Moja kwa moja, Kundi la Houthi, Ansar Allah, latangaza kwamba lililenga uwanja wa ndege wa Riyadh kwa mara ya pili leo
Kundi la Houthi Ansar Allah limetangaza kwamba lililenga uwanja wa ndege wa Riyadh katika mji mkuu wa Saudi Arabia kwa kombora la balestiki siku ya Alhamisi alasiri, huku mabalozi wakiagizwa kujificha.
Muhtasari
Polisi yaafiki kuwa upekuzi wa nyumba za Mwanamfalme Andrew ulikuwa kinyume cha sheria, mahakama yaambiwa
Uchunguzi wabaini kuwa madada watatu waliozama baharini nchini Uingereza walijiua
Polisi yaafiki kuwa upekuzi wa nyumba za Mwanamfalme Andrew ulikuwa kinyume cha sheria, mahakama yaambiwa
Chanzo cha picha, Reuters
Polisi katika kituo cha Valley Thames wamekubali kwamba
vibali vya upekuzi vilivyotumika kupekua nyumba za Andrew Mountbatten-Windsor
mapema mwaka huu vilikuwa kinyume cha sheria, Mahakama Kuu imesikia.
Imesema imekubali
"uamuzi wa mahakama ya awali wa kutoa vibali chini ya sheria maalum
iliyotumika haukuwa sahihi" walipopewa ruhusa ya kupekua mali za
mwanamfalme huyo wa zamani mnamo tarehe 19 Februari.
Andrew alikamatwa na Polisi wa Thames Valley kwa tuhuma za
utovu wa nidhamu katika ofisi ya umma. Anakana makosa yoyote.
Hati hizo zilitolewa kabla ya kukamatwa kwake na mawakili
wake wanapinga uhalali wake.
Kukamatwa kwake mwezi
Februari kuliibuka baada ya Idara ya Sheria ya Marekani kuchapisha nyaraka
zilizodokeza kwamba alikuwa ametuma taarifa za siri kwa mhalifu wa kingono aliyehukumiwa wakati
Mountbatten-Windsor alipokuwa mjumbe wa biashara wa Uingereza mwaka 2010.
Amekuwa akikanusha mara kwa mara makosa yoyote kuhusiana na
Epstein.
Uchunguzi wabaini kuwa madada watatu waliozama baharini nchini Uingereza walijiua
Chanzo cha picha, Sussex Police
Maelezo ya picha, Dada hao watatu, walioonyeshwa hapa wakiwa na baba yao, walifariki baharini. Kuanzia kushoto kwenda kulia, Jane Adetoro, Joseph, Christina Walters na Rebecca Walters
Madada watatu waliozama baharini karibu na Brighton nchini Uingereza walijiua, mchunguzi wa vifo amethibitisha.
Jane Adetoro, 36, Christina Walters, 32, na Rebecca Walters, 31, walikuwa wakiishi "maisha ya faragha sana" kufuatia kifo cha mama yao, ambaye alizama majini mwaka wa 2010, mchunguzi mkuu wa vifo Penelope Schofield alisema.
Mnamo tarehe 11 Mei, wanawake hao ambao wote walikuwa wakiishi pamoja huko Greenford, London walitembelea eneo la Birmingham karibu na mahali ambapo mama yao alifariki kabla ya kusafiri siku iliyofuata hadi ufukweni mwa Brighton, ambapo walizama katika hali mbaya ya baharini mapema asubuhi tarehe 13 Mei mwaka huu. Mchunguzi wa vifo alisema hawakuweza kuogelea.
Baba yao Joseph Jacobsen alisema lilikuwa jambo la kuhuzunisha kuwapoteza "binti zangu wote watatu wapendwa".
Alikuwa miongoni mwa wanafamilia waliofuatilia kesi hiyo kupitia video.
Katika taarifa ya hisia iliyosomwa kwa niaba yake, alisema aliwaona binti zake wakikua kutoka wasichana wadogo hadi wanawake warembo na werevu "wenye nafasi maalum moyoni mwangu".
Alisema: "Hakuna maneno yanayoweza kuelezea vya kutosha uchungu wa kufiwa na mtoto."
