Makala ya Wayne Rooney: Mfungaji bora wa mabao wa England alihofia unywaji ungemsababishia kifo

Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 5

Wayne Rooney anasema alihofia angeweza kufa au kumuua mtu katika kiwango cha matatizo yake ya unywaji pombe.

Meneja huyo wa Derby na mfungaji bora wa mabao kwa Manchester United na Uingereza alikuwa akizungumza na mtangazaji wa BBC Breakfast Sally Nugent kabla ya kutolewa kwa filamu mpya kuhusu maisha yake.

Alifichua mabaya ambayo maswala ya pombe na afya ya akili yamemchochea kufanya, na alipoulizwa ni nini hofu yake kubwa ilikuwa wakati huo, alijibu: "Labda kifo."

Akizungumzia "makosa" aliyoyafanya, kijana huyo mwenye umri wa miaka 36 aliongeza: "Hao wanaweza kuwa wasichana, inaweza kuwa kuendesha gari nikiwa mlevi, ambayo nimefanya, ingeweza kuwa kuua mtu - unaweza kujiua. - na hiyo ni hatua mbaya mtukufika.

"Nilijua nilihitaji msaada, kujiokoa lakini pia kuokoa familia yangu." Rooney pia alifichua kwamba alihisi alipaswa kuficha matatizo yake mengi kama mchezaji. "Miaka 10, 15 iliyopita, sikuweza kwenda kwenye chumba cha kubadilishia nguo na kusema ninapambana na tatizo la unywaji pombe, ninapambana na tatizo la afya ya akili. Sikuweza kufanya hivyo."

Filamu kuhusu maisha ya Rooney, inatolewa kwenye mtandao wa Amazon Prime Video siku ya Ijumaa na inaangazia maisha ya Rooney tangu utotoni hadi mwanzo wa kazi yake ya usimamizi katika Derby.

Hapa, BBC Sport inachagua mambo mengine saba muhimu ya mazungumzo kutoka kwa filamu hiyo.-

Kupigana na kunywa pombe kungeharibu taaluma yangu nikiwa mto

Rooney anakiri katika tukio moja kwamba "hakuwa mtoto mzuri sana" akiwa kijana. Anazungumza waziwazi kuhusu kujihusisha na vurugu nyingi.

"Tulikuwa tukienda Southport na kupigana sana," anasema wakati mmoja, akiongeza: "Nilirudi jicho langu likiwa limeshonwa. Nilikuwa na umri wa miaka 12 hivi."

Rooney pia anaelezea kwenda kwenye tamasha kama kijana mdogo na baadaye kujiingiza kwenye matatizo.

"Nakumbuka nilipasuliwa taya yangu huko Manchester. Nilikuwa na umri wa miaka 13 hivi."

Katika tukio moja, Rooney anaelezea tukio la aibu alipokuwa na akademi ya Everton.

"Kuna siku moja nilikuwa navuka barabara nikiwa na chupa ya kinywaji cider. Kocha wangu Colin Harvey, alisimama kuniruhusu nivuke. Siku iliyofuata, alinivuta kwenye mazoezi na kusema, sikiliza, una talanta ambayo sijawahi kuona kwa mtu yeyote wa umri wako - usiipoteze"

Rooney alidhamiria kuwa mfungaji bora mwenye umri mdogo zaidi katika Ligi ya Premia

Akiwa na umri wa miaka 16, Rooney tayari alikuwa na kipaji kikali na mwili wake ukawa ushajitokeza kama wa mwanaume wa miraba minee.

Anazungumza kwenye filamu kuhusu kujua alikuwa mchezaji bora katika mazoezi, hata wakati huo.

Mnamo tarehe 19 Oktoba 2002, alijitangaza kwa ulimwengu wote.

Ilikuwa siku tano kabla ya Rooney kutimiza miaka 17 na Everton walikuwa wakicheza na Arsenal - ambao walikuwa kwenye mbio za michuano30 bila kushindwa wakati huo.

Timu yao ilijumuisha majina kama Thierry Henry, Patrick Vieira, David Seaman na Sol Campbell.

Rooney anakumbuka hisia ya jinsi wote walikuwa wachezaji wa kupigiwa mfano.

Walakini, kijana alitaka kufanya kazi ya kipekee kwenye mchezo na kujitengenezea jina.

"Huo ulikuwa mchezo wangu wa mwisho nikiwa na umri wa miaka 16. Nilikuwa nikijipiga chini, nikifikiri, Nataka kufunga kama wenye umri wa miaka 16", Rooney anafichua.

"Baada ya kutoka kwenye benchi, anasema alikuwa na wazo moja: "Nikipata nafasi, ninapiga kutoka popote. "

Katika dakika ya mwisho, Campbell alianza kurudi nyuma, Rooney aliona nafasi hiyo ikifunguka mbele yake.

Aliachia kitu kwa kupiga kelele kilichompeleka Goodison Park porini.

Viongozi wa ligi Arsenal walipoteza rekodi yao ya kutoshindwa na mchambuzi Clive Tyldesley alituhimiza sote "kukumbuka jina" Wayne Rooney.

