Tazama kwa picha uzinduzi wa bwawa la kuzalisha umeme la Mwalimu Julius Nyerere

Chanzo cha picha, Ikulu Tanzania
Uzinduzi wa bwawa kubwa zaidi Afrika Mashariki wa kuzalisha umeme umefanyika hii leo.
Akizundua rasmi bwawa hilo, Rais Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa bwawa hilo linachangia nusu ya umeme unaotumika nchini Tanzania kwa sasa, na imepunguza visa vya kukatika kwa umeme mara kwa mara.
"Megawati zinazozalishwa na kituo hiki, zimeongeza uwezo wetu wa kuzalisha umeme na kuwa na akiba ya kutosha ya umeme. Tunaimani kwamba mradi huu utaongeza fursa za biashara,uwekezaji,uzalishaji,kutengeneza ajira na kuongeza kipato cha kila mmoja na taifa kwa jumla," alisema Rais Samia.
Bwawa hilo lililopewa jina la Rais wa kwanza wa Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere, lina uwezo wa kuzalisha megawatt 2115 za umeme, hivyo kuwa moja ya mabwawa makubwa ya kuzalisha umeme barani Afrika.
Tazama kwa picha uzinduzi wa bwawa hilo:

Chanzo cha picha, Ikulu Tanzania

Chanzo cha picha, Ikulu Tanzania

Chanzo cha picha, Ikulu Tanzania

Chanzo cha picha, Ikulu Tanzania

Chanzo cha picha, Ikulu Tanzania

Chanzo cha picha, Ikulu Tanzania