"Kuwapoteza binti zangu wote watatu wapendwa ni huzuni kubwa kuliko kitu chochote ambacho ningeweza kufikiria."
Hakuweza kuelewa ni kwa nini maisha ya binti zake yaliisha ghafla hivyo, na alitumaini kwamba wangeungana tena na mama yao "katika maisha ya milele ya uangalizi wa Mungu", aliongeza.
Kundi la Houthi, Ansar Allah, latangaza kwamba lililenga uwanja wa ndege wa Riyadh kwa mara ya pili leo
Chanzo cha picha, Getty Images
Kundi la Houthi Ansar Allah limetangaza kwamba lililenga uwanja wa ndege wa Riyadh katika mji mkuu wa Saudi Arabia kwa kombora la balestiki siku ya Alhamisi alasiri, katika shambulio la pili lililodaiwa na kundi hilo dhidi ya uwanja wa ndege wa Riyadh ndani ya saa chache.
Msemaji wa jeshi la Houthi Yahya Saree alisema kupitia Telegram: "Vikosi vyetu vya kijeshi viliweza kulenga Uwanja wa Ndege wa King Khalid huko Riyadh kwa kombora la balestiki alasiri ya leo, na vilifanikiwa kulenga shabaha yake, na kusababisha uharibifu na kuvuruga trafiki ya anga kwenye uwanja huo."
Awali milipuko kadhaa ilisikika katika mji mkuu wa Saudi Arabia, Riyadh, siku ya Alhamisi, huku wanadiplomasia wakiripoti kuagizwa kujificha ndani ya balozi zao, huku mvutano ukiongezeka kati ya Saudi Arabia na kundi la Wahouthi Ansar Allah nchini Yemen, kulingana na AFP.
Wakazi waliambia shirika hilo kwamba shule za kimataifa zimechukua hatua za tahadhari, huku angalau mtoto mmoja akimpeleka kwenye chumba cha chini kwa ajili ya usalama wao. Watu wawili wanaofanya kazi katika Wilaya ya Fedha ya King Abdullah pia waliripoti kwamba baadhi ya makampuni yamehama ofisi zao.
Chanzo cha milipuko hiyo na maeneo yaliyoathiriwa bado hakijabainika.
Kundi la Wahothi la Ansar Allah, lilitangaza mapema Alhamisi kwamba lilikuwa limelenga Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mfalme Khalid huko Riyadh kwa kombora la balestiki, likidai lililenga shabaha yake na kuvuruga shughuli za uwanja wa ndege. Hakukuwa na uthibitisho wa haraka kutoka Saudi Arabia kuhusu dai hili.
Msemaji wa jeshi la kundi hilo, Yahya Saree, alitoa onyo jipya kwa mashirika ya ndege ya kimataifa dhidi ya kutumia anga ya Saudia, akisema kwamba alikuwa anatoa onyo hilo "kwa mara ya mwisho".
Hii ilikuja baada ya mamlaka ya Saudi Arabia kutangaza kwamba watu watatu waliuawa na wengine 36 kujeruhiwa katika mashambulizi yaliyolenga viwanja vya ndege vya Mfalme Khalid na Abha siku ya Jumanne na Jumatano, huku muungano unaoongozwa na Saudi Arabia ukisema ulijibu mashambulizi kwa kushambulia maeneo 82 ya kijeshi ya kundi hilo nchini Yemen.
Araqchi: Uharibifu wa vifaa vya kijeshi vya Marekani ni mkubwa zaidi kuliko takwimu rasmi
Chanzo cha picha, AFP via Getty Images
Maelezo ya picha, Araqchi
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araqchi, anasema
kiwango halisi cha uharibifu wa vifaa vya kijeshi vya Marekani ni kikubwa zaidi
kuliko takwimu zilizotangazwa.
"Mnamo mwezi Mei, Huduma ya Utafiti ya Bunge la
Marekani ilikiri kuwa vikosi vya jeshi la Iran vilikuwa vimeharibu ndege 42 za
kijeshi za Marekani. Sasa, idadi hiyo imepanda hadi 81," aliandika katika
ujumbe kwenye mtandao wa kijamii wa X.
