Maamuzi mabaya yalivyomgharimu Mkurugenzi wa Nvidia Jensen Huang

Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 5

Mwanamume huyu moja kati ya waanzilishi wa kampuni hiyo yenye mafanikio makubwa ya kutengeneza chipu za akili mnemba (AI), tangu hatua za mwanzo na kuiongoza wakati wa vipindi vigumu kwa ari isiyochoka na dhamira isiyoyumba, hatimaye alianguka kutokana na masuala ya maisha yake binafsi ya kimapenzi.

Ni simulizi ya kushangaza na, kwa namna fulani, ya kizamani kwa kampuni ya teknolojia inayojivunia kutazama mbele na kubuni mustakabali.

Tukio hilo lilizaa machapisho ya mtandaoni yenye mzaha huku nyingi zilizosambaa mtandaoni, zikimuonyesha Huang kama mwanaume aliyenaswa na kamera ya "kiss-cam" katika tamasha la Coldplay akiwa na mfanyakazi mwenzake ambaye ni 'mke wa mtu'.

Nyingine zilimuonyesha akiimba wimbo maarufu wa George Michael, Careless Whisper, unaozungumzia usaliti katika mahusiano.

Jambo la kushangaza ni kwamba mzaha huo kwa sehemu kubwa ulikuwa umetengenezwa kwa kutumia AI, teknolojia ambayo Huang mwenyewe alikuwa akisaidia kuiendeleza.

Nilikutana na viongozi wawili wa kampuni za teknolojia katika Silicon Valley na kuwauliza walikuwa wanachukuliaje matukio ya sasa; walijibu kwa neno moja tu: "meme".

Hata hivyo, hawakuamini kwamba Huang angelazimika kujiuzulu kutokana na madai ya kuwa na uhusiano wa kimapenzi nje ya ndoa.

Kwa mtazamo wao, kilichokuwa hatarini kilikuwa kikubwa mno.

Walisema kuwa sekta nzima ya akili mnemba (AI) iliitegemea sana Nvidia na chipu zake kiasi kwamba ilikuwa vigumu kuhoji au kubadilisha mfumo ambao ulikuwa ukiendelea kuleta mafanikio makubwa.

Kwa maneno mengine, waliamini kwamba mchango wa Huang kwa Nvidia na sekta ya AI ulikuwa mkubwa sana kiasi kwamba haikuonekana rahisi kwake kuondolewa kutokana na kashfa ya maisha yake binafsi.

Kwa maneno mengine, Silicon Valley ilikuwa upande wake.

Lakini hiyo ilikuwa kabla ya uvumi kuhusu uhusiano mwingine wa kimapenzi kusambaa, safari hii ukihusisha mfanyakazi mwenzake, na bodi ya kampuni ikaamua kwamba sasa alivuka mipaka.

Ghafla, tabia yake ilianza kuonekana kwa mtazamo tofauti.

Badala ya kuonekana kama kiongozi shupavu na mwenye maono pekee, alionekana kama mtu anayoweza kufanya maamuzi mabaya na kisha kufanya siri.

Kwa wengi, suala hilo halikuhusu tu maisha yake binafsi.

Liliibua maswali kuhusu uwezo wake wa kufanya maamuzi sahihi na uadilifu wake kama kiongozi wa moja ya kampuni muhimu zaidi katika sekta ya akili mnemba duniani.

Muda mrefu wa kazi na ushindani

Huang daima alihakikisha anajitofautisha na wengine.

Wakati wa masharti y akipindi cha janga la Covid-19, alikuwa akitoa hotuba za uzinduzi wa matukio ya kampuni moja kwa moja kutoka jikoni kwake.

Video hizo zilivuta hisia nyingi mtandaoni, na baadaye ilibainika kuwa sehemu ya mazingira yaliyoonekana kwenye matangazo hayo yalikuwa yametengenezwa kwa teknolojia ya AI.

Mara chache Huang huonekana bila kuvaa jaketi lake la ngozi, ambalo limekuwa sehemu ya utambulisho wake.

Wakati mmoja alitania kwamba alikuwa na suti moja tu na hata alilazimika kukopa tai kutoka kwa mchumba wa binti yake.