Alijua kuwa alikuwa bora zaidi ulimwenguni akiwa na miaka 18

Rooney alikuwa mvulana wa dhahabu wa Uingereza katika michuano ya Ulaya mwaka 2004 nchini Ureno, kabla ya kuvunjika mguu kuhitimisha mchuano wake - na bila shaka wa England - dhidi ya wenyeji katika robo fainali.

Akiwa na umri wa miaka 18 tu, katika mchezo wa ufunguzi, aliitia hofu timu ya Ufaransa iliyokuwa inajivunia kama Henry, Zinedine Zidane na Lilian Thuram.

"Beki wao wa kati waliogopa kwenda karibu, waliweza kuona kimwili ningeweza kukabiliana nao. "

Wakati fulani alimshinda Thuram, mmoja wa mabeki bora zaidi duniani wakati huo, kwa changamoto ambayo angeweza kupata kadi nyekundu.

"Nilipigana naye kikumbo kwenye taya yake na kumtazama tena kana kwamba ninasema, sasa unajua mimi ni nani. "

Ufaransa ilishinda mechi hiyo kwa mabao 2-1, lakini Henry anakiri kwamba England "ilikuwa na mchezo mzuri kuwashinda" na timu yake ingefaa kushinda.

Anasema kuhusu Rooney kwamba "ungemwangalia na ungejua tu anataka kufanikiwa. "

"Nakumbuka nikifikiria, Mimi ndiye mchezaji bora zaidi duniani" Rooney anatafakari, na kuongeza: "Ninaamini, wakati huo, nilikuwa. "

Kwa makusudi alitoka kwenda kumuumiza mchezaji wa Chelsea mnamo 2006

Mnamo mwaka 2006, Chelsea iliyokuwa chini ya Jose Mourinho kuwapa changamoto Manchester United huko England.

Mnamo tarehe 29 Aprili mwaka huo, Chelsea ilicheza na Manchester United kwenye Uwanja wa Stamford Bridge, ikihitaji pointi moja tu kupata taji la pili mfululizo la Premier League. Walishinda 3-0.

Rooney hakuweza kukabiliana vyema na hali hiyo.

"Nilivaa buti mpya, zenye ncha ndefu kwa sababu nilitaka kumuumiza mtu," anakiri.

"Vilikuwa halali, lakini vikubwa kuliko ambavyo ningevaa kawaida.

Mgongano na John Terry ulimwacha akiwa na tundu sehemu ya juu ya kiatu chake na kuhitaji magongo."

Hakuwa na tatizo lolote na tabia ya Ronaldo kwenye Kombe la Dunia la 2006

Kombe la Dunia la 2006 litakumbukwa kwa kiasi kikubwa na mashabiki wa Uingereza kwa kupoteza tena robo fainali dhidi ya Ureno, ambapo Rooney alitolewa nje kwa kadi nyekundu kwa kumkanyaga Ricardo Carvalho.

Kufuatia tukio hilo, mchezaji mwenzake wa Manchester United, Cristiano Ronaldo alionekana kumshawishi mwamuzi amtoe kwa kadi nyekundu.

Rooney alipotolewa, kamera zilimchukua Ronaldo akiwakonyeza wachezaji wenzake wa Ureno.

Nilivunja vitu vichache kwenye chumba cha kubadilishia nguo nilipoingia," Rooney anatafakari.

Ilikuwa sehemu ya upweke zaidi ambayo nimewahi kuwa. Nakumbuka nikifikiria, ikiwa tutashinda, nitakosa nusu-fainali, pengine fainali. Tukitoka, ni kosa langu."

Rooney anasema alimwambia Ronaldo baada ya tukio hilo kwamba "hakuwa na shida" na jinsi alivyofanya na kwamba wanapaswa kuzingatia kushinda Ligi ya Premia, jambo ambalo waliendelea kufanya.

Anaamini alikuwa sahihi kukabiliana na Sir Alex Ferguson

Oktoba 2010, Rooney alishangaza ulimwengu wa soka kwa kutuma ombi la uhamisho kwenda Manchester United.

Pia alifanya jambo lisilofikirika kwa kumkabili meneja Sir Alex Ferguson.

"Tulimuuza [Carlos] Tevez, kisha tukamuuza Ronaldo. Nilikuwa mchezaji mmoja niliyebaki na hadhi ya juu," Rooney anaonyesha.

"Niliingia katika ofisi ya Alex Ferguson na nikasema, mpango hapa ni gani?

Jibu lake lilikuwa, "toka ofisini kwangu."

Walinzi wa zamani wa United Gary Neville na Rio Ferdinand wanazungumza kwenye filamu hiyo kuhusu kusikitishwa kwao na jinsi mwenzao alivyoshughulikia mambo wakati huo.

Hata hivyo, Rooney anashikilia kuwa alikuwa sahihi kutilia shaka sera ya uhamisho ya Ferguson.

"Ukiangalia miaka mitano kutoka kwa mkutano huo, Alex Ferguson alijua kule ambapo klabu ilikuwa ikienda, alitoka haraka sana kadiri alivyoweza na bado mambo hayajakuwa sawa."