Bw. Araghchi aliendelea kusema: "Ushahidi? Kamandi Kuu
ya Marekani (CENTCOM) hairuhusu hata seneta wa Bunge kutembelea na kukagua
kambi ambazo inadai kuwa ziko katika hali ya kawaida kabisa."
Abbas Araqchi aliongeza katika ujumbe wake: "Watu
hawawezi 'kudanganywa' milele kuhusu suala hili."
Pete Hegseth atembelea meli ya kubeba ndege ya Abraham Lincoln - kunani?
Chanzo cha picha, Reuters
Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Pete Hegsett, amewapongeza wanajeshi wa meli kubwa ya kubeba ndege za kivita ambayo muda wake wa doria uliongezwa wakati wa mvutano na Iran, jambo lililozua wasiwasi kuhusu hali ya wafanyakazi hao.
Meli hiyo, Abraham Lincoln, ilikaa zaidi ya miezi nane bila kutia nanga bandarini, huku kukiwa na ripoti za kushuka kwa morali, uhaba wa vifaa, na visa vya watu kujaribu kujiua.
Akiwa katika ziara yake kwenye meli hiyo, Bw. Hegsett aliishutumu vyombo vya habari kwa kujaribu kuwafanya wanajeshi hao kuwa alama ya operesheni iliyofeli. Alisema kuwa wafanyakazi hao walionyesha ushujaa wa kipekee.
Hegsett alisema kuwa licha ya kasi kubwa ya shughuli za kivita, kikosi hicho hakikupata maafa yoyote wala kuhusika katika ajali za ndege.
Meli hiyo inatarajiwa kuwasili katika bandari ya San Diego, kwenye Pwani ya Magharibi ya Marekani, baadaye wiki hii.
Vyombo vya habari vya Marekani: Pentagon inajiandaa kuanza upya operesheni kubwa ya kijeshi dhidi ya Iran
Chanzo cha picha, Reuters
Vyombo viwili vya habari vya Marekani vimeripoti kuwa
Pentagon inajiandaa kwa uwezekano wa shambulio jipya dhidi ya Iran katika siku
zijazo.
Tovuti ya habari ya Axios, ikinukuu maafisa wa Marekani,
iliripoti kuwa katika siku za hivi karibuni, Pentagon ilitoa agizo kwa CENTCOM
(Kamandi Kuu ya Marekani katika Mashariki ya Kati) kukamilisha maandalizi yake
ya kuanza upya operesheni kubwa za kijeshi dhidi ya Iran.
Jarida la The Atlantic pia liliripoti katika taarifa ya
kipekee, likinukuu maafisa wawili wa Marekani, kwamba Ikulu ya Marekani (White
House) imeitaka Pentagon kuandaa chaguzi za kushambulia maeneo muhimu ya Iran
ambazo zinaweza kutekelezwa kabla ya uchaguzi wa katikati ya muhula.
Kulingana na The Atlantic, Donald Trump ana hamu kubwa ya
kushusha bei ya mafuta na kupata maendeleo makubwa katika mzozo na Iran kabla
ya uchaguzi huo.
Kwa mujibu wa Axios, agizo hilo la Pentagon halikutaja
tarehe mahususi ya kuanza kwa mashambulio hayo, na Donald Trump bado hajafanya
uamuzi wa mwisho.
Hata hivyo, vyanzo vya Marekani na Israel vimeiambia Axios
kuwa hatua hiyo inaweza kuchukuliwa kabla ya uchaguzi wa katikati ya muhula wa
Marekani na huenda kabla ya uchaguzi wa Israel, ambao hufanyika wiki moja
mapema.
Uchaguzi wa katikati ya muhula wa Marekani utafanyika chini
ya mwezi mmoja ujao, tarehe 3 Novemba.
Syria yatathmini uwezekano wa kuisaidia Saudi Arabia kijeshi dhidi ya Wahouthi
Chanzo cha picha, Getty Images
Syria kwa sasa inachunguza kwa makini uwezekano wa kutoa msaada wa kijeshi kwa mshirika wake mkuu, Saudi Arabia, huku vita dhidi ya Wahouthi wanaoungwa mkono na Iran nchini Yemen vikiendelea kushamiri.
