Ugunduzi 7 muhimu na wa kushangaza zaidi wa 2025

Chanzo cha picha, Photo credit: Marilyn Sargent/Berkeley Lab
Ugunduzi wa kisayansi ni matokeo mapya yanayobadilisha jinsi tunavyoelewa ulimwengu. Hutokea kupitia tafiti za kisayansi, fikra, au wakati mwingine bahati tu.
Kwa mazuri au mabaya, hizi hapa gunduzi saba ambazo ni mafanikio ya mwaka 2025 na zimebadilisha maisha yetu.
Kompyuta yenye kasi zaidi duniani
Januari, kompyuta yenye kasi zaidi duniani ilizinduliwa katika Maabara ya Kitaifa ya Lawrence Livermore huko California. Inaitwa El Capita, ni kompyuta ya tatu ya aina hiyo, ambapo Inaweza kufanya hesabu za 1.8 kwantilioni kila sekunde.
Kama kila mtu Duniani angekuwa na kikokotoo na kufanya kazi saa 24 kwa siku, siku 7 kwa wiki, akifanya hesabu moja kwa kila sekunde, itamchukua binadamu zaidi ya miaka bilioni kadhaa kumaliza idadi ya hesabu ambazo El Capitan hukamilisha kwa sekunde moja tu.
Kompyuta yako ya kawaida ya mkononi inaweza kufanya hesabu bilioni kadhaa kwa sekunde. El Capitan ina kasi ya takriban mara milioni moja kuliko kompyuta yako ya nyumban
Kompyuta hiyo kubwa itatumika kupanga akiba ya silaha za nyuklia ya Marekani na kutafiti muundo wa silaha mpya. Ujenzi wake ulianza Mei 2023 na uligharimu dola milioni 600.
Mabadiliko ya tabia nchi

Chanzo cha picha, Getty Images
Takwimu zilizochapishwa mwezi Januari zilifichua kwamba mwaka 2024 ulikuwa mwaka wa kwanza wa kalenda kurekodiwa kuwa na wastani wa halijoto duniani 1.6°C (2.8°F) juu ya viwango vya kabla ya viwanda.
Habari hizo zilikuja karibu muongo mmoja baada ya nchi 195 kupitisha Mkataba wa Hali ya Hewa wa Paris, ambapo walikubaliana kuchukua hatua za kupunguza halijoto duniani ambayo husababisha mabadiliko ya hali ya hewa kutokana na shughuli za binadamu, na kusababisha joto la zaidi 1.5°C, juu ya wastani wa kabla ya viwanda.
Baadaye mwaka huo, mwezi Juni, wanasayansi walitangaza kwamba ongezeko la asidi baharini lilikuwa limezidi kikomo ambacho sayari inaweza kuhimili.
Tiba ya VVU
Njia ya kupata tiba ya VVU ilifichuliwa mwezi Mei wakati watafiti huko Melbourne, Australia, walipotangaza kuwa wamepata njia ya kulazimisha virusi kuondoka kwenye seli za binadamu.
Kabla ya ugunduzi wao, moja ya changamoto kuu katika kutibu VVU ni kwamba virusi vnaweza kujificha kwenye seli nyeupe za damu, ikimaanisha kuwa vinaweza kufufuka wakati wowote.
Watafiti walitumia teknolojia ya mRNA ili kufanya virusi vionekane - mafanikio ambayo hapo awali yalidhaniwa hayawezekani.
Karibu watu milioni 40 duniani kote wanaishi na VVU na hulazimika kutumia dawa za kukandamiza virusi hivyo ili vikosi nguvu.
Watafiti pia wanaamini ugunduzi wao unaweza kusaidia kutibu magonjwa mengine yanayohusisha seli nyeupe za damu, ikiwa ni pamoja na saratani.
Ishara ya maisha katika sayari ya Mirihi

Chanzo cha picha, NASA
Utafiti kwenye mwamba katika sayari ya Mirihi ulionyesha alama ambazo zinaashiria uwezekano wa kuwepo kwa uhai," kaimu msimamizi wa NASA, Sean Duffy alitangaza mwezi Septemba.
Mwamba huo, unaodhaniwa kuwa na umri wa takriban miaka bilioni 3.5, uligunduliwa na chombo cha NASA cha Perseverance wakati wa uchunguzi wake Julai 2024.
Tangu wakati huo, wanasayansi wa sayari wamekuwa wakijaribu kujua ni nini kiliunda alama hizo. Nadharia kuu ni kwamba zilitoka kwa vijidudu vya kale vya Mirihi.
Ikiwa kila kitu kitaenda kama kilivyopangwa, sampuli ya mwamba huo italetwa Duniani siku moja na kuchunguzwa kwa kina juu ya dalili za maisha ya zamani.
Kutawanyika kwa neutrino kumeonekana
Mwezi Julai, athari inayohusisha neutrino hatimaye ilionekana baada ya miaka 50 ya utafutaji. Kwa mara ya kwanza nadharia hiyo ilielezwa mwaka 1974, ambapo neutrino hutawanyika katika mtambo wa nyuklia dhidi ya kiini cha atomiki.
Wanasayansi wanasema ugunduzi huu ni muhimu na unaweza kuashiria enzi mpya juu ya ugunduzi wa neutrino.
Picha ya kwanza ya kiinitete cha binadamu
Septemba kwa mara ya kwanza kabisa, kiinitete cha binadamu kinapojipandikiza kwenye uterasi bandia kilinaswa kwenye kamera. Video na picha zisizo na mawimbi.
Kushindwa kwa vipandikizi husababisha asilimia 60 ya mimba kuharibika. Watafiti walionasa picha hizo wanatumai watachangia katika uelewa bora wa mchakato huo, ambao unaweza kusaidia kuboresha ya uzazi, katika mimba ya asili na utungisho wa ndani ya kizazi (IVF).
Ulimwengu unapungua kasi

Chanzo cha picha, (Image credit: Shutterstock)
Data iliyotolewa mwezi Machi ilikubaliana na nadharia zilizoanzishwa hapo awali kwamba Ulimwengu unapanuka, lakini iliendelea kupendekeza kwamba kiwango cha kasi kinapungua polepole.
Miezi michache baadaye, mwezi Juni, wanachama wa Mradi wa Kosmolojia ya Supernova walichapisha matokeo mapya ambayo yalionekana kuunga mkono nadhari iliyotolewa mwezi Machi.















