Trump aahidi 'pigo kali sana' dhidi ya Iran iwapo itathibitika kuhusika na tukio la flydubai

Rais wa Marekani Donald Trump ameapa kuipiga Iran "pigo kali sana" ikiwa itathibitishwa kuwa ilihusika katika shambulio dhidi ya rubani wa shirika la ndege la flydubai.

Muhtasari

Ruka Video uendelee
  • Wicknell Chivayo
  • Kijanangoma
  • xx
  • Besigye
  • .
  • xx
  • xx
  • xx
  • Lungu
  • xx
  • xx
  • d
  • s
  • a
  • Sonko
  • xx
  • xx
  • xx
  • xx

Moja kwa moja

Na Asha Juma

  1. Mkurugenzi wa zamani wa Umoja wa Mataifa aliyepinga njaa ya Gaza alaani kufutwa

    Gaza

    Aliyekuwa afisa mwandamizi wa shirika la chakula la Umoja wa Mataifa amesema amewasilisha rufaa kupinga kufutwa kazi kwake, akidai kuwa hatua hiyo ilichochewa na msimamo wake kuhusu njaa inayoendelea Gaza, Reuters imeripoti.

    Benjamin Davis, mwenye umri wa miaka 62, raia wa Marekani na Hispania ambaye alikuwa mkurugenzi katika Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), alisema kufutwa kwake kazi kulihusishwa na maoni yake kuhusu hali ya kibinadamu katika Gaza.

    Kwa mujibu wa nyaraka zilizoonwa na Reuters, Davis aliarifiwa kuwa ajira yake itakwisha tarehe 30 Septemba kwa ombi la Mkurugenzi Mkuu wa FAO, Qu Dongyu.

    Nyaraka hizo zilitaja madai ya ukiukwaji wa viwango vya kimataifa vya utumishi wa umma, vinavyowataka watumishi kutenda kazi kwa kutokuwa na upendeleo. Hata hivyo, Davis alipinga tuhuma hizo.

    "Ninahisi huu ni ukosefu mkubwa wa haki. Nimechukuliwa hatua za kinidhamu bila kufuata utaratibu wa haki kwa sababu nilizungumzia suala ambalo liko katika kiini cha wajibu wa FAO kuhusu haki ya kupata chakula, ambayo ni haki ya msingi zaidi ya binadamu," aliiambia Reuters.

    Alisema kuwa tayari amewasilisha rufaa dhidi ya uamuzi huo.

    Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) halikutoa majibu ya haraka kwa ombi la kutoa maoni kuhusu madai ya Davis au sababu za kufutwa kwake kazi.

    Davis alisema amefanya kazi katika FAO kwa miaka 26 chini ya mkataba unaohuishwa mara kwa mara, na kwamba kufutwa kwake kazi kunahusiana na harakati za baadhi ya wafanyakazi waliokuwa wakizungumza kuhusu vita vya Gaza.

    Unaweza kusoma;

  2. Trump aahidi 'pigo kali sana' dhidi ya Iran iwapo itathibitika kuhusika na tukio la flydubai

    Trump

    Rais wa Marekani Donald Trump ameapa kuipiga Iran "pigo kali sana" ikiwa itathibitishwa kuwa ilihusika katika shambulio dhidi ya rubani wa shirika la ndege la flydubai wakati wa safari kuelekea Tel Aviv, akiongeza kuwa "anaipenda nadharia hiyo."

    Trump alisema kwamba Wairani "watapokea pigo kali sana" akijibu swali la mwandishi wa habari kuhusu iwapo Marekani itachukua hatua endapo Tehran itabainika kuwa ndiyo iliyohusika na tukio hilo.

    Akizungumza na waandishi wa habari katika Ikulu ya White House, Rais wa Marekani Donald Trump alisema anaamini kuwa Iran inaweza kuwa ilihusika katika tukio hilo.

    "Ningesema ndiyo, kutokana na taarifa ninazosikia, lakini tunalifanyia kazi suala hili hivi sasa," alisema Trump.

    Wakati huo huo, siku ya Ijumaa, mshauri wa Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Anwar Gargash, alimsifu rubani wa ndege ya flydubai, aliyefahamika kwa jina la Machar, kwa ujasiri wake baada ya kushambuliwa na rubani msaidizi akiwa angani.