Kwa mujibu wa taarifa zilizochapishwa na shirika la habari la Reuters, likinukuu afisa wa Marekani pamoja na afisa wa jeshi la Syria mwenye ufahamu wa suala hilo, chaguzi za kutuma wanajeshi Syria nchini Yemen bado zinajadiliwa.
Vyanzo hivyo vimesema kuwa miongoni mwa chaguzi zinazozingatiwa ni kutoa msaada wa kujihami ili kuisaidia Saudi Arabia kujilinda dhidi ya mashambulizi.
Pia kutuma vikosi vyenye uwezo wa kushiriki katika operesheni za mashambulizi ili kusaidia vikosi vya Yemen vinavyoungwa mkono na Saudi Arabia katika mapambano dhidi ya Wahouthi.
Ripoti hiyo inaashiria uwezekano wa kuongezeka kwa ushiriki wa Syria katika mzozo wa Yemen iwapo uamuzi wa mwisho wa kutuma vikosi utapitishwa.
Taarifa kama hizo pia ziliripotiwa na tovuti ya habari ya Marekani Axios, ambayo ilisema kuwa mipango hiyo bado iko katika hatua ya tathini na haijathibitishwa rasmi na mamlaka za Syria au Saudi Arabia.
Ikiwa hatua hiyo itatekelezwa, inaweza kuashiria mabadiliko muhimu katika ushirikiano wa kijeshi wa kikanda na kuongeza shinikizo dhidi ya kundi la Wahouthi katika vita vinavyoendelea nchini Yemen.
Wanamgambo wa Houthi wasema wameshambulia uwanja wa ndege wa Riyadh
Chanzo cha picha, AFP via Getty Images
Kundi la Houthi (Ansar Allah) limesema limeshambulia Uwanja wa Ndege wa Riyadh kwa kombora la balistiki
Kundi la Houthi la Ansar Allah lilitangaza Alhamisi kuwa limelenga Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa King Khalid katika mji mkuu wa Saudi Arabia, Riyadh, kwa kutumia kombora la balistiki.
Tangazo hilo limetolewa saa chache baada ya mamlaka za Saudi Arabia kuripoti kuwa mtu mmoja aliuawa katika shambulio lililolenga uwanja huo wa ndege mapema wiki hii.
Hadi sasa, Saudi Arabia haijathibitisha mara moja madai ya Wahouthi kuhusu shambulio hilo jipya.
Wakati huo huo, vyombo vya habari vya Yemen viliripoti kuwa Vikosi vya Homeland Shield, Giants Brigades, na Joint Forces vimedhibiti kikamilifu eneo la mapambano la Kahbub Front mapema Alhamisi asubuhi.
Tetesi za soka Jumatano: Manchester United, Liverpool zamuwania Truffert
Chanzo cha picha, Getty Images
Manchester
United wanatarajiwa kupata ushindani mkali kutoka kwa Liverpool katika mbio za
kumsajili beki wa kushoto wa Bournemouth na timu ya taifa ya Ufaransa, Adrien
Truffert (24), ambaye thamani yake inakadiriwa kuwa pauni milioni 60.
Mlinzi wa Brazil na Athletico Paranaense, Arthur Dias (19), anafuatiliwa na Barcelona baada ya
hapo awali kuvutia ofa ya pauni milioni 18 kutoka Tottenham Hotspur.
Newcastle
United wanaonekana kuwa mbele ya Nottingham Forest katika harakati za kumsajili
kiungo wa Lyon, Tyler Morton (23). Morton ameonesha kiwango kizuri nchini
Ufaransa tangu alipoondoka Liverpool mwaka uliopita.
Liverpool, Chelsea
na Arsenal wote wanafuatilia maendeleo ya beki wa England Jarell Quansah (23),
ambaye anaendelea kung'ara akiwa na Bayer Leverkusen.
Nahodha wa Arsenal,
Martin Odegaard (27), anatarajiwa kufuata nyayo za kocha Mikel Arteta kwa
kusaini mkataba mpya wa muda mrefu katika Uwanja wa Emirates.
Arsenal wako
tayari kufanya jaribio jipya la kumsajili mshambuliaji wa Atletico Madrid na
Argentina, Julian Alvarez (26), mwezi Januari.
