Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za soka Ulaya: AC Milan inamtaka Bruno Fernandes
AC Milan inafuatilia hali ya kiungo wa Manchester United na timu ya taifa ya Ureno, Bruno Fernandes, mwenye umri wa miaka 32, ambaye bado hajafikia makubaliano ya kuongeza mkataba wake na klabu hiyo. (Corriere dello Sport)
Manchester United inajiandaa kushindana na Tottenham Hotspur kuwania saini ya mshambuliaji wa Freiburg na timu ya taifa ya Croatia, Igor Matanovic, mwenye umri wa miaka 23, anayekadiriwa kugharimu pauni milioni 50 katika dirisha la usajili la Januari. (Goal)
Kiungo wa Norway Martin Odegaard, 27, na mshambuliaji wa Ujerumani Kai Havertz, 27, wanakaribia kuingia katika miezi 18 ya mwisho ya mikataba yao na Arsenal, lakini klabu hiyo bado haijaanza mazungumzo na wachezaji hao kuhusu kuongeza mikataba yao. (Standard)
Trabzonspor imefufua nia ya kumsajili mshambuliaji wa Brazil, Richarlison, 29, huku Tottenham ikitarajia kupata ada ya uhamisho ya takriban pauni milioni 10 kwa ajili ya mchezaji huyo. (The i Paper)
Juventus inafanyia kazi mpango wa kumsajili moja kwa moja mshambuliaji wa Ujerumani, Nick Woltemade, 24, ambaye yuko klabuni hapo kwa mkopo kutoka Newcastle United. Juventus huenda ikajumuisha winga wa Ureno Francisco Conceicao, 23, katika makubaliano ya kubadilishana wachezaji hao. (Gazzetta dello Sport kupitia Goal)
Kiungo mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa ya England, Jack Grealish, 31, hayumo katika mipango ya usajili ya Celtic, licha ya klabu kadhaa kumfuatilia. Grealish, ambaye yuko Everton kwa mkopo kutoka Manchester City, anatarajiwa kumaliza mkataba wake na City mwishoni mwa msimu huu. (Football Insider)
Winga wa Nottingham Forest na timu ya taifa ya England, Callum Hudson-Odoi, 26, anatajwa kuwa miongoni mwa wachezaji wanaosakwa na Roma katika dirisha la usajili la Januari. (Teamtalk)
Beki wa Uruguay Ronald Araujo, 27, amesema bado ni mapema kufikiria kuhusu kugeuza uhamisho wake wa mkopo kutoka Barcelona kwenda Liverpool kuwa wa kudumu. (The Athletic)
Hata hivyo, Barcelona imeipa Liverpool ruhusa ya kukamilisha usajili wa Araujo kwa ada ya pauni milioni 47. (Mirror)
Mshambuliaji wa Tottenham, Mikey Moore, 19, anatarajiwa kubaki Cologne hadi mwisho wa msimu huu, kwa kuwa mkataba wake wa mkopo hauna kipengele kinachoiruhusu Tottenham kumrejesha mapema. (Talksport)
Tottenham imejiunga na Juventus, Como na Galatasaray katika kuhusishwa na kiungo na nahodha wa timu ya taifa ya Uturuki, Hakan Calhanoglu, 32, ambaye anaendelea na mazungumzo ya kuongeza mkataba wake na klabu yake ya sasa, Inter Milan. (Tuttomercato)