi kuwatumia raia wote wa Zimbabwe , sio wanachama wa Zanu Pf pekee.
Maelezo ya picha, Pia aliahidi kuwatumia raia wote wa Zimbabwe , sio wanachama wa Zanu Pf pekee.
Viongozi kutoka mataifa jirani ya Zimbabwe walihudhuria
Maelezo ya picha, Viongozi kutoka mataifa jirani ya Zimbabwe walihudhuria
Alikuwa waziri wa zamani wa ulinzi , usalama na amekuwa na uhusiano wa karibu na Jeshi
Maelezo ya picha, Alikuwa waziri wa zamani wa ulinzi , usalama na amekuwa na uhusiano wa karibu na Jeshi
Jeshi liliingilia kati na kumng'atua mamlakani Robert Mugabe
Maelezo ya picha, Jeshi liliingilia kati na kumng'atua mamlakani Robert Mugabe
Umati mkubwa wa watu ulifurahia wakati wa kupigwa kwa mizingia 21 kama heshima ya kumkaribisha rais mpya huku ndege za kijesh zikiwa angani
Maelezo ya picha, Umati mkubwa wa watu ulifurahia wakati wa kupigwa kwa mizingia 21 kama heshima ya kumkaribisha rais mpya huku ndege za kijesh zikiwa angani
Raia wengi wa Zimbabwe waliunga mkono hatua ya jeshi ya kuingilia kati kumuondoa Mugabe
Maelezo ya picha, Raia wengi wa Zimbabwe waliunga mkono hatua ya jeshi ya kuingilia kati kumuondoa Mugabe