Silaha 9 za teknolojia ya juu zitakazobadili vita vya siku zijazo

m

Chanzo cha picha, US Air Force

Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 4

Silaha zinapitia mabadiliko makubwa zaidi tangu mwanzo wa enzi ya nyuklia. Kwa karibu karne moja, ubora wa jeshi ulibainishwa na nguvu ya farasi, vilipuzi, silaha nzito, makombora ya masafa marefu, na ndege za kasi.

Leo uwanja wa vita unaelekea kwa kasi kwenye silaha zisizoonekana, kupitia akili unde, sumakuumeme, na anga ya juu.

Kadri mataifa yanavyoshiriki katika mbio za silaha za teknolojia zisizoonekana, dhana ya jadi ya vita ambapo risasi na wanajeshi wa binadamu huamua ushindi, inapotea.

Silaha 9 ambazo ziatatumika siku za mbeleni.

Miale

mj

Chanzo cha picha, shutterstock

Maelezo ya picha, Mwale kutoka katika mfumo wa silaha za leza ukishambulia wakati wa jaribio lililofanikiwa 2024

Silaha hii ni mfumo wa nishati inayorusha miale yenye nguvu, ili kuchoma silaha za adui zikiwemo ndege, magari, sensa zisizoonekana, au kulipua mabomu.

Ni silaha isiyo na gharama kubwa katika kuiendesha na ina miale isiyokwisha ilimradi tu kuna Nishati.

Silaha hii imeundwa kwa ajili ya ulinzi wa anga dhidi ya ndege zisizo na rubani za bei nafuu.

Mawimbi ya sukamuumeme

m

Chanzo cha picha, Jeshi la Anga la Marekani

Maelezo ya picha, Mfumo huu umeundwa ili uweze kusafirishwa na kutumiwa haraka, ukiwekwa kwenye chombo cha kawaida cha usafirishaji

Silaha ya mawimbi ya sumakuumeme na silaha ya frekwensi za redio hutoa miale mipana yenye nguvu mara 150,000 zaidi kuliko microwave ya jikoni.

Imeundwa kuchoma vifaa vya elektroniki vya droni zinazoingia kwenye anga kwa wakati mmoja badala ya kuzilenga moja baada ya nyingine.

Akili Unde

k

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mfumo wa Phalanx unaweza kurusha hadi risasi 4,500 kwa dakika

Hizi ni silaha ambazo ni automatiki za ulinzi zinazotumia algoriti za AI kufuatilia, kuongoza, na kushambulia vitisho vinavyoingia, kuliko kutumia silaha zinazolengwa na binadamu.

Ingawa binadamu wanaweza kuzidhibiti silaha hizi, lakini kuna maswali kuhusu matumizi ya silaha zinazojiendesha zenyewe kwa akili unde.

Silaha za sauti

k

Chanzo cha picha, Alamy

Maelezo ya picha, Meli ya USS Blue Ridge ina silaha ya sauti ambayo inaweza kuwazuia na kuwavuruga wanajeshi

Silaha zinazotumia mawimbi ya sauti kali ili kusababisha usumbufu wa kimwili, kuchanganyikiwa, au uharibifu wa ndani ya sikio.

Silaha hii ni tofauti na spika ya kwenye lori ambayo hutumika kwa udhibiti wa umati na ulinzi dhidi ya uharamia.

Bunduki za Hypersonic:

n

Chanzo cha picha, Alamy

Maelezo ya picha, Hii hutumia nguvu za sumakuumeme badala ya unga wa bunduki ili kuongeza kasi ya makombora

Ni silaha za kielektroniki zinazotumia makombora ya chuma, na kuyarusha kwa kasi ya hypersonic.

Silaha hii ya hypersonic ina uwezo wa hali ya juu, inayotumia sumakuumeme na mikondo ya umeme badala ya unga wa bunduki au vilipuzi vya kemikali.

Na hurusha makombora kwa kasi kubwa.

Miale ya Joto

k

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Silaha hii pia imeundwa kuzuia adui kwa kusababisha kutoona kwa muda

Ni silaha za nishati zilizoundwa kulenga shabaha binadamu.

Mifano ni "miale ya joto" ambayo huchoma ngozi bila uharibifu wa kudumu.

Silaha hii pia imeundwa kuzuia adui kwa kusababisha kutoona kwa muda.

Silaha za anga za mbali

n

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kushambuliwa kwa setilaiti moja tu katika mzunguko wa Dunia kunaweza kusababisha athari mbaya

Silaha za anga za juu ambazo hupaishwa hadi anga za juu ili kushambulia maeneo ya ardhini bila kutabirika, ikipita ngao za ulinzi wa makombora.

Hutumwa kichwa cha kombora kwenye mzunguko wa Dunia kabla ya kurudi kwa kutegemea uzito na kasi ya kutokea angani ili kufanya shambulio.

Ndege za kivita kama droni

k

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Ndege aina ya YFQ-42A na YFQ-44A ndizo ndege za kwanza za Jeshi la Anga la Marekani zinazojiendesha kama droni

Ndege za kivita zinazojiendesha zenyewe au zinazoendeshwa na AI (kama vile YFQ-42A na YFQ-44A ya Jeshi la Anga la Marekani) zimeundwa kufanya kazi kama droni.

Zinaruka pamoja na ndege za kivita zenye marubani, au zikitekeleza misheni za peke yao, ni dalili kuwa AI tayari imewashinda marubani wa kibinadamu katika mapigano ya angani.

Silaha za akili na neva

mm

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wazo la silaha za kudhibiti akili zinazofanya kazi kutoka mbali linapatikana zaidi katika hadithi za kutunza za kisayansi na bado haziijathibitishwa kwa sasa.

Hii ni silaha ya majaribio inayolenga kuvuruga utendaji kazi wa neva wa adui, nguvu, au hisia kupitia nishati, mawimbi ya sauti, au frekwensi na kutoa athari za kisaikolojia.

Wazo la silaha za kudhibiti akili zinazofanya kazi kutoka mbali linapatikana zaidi katika hadithi za kutunga za kisayansi na bado haziijathibitishwa kwa sasa.