    Katika ujumbe aliochapisha kwenye jukwaa la X, Gargash aliandika:

    "Rubani huyo Mhindi anastahili kutambuliwa kwa kiwango cha juu kabisa, kwani alionyesha maana halisi ya ujasiri na uwajibikaji alipokabiliana na kitendo hatari cha kigaidi na maafa yaliyokuwa yakikaribia kutokea."

    Aliongeza kuwa:

    "Utaalamu wake na maadili yake katika mazingira magumu zaidi yanamfanya kuwa shujaa wa kweli."

    Kauli hizo zimekuja huku uchunguzi ukiendelea kuhusu tukio la ndege ya flydubai FZ1073, lililotokea wakati wa safari kutoka Dubai kuelekea Tel Aviv, na ambalo lilizuiwa kugeuka kuwa janga kutokana na hatua za haraka za rubani mkuu.

    Unaweza kusoma;

  3. Netanyahu asema rubani msaidizi wa flydubai 'aliingizwa katika itikadi kali za Kiislamu'

    Ndege ya flydubai ikijiandaa kutua katika Uwanja wa Ndege wa Ben Gurion tarehe 30 Septemba 2026.
    Maelezo ya picha, Ndege ya flydubai ikijiandaa kutua katika Uwanja wa Ndege wa Ben Gurion tarehe 30 Septemba 2026.

    Shirika la ndege la El Al limetangaza kufutwa kwa safari za kuwarejesha Waisraeli kutoka Dubai

    Ijumaa asubuhi, shirika la ndege la El Al lilitangaza kufutwa kwa safari zilizokuwa zimepangwa kwa ajili ya kuwarejesha Waisraeli kutoka Dubai, baada ya shirika la flydubai kusitisha safari zake za kwenda na kutoka Israel.

    Msemaji wa shirika hilo la ndege la Israel aliiambia AFP kwamba bado hakuna tarehe mpya iliyowekwa kwa safari hizo. Wakati huo huo, Wizara ya Uchukuzi ya Israel ilifafanua kuwa Israel bado haijapata idhini inayohitajika kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) ili kuendesha safari hizo.

    Siku ya Alhamisi, El Al ilikuwa imetangaza kuwa itafanya safari mbili maalumu za kuwarejesha Waisraeli waliokuwa Dubai kufuatia kusimamishwa kwa safari za flydubai.

    Katika matamshi ya hivi karibuni ya Israeli, Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu alisema Alhamisi kwamba rubani msaidizi ambaye alijaribu kuidungua ndege ya abiria iliyokuwa ikielekea Israel alikuwa "ameingizwa katika itikadi kali za Kiislamu."

    Katika mahojiano na kituo cha habari cha Fox News, Netanyahu alisema:

    "Tunajua kwamba ameathiriwa na mafundisho ya itikadi kali za Kiislamu."

    Sababu halisi ya tukio hilo, ambalo lilikaribia kusababisha maafa Jumatano katika safari ya ndege ya flydubai FZ1073 kutoka Dubai kuelekea Tel Aviv, haijawekwa wazi.

    Akizungumza na kipindi cha Fox & Friends, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alisema kuwa ndani ya siku chache zijazo ingewezekana kubaini kama rubani msaidizi wa ndege hiyo alikuwa na uhusiano wowote na Iran.

    Unaweza kusoma;

  4. Uamuzi wa tume dhidi ya Man City una athari kwa soka- FA

    Manchester City ilipatikana na hatia katika mashtaka 114 kati ya 115 yaliyokuwa yamewasilishwa dhidi yake.

    Uamuzi wa tume huru dhidi ya Manchester City una "athari kubwa kwa uadilifu wa mchezo", kwa mujibu wa Chama cha Soka cha England (FA).

    Katika taarifa yake, FA ilisema:

    "Tunazingatia kwa makini uamuzi huo pamoja na athari zake, na tutachukua hatua pale itakapofaa."

    Taarifa hiyo ya FA imekuja baada ya kuthibitishwa Jumanne kwamba Manchester City ilipatikana na hatia kwa makosa yote yaliyohusiana na ukiukaji wa kanuni za kifedha za Ligi Kuu ya England kati ya misimu ya 2009-10 na 2017-18.

    City imekuwa ikikanusha makosa hayo mara kwa mara, na ina hadi Ijumaa kuwasilisha rufaa dhidi ya uamuzi huo.

    FA iliongeza:

    "Kwa kuwa taratibu za kisheria kati ya Premier League na Manchester City Football Club bado zinaendelea, hatuna nia ya kutoa maoni zaidi kwa hatua hii."