Inaelezwa kuwa mchezaji huyo
sasa anafikiria kwa umakini uwezekano wa kuhamia klabu hiyo ya London
Kaskazini.
Beki wa zamani
wa Real Madrid, Dani Carvajal (34), bado hana klabu baada ya mpango wake wa
kujiunga na Getafe kuvunjika.
Vigogo wa
Bundesliga, Bayern Munich na Borussia Dortmund, wanamuwania chipukizi wa Tottenham
Hotspur, Luca Williams-Barnett, ambaye aliichezea Spurs kwa mara ya kwanza
akiwa na umri wa miaka 16.
Trump kuzungumza na Putin kuhusu kifo cha mfanyakazi wa maabara ya tauni nchini Urusi
Chanzo cha picha, AFP via Getty Images
Maelezo ya picha, Mwathiriwa huyo alikuwa akifanya kazi katika Taasisi ya Kupambana na Tauni (Anti-Plague Institute) iliyoko katika mji wa Irkutsk, Siberia.
Rais wa Marekani Donald Trump amesema amepanga kufanya mazungumzo ya simu na Vladimir Putin kuhusu kifo cha mfanyakazi wa maabara katika kituo cha utafiti wa tauni nchini Siberia.
Maafisa wa Urusi wamesema wanafanya uchunguzi kuhusu kifo cha mfanyakazi huyo mwenye umri wa miaka 28, lakini bado hawajathibitisha kwamba ugonjwa unaoshukiwa ni tauni ya mapafu. Pia wamesisitiza kuwa hakuna hatari ya kutokea kwa mlipuko wa ugonjwa huo.
Akizungumza na waandishi wa habari Jumatano jioni, Trump alisema haamini kwamba tukio hilo linahusiana na silaha ya kibaolojia, akiongeza kuwa: "Tutafahamu ukweli hivi karibuni, lakini kwa sasa hatufikiri hivyo."
"Ukiwasikiliza wao, hali iko chini ya udhibiti," alisema akimaanisha mamlaka za Urusi."Tunatumaini kweli iko hivyo," aliongeza.
Ripoti zilizojitokeza Ijumaa zilisema karibu watu 200 wamewekwa chini ya uangalizi wa kiafya baada ya kifo hicho.
Akirejelea mwitikio wa awali wa China wakati wa janga la Covid-19, Trump alisema: "China haikusema mengi, na Urusi pia haisemi mengi. Lakini wanasema wana hali hiyo chini ya udhibiti mkubwa."
Tauni ya mapafu ni maambukizi makali ya mapafu yanayochukuliwa kuwa aina hatari zaidi ya ugonjwa wa tauni kutokana na uwezo wake mkubwa wa kusambaa na kusababisha vifo iwapo hautatibiwa mapema.
Trump alisema Marekani iko katika "mazungumzo ya kina" na Urusi kuhusu suala hilo. Hata hivyo, msemaji wa Kremlin, Dmitry Peskov, amesema hakuna mazungumzo ya simu yaliyopangwa kati ya Trump na Putin.
Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) ameitaka Urusi kuwa wazi zaidi na kutoa taarifa za ziada kuhusu vipimo vya maabara vilivyofanywa kwa mtu aliyefariki dunia.
"Hatujapata bado taswira kamili ya tukio hili," alisema Tedros Adhanom Ghebreyesus, akiongeza kuwa WHO pia inatafuta "uthibitisho wa ripoti za vyombo vya habari kuhusu mfanyakazi wa pili mwenye homa ya mapafu yenye chanzo kisichojulikana."
Ghebreyesus aliiomba Urusi kutoa "taarifa kwa wakati, kamili na za uwazi" ili kufafanua "taarifa zinazokinzana" na kusaidia WHO kutathmini hatari zinazoweza kujitokeza kwa afya ya umma.
Wahitimu 20 waokolewa baada ya kutekwa nyara Nigeria
Chanzo cha picha, Reuters
Kundi la vijana 20 waliotekwa nyara kusini mashariki mwa Nigeria wiki iliyopita wameokolewa, polisi wamesema.
