Caroline Levitt kujiuzulu kama msemaji wa Ikulu ya Marekani - Trump

Chanzo cha picha, Getty Images
Rais wa Marekani Donald Trump amesema Msemaji wa Ikulu ya Marekani, Caroline Levitt, atajiuzulu wadhifa huo mwishoni mwa mwezi huu.
Trump amesema katika ujumbe kwenye mitandao ya kijamii kwamba Levitt anaondoka kwenye nafasi hiyo ili kutumia muda zaidi na watoto wake wadogo pamoja na familia yake, akisema kuwa anaelewa na kuheshimu uamuzi huo kikamilifu.
Trump amemtaja Caroline Levitt kuwa miongoni mwa wasaidizi wake anaowaamini zaidi.
Rais huyo ameongeza kuwa Levitt sasa atakuwa mmoja wa washauri wake muhimu wa nje ya serikali na ataendelea kuwa sauti yenye ushawishi ndani ya Chama cha Republican.
Levitt, mwenye umri wa miaka 28, aliteuliwa kuwa msemaji wa Ikulu mwaka jana na kuwa mtu mwenye umri mdogo zaidi kuwahi kushika wadhifa huo.
Hadi sasa haijafahamika mara moja ni nani atakayemrithi katika nafasi hiyo.






