    "Hata hivyo, tutaendelea kufuatilia maendeleo ya suala hili kwa karibu."

    Vyanzo vilivyonukuliwa na BBC Sport vimedokeza kuwa City inatarajiwa kudai katika rufaa yake kwamba baadhi ya mikataba muhimu ya udhamini ilifadhiliwa na serikali ya Abu Dhabi, badala ya wamiliki wa klabu hiyo.

    Miongoni mwa hitimisho la jopo huru ni kwamba City ilipanga kile kilichoelezwa kama "mikataba ya bandia" na washirika kadhaa wa kibiashara ili kuficha ufadhili wa siri unaokadiriwa kuzidi pauni milioni 830.

    Kwa upande wake, Premier League inadai kuwa Manchester City ilikiuka kwa mfumo na kwa kipindi cha karibu muongo mmoja kanuni za ligi hiyo za kifedha.

    Iwapo rufaa itawasilishwa, kesi hiyo inaweza kuendelea kwa muda zaidi huku ikitarajiwa kuwa na athari kubwa kwa mustakabali wa Manchester City na uaminifu wa usimamizi wa fedha ndani ya soka la England.

  5. Marekani yatuma meli ya tatu ya kubeba ndege Mashariki ya Kati

    .

    Jeshi la Marekani linatuma kikundi cha tatu cha meli za kivita kinachoongozwa na meli ya kubeba ndege Mashariki ya Kati, huku Rais Donald Trump akionya kuwa huenda mashambulizi mapya dhidi ya Iran yakafanyika.

    Upelekwaji huo, unaojumuisha kikosi maalumu cha mashambulizi, unaonyesha jinsi hali ya vita vya Trump dhidi ya Iran inavyoendelea kubadilika kwa kasi, wakati uchaguzi wa katikati ya muhula nchini Marekani ukikaribia.

    Trump ametishia kuwa kuongezeka kwa mashambulizi baada ya uchaguzi huo bado ni chaguo linalowezekana, licha ya ahadi zake za awali kwamba vita hivyo vingedumu kwa wiki chache tu.

    Kundi la meli hizo, ambazo sasa zinaelekea Mashariki ya Kati, kwa pamoja zina zaidi ya mabaharia 7,000 na wanajeshi 2,000 wa Majini wa Marekani.

    Kundi hilo linajumuisha kikundi cha meli za kivita kinachoongozwa na USS Theodore Roosevelt, pamoja na kikosi cha USS Makin Island, ambacho kina meli mbili za wanajeshi.

    Kwa mujibu wa afisa mmoja wa Marekani, ambaye hakutaka kutajwa jina kwa sababu ya unyeti wa operesheni za kijeshi, hatua hiyo inaweza kumaanisha kuwa meli tatu za kubeba ndege zitakuwa katika eneo hilo ifikapo mwishoni mwa Oktoba.

    Kwa kuzingatia wanajeshi ambao tayari wako Mashariki ya Kati, hatua hiyo itafanya uwepo wa wanamaji na wanajeshi wa Majini wa Marekani katika eneo hilo kufikia zaidi ya 20,000, pamoja na mamia ya ndege.

    Jeshi la Wanamaji la Marekani lilikuwa na vikundi vitatu vya meli za kivita vinavyoongozwa na meli za kubeba ndege Mashariki ya Kati mwezi Aprili, kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2003.

    Pia unaweza kusoma:

  6. Eritrea yakata uhusiano na Ethiopia huku hofu ya mzozo mpya ikiongezeka

    .

    Eritrea imekata uhusiano wote wa kidiplomasia na Ethiopia baada ya serikali ya Ethiopia kuamuru kufungwa kwa ubalozi wake mjini Asmara na kuwatangaza wanadiplomasia 10 wa Eritrea kuwa watu wasiokubalika

    Hatua hiyo imekuja baada ya milipuko kusikika usiku kucha mjini Addis Ababa, jambo lililozua hofu kuwa mapigano mapya kaskazini mwa Ethiopia yanaweza kuenea zaidi.

    Addis Ababa imezituhumu Eritrea, Sudan na Misri kwa kuunga mkono muungano wa upinzani unaoongozwa na Tigray People's Liberation Front (TPLF), ambao umekuwa ukipigana na vikosi vya serikali ya shirikisho ya Ethiopia tangu wiki iliyopita. Nchi hizo tatu zimekanusha madai hayo.