Kutokana na mafanikio yake, Huang alizunguka kwa watu wenye ushawishi mkubwa duniani, akifahamiana na viongozi na wafanyabiashara maarufu kama Donald Trump, Elon Musk na King Charles.

Mara ya mwisho mwandishi wa makala haya alipomwona ilikuwa mwaka jana katika Kasri la St James's, ambako Huang alikuwa akipokea tuzo maarufu ya Malkia ya Uhandisi.

Ingawa waandishi wa habari walikuwa wameambiwa kwamba hangezungumza nao, Huang aliwasogelea mwenyewe na kufanya mazungumzo ya takribani dakika kumi.

Alizungumza kwa ufasaha na kwa matumaini makubwa kuhusu maendeleo ya AI na nafasi ya Uingereza katika sekta hiyo.

Kwa watu wengi, Huang alikuwa sura na nembo ya Nvidia yenyewe. Alisimamia moja kwa moja mamia ya wafanyakazi, takribani 200.

Pia alijulikana kwa kutarajia viwango vya juu vya utendaji. Katika kitabu The Nvidia Way, mwandishi Tae Kim anasema muda wa kufanya kazi ndani ya kampuni ulikuwa mrefu na mazingira ya kazi yalikuwa ya ushindani mkubwa.

Maoni ya Huang mara nyingi yalikuwa ya moja kwa moja na makali.

Hakusita kukosoa makosa ya wafanyakazi hadharani wakati wa mikutano mikubwa ya kampuni.

Sasa, hata hivyo, ni mapungufu yake mwenyewe ambayo yako wazi kwa kila mtu.

Na kwa wengi, hali hiyo imesababisha kile kinachoonekana kama mwisho mgumu na wa ghafla wa moja ya taaluma zilizokuwa na ushawishi mkubwa zaidi katika sekta ya teknolojia.

Nvidia bila Huang

Amefanya kazi Nvidia kwa miaka 13, na kwa wale wanaofuatilia kwa karibu mafanikio ya kifedha ya kampuni hiyo, mara nyingi huonekana kwenye mikutano ya kutangaza matokeo ya biashara kwa wawekezaji.

Yeye mwenyewe ni bilionea na mmoja wa viongozi wanawake wenye ushawishi mkubwa katika sekta ya teknolojia.

Hata hivyo, Kress si mhandisi, ilhali bidhaa za Nvidia zinategemea teknolojia za hali ya juu na maarifa ya kina ya kiufundi.

Sasa atapaswa kuwahakikishia wawekezaji kwamba biashara ya Nvidia itaendelea kama kawaida, kwamba ubunifu ulioifanya kampuni hiyo kuwa maarufu hautapungua, na kwamba vipaji bora havitaondoka pamoja na Huang.

Hali yoyote ya kutokuwa na uhakika ndani ya Nvidia inaweza kuwa habari mbaya kwa sekta nzima ya akili mnemba (AI), kwa kuwa chipu zake zinazoendelea kuboreshwa ndizo zinazoendesha mifumo mingi yenye nguvu zaidi ya AI duniani.

Kuhusu Huang mwenyewe, kwa sasa inadhaniwa kuwa uchunguzi kuhusu uhusiano wake na mwanamke aliyeshutumiwa kuwa jasusi wa China utaendelea.

Matokeo ya uchunguzi huo huenda yakawa na mchango mkubwa katika kuamua hatua zake zinazofuata.

Licha ya utata unaomzunguka, huenda Huang asikose ofa za kazi.

Kwa kweli, washindani wa Nvidia wanaweza kuwa bado wanaamini kwa shida kwamba mmoja wa wapinzani wao wakubwa ameondoka kwenye uwanja wa ushindani.

Elon Musk tayari amesema kwamba itakuwa "heshima" kufanya kazi naye katika kampuni ya SpaceX.

Hata hivyo, ni muhimu kukumbuka kwamba hata kama itabainika kuwa Huang hakuisaliti kampuni yake wala nchi yake, bado alimsaliti mke wake, Lori Huang, baada ya miaka 41 ya ndoa.

Na kwa Lori, suala hili halihusu teknolojia, mvuto wa umaarufu au kampuni zenye thamani ya mabilioni ya dola.

Ni suala la kibinafsi, lenye maumivu na athari zake katika maisha ya watu halisi.