Gwaride la kusisimua lafanyika Korea Kaskazini

Iliyochapishwa

'Siku ya jua' mjini Pyongyang iliadhimishwa kwa maonyesho ya makombora, mwendo bila kukunja magoti na mapambo ya nguo (pom-poms)

Wanajeshi wa Korea Kaskazini katika maadhimisho ya 105 ya kuzaliwa kwa rais mwanzilishi wa taifa hilo.
Maelezo ya picha, Korea Kaskazini imeandaa gwaride kubwa na la kusisimua katika mji mkuu Pyongyang kuadhimisha miaka 105 tangu kuzaliwa kwa kiongozi mwanzilishi wa taifa hilo, Kim Il-sung.
Mwanajeshi apiga saluti.
Maelezo ya picha, Maadhimisho hayo yanajulikana kama 'Day of the Sun' ama siku ya jua, kwani Kim Il-sung mara nyingi huwa anatambulishwa kwa ishara jua.
Korea Kaskazini
Maelezo ya picha, Maadhimisho hayo yalionekana kama maonyesho ya nguvu za kijeshi wakati kumekuwa na uhusiano baridi baina ya Marekani na Korea Kaskazini.
Wanajeshi wa Korea Kaskazini wakiwa na silaha
Maelezo ya picha, Mwandishi wa BBC aliyehudhuria maadhimisho hayo anasema kwamba alihisi ardhi ikitetemeka wakati wanajeshi walipokuwa wakipita pamoja na makombora.
Wanajeshi wanawake wakitembea bila kukunja magoti kwa usahihi kamili.
Maelezo ya picha, Wanajeshi wanawake wakitembea bila kukunja magoti katika onyesho la kusisimua.
Bendera ya Korea Kaskazini ilipeperushwa katika maadhimisho hayo.
Maelezo ya picha, Bendera ya Korea Kaskazini ilipeperushwa kwa nguvu.
Kundi la wanaume wakiwa wamebeba mapambo yanayowekwa kwenye nguo ama kofia (pom-poms)
Maelezo ya picha, Kundi la wanaume wakiwa wamebeba mapambo yanayowekwa kwenye nguo ama kofia (pom-poms)
Ndege angani zimeunda umbo la takwimu 105.
Maelezo ya picha, Ndege angani zimeunda umbo la takwimu 105.
Kim Jong-un apungia mkono umati mkubwa wa watu.
Maelezo ya picha, Kiongozi wa Korea Kusini Kim Jong-un, mjukuu wa rais mwanzilishi wa taifa hilo, awapungia mkono watu waliohudhuria maadhimisho hayo.
Mwanajeshi akipiga picha za gwaride la wanajeshi wakati wa maadhimisho hayo.
Maelezo ya picha, Mwanajeshi apiga picha za maadhimisho hayo.