    Tume ya Umoja wa Afrika imezitaka nchi hizo tatu kujizuia na kuepuka hatua au matamshi yanayoweza kuongeza mvutano na kuhatarisha amani na utulivu wa eneo hilo.

    Mapigano hayo ndiyo makabiliano makubwa zaidi nchini Ethiopia tangu kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe vya mwaka 2020 hadi 2022, ambavyo vilisababisha vifo vya mamia ya maelfu ya watu. Eritrea ilipigana ikiunga mkono serikali ya shirikisho ya Ethiopia katika vita hivyo.

    Wizara ya Mambo ya Nje ya Ethiopia ilisema Alhamisi kuwa imeamua kufunga ubalozi wake mjini Asmara kutokana na kile ilichokiita "vitendo vya uhasama na uchokozi wa moja kwa moja na usio wa moja kwa moja dhidi ya Ethiopia".

    Wizara hiyo pia ilisema kuwa wanadiplomasia 10 wa Eritrea, ambao haikuwataja majina, wanapaswa kuondoka Ethiopia ndani ya saa 48.

    Soma Zaidi:

  7. Uingereza yasisitiza Man City lazima iwajibike

    .

    Serikali ya Uingereza imesisitiza kuwa Manchester City "haiko juu ya sheria" baada ya Meya wa Greater Manchester, Andy Burnham, kukosolewa kwa matamshi yake kuhusu ukiukaji wa kanuni za kifedha za Ligi Kuu dhidi ya klabu hiyo.

    Waziri Mkuu alisema Jumatano kuwa angekuwa na "wasiwasi mkubwa" iwapo wamiliki wa Manchester City wangeamua kuiuza klabu hiyo baada ya Manchester City kupatikana na hatia na tume huru katika sehemu kubwa ya mashtaka 115 yanayowakabili.

    Kauli hizo zilikosolewa vikali na Chama cha Conservative, kilichozitaja kuwa "zisizoendana kabisa na uhalisia" na "za kushangaza", huku watu wengi katika jumuiya ya soka wakionyesha kushangazwa na kauli hizo.

    Baada ya ukosoaji huo, serikali ya Uingereza ilitoa taarifa ikisema Waziri Mkuu amekuwa wazi kuwa uamuzi wa awali ni wa muhimu na kwamba hakuna anayepaswa kuonekana kuwa yuko juu ya sheria.

    Katika jaribio la kufafanua msimamo wa Waziri Mkuu, msemaji wa Ofisi ya Waziri Mkuu aliongeza kuwa mchakato huo bado unaendelea chini ya tume huru na ni muhimu uruhusiwe kukamilika na matokeo yake yaheshimiwe.

    "Pale ambapo makosa yatathibitishwa, wale watakaobainika kuhusika wanapaswa kukabiliwa na hatua zinazostahili," alisema msemaji huyo.

    Manchester City inakanusha kufanya makosa yoyote na ina hadi Ijumaa kuwasilisha rufaa yake.

    Pia unaweza kusoma:

  8. Rais Samia avunja ukimya kuhusu kifo cha Wicknell Chivayo

    .
    Maelezo ya picha, Wicknell Chivayo na Samia Suluhu

    Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amemtumia salamu za pole mfanyabiashara wa Zimbabwe Wicknell Chivayo kufuatia kifo chake katika ajali ya helikopta iliyoua pia mke wake na watu wengine watatu huko Marondera, Zimbabwe.

    Katika ujumbe wa pole uliotolewa Alhamisi, Oktoba 1, Rais Samia alimtaja Chivayo kuwa “mjasiriamali kijana na mwenye maono” ambaye aligusa maisha ya watu wengi.

    “Ni kwa masikitiko makubwa ninayoomboleza kifo cha mfanyabiashara wa Zimbabwe, Bw Wicknell Chivayo, mke wake mpendwa na watu wengine watatu waliopoteza maisha kwa huzuni katika ajali ya helikopta iliyotokea Marondera,” Samia alisema.

    “Zimbabwe na Afrika zimepoteza mjasiriamali kijana na mwenye maono, ambaye amegusa maisha ya watu wengi.”

    Rais Samia alitoa salamu za pole kwa niaba ya Serikali na wananchi wa Tanzania kwa Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa, familia ya Chivayo, familia za waathiriwa wengine na wananchi wa Zimbabwe.

    Alimalizia ujumbe wake kwa kuwaombea waliofariki.

    “Roho zao zipumzike kwa amani. Amina.”

