Picha za wanyama za kuchekesha zaidi 2017

Happy Sea Otter
Iliyochapishwa

Huu hapa ni mkusanyiko wa picha za kuchekesha na kusisimua za wanyama zilizopigwa mwaka huu, miongoni mwa picha hizi ikiwa moja ya dubu wanaoonekana kukoleza uhusiano wao pamoja na nyingine ya sili.

Picha hizi ziliteuliwa kushindania tuzo za picha za ucheshi za wanyama mwaka huu, katika vitengo vitano.

Jumla ya picha 3,500 ziliwasilishwa kwa mashindano hayo.

Shindano hili huandaliwa kuchangisha pesa na kusaidia shirika la kutetea uhifadhi wa wanyama la Wakfu wa Born Free.

Owls
Maelezo ya picha, Picha hii ya Tibor Kercz ilipewa kichwa 'Nisaidie'

Mshindi wa jumla Tibor Kercz kwa picha hii yake ya bundi anayeonekana kuhitaji usaidizi kujishikilia vyema kwenye tawi mti alitunukiwa kikombe ambacho kilitengenezwa na wanaume na wanawake wenye ulemavu kutoka Tanzania.

Kadhalika, alipewa vifaa zaidi vya kupigia picha.

Alishinda pia tuzo kwenye kitengo cha picha ya kuvutia zaidi ya mtandaoni pamoja na kujishindia safari ya kwenda mbugani Kenya.

Kabla ya picha hii ya Andrea Zampatti kushinda kitengo cha picha za ardhini, picha hii yake ya panya anayeonekana kuangua kicheko ilisambazwa sana mitandao ya kijamii mapema mwaka huu.

Dormouse
Maelezo ya picha, Raha mustarehe!

Na ingawa bahari ni kubwa, picha hii iliyoshinda kitengo cha picha za chini ya bahari inaonesha viumbe wanaweza bado kukaribiana sana.

Turtle and fish
Maelezo ya picha, Picha hii ilipewa kichwa 'kofi'

Kitengo cha picha za angani, picha hii ya njiwa mmoja wao akionekana kufuata njia ya moshi wa ndege, iliyopigwa na John Threlfal Preston, Lancashire ndiyo iliyoshinda.

Birds.

Hapa chini ni baadhi ya picha nyingine zilizofanya vyema.

Penguins
Maelezo ya picha, Twende kanisani
Rabbit
Maelezo ya picha, Kunani?
Polar bears
Maelezo ya picha, Nibebe
Wilderbeest
Polar bears
Maelezo ya picha, Mapenzi tele
Seals
Maelezo ya picha, Eti nini!?