Moja kwa moja , Netanyahu akubali kugawana mamlaka na upinzani ili kuunda serikali Israel
Waziri Mkuu wa mpito wa Israel, Benjamin Netanyahu, anatarajiwa kukutana na kiongozi wa upinzani Gadi Eisenkot leo asubuhi kwa mazungumzo ya kutatua mkwamo wa kisiasa uliojitokeza baada ya uchaguzi.
Muhtasari
Eisenkot na Netanyahu kufanya mazungumzo ya kuunda serikali
Moja kwa moja
Na Beldeen Waliaula
Saudi Arabia yadungua kombora la wahouthi lililolenga mji mkuu Riyadh
Chanzo cha picha, EPA
Muungano
wa kijeshi unaoongozwa
na Saudi Arabia unaopambana na waasi wa wahouthi nchini Yemen, umesema umedungua kombora la balistiki
lililokuwa likielekea katika mji
mkuu wa nchi hiyo, Riyadh.
Msemaji
wa muungano huo wa
kijeshi, Turki al-Maliki, amesema
kupitia mtandao wa kijamii wa X kuwa mifumo ya ulinzi wa anga ilifanikiwa
kulinasa na kulidungua
kombora hilo la balistiki lililorushwa na waasi wa Houthi kuelekea Riyadh.
Awali,
waasi wa Houthi walitangaza kuwa walikuwa wamelenga uwanja wa ndege wa Riyadh
pamoja na miundombinu ya mafuta, gesi, umeme na mifumo ya rada ya Saudi Arabia
katika operesheni tano za kijeshi zilizotekelezwa ndani ya saa 48 zilizopita.
Mwezi
Novemba, vikosi vinavyoungwa mkono na Saudi Arabia nchini Yemen viliondoka
katika maeneo yaliyo karibu na Mlango Bahari wa Bab al-Mandab, eneo lenye
umuhimu mkubwa wa kimkakati katika Bahari ya Shamu, na kuyaachia makundi ya wahouthi yaliyokuwa yameanzisha
mashambulizi makubwa.
Netanyahu akubali kugawana mamlaka na upinzani kuunda serikali Israel
Chanzo cha picha, Getty Images
Waziri
Mkuu wa mpito wa Israel, Benjamin Netanyahu, anatarajiwa kukutana na kiongozi
wa upinzani Gadi Eisenkot leo
asubuhi kwa mazungumzo yanayolenga kutatua mkwamo wa kisiasa uliojitokeza
kufuatia uchaguzi wa mwezi uliopita.
Hapo jana, Netanyahu
alisema kuwa yuko tayari kukubali Eisenkot kuwa
Waziri Mkuu wa kwanza katika serikali ya umoja wa kitaifa itakayoongozwa kwa
zamu.
Miungano
miwili inayoongozwa na Waarabu, United Arab List na Joint List, ilipata jumla
ya viti 19, idadi ambayo haijawahi kushuhudiwa, kufuatia ongezeko la idadi ya
wapiga kura kutoka jamii ya Waarabu.
Hali
hiyo imeziweka miungano hiyo katika nafasi ya kuwa na ushawishi mkubwa katika
mazungumzo ya kuunda serikali.
Hata
hivyo, kabla ya uchaguzi, vyama vyote vya Kiyahudi isipokuwa kimoja viliahidi
kutoshirikiana na miungano hiyo kuunda serikali.
Katika
mahojiano na kituo cha televisheni cha Channel 12 cha Israel, kiongozi wa chama cha Raam chenye
msimamo wa wastani wa Kiislamu, Mansour Abbas, alipendekeza kuwa yeye na chama
chake wanaitambua Hamas kama "kundi la
kigaidi".
Hatua
hiyo inaweza kufungua njia kwa chama chake kujiunga na muungano wa kisiasa
unaolenga kumuondoa Netanyahu madarakani.
Eisenkot
amepiga hatua katika juhudi za kupata wingi wa viti anaohitaji kuunda serikali,
baada ya kufikia makubaliano ya kuunda muungano na chama cha Yisrael Beiteinu
pamoja na chama cha The Democrats.
Chama
cha Eisenkot cha mrengo wa kati, Yashar, pamoja na vyama vingine vitatu vya
upinzani vinavyoongozwa na Wayahudi, vilipata jumla ya viti 48 katika uchaguzi
wa Oktoba.
Muungano
wa Netanyahu ulipata viti 53, huku pande zote mbili zikikosa kufikia wingi wa
viti katika Bunge la Israel, Knesset, lenye jumla ya viti 120.
Eisenkot
ana wiki moja kabla ya muda wa kuunda serikali kufik mwisho, tarehe 6 Disemba.
Katika
ujumbe aliouchapisha kwenye mitandao ya kijamii hapo jana, Netanyahu alisema, "Wajibu wangu kama kiongozi
unanilazimu kuweka kila kitu kando, ikiwemo kanuni ya chama kilichopata viti
vingi zaidi."
Aliongeza
kuwa atahudumu mwanzoni kama "Waziri Mkuu msaidizi" katika mpangilio
huo wa kugawana madaraka.
Eisenkot,
ambaye aliwahi kuwa mkuu wa jeshi la Israel, alijibu haraka kwa kumwalika
Netanyahu katika "mazungumzo ya kweli na ya haraka".