    Uchunguzi wa ajali waendelea

    Ujumbe huo wa pole umetolewa wakati mamlaka za Zimbabwe zikiendelea kuchunguza mazingira ya ajali hiyo iliyosababisha vifo.

    Helikopta hiyo ilianguka Jumatano, Septemba 30, katika shamba la Kudenga, eneo la Marondera, mashariki mwa mji mkuu Harare.

    Polisi wa Zimbabwe baadaye walithibitisha kuwa watu watano walikuwa ndani ya helikopta hiyo: Chivayo, mke wake Lucy Rujeko Muteke, Saneliswe Magagula, rubani Calvin Tafirei Soda na rubani msaidizi Courage Mutavirwa.

    Watu wote watano waliokuwa ndani ya helikopta hiyo walifariki katika ajali hiyo.

    Wataalamu wa sayansi ya uchunguzi na wataalamu wa masuala ya anga walitumwa katika eneo la ajali huku wachunguzi wakianza kuchunguza mabaki ya helikopta na ushahidi mwingine.

    Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Zimbabwe, George Mashababe, alisema wachunguzi walibaini dalili za helikopta kugonga chini na mafuta kumwagika na kusababisha moto.

    Hata hivyo, chanzo kamili cha ajali hiyo bado hakijabainika.

    Salamu za pole kutoka viongozi wa Afrika

    Rais Samia ni miongoni mwa viongozi kadhaa wa Afrika waliotoa salamu za pole kufuatia kifo cha Chivayo.

    Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa alithibitisha kifo cha Chivayo na kueleza masikitiko yake, huku Rais wa Kenya William Ruto pia akimlilia na kumtaja Chivayo kuwa “rafiki mpendwa.”

    Chivayo alikuwa mfanyabiashara maarufu wa Zimbabwe aliyejulikana kwa shughuli zake za biashara, uhisani na uhusiano wake wa karibu na viongozi na watu mashuhuri wa biashara barani Afrika.

    Soma Zaidi:

  9. Christa Pike yuko katika hali mahututi baada ya kunusurika sindano mbili za kifo

    .

    Mfungwa wa Tennessee anayekabiliwa na adhabu ya kifo, Christa Pike, yuko katika hali mahututi hospitalini akipatiwa matibabu ya kuokoa maisha baada ya kunusurika majaribio mawili ya kunyongwa kwa sindano yenye sumu, tukio lililosababisha gavana wa jimbo hilo kusitisha utekelezaji wote wa adhabu za kifo kwa mwaka huu.

    "Wakati huu hatuna taarifa nyingi kuhusu hali yake ya afya au uwezekano wa kupona, lakini tunajua bado yuko hai," wakili wake Randy Spivey aliwaambia waandishi wa habari Alhamisi.

    Mawakili wake sasa wanaitaka hukumu yake ya kifo ibadilishwe. Pike, mwenye umri wa miaka 50, alihukumiwa kifo mwaka 1996 kwa mauaji ya Colleen Slemmer.

    Kwa mujibu wa mawakili wake, Pike alidungwa dozi mbili za dawa ya pentobarbital, inayotumika kutekeleza hukumu ya kifo siku ya Jumatano lakini hakufariki. Baadaye alipelekwa hospitalini kwa gari la wagonjwa.

    Pike alikuwa na umri wa miaka 18 alipomshambulia, kumtesa na kumuua Slemmer, mwenye umri wa miaka 19, pamoja na aliyekuwa mpenzi wake wakati huo, Tadaryl Shipp.

    Jaribio la kutekeleza hukumu yake ya kifo lilikuwa limekumbwa na mvutano wa kisheria wa dakika za mwisho, kabla ya Mahakama Kuu ya Marekani kuruhusu kutumiwa kwa njia hiyo ya kudungwa sindano.

    Mama wa Slemmer, May Martinez, ambaye alikuwa miongoni mwa waliotaka Pike auawe na alisafiri hadi Tennessee kushuhudia utekelezaji huo, aliiambia NBC News baada ya jaribio hilo kushindikana kwamba, "kulikuwa na vurugu na mkanganyiko mkubwa."

    Alhamisi, mawakili wa Pike walitoa maelezo zaidi kuhusu kilichotokea, wakielezea tukio la kutisha lililofanyika kwa usiri mkubwa.

    "Jana usiku timu ya utekelezaji hukumu hiyo ilijaribu kumdunga sindani kwa njia ya mshipa kwa saa moja nzima," alisema Spivey. "Nilihesabu sindano saba alizodungwa kwenye mkono wake wa kushoto pekee, moja ikiwa imepinda ilipotolewa baada ya jaribio kushindikana."

