Ronaldo ana cha kuthibitisha?, Ureno dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (18:00 BST)
Mjadala umeendelea kwa miaka mingi kuhusu kama Ureno ingenufaika zaidi bila uwepo wa Cristiano Ronaldo lakini inaonekana hakuna hatari ya karibu ya nyota huyo wa kimataifa mwenye umri wa miaka 41 kupoteza nafasi yake katika kikosi cha kwanza.
Kocha mkuu wa Ureno Roberto Martinez hapo awali amepuuza mazungumzo kuhusu Ronaldo kama "amebebwa", akionyesha rekodi ya nahodha huyo ya mabao 25 katika mechi zake 32 zilizopita. Haijalishi kwamba mengi ya mabao hayo yalitokana na timu zilizo nje ya nafasi ya 30 bora katika viwango vya Fifa.
Ronaldo ndiye mchezaji mwenye rekodi ya dunia kwa wanaume kwa mechi na mabao mengi. Kwa kiasi kikubwa, Ronaldo anapimwa kwa mabao, na amecheza mechi tisa bila bao katika mashindano makubwa.