Wahitimu hao walitekwa nyara tarehe 1 Oktoba walipokuwa wakisafiri kwenda kushiriki mpango wa kitaifa wa huduma kwa jamii katika majimbo ya Abia na Akwa Ibom, kusini mwa nchi hiyo.
Walifanikiwa kuokolewa na polisi kwa ushirikiano na vyombo vingine vya usalama.
Msemaji wa polisi, Ani Iniedu, alisema katika taarifa iliyotolewa Jumatano kwamba kundi hilo liliokolewa katika eneo la Amakohia Ubi, jimbo la Imo, baada ya operesheni endelevu ya utafutaji na uokoaji.
Vijana hao kwa sasa wanapatiwa huduma na wamepelekwa kufanyiwa uchunguzi wa afya ili kutathmini hali zao baada ya kuokolewa.
Polisi, jeshi na vyombo vingine vya usalama vilifanya misako katika misitu na maficho yanayoshukiwa kutumiwa na wahalifu kwa kutumia taarifa za kiintelijensia, alisema. Hata hivyo, hakueleza iwapo fidia yoyote ililipwa au kama kuna watu waliokamatwa.
Kundi hilo la vijana lilikuwa linashiriki katika mpango wa National Youth Service Corps (NYSC), ambao ni programu ya lazima ya huduma kwa jamii ya mwaka mmoja kwa wahitimu wengi wa vyuo vikuu nchini Nigeria. Washiriki hupangiwa kuhudumu katika maeneo mbalimbali ya nchi.
Vijana hao walikuwa wakisafiri katika mabasi mawili kwenye barabara kuu kutoka Ibadan, kusini-magharibi mwa jimbo la Oyo, kuelekea kambi za mafunzo ya awali ya NYSC katika majimbo ya Abia na Akwa Ibom, wakati watu wenye silaha walipoyashambulia mabasi hayo.
Wanajeshi wa Eritrea waingia Tigray huku mapigano yakizidi kupamba moto
Chanzo cha picha, AFP via Getty Images
Maelezo ya picha, Wanajeshi wa Eritrea walishiriki katika mapigano ya Tigray wakati wa vita vya mwaka 2020 hadi 2022.
Wanajeshi wa Eritrea
wameingia kaskazini mwa Ethiopia wakielekea eneo la Tigray, ambako mapigano
makali yameripotiwa kati ya jeshi la serikali na vikosi vya kikanda, kwa mujibu
wa wakazi wa mji wa Adigrat waliozungumza na BBC.
Mapigano hayo yalianza
wiki mbili zilizopita baada ya miezi kadhaa ya mvutano kati ya serikali ya
Ethiopia na Chama cha Ukombozi wa Watu wa Tigray (TPLF), kinachodhibiti eneo
hilo. Pande zote mbili zinatuhumiana kwa kukiuka makubaliano ya mwaka 2022 yaliyomaliza
vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miaka miwili.
Serikali ya Ethiopia
pia imeishutumu Eritrea kwa kuiunga mkono TPLF, tuhuma ambazo Asmara imekuwa
ikizikanusha.
Mivutano ya sasa
imeongezeka wiki chache baada ya kuundwa mwezi Septemba kwa muungano mpya wa
makundi yenye silaha nchini Ethiopia, ambao unajumuisha TPLF.
Mwishoni mwa juma,
vikosi vya TPLF viliondoka Mekelle, mji mkuu wa Tigray ulioko takriban kilomita
115 kusini mwa Adigrat, na kuiacha chini ya udhibiti wa jeshi.
Eritrea ilikuwa
mshirika muhimu wa Ethiopia katika vita vya mwaka 2020 hadi 2022 dhidi ya TPLF.
Mzozo huo ulikuwa miongoni mwa migogoro iliyosababisha vifo vingi zaidi katika
karne hii na uliisukuma Tigray kwenye hatari kubwa ya njaa.
Hata hivyo, uhusiano
kati ya nchi hizo mbili jirani umezorota tangu kumalizika kwa vita hivyo, hasa
kutokana na azma ya Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed, ya kupata ufikiaji wa
moja kwa moja wa bandari za Eritrea katika Bahari ya Shamu.