    Spivey alisema mashahidi waliokuwa wakifuatilia utekelezaji huo waliwekwa katika chumba chenye giza nyuma ya pazia lililofungwa baada ya dozi ya pili kuingizwa mwilini mwa Pike, huku ikiwa wazi kwamba Pike bado alikuwa anapumua dakika kadhaa baadaye.

    "Hakuna aliyekuwa akijua kilichokuwa kinaendelea nyuma ya pazia hilo," alisema. "Sikujua ni lini au kama wataalamu wa afya walianza kumsaidia."

    Spivey alisema Gavana wa Tennessee anapaswa sasa kubadilisha hukumu ya kifo ya Christa, ombi ambalo awali lilikuwa limekataliwa.

    Wakili mwingine wa Pike, Stephen Ferrell, alisema timu ya utetezi pia inachunguza njia nyingine za kisheria.

    "Tunataka kulifikiria suala hili kwa makini na kuhakikisha Christa anapona ili aweze kutoa maoni yake kuhusu hatua anazotaka zichukuliwe," alisema.

    Gavana wa Tennessee, Bill Lee, ameagiza uchunguzi huru kufanyika kuhusu jaribio hilo lililoshindikana la kutekeleza hukumu ya kifo na amesema uchunguzi huo utakuwa wa kina.

    "Uchunguzi huu utakuwa wa kina na utachukua muda," alisema Alhamisi.

    Soma Zaidi:

  10. Vikosi vya Yemen vyadai kulenga maghala ya silaha ya Wahouthi

    .

    Vikosi vya serikali ya Yemen vinavyotambuliwa kimataifa vimetangaza kuwa vimeshambulia malengo "muhimu sana" katika mji mkuu wa Yemen, Sanaa, huku mashambulizi ya anga yakiripotiwa pia kufanyika katika majimbo ya Saada na Taiz.

    Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari, milipuko mikubwa ilisikika katika mji wa Sanaa unaodhibitiwa na kundi la Ansar Allah la Wahouthi Alhamisi jioni.

    Picha zilizochapishwa na shirika la habari la AFP zilionyesha moshi mzito ukifuka juu ya mji huo, huku shirika la habari la Sabah linalohusishwa na Wahouthi likieleza mashambulizi hayo kama "uchokozi wa Saudi Arabia".

    Katika taarifa iliyotolewa kupitia X, msemaji wa vikosi vya serikali ya Yemen, Kanali Majid al-Nuzali, alisema mbali na mashambulizi ya Sanaa, maeneo 11 pia yalilengwa katika jimbo la Saada kaskazini-magharibi mwa Yemen.

    Kuhusu Taiz, msemaji huyo alisema ndege za kijeshi zilifanya mashambulizi 27 ya anga yaliyolenga kwa usahihi maeneo mbalimbali ya Wahouthi, yakilenga mfumo mzima wa kijeshi wa kundi hilo.

    Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mashambulizi hayo yalilenga ghala la makombora, vituo vya amri na udhibiti, maghala ya silaha na vifaa, maeneo ya wapiganaji wa kundi hilo pamoja na magari na vifaa vya kijeshi.

    Vikosi vya serikali vilisema mashambulizi hayo yalifanikiwa kulenga malengo yake kwa usahihi mkubwa, na kusababisha kuharibiwa kwa magari kadhaa ya kijeshi pamoja na kuuawa au kujeruhiwa kwa idadi kubwa ya wapiganaji wa Wahouthi.

    Wakati huo huo, muungano unaoongozwa na Saudi Arabia ulisema Alhamisi jioni kuwa uliangusha makombora mawili ya balistiki na ndege nne zisizo na rubani juu ya mji wa Jazan kusini mwa Saudi Arabia, karibu na maeneo ya mafuta na nishati ambayo yamelengwa katika wiki za hivi karibuni.

    Malengo mengine pia yalitunguliwa juu ya mji wa Khamis Mushait kusini-magharibi mwa Saudi Arabia ambako kuna kituo cha jeshi la anga.

    Kwa mujibu wa Idara ya Ulinzi wa Raia ya Saudi Arabia, mabaki ya kombora la balistiki lililotunguliwa eneo hilo yalisababisha uharibifu mdogo wa mali.

