Bingwa
wa zamani wa dunia wa bondia, Zolani
“Last Born” Tete amepigwa risasi na kuuawa nje ya nyumba yake katika mkoa wa
Eastern Cape nchini Afrika Kusini hapo jana,
polisi na Waziri wa Michezo wa nchi hiyo wametoa taarifa.
Tete,
mwenye umri wa miaka 38, alikuwa akielekea nyumbani kwake katika mji wa
Mdantsane wakati wanaume wawili waliokuwa na silaha na waliovaa barakoa
waliposhuka kutoka kwenye gari na kuanza kumfyatulia risasi.
Kuuawa
kwa Tete kunaamsha tena mjadala
kuhusu uhalifu
wa
kimabavu Afrika Kusini. Taifa hilo linaendelea kuwa miongoni mwa nchi
zenye viwango vya juu zaidi vya mauaji duniani licha ya kupungua kwa idadi ya
mauaji katika kipindi cha hivi karibuni.
Kifo
cha bingwa huyo wa bondia duniani pia kimewagusa sana wakazi wa
Mdantsane, mji wa Eastern Cape, mji
ambao umezalisha baadhi ya mabondia waliofanikiwa
zaidi nchini Afrika Kusini.
Mwanamke
mwenye umri wa miaka 27 aliyekuwa akisafiri pamoja na Tete alipigwa
risasi mara kadhaa na kukimbizwa hospitalini.
Polisi
wameanza uchunguzi, huku chanzo na sababu ya bondia huyo kushambuliwa bado
haijajulikani.
Tete
alitwaa taji la dunia la IBF katika uzani wa junior-bantamweight mwaka 2014
baada ya kumshinda Mjapani Teiru Kinoshita mjini Kobe, Japan. Baadaye alitwaa
pia taji la WBO
katika uzani wa bantamweight.
Kimataifa,
Tete anakumbukwa zaidi kwa kumpiga ndani ya sekunde 11 raia mwenzake wa
Afrika Kusini, Siboniso Gonya, mjini Belfast, Ireland Kaskazini, mwezi Novemba
2017.
Ushindi
huo uliweka rekodi ya kumalizika kwa haraka zaidi
pambano la kuwania taji la dunia.