Familia: 'Mwaka mmoja bila Polepole umekuwa mgumu sana'
Familia: 'Mwaka mmoja bila Polepole umekuwa mgumu sana'
Iliyochapishwa
Imetimia mwaka mmoja toka aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba na mkosoaji mkubwa wa serikali ya
Tanzania Humphrey Polepole kutoweka huku familia yake ikisema ametekwa na watu wasiojulikana.
Kaka wa Humphrey, Godfrey Polepole ameiambia BBC hii leo kuwa familia yake inapitia wakati mgumu huku juhudi zao za kumtafuta ndugu yao zimegonga mwamba na hawajapata ushirikiano wa kutosha kutoka mamlaka za Tanzania. Familia hiyo inaituhumu serikali kwa kupotea kwa ndugu yao, madai ambayo mara kadhaa yamekanushwa vikali na serikali ya Tanzania.



