Tetesi za soka Ulaya Jumatatu: Juventus wajiondoa katika mpango wa kumsajili Matinez

Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 3

Kipa wa Aston Villa na timu ya taifa ya Argentina, Emiliano Martinez (33), hatajiunga na Juventus msimu huu wa joto kama ilivyotarajiwa kufuatia mazungumzo kati ya klabu hizo. (Athletic - usajili unahitajika)

Manchester City ina nia ya kumsajili winga wa Ureno, Pedro Neto (26), kutoka Chelsea lakini klabu hiyo inakabiliwa na ushindani kutoka kwa Al-Hilal. (Talksport)

Kocha mpya wa Real Madrid, Jose Mourinho, ameridhia mpango wa kumsajili kiungo wa Uhispania na Arsenal, Martin Zubimendi (27). (Teamtalk)

Nottingham Forest imejiunga na kinyang'anyiro cha kumsajili Liam Delap kutoka klabu ya Chelsea, huku mshambuliaji huyo wa Uingereza mwenye umri wa miaka 23 akiwa na nia ya kusalia katika Ligi Kuu ya England. (Talksport)

Klabu ya Everton inaongoza katika mbio za kumsajili Delap, baada ya Chelsea kufahamishwa kwamba mchezaji huyo anaweza kuondoka klabuni hapo msimu huu wa joto. (Teamtalk)

Newcastle inajiandaa kuwasilisha ofa ya euro milioni 55 (pauni milioni 47) kumsajili mshambuliaji wa Villarreal raia wa Georgia, Georges Mikautadze (25), ambaye pia ananyatiwa na klabu ya Barcelona. (Fichajes - kwa Kihispania)

Mshambuliaji wa Nigeria, Victor Osimhen (27), hajatoa kaauli yoyote kuhusu uwezekano wake wa kuhama klabu ya Galatasaray msimu huu wa joto, huku Arsenal wakionyesha nia ya kumsajili. (Caught Offside)

Coventry City wako katika hatua za mwisho za kumsajili Sidiki Cherif kutoka Fenerbahce baada ya kufikia makubaliano kuhusu mshambuliaji huyo wa Guinea mwenye umri wa miaka 19. (Give Me Sport)

Everton ina hamu kubwa ya kumsajili kiungo wa Muingereza, Marcus Tavernier (27), kutoka Bournemouth kabla ya dirisha la usajili kufungwa. (Football Insider)

Mpango wa mshambuliaji wa Leeds United raia wa Suriname, Joel Piroe (27), kujiunga na West Ham United uko katika hatua za mwisho. (Voetbal International - kwa Kiholanzi)

Hull City wapo katika hatua za juu za mazungumzo ya dili la pauni milioni 21 kumsajili mshambuliaji wa Panathinaikos, Andreas Tetteh, huku klabu ya Roma nayo ikionyesha nia ya kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Ugiriki. (Ekrem Konur)

Kocha wa AC Milan, Ruben Amorim, amemwondoa Youssouf Fofana katika mipango yake ya msimu huu, huku Nottingham Forest na Crystal Palace sasa zikionyesha nia ya kumsajili kiungo huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 27. (Football Insider)

Atletico Madrid wanataka kuipiku Barcelona katika kumsajili kiungo wa Morocco, Azzedine Ounahi (26), ambaye klabu ya Girona inamthamini kwa takriban euro milioni 25 (pauni milioni 21.3). (Fichajes - kwa Kihispania)

Imetafsiriwa na Ambia Hirsi