Texas yatekeleza hukumu ya kwanza ya kifo tangu hukumu ya Christa Pike kushindikana
Chanzo cha picha, Getty Images
Jamaal Howard, mfungwa aliyekuwa akisubiri hukumu ya
kifo, aliuawa kwa sindano ya sumu huko Texas siku ya Jumatano.
Alikuwa na umri wa miaka 46.
Alipatikana na hatia ya kumuua mfanyakazi wa duka mwaka 2000 wakati wa tukio la wizi.
Baada ya Christa Pike kunusurika
jaribio la kuuawa kwa sindano wiki iliyopita, mawakili wa Howard waliomba
hukumu dhidi yake isimamishwe.
Walisema kulikuwa na hatari kwa
sababu Texas ilipanga kutumia dawa ileile, pentobarbital, iliyotumika
kwa Pike.
Mahakama Kuu ya
Marekani zilikataa maombi yao.
"Texas haipaswi kuwa na haraka ya kufuata nyayo za Tennessee; kusitishwa kwa utekelezaji wa hukumu hiyo kungezuia jambo hilo kutokea," mawakili wa Howard walikuwa wamehoji, kwa mujibu wa CBS.
Mawakili wa Howard pia walimwomba Gavana wa Texas, Greg Abbott, ambaye ni Mwanachama wa Chama cha Republican, kuahirisha utekelezaji wa hukumu hiyo kwa siku 30 ili waweze kutafuta taarifa zaidi kuhusu dawa iliyopangwa kutumika katika utekelezaji huo. Hata hivyo, gavana hakukubali ombi hilo la kuahirisha hukumu.
Hatimaye, Howard alipewa sindano
hiyo na akafariki saa 20:03 kwa saa za huko Texas.
Pike alikuwa "mwenye hasira na kuchanganyikiwa" baada ya kuamka, mawakili wake wasema
Chanzo cha picha, Tennessee Department of Corrections
Wakili wa Christa Pike, muuaji aliyetiwa hatiani, amesema kwamba aliamka hospitalini akiwa “amekasirika na kuchanganyikiwa” baada ya jaribio la kumtekeleza hukumu ya kifo kushindikana wiki iliyopita.
Maneno yake ya kwanza yalikuwa kuuliza, “Niko wapi?” na “Wewe ni nani?”, kwa mujibu wa wakili wake, Randy Spivey, aliyesema hayo katika mkutano na waandishi wa habari.
Pike, ambaye alihukumiwa kifo baada ya kumuua Colleen Slemmer pamoja na mpenzi wake wa wakati huo mwaka 1995, alinusurika baada ya majaribio mawili ya kumpa sindano ya sumu kwa ajili ya kutekeleza hukumu hiyo mnamo tarehe 30 Septemba katika jimbo la Tennessee.
Wataalamu na timu yake ya kisheria wanasema kupona kwake kunaonekana kuwa jambo lisilo la kawaida sana, na kwamba hakuna mfungwa mwingine nchini Marekani anayejulikana kuwa amenusurika baada ya sindano ya sumu kutumika katika utekelezaji wa hukumu ya kifo.
Mahakama siku ya Jumatano iliagiza jimbo la Tennessee kuhifadhi ushahidi wote unaohusiana na jaribio hilo la utekelezaji wa hukumu ya kifo lililoshindikana.
Pike, mwenye umri wa miaka 50, bado anapata matibabu ya muhimu hospitalini na anafungwa mikono na miguu akiwa kitandani, kulingana na mawakili wake waliotoa taarifa baada ya kusikilizwa kwa kesi mahakamani siku ya Jumatano.
Spivey alisema kuwa timu yake ya kisheria iliamini kwa siku kadhaa kwamba Pike alikuwa amepatwa na kifo cha ubongo, na walitarajia kwamba angeondolewa kwenye mashine za kumsaidia kupumua wakati wowote.
Hata hivyo, katika tukio ambalo Spivey aliliita “mshtuko kwa kila mtu”, Pike alianza kuzungumza siku ya Jumanne, ingawa anakumbuka kwa kiasi kidogo tu yaliyotokea wakati wa jaribio hilo la kutekeleza hukumu ya kifo.