Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa: Al-Nassr inamtaka Luis Diaz
Klabu ya Saudi Pro League, Al-Nassr, inamtaka Luis Diaz, 28, wa Liverpool, wakifuatilia hali ya mkataba wa winga huyo wa Colombia huko Anfield. (Telegraph)
Mabingwa wa Bundesliga, Bayern Munich, bado wana imani ya kumshawishi kiungo mshambuliaji wa Bayer Leverkusen, Florian Wirtz, 22, kujiunga nao msimu huu wa joto, na sio Liverpool. (SZ)
Chelsea wamevutiwa na kiwango cha Jadon Sancho hivi karibuni na wanaweza kutumia kipengele cha mkataba cha kumnunua kwa pauni milioni 25 walichokubaliana na Manchester United na kumsajili winga huyo wa Uingereza mwenye umri wa miaka 25 kwa mkataba wa kudumu. (i Sport)
Brentford wako katika mazungumzo na Liverpool kuhusu mpango wa kumsajili kipa wa Jamhuri ya Ireland mwenye umri wa miaka 26, Caoimhin Kelleher. (Sky Germany)
Liverpool wanataka zaidi ya pauni milioni 20 kwa Kelleher. (Athletic)
Napoli wako karibu kukamilisha makubaliano ya masharti binafsi na mshambuliaji wa Canada mwenye umri wa miaka 25 wa Lille, Jonathan David, ambaye pia amewasiliana na Juventus. (Sky Sports)
Chelsea wamejiunga na Juventus kuzungumza na Sporting Lisbon kuhusu upatikanaji wa mshambuliaji wa Sweden mwenye umri wa miaka 26, Viktor Gyokeres, ambaye pia anasakwa na Arsenal. (Record)
Juventus wanavutiwa kumsajili mshambuliaji wa Brazil mwenye umri wa miaka 18 wa Real Madrid, Endrick, kwa mkopo. (Calciomercato)
Meneja wa zamani wa Juve, Massimiliano Allegri, anatarajiwa kurejea AC Milan kama meneja mpya. Kocha huyo mwenye umri wa miaka 57 alitumia miaka minne San Siro kati ya 2010 na 2014. (Calciomercato)
Ipswich Town wamempa mshambuliaji wa Hispania mwenye umri wa miaka 19 wa Chelsea, Marc Guiu, mkataba wa mkopo ili acheze Championship msimu ujao. (Fabrizio Romano)