Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Ndege 5 za kivita zenye kasi zaidi
Kwa miaka mingi F-16 ya Marekani ndio ndege iliyokuwa na kasi zaidi angani. F-16A ilianza safari yake ya kwanza mwaka wa 1976, na ndege hiyo ilianza kutumika na Jeshi la Anga la Marekani mwaka 1979.
Ndege ya kivita ya F-16 imebadilika katika kipindi cha miaka 50 ya huduma, jambo ambalo limeisaidia kubaki kuwa ndege muhimu katika mapigano ya zama hizi.
Hapo awali ndege hiyo iliundwa kama ndege ya gharama nafuu, injini moja, na nyepesi. Katika kipindi chote, imejidhihirisha kuwa na uwezo mkubwa, imetumika katika majukumu ya mapigano ya angani, misheni za kushambulia na ulinzi wa anga.
Ingawa F-16 imetumia injini tofauti katika maisha yake - kasi ya juu iliyoripotiwa na USAF bado haijabadilika. Takwimu rasmi ya F-16 ni Mach 2.0 au maili 1,500 kwa saa.
Ni ndege gani za kivita zenye kasi zaidi kwa sasa? Tuangalie ndege tano ambazo zimezidi kasi ya F-16.
The F-15E Strike Eagle
Ni ndege ya kivita ya Marekani ya muda mrefu. Ndege aina ya F-15A iliruka kwa mara ya kwanza mwaka 1972 na kuanza kufanya kazi mwaka 1976.
Ndege hiyo inaendeshwa na injini mbili za Pratt & Whitney F100-PW-220 au 229. Kimsingi, hii ni aina ile ile ya F-16, ingawa F-16 ni ndege ya injini moja.
Ikiendeshwa na injini hizo mbili, F-15E ina kasi ya Mach 2.5 au maili 1,875 kwa saa. F-15E Strike Eagle ni ndege yenye uwezo wa kufanya kazi mbalimbali; ingawa kazi yake kuu inaelezewa kama ndege ya kushambulia kutoka angani hadi ardhini, inaweza pia kutumika katika misheni za mapigano ya angani.
Hii ni ndege inayoweza kusafiri ndani ya anga ya adui, kufanya shambulizi la ardhini, na kurudi nyumbani, ni ndege iliyojengwa kwa ajili ya mapigano endelevu. Maboresho ya hivi karibuni pia yamefanya F-15 kuwa bora zaidi katika kupigana na ndege zisizo na rubani.
F-14 Tomcat
Ndege nyingine ya kivita ni F-14 Tomcat, ina kasi ya juu ya Mach 2.34, ambayo ni sawa na maili 1,734 kwa saa. Ndege ya F-14 Tomcat ilistaafu kutoa huduma kwa Jeshi la Wanamaji la Marekani mwaka 2006 ilipobadilishwa na ndege ya F/A-18 Super Hornet.
Tomcat ni ndege inayeonyeshwa katika filamu za "Top Gun" zinazoigizwa na Tom Cruise. Hata hivyo, ndege hiyo ni zaidi ya filamu - historia yake ya operesheni inarudi katika Vita vya Vietnam, wakati ndege hiyo alipotumika kusaidia uhamishaji wa watu huko Saigon Aprili 1975.
F-14 iliendelea kutumika kwa miaka thelathini na ilihusika katika Vita vya Ghuba, nchini Libya na Afghanistan.
Wakati wa vita vya Iran/Iraq katika miaka ya 1980, inaaminika kwamba ndege za kivita za Iran aina ya F-14 zilisababisha vifo vya takriban watu 150 katika mapigano ya angani.
MiG-31 Foxhound
MiG-31 Foxhound inaendeshwa na injini mbili za turbofan za Soloviev D-30F6, Foxhound ina kasi ya juu ya Mach 2.83 au maili ya 2,100 kwa saa.
MiG-31 ilianzishwa kuchukua nafasi ya MiG-25 Foxbat, ingawa kuna tofauti kubwa kati ya Foxbat na Foxhound. Foxhound ilikuwa ndege ya kwanza ya kizazi cha nne ya Umoja wa Kisovieti wakati huo.
Haikuwa tu na kasi kubwa, pia ilikuwa na vifaa vyenye uwezo wa hali ya juu vilivyowatia wasiwasi Wamagharibi. Miongoni mwa vifaa hivyo ni rada iliyoruhusu ndege hiyo kufuatilia maeneo mengi na iliruhusu hadi kufuatilia maeneo 10 kwa wakati mmoja.
MiG-31 ilianza kutumika mwaka 1981. Tangu kuanzishwa kwake, ndege hiyo imetengenezwa katika aina mbalimbali. Hii inajumuisha MiG-31D, yenye silaha za kupambana na setilaiti.
Aina nyingine maarufu ni MiG-31BM; hii inaweza kufuatilia hadi maeneo 24 kwa wakati mmoja na ina uwezo wa kufanya mashambulizi.
Dassault Mirage 2000
Kasi ya juu ya Dassault Mirage 2000 inaweza kufikia Mach 2.2 (maili 1,630 kwa saa). Ndege hiyo ya kivita ya Ufaransa ilianza kutumika na Jeshi la Anga la Ufaransa mwaka 1984 na ilisafirishwa hadi nchi mbalimbali, miongoni mwao India, Peru, na Brazil.
Ndege hiyo ya kivita ya kizazi cha nne ambayo inaweza kutekeleza majukumu mbalimbali ya mstari wa mbele ikiwa ni pamoja na kubebba silaha za nyuklia, na kuzuia makombora ya adui.
Iliundwa kuwa ndege ya gharama nafuu na nyepesi ambayo inaweza kushindana na ndege za Umoja wa Kisovieti kama MiG-29.
Sukhoi Su-27 Flanker
Tukirudi Urusi, tunamalizia orodha kwa kuangalia ndege ya kizazi cha nne ya enzi ya Usovieti, Sukhoi Su-27 Flanker. Hii ni ndege ya injini mbili ambayo iliundwa kukabiliana na ndege za Marekani kama vile F-14 Tomcat na F-15 Eagle.
Ina uwezo wa kufikia kasi ya takriban Mach 2.35, au maili 1,742 kwa saa. Ndege hiyo iliruka kwa mara ya kwanza mwaka 1977 na kuanza kufanya kazi mwaka 1985.
Kama ilivyo kwa ndege nyingi za zamani hizi, kumekuwa na aina nyingi za ndege aina ya Flanker zilizoanzishwa kwa miaka mingi. Hii inajumuisha ndege aina ya Su-27S Flanker-B yenye kiti kimoja, toleo la kwanza.
Aina nyingine ya kuvutia ni P-42, katika kipindi cha miaka miwili kuanzia 1986 hadi 1988, ndege hiyo ilivunja rekodi 27, ambazo baadhi yake zilikuwa zimeshikiliwa na F-15 Streak Eagle.
Ingawa ndege ya kawaida aina ya Su-27 Flanker huenda isijivunie rekodi za P-42, lakini bado ina kasi ya kutosha kuorodheshwa miongoni mwa ndege za kasi zaidi za Urusi na Usovieti .