Vyombo vya habari vya Marekani: Pentagon inajiandaa kuanza upya operesheni kubwa ya kijeshi dhidi ya Iran

Chanzo cha picha, Reuters
Vyombo viwili vya habari vya Marekani vimeripoti kuwa Pentagon inajiandaa kwa uwezekano wa shambulio jipya dhidi ya Iran katika siku zijazo.
Tovuti ya habari ya Axios, ikinukuu maafisa wa Marekani, iliripoti kuwa katika siku za hivi karibuni, Pentagon ilitoa agizo kwa CENTCOM (Kamandi Kuu ya Marekani katika Mashariki ya Kati) kukamilisha maandalizi yake ya kuanza upya operesheni kubwa za kijeshi dhidi ya Iran.
Jarida la The Atlantic pia liliripoti katika taarifa ya kipekee, likinukuu maafisa wawili wa Marekani, kwamba Ikulu ya Marekani (White House) imeitaka Pentagon kuandaa chaguzi za kushambulia maeneo muhimu ya Iran ambazo zinaweza kutekelezwa kabla ya uchaguzi wa katikati ya muhula.
Kulingana na The Atlantic, Donald Trump ana hamu kubwa ya kushusha bei ya mafuta na kupata maendeleo makubwa katika mzozo na Iran kabla ya uchaguzi huo.
Kwa mujibu wa Axios, agizo hilo la Pentagon halikutaja tarehe mahususi ya kuanza kwa mashambulio hayo, na Donald Trump bado hajafanya uamuzi wa mwisho.
Hata hivyo, vyanzo vya Marekani na Israel vimeiambia Axios kuwa hatua hiyo inaweza kuchukuliwa kabla ya uchaguzi wa katikati ya muhula wa Marekani na huenda kabla ya uchaguzi wa Israel, ambao hufanyika wiki moja mapema.
Uchaguzi wa katikati ya muhula wa Marekani utafanyika chini ya mwezi mmoja ujao, tarehe 3 Novemba.




