    Mapema Alhamisi, muungano huo ulidai kuwa Wahouthi walilenga kituo cha usambazaji umeme mjini Medina wiki hii, na kusababisha transfoma moja kuharibika, ingawa mfumo wa usambazaji umeme haukuathirika kwa kiwango kikubwa.

    Muungano huo ulisema uchunguzi wa mabaki ya ndege isiyo na rubani ulithibitisha kuhusika kwa Wahouthi katika shambulio hilo la Jumanne. Kituo hicho cha umeme kinahudumia eneo la Msikiti wa Mtume mjini Medina.

    Hata hivyo, shirika la habari la Sabah linaloendeshwa na Wahouthi, likinukuu chanzo cha kijeshi katika Wizara ya Ulinzi ya serikali yao, lilikanusha madai hayo ya Saudi Arabia na kuyataja kutokuwa na msingi.

    Chanzo hicho kilisema tuhuma hizo ni "uongo" unaolenga kugeuza mjadala kutoka kile kilichodaiwa kuwa kushindwa kwa Saudi Arabia kuthibitisha madai yake ya awali kuhusu shambulio lililolenga Makka.

    Wiki mbili zilizopita, Saudi Arabia ilitangaza kuwa iliangusha ndege isiyo na rubani iliyodaiwa kurushwa na Wahouthi kusini mwa Makka kabla ya kuingia katika anga maalumu la mji huo mtakatifu.

    Muungano huo ulisema hilo lilikuwa jaribio la pili tangu mwaka 2017 la kulenga Makka, madai ambayo Wahouthi wamekanusha, wakisisitiza kuwa hawajalenga Makka wala eneo lolote takatifu la Kiislamu.

    Muungano unaoongozwa na Saudi Arabia umeeleza kuwa mashambulizi dhidi ya Medina ni sehemu ya juhudi za Wahouthi za kulenga maeneo matakatifu ya Kiislamu na kuchochea hisia za Waislamu duniani.

    Pia umesisitiza kuwa utaendelea kuchukua hatua zote zinazohitajika kulinda maeneo matakatifu pamoja na waumini wanaoyatembelea.

    Pia unaweza kusoma:

  11. Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa: Real Madrid yavutiwa na Quansah

    .

    Real Madrid inaonyesha nia ya kumsajili beki wa England mwenye umri wa miaka 23, Jarell Quansah, anayekipiga Bayer Leverkusen. Quansah alikuwa akiwaniwa na Arsenal, ambayo iliwasilisha ofa ya kumsajili majira ya joto yaliyopita, huku Chelsea nayo ikiulizia upatikanaji wake. (Bild - in German)

    Mchezaji chipukizi wa Mexico Gilberto Mora, 17, yupo kwenye rada ya Liverpool, huku Borussia Dortmund na Benfica pia zikimwania kiungo huyo wa Club Tijuana. (Teamtalk)

    Kiungo wa Hispania na Barcelona Dani Olmo, 28, anataka kumalizia soka lake la kulipwa katika klabu ya Dinamo Zagreb. (Fichajes - in Spanish)

    Mshambuliaji wa Canada mwenye umri wa miaka 26, Jonathan David, ameanza kuishawishi Atletico Madrid kwamba inapaswa kugeuza uhamisho wake wa mkopo kutoka Juventus kuwa wa kudumu kwa ada ya pauni milioni 21. (Fichajes - in Spanish)

    Inter Milan ina nia ya kumsajili kiungo wa kati wa Italia Alessandro Romano, 20, iwapo kiungo wa Uturuki Hakan Calhanoglu ataondoka klabuni mwishoni mwa mkataba wake majira ya joto yajayo. (Gazzetta dello Sport - in Italian)

    Roma ilishindwa kumsajili kwa mkopo mshambuliaji wa Real Madrid na timu ya taifa ya Brazil, Endrick, 20, katika dirisha la usajili la majira ya joto, lakini bado ina nia ya kufanya jitihada mpya za kumpata mwezi Januari. (Gazzetta dello Sport - in Italian)

    Barcelona ilifanya uchunguzi kuhusu uwezekano wa kumsajili beki wa Croatia Josko Gvardiol msimu uliopita, lakini ilikuwa wazi kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 hakuwa na nia ya kuondoka Manchester City. (Mundo Deportivo - in Spanish)

    Barcelona na Inter Milan zinafuatilia kwa karibu hali ya beki wa Stuttgart, Finn Jeltsch, 20, huku vilabu kadhaa vya Ligi Kuu England navyo vikionyesha nia ya kumsajili Mjerumani huyo. (Sky Sports Germany)

    Bologna imefikia makubaliano ya kumsajili aliyekuwa beki wa Manchester United na Inter Milan, Matteo Darmian, 36, kwa uhamisho wa bure baada ya kuondoka Inter mwishoni mwa msimu uliopita. (Fabrizio Romano)

    Pia unawezakusoma:

  12. Putin aonya Magharibi: Urusi iko tayari kutumia silaha zote kulinda Kaliningrad

    .

    Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema nchi yake itatumia silaha zote ilizonazo iwapo itahisi kuwa eneo lake la Kaliningrad katika Bahari ya Baltiki limevamiwa moja kwa moja.

    Putin alisisitiza kuwa Moscow "haitishi mtu yeyote", bali inajibu tu matamshi ya viongozi wa Magharibi wanaodai kuwa Urusi inajiandaa kwa vita mwaka 2029 au 2030.

    Katika wiki hii, Urusi imeishutumu Nato kwa kuandaa mpango wa kuizingira Kaliningrad, eneo la Urusi linalopakana na Lithuania na Poland. Urusi imeonya kuwa inaweza hata kutumia silaha za nyuklia ikiwa Magharibi itajaribu kulitenganisha eneo hilo na sehemu nyingine za Russia.

    Kwa upande wake, Nato imejaribu kutuliza mvutano huo ikisisitiza kuwa ni muungano wa kujihami pekee na kuitaka Urusi kusitisha vitisho vyake vya matumizi ya silaha za nyuklia.

    Wakati huo huo, Poland na mataifa ya Baltiki yamekabiliwa na ongezeko la matukio ya kile kinachoitwa vita vya mseto yanayodaiwa kuhusishwa na Urusi katika miezi ya hivi karibuni.

    Wiki iliyopita, Poland ilisema helikopta ya kijeshi ya Urusi iliingia kwa muda katika anga yake karibu na Kaliningrad, huku Lithuania ikieleza kuwa wananchi wake wanaishi katika hali ya hofu ya mara kwa mara kutokana na vitisho vya Urusi, ikiwemo ndege zisizo na rubani kuingia katika anga la nchi hiyo.

    Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz alisema Alhamisi kuwa nchi yake inajiandaa kukabiliana na mashambulizi zaidi ya vita vya mseto, "ikiwemo mashambulizi makubwa", baada ya ndege isiyo na rubani iliyokuwa na vilipuzi kupatikana mwezi Agosti katika uwanja wa ndege wa Leipzig karibu na ndege za mizigo za Ukraine.

    Akizungumza katika kongamano la sera za kigeni la Valdai, Putin alisema anaamini migogoro ya kimataifa itaendelea kuwepo, lakini hali itaimarika kadri anavyoona "utawala wa Magharibi" ukidhoofika.

    Licha ya kuanzisha uvamizi nchini Ukraine mnamo mwezi Februari 2022, alirudia kulaumu Magharibi kwa kuchochea vita hivyo, akidai kuwa Urusi ililazimika kujilinda na kuchukua hatua za kijeshi.

    Pia alisema mashambulizi ya Urusi dhidi ya miundombinu ya kiuchumi ya Ukraine ni jibu kwa mashambulizi ya Ukraine dhidi ya viwanda vya kusafisha mafuta vya Urusi na meli zake katika Bahari Nyeusi.

    "Sasa kutoka kila upande tunasikia wito wa kusema, 'tusitishe'. Lakini wao ndio walioanzisha," alisema Putin.

    Putin alikiri kuwa mashambulizi ya Ukraine dhidi ya viwanda vya kusafisha mafuta yamekuwa na mafanikio fulani na kusababisha Urusi kupoteza takriban asilimia 1 ya pato lake la taifa (GDP). Ukraine inasema ilianza kulenga miundombinu ya mafuta ya Urusi kwa sababu inasaidia kufadhili vita hivyo.

    Tangu vita kuanza mwaka 2022, Urusi imekuwa ikiongeza mashambulizi dhidi ya miundombinu ya nishati ya Ukraine kila majira ya baridi. Miundombinu mingine ya kiraia pia imeendelea kulengwa, huku daraja muhimu mjini Kyiv likishambuliwa kwa kutumia ndege zisizo na rubani siku ya Alhamisi.

    Soma Zaidi:

  13. Hujambo. Karibu katika matangazo yetu mubashara. Tarehe ni 02/10/2026.